Katika blogu hii, tutachunguza njia mbalimbali za kuimarisha ufahamu wetu wa Biblia. Tutajadili mbinu za kusoma Biblia kwa ufanisi, vidokezo vya kukariri maandiko matakatifu, na mikakati ya kutumia somo la Biblia katika maisha yetu ya kila siku. Iwe wewe ni mtaalam wa Biblia mzoefu au unaanza tu safari yako ya imani, "Jifunze Biblia Zaidi" ni rasilimali kamili ya kukusaidia kuongeza ufahamu wako wa Maandiko Matakatifu na kumkaribia Mungu zaidi.

JE, NI HALALI WANAWAKE KUHUBIRI MIMBARINI?

JE, NI HALALI WANAWAKE KUHUBIRI MIMBARINI?


Nataka wanaume wasalishe kila mahari……. Huku wakiinua mikono iliyotaka……………simpi ruhusa mwanamke kufundisha wala kumtawala mwanaume………..1Timotheo 2:8-12, Mwanzo 3:16-17
Kanisa lolote linalowaweka wanawake kuhuibiri mimbarini ni kuinua ibada ya Tamuzi na kuiharalisha, Nabii Ezekieli alipoona machafuko kama hayo alishangaa sana.Mungu  alimwambia utaona makubwa zaidi ya hayo.
“ndipo akanileta mpaka mlango wa kuingilia katika nyumba ya BWANA ulioelekea upande wa kaskazini na tazama, wanawake wakimlilia Tamzi”Ezekieli 8:14,Nehemia 8:4
Tangu mwanadamu alioumba, mwanaume ndiye aliye kabadhiwa madaraka.wakati Adamu anakabidhiwa ukuhani,na madaraka, “mungu alimwambia matunda ya mti wa ujuzi wa mema na mabaya usile.MWANZO 1:16 siyo msile kwa Hawa akizungumza na nyoka alijibu usile.MWANZO 3:1HATA kazi ya uongozi alikabidhiwa mwanaume ,na ndiye aliye waita viumbe majina MWANZO 2:20……… Kanuni hiyoaliichagua Mungu mwenyewe sisi hatuna ruhusa, kuhoji au kulekebisha mpango ulowekwa na MUNGU tangu zamani, mimbari imekuwa ikitumiwa na wanaume .1Wafalme8:54, 2 Nyakati6:12-13.

MIMBALI IPO HADI LEO?

 JIBU “wengi watasimama katika mimbari zetu wakiwa wamenyanyua mienge ya unabii wa uongo mikononi mwao” Matukio 165 .TM 409, 1411, 1898.Ieleweke kwamba kunatofauti kati ya mimbari na huduma za patakatiifu
       I.            Mimbari ni mahari ambapo wafalme ,waamzi,makuhani na viongozi wote waisraeli walikuwa , wakiwafundisha watu na kutoa maelezo jinsi watu wanavyopasa kumtumikia Mungu, Luka 4:16,Matendo 2:14.
    II.            Patakatifu waliruhusiwa makuhani pekee yao tu.Mfano chumba cha pili cha patakatifu  pa patakatifu aliingia kuhani mkuu  pekee yake  Walawi 16:1-34 kutoka sura ya 25 na sura ya 29.
Mimbari ndio ofisi takatifu kwa ajili ya makuhani  wa leo ,lakini wanatakiwa watu kama kalebu,walio  
majasiri kwa watu wanotambua ukweli kutoka kwenye makosa TM 407.
“Wachungaji na wazee  wa makanisa wameitwa kwa kazi ya ukuhani wa leo wanapaswa kuanza kazi hiyo katika familia zao ambayo ni makanisa madogo”2T 620 1Timotheo 3:1-7
“Wachungaji na wazee wameitwa kwa kazi ya ukuhani  wa leo kutoa kafara ya kiroho”FE 461 Tito 1:5-8
“Siyo kila mtu anaweza kuwa mwalimu wa Neno la Mungu kwenye Mimbari” 4T118
“hakuna mtu anayefaa kusimama katika mimbari takatifu.Mpaka awe ametakaswa na kuguswa na Neno la Mungu katika moyo wake. 4T526.
“Mpaka ambayo neno la Mungu liliweka kwa ajili ya watu wa Mungu imevunjwa na kuanguka chini. Wale ambao walikuwa wanafahamu njia ambayo Mungu amewaongoza watu wake kwa wakati uliopita .baada ya kuuliza mapito ya zamani na kuutetea msimamo wetu kama watu wapekee wameonyesha mikono yao kushikamana na dunia.sauti ya maonyo yamenyamanzishwa.Macho ya watu wa Mungu yametiwa giza wakati huo kanisa likienda mbio kwenda duniani” 4T uk. 513.
Hatuna shaka tunapoona mambo yanayotokea duniani yakipenya na kuingia kanisani na kutolewa kwa nguvu,ni kwa sababu viongozi ambao wangeongoza watu kupitia katika njia ya ulimwengu.



