Katika blogu hii, tutachunguza njia mbalimbali za kuimarisha ufahamu wetu wa Biblia. Tutajadili mbinu za kusoma Biblia kwa ufanisi, vidokezo vya kukariri maandiko matakatifu, na mikakati ya kutumia somo la Biblia katika maisha yetu ya kila siku. Iwe wewe ni mtaalam wa Biblia mzoefu au unaanza tu safari yako ya imani, "Jifunze Biblia Zaidi" ni rasilimali kamili ya kukusaidia kuongeza ufahamu wako wa Maandiko Matakatifu na kumkaribia Mungu zaidi.

USIWE NA MIUNGU MINGINE ILA MIMI :KUTOKA 20:3

SOMO  : AMRI  YA  1

USIWE NA MIUNGU MINGINE ILA MIMI :KUTOKA 20:3

Katika kitabu cha Kutoka 20:1-17 ndipo pana Amri zote kumi, hapo zimeandikwa kama mhutasari Je umewahi kufahamu kuwa Biblia yote ina zifafanua amri hizi? Hebu twende  pamoja kwa moyo wa unyenyekevu, tuone angalau kwa ufupi, jinsi Biblia yenewe inavyofafanua Amri ya kwanza. Pia zingatia ya kwamba ni vizuri tujifunze amri hizi, tuzifahamu na kuzishika, maana kwakufanya hivyo, tutakuwa tumeanza kuifahamu Biblia, na kubwa kabisa, tutakuwa tumefahamu kanuni ya kumpenda Mungu; kama tunavyosoma:-

 Kwa maana huku ndio kumpenda Mungu, kwamba tuzishike amri zake.Wala Amri zake si nzito.  1 Yohana 5:2-3.

Yeye  aliye na Amri zangu, na kuzishika, yeye ndie anipendae, naye anipendae atapendwa na baba yangu; name nitampenda nakujidhirisha kwake”   Yohana 14:21.

SWALI
Je kama mtu anaenda kanisani kila siku, lakini hazishiki amri za Mungu je, Biblia inasema huyo niwa namna gani?
Yeye asemaye nimekujuwa wala hazishiki Amri zake, ni mwongo, wala kweli haimo ndazni yake.            1 Yohana 2:3 - 4

 Hivi kipimo cha kumtambua mtumishi wa Mungu mwaminifu ni nini?
Sikiliza Biblia yenyewe inavyosema.

“Nakatika hili twajua yakuwa tumemjua yeye, ikiwa tunashika amri zake.1 Yohana 2:3

Umesikia ndugu yangu, yakwamba kumpenda Mungu nikuzishika amri zake.Je unazishika? Zingatia yakwamba mtu anadai kuwa anamjua Mungu lakini huyo anayesema hivyo ikiwa hazishki wala kuzitii Amri (1) Nimwongo (2) Hata kweli ya neno la Mungu haimo ndani yake. Kweli ni nini Yohana 17:17 ina sema kweli ni neno la Mungu. Tazama hata na kipimo cha kumtatambua mtu wa Mungu mwaminifu ni njinsi huyo mtu anavyo zishika amri za Mungu .
Huu ndio ukweli ukiupenda ama usiupende utabaki kuwa ukweli wa milele.

Sasa hebu tuanze amri ya kwanza.

“Mungu akanena maneno haya yote akasema, Mimi ni Bwana, Mungu wako, niliyekutoa katika nchi ya Misri katika nyumba ya utumwa, usiwe na Miungu mingine ila mimi Kutoka  20:1-3.

Unaweza kuwa na swali, mbona sijawahi kuwa mtumwa mbona hatutawaliwi na Misri, na ukadhani amri hii haikuhusu.Utumwa unaozungumzwa hapa niuitumwa wa dhamnbi.Ingawa hatukuwa watumwa wa Misri lakini dhambi zile za misiri tumeshiliki kuzitenda, huo ndio utumwa unaotajwa hapa.

“Lakini Mungu ashukuriwe, kwa maana mlikuwa watumwa wadhambi, lakini mlitii kwa mioyo yenu ile namna ya elimu ambayo mliwekwa chini yake; namlipokwisha  kuwekwa huru mbali na dhambi,mkawa watumwa wa haki”.   Warumi 6:17-18

Sasa  jambo lakujifunza katika amri hii, tunapaswa tuchunguze tufahamu kwanini Mungu amekataza mwanadamu asiwe na Miungu mingine;.

SABABU YA 1.
Umestahili wewe Bwana wetu na Mungu wetu, hupokea utukufu na heshima na uweza; kwakuwa wewe ndiwe uliyeumba vitu vyote, nakwasababu ya mapenzi yako vilikuwako, navyo vikaumbwa”.   Ufunuo  4:11.

