KUSIMAMA AU KUKAA
WAKATI WA KUOMBA NI KINYUME NA MPANGO WA MUNGU.
Namshikuru
mungu kunipatia nafasi hii ya kuandaa nakala hii.ndugu msomaji unayetoa au
kutenga muda kwa kusoma nakala hii Mungu akujalie na akupe hekima na maarifa ya
kumjua yeye na kuenenda kwa kufuata neno
lake kama lisemavyo nawe utapata uzima
wa milele usikubali kudanganywa na walimu wa uwongo na kufuata mapokeo ya
wanadamu. Makanisa mengi ulimwenguni yamekwenda kinyume na mpango wa Mungu. Hekima
na kicho kimetoweka makanisani. Makanisamengi wanaomba wakiwa wamesimama au
wamekaa.Hata na kanisa la sabato,soma Biblia na Roho ya unabii uone kile Mungu anachosema kuhusu maombi ,pia katika nakala
hii tutaona na baadhi ya mapokeo yaliyoingia ndani ya kanisa la wasabato yaliyo
kinyume na la Mungu,Bima ya maisha,Idara
ya wanawake na kuomba wakiwa wamesimama au wamekukaa.
KUOMBA
“Njooni
tuabudu,tusujudu,tupige magoti mbele za BWANA aliyetuumba” ZABURI 95:6
“Kwa nafasi
yangu nimeapa neno hili limetoka kinywani mwangu katika haki, wala halitarudi
ya kwamba mbele zangu kila goti litapigwa,kila ulimi utaapa”ISAYA 45:23
Katika jambo
hili Mungu ametoa msimamo kwa kila mwanadamu anavyopaswa kuja mbele zake.Mfalme
Daudi anatumia neno “Njooni tuabudu,tupige magoti mbele za BWANA” alielewa kuwa
Mungu anapaswa kuabudiwa kwa unyenyekevu.Maana ndio msimamo wa wacha
Mungu.Isaya naya anasema kilekile sawa na daudi. Neno kupiga magoti ni agizo la
Mungu , maana amesema kila goti litapigwa mbele zangu na kwenda kinyume na
mpango huo ni makosa au uasi.
Kielelezo
hiki cha kupiga magoti, kiliendelezwa na watakatifu kizazi hadi kizazi Mtume Paulo anasema “kumbukeni wale
waliowaongoza kwa neno la Mungu tena kwa kuchunguza sana mwisho wa
mwenendo wao waigeni imani yao”.WAEBRANIA 13:7.
Tuone
mifano michache ya watakatifu namna
walivyo mwomba Mungu.Mtume Paulo anasema
“Kwa hiyo tena
Mungu alimwadhimisha mno,akamkilimia jina lipitalo kila jina,ili kwa
jina la yesu kila goti lipigwe na vitu vya mbinguni , na vya duniani na chini ya nchi;na kila ulimi ukiri
ya kuwa YESU KRISTO NI BWANA, kwa utukufu wa Mungu Baba”WAFILIPI 2:9-11.
“YESU ambaye ni jiwe kuu la
pembeni Efeso 2;20 akapiga magoti
akaomba”LUKA 22:41
NABII DANIEL “Alipiga magoti mara tatu kila siku
akisali,akimshukuru mbele za Mungu wake”
DANIEL 6:10
EZRA KUHANI “Na wakati wa sadaka ya
jioni,nikainuka baada ya kunyenyekea kwangu nguo yangu na joho yangu
imeraruliwa,nikaanguka magoti nikiinia juu mikono yangu mbele za BWANA Mungu Wangu”
MTUME PAULO “Alipokwisha kunena haya akipiga
magoti, akaomba pamoja nao wote. MATENDO 20:36, 21:5.
MTUME PETRO: “Petro akawatoa nje wote,akipiga
magoti akiomba “
STEFANO:”Akapiga magoti ,akalia kwa sauti
kuu” MATENDO 7:60
“Tukisali
katika chumba chetu au kanisani inatulazimu kupiga magoti mbele za mungu popote tuombapo ni haki kupiga magoti”MANABII
NA WAFALME UK 21
Ndugu
msomaji , linganisha jinsi watu wa mungu
walivyofanya na ujiulize kile kinacho fanywa na makanisa ya leo na hata wewe mwenyewe.swali , wanao omba hali
wamesimama au kukaa, agizo hilo walilitoa wapi? Jibu ni kwamba kuomba watu
wakiwa wamesimama waliridhi desturi ya mafalisayo wapinzani wa yesu .MATHAYO
6:5-23:1-30, LUKA 18:9-12. Nanyi mwaicha amri ya Mungu na kuyashika maagizo ya
wanadamu.MATHAYO 15:6-12, MARKO 7:6-9.
Mpendwa
msomaji Mungu akusaidie,kufanya mabadiliko katika jambo hili usiendelee kufanya
kinyume na mpango wa mungu.Na kama utaendelea kuomba umesimama au umekaa
,utambue kuwa huna sehemu yoyote miongoni mwa wacha Mungu.
KWA MAWASILIANO ZAIDI WASILIANA NASI
0756959525,0752164685
KWA MAWASILIANO ZAIDI WASILIANA NASI
0756959525,0752164685