KWA MAWASILIANO ZAIDI WASILIANA NASI
0756959525,0752164685








Share:

KUSIMAMA AU KUKAA WAKATI WA KUOMBA NI KINYUME NA MPANGO WA MUNGU.

KUSIMAMA AU KUKAA WAKATI WA KUOMBA NI KINYUME NA MPANGO WA MUNGU.
UTANGULIZI:
Namshikuru mungu kunipatia nafasi hii ya kuandaa nakala hii.ndugu msomaji unayetoa au kutenga muda kwa kusoma nakala hii Mungu akujalie na akupe hekima na maarifa ya kumjua yeye na kuenenda  kwa kufuata neno lake kama lisemavyo  nawe utapata uzima wa milele usikubali kudanganywa na walimu wa uwongo na kufuata mapokeo ya wanadamu. Makanisa mengi ulimwenguni yamekwenda kinyume na mpango wa Mungu. Hekima na kicho kimetoweka makanisani. Makanisamengi wanaomba wakiwa wamesimama au wamekaa.Hata na kanisa la sabato,soma Biblia na Roho ya unabii uone kile Mungu  anachosema kuhusu maombi ,pia katika nakala hii tutaona na baadhi ya mapokeo yaliyoingia ndani ya kanisa la wasabato yaliyo kinyume na  la Mungu,Bima ya maisha,Idara ya wanawake na kuomba wakiwa wamesimama au wamekukaa.
KUOMBA
“Njooni tuabudu,tusujudu,tupige magoti mbele za BWANA aliyetuumba”  ZABURI 95:6
“Kwa nafasi yangu nimeapa neno hili limetoka kinywani mwangu katika haki, wala halitarudi ya kwamba mbele zangu kila goti litapigwa,kila ulimi utaapa”ISAYA 45:23
Katika jambo hili Mungu ametoa msimamo kwa kila mwanadamu anavyopaswa kuja mbele zake.Mfalme Daudi anatumia neno “Njooni tuabudu,tupige magoti mbele za BWANA” alielewa kuwa Mungu anapaswa kuabudiwa kwa unyenyekevu.Maana ndio msimamo wa wacha Mungu.Isaya naya anasema kilekile sawa na daudi. Neno kupiga magoti ni agizo la Mungu , maana amesema kila goti litapigwa mbele zangu na kwenda kinyume na mpango huo ni makosa  au uasi.
Kielelezo hiki cha kupiga magoti, kiliendelezwa na watakatifu  kizazi hadi kizazi  Mtume Paulo anasema “kumbukeni wale waliowaongoza kwa neno la Mungu tena kwa kuchunguza sana  mwisho wa  mwenendo wao waigeni imani yao”.WAEBRANIA 13:7.
Tuone mifano  michache ya watakatifu namna walivyo mwomba Mungu.Mtume Paulo anasema
            “Kwa hiyo  tena  Mungu alimwadhimisha mno,akamkilimia jina lipitalo kila jina,ili kwa jina la yesu kila goti lipigwe na vitu vya mbinguni , na vya  duniani na chini ya nchi;na kila ulimi ukiri ya kuwa YESU KRISTO NI BWANA, kwa utukufu wa Mungu Baba”WAFILIPI 2:9-11.
            “YESU ambaye ni jiwe kuu la pembeni  Efeso 2;20 akapiga magoti akaomba”LUKA 22:41
NABII DANIEL “Alipiga magoti mara tatu kila siku akisali,akimshukuru mbele za Mungu wake”
                           DANIEL 6:10    
EZRA KUHANI “Na wakati wa sadaka ya jioni,nikainuka baada ya kunyenyekea kwangu nguo yangu na joho yangu imeraruliwa,nikaanguka magoti nikiinia juu mikono yangu mbele za BWANA  Mungu Wangu”
MTUME PAULO “Alipokwisha kunena haya akipiga magoti, akaomba pamoja nao wote. MATENDO 20:36, 21:5.
MTUME PETRO: “Petro akawatoa nje wote,akipiga magoti akiomba “
STEFANO:”Akapiga magoti ,akalia kwa sauti kuu” MATENDO 7:60
“Tukisali katika chumba chetu au kanisani inatulazimu kupiga magoti mbele za mungu  popote tuombapo ni haki kupiga magoti”MANABII NA WAFALME UK 21
Ndugu msomaji , linganisha  jinsi watu wa mungu walivyofanya na ujiulize kile kinacho fanywa na makanisa ya leo na hata  wewe mwenyewe.swali , wanao omba hali wamesimama au kukaa, agizo hilo walilitoa wapi? Jibu ni kwamba kuomba watu wakiwa wamesimama waliridhi desturi ya mafalisayo wapinzani wa yesu .MATHAYO 6:5-23:1-30, LUKA 18:9-12. Nanyi mwaicha amri ya Mungu na kuyashika maagizo ya wanadamu.MATHAYO 15:6-12, MARKO 7:6-9.
Mpendwa msomaji Mungu akusaidie,kufanya mabadiliko katika jambo hili usiendelee kufanya kinyume na mpango wa mungu.Na kama utaendelea kuomba umesimama au umekaa ,utambue kuwa huna sehemu yoyote miongoni mwa wacha Mungu.