“Eee Bwana wa Majeshi, Mungu wa Israeli, ukaaye juu ya Makerubi, wewe naam, wewe peke yako, ndiwe Mungu wa Falme zote za dunia.Wewe ndie ulieziumba mbingu na nchi. 
Isaya 37:16.

“Bwana Mungu akamfanya mtu kwa mavumbi ya ardhi, akampulizia puani pumzi ya uhai; mtu akawa nafsi hai”.  Mwanzo  2:7.

Sababu ya kwanza iliyofanya Mungu akataze mwanadamu asiwe na Miungu mingine; ni kwasababu ndie  alietuumba tena ndie aliviumba vitu vyote.

SABABU  YA 2.
“Mtanifananisha na nani, nakunisawazisha naye, na kunilinganisha naye, ili tuwe sawasawa? Isaya 46:5,   44:6.

Kumbukeni mambo yazamnai za kale; maana mimi ni Mungu wala hapana mwingine; mimi ni Mungu, wala hapana aliye kama mimi”.  Isaya 46:9.

Mimi ni Alfa na Omega,Mwanzo na mwisho asema Bwana Mungu, aliyeko na aliekuwako, na atakayekuja, mwenyezi  . Ufanuo 1:8.

Sababu ya pili iliyofanya Mungu akataze mwanadamu asiwe na Miungu mingine, nikwa sababu hakuna Mungu mwingine alie kama yeye, hakuna wakumlinganisha nae, hakuna wakumfanananisha nae. Zingine maandiko yanasema, aliyekuwako aliyeko na atakae kuja. Maana yake ni wamilele, na ndio maana amri inasema, Usiwe na Miungu mingine ila mimi.Je  rafiki yangu huyu ndie Mungu unaemwabudu? Kama ulikuwa haujamfahamu tafadhali anza sasa kumwabudu mfalme wa uzima.

Amri hizi zote huonyesha kanuni ya upendo.Amri yakwanza haiwezi kushikwa na yapili kuvunjwa.Napenda tu tumpendavyo Mungu kadri iwezekanavyo, ndivyo itakavyo wezekana kumpenda jirani bila upendeleo.Kristo aliwafundisha wasikilizaji wake  kuwa amri za Mungu niza muhimu zote, wala hazitengani.Hakuna ya muhimu kuliko nyingine kumpenda Mungu kutadhirika katika kuzishika amri zake zote.  Tumaini la vizazi vyote 340: 3  Elen  G. White

 Hebu tujifunze kidogo ukuu wake na  kiti chake cha enzi ndipo ujue huyu ndie Mungu anaestahli kuabudiwa:

Kiti chake cha enzi na jinsi alivyo nabii yohana anasema:-
Namara nalikuwa katika Roho natazama, kiti cha enzi kimewekwa mbinguni na mmoja ameketi juu ya kile kiti; nay eye aliyeketi alionekana  mithiri ya jiwe la yasipi na akiki, na upinde wa mvua likuzunguka kile kiti cha enzi, ukonekana mithili ya zumaridi.

Ufunuo  4:2 -3
Tuendelee kuona kiti chake cha enzi.

“Katika  mwaka ule aliokufa Mfalme Uzia balimwona Bwana ameketi katika kiti cha enzi, kilicho juu sana nakuinuliwa juu sana napindo za vazi lake zikalijaza hekalu.” Isaya 6:1
“na katika kila kiti cha enzi kunatoka umeme na sauti na ngurumo, nataa saba za moto zikiwaka mbele ya kile kiti cha enzi, ndizo roho saba za Mungu.Nambele ya kiti  cha enzi  kulikuwa na mfano wa bahari ya kioo, kama biurauli, nakatikati ya kile kiti cha enzi, na pande zote za kile kiti, walikuwako wenye uhai wanne, wamejaa macho mbele na nyuma .Ufunuo 4:5-6

Jinsi alivyo –ukuu wake.
Kichwa chake kikoje, macho yake, Miguu yake na sauti yake vikoje, sikiliza:-

“Kichwa chake na nywele zake zilikuwa nyeupe kama sufu  nyeupe, kama theruji, na macho yake kama mwali wa moto, na miguu yake kama shaba iliyosunguliwa sana. Kana kwamba imesafishwa katika tanuru; na sauti yake kama sauti ya maji mengi.”    Ufunuo   1:14-15.

Hebu tuendelee kuchunguza katika neno lake, Mungu aliekataza mwanadamu asiwe na Mungu mingine, ukuu wake ulivyo: sasa hebu tuangalie mwili wake, uso wake, macho yake, mikono na miguu vikoje. Sikiliza neno linavyosema:-

Mwili wake pia ulikuwa kama zambarajadi safi, na uso wake mfano wa umeme, na mamcho yake kama taa za moto, na  mikono yake na miguu yake, rangi yake kama shaba iliyosuguliwa sana, na sauti ya maneno yake kama sauti ya umati wa watu”.  Daniel   10:6

Mungu ni mzee, maandiko yanasema ni mzee wa siku hebu tuthibitishie hayo, tuangalie na mavazi yake nywele zake, nakiti chake cha enzi jinsi kilivyo:-

“Nikatazama hata viti vya enzi vikawekwa, na mmoja alie mzee wa siku ameketi; mavazi yake yalikuwa meupe kama theruji, na nygwele za kichwa chake kama sufu safi; kiti chake cha enzi kilikuwa miali ya moto, na gurudumu zake kama moto uwakao.”   Daniel   7:9

Ni mavazi gani hayo ambayo ni meupe kama theruji?.

Umejivika nuru kama vazi, umezitandika mbingu kama pazia”  Zaburi 104:2

Hebu tuchunguze Umri wake:-

“Tazama, Mungu ni mkuu, nasi hatumjui, hesabu ya miaka yake  haitafutiki”    Ayubu  36:26

“Natena, wewe, Bwana hapo mwanzo uliitia misingi ya nchi, na mbingu nikazi ya mokono yako, hizo zitaharibika, bali wewe unadumu; nazo zote zitachakaa kama nguo, nakama mavazi utazizinga, nazo zitabadilika; lakini wewe, u yeye Yule, namiaka yako haitakoma”.                     Ebrania  1:10-12

“Yehova, wa milele, mwenye uwezo wakuwepo mwenyewe, ambaye hakuumbwa, yeye mwenyewe akiwa chanzo na mpaji wa wote, ni yeye peke yake mwenye haki yakuheshimiwa na kuabudiwa.Mwanadamu amekatazwa kutoa nafasi ya kwanza wa kitu au kiumbe chochote katika upendo na  utumishi wake. Chochote kinachopelekea kupunguza upendo wetu kwa Mungu au kuingilia utumishi wetu kwake, hicho tunakifanya kiwe Mungu” (Mwsingine).1 Wazee na manabii Uk 293 -294 E.G White.

Hebu sasa tuchunguze uwezo wake.
“Tazama, mimi ni Bwana, Mungu wa wote wenye mwili; Je! Kuna neno gumu lolote nisiloliweza?.   Yeremia 32:27

“Lakini Mungu wetu yuko mnbingni, alitakalo lote amelitenda”.  Zaburi  115:3
“Yesu akawakazia macho, akasema, kwa wanadamu haiwezekani bali kwa Mungu sivyo: maana yote yawezekana kwa Mungu”  Marko 10:27

Wala  hakuna kiube kisichokuwa wazi mbele zake, lakini vitu vyote vi utupu nakufunuliwa machoni pake yeye aliye na mambo yetu”.  Ebrania 4:14

“Ee Bwana, umenichunguza nakunijua. Wewe wajua kuketi kwangu nakuondoka kwangu; umelifahamu wazo langu tokea mbali. Umepepeta kwenda kwangu na kulala kwangu, umeelewa na njia zangu zote.Maana hamna neno ulimini mwangu usilolijua kabisa, Bwana. Umenizingira nyuma na mbele, ukaniwekea mkono wako.Maarifa hayo ni yaajabu, yanishinda mimi, hayadirikiki, siwezi kuyafikia. Niende wapi  nijiepushe na roho yako? Niende wapi niukimbie uso wako? Kama ningepanda mbinguni, wewe uko ningefanya kuzimu kitanda changu, wewe uko. Ningezitwaa mbawa za asubuhi, nakukaa pande zote za mwisho wa bahari; huko nako mkono wako utaniongoza, na mkono wako wa kuume  utanishika. Kama nikisema, hakika giza  litanifunika, na nuru inizungukayo ingekuwa usiku; Giza nalo halikufichi kitu, bali usiku huangza kama mchana, giza na mwanga kwako nisawasawa”  Zaburi 139: 1- 12.