KWA MAWASILIANO ZAIDI WASILIANA NASI
0756959525,0752164685
Share:

KWA MAWASILIANO ZAIDI PIGA SIMU NAMBA


KWA MAWASILIANO ZAIDI PIGA SIMU NAMBA
0766815470,0752164685,0756959525
Share:

MCHENI MUNGU NA KUZISHIKA AMRI ZAKE

MCHENI MUNGU NA KUZISHIKA AMRI ZAKE


UTANGULIZI
“Dunia inaomboleza,inazimia,ulimwengu unadhoofika,unazimia,watu wakuu wa dunia wanadhoofika.tena dunia imetiwa unajisi kwa watu wanaoikaa,kwa maana wameziasi sheria,wameibadili amri.wamelivunja agano la milele.Ndiyo sababu laana imeila dunia hii,na watu wanaoikaa wameonekana kuwa na hatia,ndiyo sababu watu wanaoikaa dunia wameteketea,watu waliosalia wakawa wachache tu” ISAYA 24:4-6
Mpendwa msomaji,tafakari sana aya hizi za utangulizi.
Unaweza kuungana na kile maandiko yanachoonyesha kuhusu hali halisi ya Dunia yetu hii leo.
Laana inaila dunia yetu hii leo kwa sababu zifuatazo
1.      “Wameziasi sheria”
2.      “Wameibadili amri”
3.      “wamelivunja agano la milele”
Hivyo katika waraka huu, mungu anahitaji kutuonyesha namna ya kuepukana na laana hiyo.ila tu nai mpaka pale tutakapogundua mambo yafuatayo:-
1.      Amri hizo za mungu ni zipi?na ni ngapi?
2.      Amri hizo za mungu ni za muhimu mpaka sasa?(kizazi hiki)
3.      Amri hizo za mungu,kila mtu anapaswa kuzijua na kuzitii? Na anwajibishwa kwa kutozifahamu au kuzivunja? Kwa hayo na yanayotokana na hayo ndiyo lengo la waraka huu.mungu akubariki uanaposoma Neno Lake.
AMRI ZA MUNGU NI ZIPI NANI NGAPI?
1.      Usiwe na miungu mingine ila mimi.KUTOKA 20:3
2.      Usijifanyie sanamu ya kuchonga,wala mfano wa kitu chochote kilicho juu mbinguni,wala kilicho chini duniani,wala kilich majini chini ya dunia.usivisujudie wala kuvitumikia;kwa kuwa  mimi ,BWANA Mungu wako ni Mungu mwenye wivu;nawapatiliza wana maovu ya baba zao,hata kizazi cha tatu na cha nne chawanichukiao,name nawarehemu maelfu elfu wanipendao na kuzishika amri zangu.KUTOKA 20:4-6
3.      Usilitaje bure jina la BWANA,Mungu wako maana BWANA hata mhesabia kuwa hana hatia mtu alitajae jina lake bure.KUTOKA 20:7
4.      Ikumbuke siku ya Sabato uitakase.Kwa siku sita utafanya kazi zako zote, lakini siku ya saba ni Sabato kwa BWANA Mungu wako. Siku hiyo hutafanya kazi yo yote, wewe wala mwana wako au binti yako, wala mtumishi wako wa kiume au wa kike wala wanyama wako, wala mgeni aliye ndani ya malango yako.Kwa kuwa kwa siku sita, BWANA aliumba mbingu na nchi, bahari na vyote vilivyomo ndani yake, lakini akapumzika siku ya saba. Kwa hiyo BWANA akaibariki siku ya Sabato na kuifanya takatifu.KUTUKA 20:8-11.Katika  amri ya nne,tunaagizwa  kuitunza sabato.