Rafiki yangu umeona uwezo wa muumbaji wetu, yakwamba hakuna neno asiloliweza, analolitaka huko mbinguni analitenda, yote yawezekana kwake, wala hakuna kiumbe kisichokuwa wazi mbele yake.Angalia maandiko yanafafanua kwamba, hata kama mtu angeenda kuzimu, maana leo kuna watu wanasikika kuwa wanaenda kuzimu, kupata nguvu ya miujiza, uongo, na  kupata utajirisho toka nguvu za giza, neno linasema huko nako atakuona, huko nako mkono wake upo.Yakwamba niwapi utaenda ujiepushe na uso wake hakuna.Huyu ndie Mungu anae sitahili kuabudiwa.Nandio  maana amri inasema; “usiiwe na miungu mingine ila mimi”.

Je ufalme wake na kiti chake cha enzi vina ukomo?.

Kiti chako cha enzi,Mungu niche milele na milele, fimbo ya ufalme wako ni fimbo ya adili”.      Zaburi 45:6.

Je! Wewe waweza kuuvumbua ukuu wa Mungu? Waweza kuufikilia upeo wa huyo mwenyezi? Ni juu mno kama mbingu; waweza kufanya nini wewe? Niwenyekina kuliko kuzimuni; waweza kujua nini wewe? Cheo  chake  nikirefu kuliko dunia, nikipana zaidi ya bahari.Yeye akipita, na kufunga watu, nakuwaita hukumuni, ni nani basi awezaye kumzuai?. Ayubu 11:7-10.


Mungu ni roho; lakini ni nafsi, maana mtu aliumbwa kwa sura yake. Kazi ya mikono ya Mungu kwenye viumbe si mungu mwenyewe.Viumbe vya asili ni ufunuo wa tabia ya Mungu; kwanjia ya viumbe hivyo twaweza kuufahamu upendo wake; uwezo wake, na utukufu wake; lakini haitupasi kuvihesabu viumbe kama ni Mungu.Akili ya kazi ya sanaa ya wanadamu hutoa ustadi mzuri ajabu, vitu vinavypendeza macho, navitu hivi  hutupa sisi wazo Fulani la fundi huyo wasanaa. Lakini viumbe vikiwa ufunuo wa mawazo ya Mungu, siyo viumbe bali Mungu alieviumba ambae hupaswa kutukuzwa”.     1 Kutayarisha njia Uk.86:2  Elen G. White

Huyu ndie Mungu anayestahili kuabudiwa .Na ndiyo maana amri inasema”usiwe na miungu mingine ila mimi” .Hebu tunapoelekea kumaliza somo letu tuangalie je leo mwanadamu anayekufa nakuoza anaweza kumuona Mungu? Mtumishi wa Mungu Musa ambae maandiko yanasema alikuwa mpole kuliko wanadamu wote dunian,aliwahi kusii aonyeshwe utukufu wa Mungu :Jibu alilopewa Musa: Ndio jibu letu sote, sikiliza:-


MUSA
Akasema, nakusihi unionyeshe utukufu wako Kutoka 33:18

Jibu la Bwana
Kisha akasema, huwezi kuniona uso wangu, maana mwanadamu hataniona akaishi”.               Kutoka 33:20

Rafiki  yangu tunapomaliza somo letu zingatia yafuatayo:-
“Moyo wangu na uwe mkamilifu katika amri zako nisije mimi nikaaibika”  Zaburi 119:80
“Ee Bwana, unifundishe njia ya amri zako, name nitaishika hata mwisho Zaburi 119:33
“Wokovu  umbali nawasio haki, kwa maana hawajifunzi Amri”.  Zaburi 119:155
“Lakini mtu mbaya akighairi, nakuacha dhambi zake zote alizozitenda. Nakuzishika amri zangu zote, nakutenda  yaliyo halali na haki, hakika ataishi, hatakufa”. Ezekieli 18:21

“Mkinipenda mtazishika amri zangu” Yohana 14:15

“Mpaka mbingu na nchi zitakapopita, yodi moja au nukta moja ya torati haitondoka, hata yote hatimae”.Jua liwakalo na nchi isimayo imara nimashahidi wa Mungu kwamba sheria yake n yamilele.Hata kama mbingu na nchi zitapita, lakini sheria ya Mungu itadumu.Kawaida ya mfano kwamba Yesu nimwanakondoo wa Mungu, itapita wakati wakifo cha Yesu, lakini Amri za Mungu zitadumu kama kiti chake enzi kidumuvyoTumaini la vizazi Uk. 166:3 
(Elen G. White).

Mpendwa msomaji endelea kufuatilia makala hii na Mungu akubariki AMINAAA!!!!!!
                               ITAENDELEA.

 KWA MAWASILIANO ZAIDI WASILIANA NASI
0756959525,0752164685
Share:

Popular Posts

Lebo

Recent Posts

Pages