SABATO NI SIKU IPI?
Biblia inatuambia kuwa sabato ni siku ya saba katika wiki.biblia inasema :-
“Baada ya siku ya sabato, maria Magdalena, salome na maria mama yake yakobo walinunua manukato ili waupake mwili wa yesu .basi alfajiri na mapema siku ya jumapili,walifika kaburini,jua lilipoanza kuchomoza”.
MARKO 16:1-2(BIBLIA-HABARI NJEMA, KISWAHILI CHA KISASA)
Hivyo hapo na habari ya ufufuko wa Yesu,tunaona kuwa alifufuka jumapili amboyo ndiyo siku ya kwanza  ya juma  soma MATHAYO 28:1
Ø  Pia biblia inatuonyesha siku ya kifo chake,ilikuwa ijumaa ambayo ndiyo maandalio ya sabato.
“Siku hiyo ilikuwa ijumaa,na maandalio ya siku ya sabato yalikuwa yanaanza .wale wanawake  walioandamana na yesu kutoka  Galilaya walimfuata Yosefu, wakaliona lile kaburi na jinsi mwili wake Yesu ulivyowekwa .Halafu wakarudi nyumbani,wakayatayarisha manukato na marashi ya kuupaka mwili wa Yesu .Siku ya sabato walipumzika kama ilivyoamriwa na sheria”LUKA 23:54-56
(BIBLIA TOLEO LA HABARI NJEMA KISWAHILI CHA KISASA)
Kwahiyo tunaona kuwa sabato siyo ijumaa wala Jumapili bali ni Jumamosi
5. Waheshimu baba yako na mama yako, ili upate kuishi siku nyingi katika nchi anayokupa   BWANA Mungu wako.KUTOKA 20:12
6. Usiue. KUTOKA 20:13

7. Usizini. KUTOKA 20:14

8. Usiibe. KUTOKA 20:15

9. Usitoe ushuhuda wa uongo dhidi ya jirani yako. KUTOKA 20:16
10. Usiitamani nyumba ya jirani yako. Usimtamani mke wa jirani yako, wala mtumishi wake wa kiume au wa kike, wala ng’ombe wake au punda wake wala cho chote kile alicho nacho jirani yako. KUTOKA 20:3-17, KUMBUKUMBU LA TORATI 5:7-21
Ø  Amri za Mungu ni za muhimu kwa Nyakati zote na vizazi vyote.Yesu anatoa agizo hili juu ya umuhimu wa amri za Mungu:-
“……………………….lakini ukitaka kuingia katika uzima zishike amri MATHAYO 19:17
“Msidhani kwamba nimekuja kuondoa Torati au Manabii, sikuja kuondoa bali kutimiza.Kwa maana,amin, nawaambia, mpaka mbingu na dunia zitakapopita, hakuna hata herufi moja ndogo wala nukta itakayopotea kwa namna yo yote kutoka kwenye Torati mpaka kila kitu kiwe kimetimia. Kwa hiyo, ye yote atakayevunja mojawapo ya amri ndogo kuliko zote ya amri hizi, naye akawafundisha wengine kufanya hivyo, ataitwa mdogo kabisa katika Ufalme wa Mbinguni, lakini ye yote azitendaye na kuzifundisha hizi amri ataitwa mkuu katika Ufalme ya Mbinguni.Kwa maana nawaambia, haki yenu isipozidi haki ya waandishi wa sheria na Mafarisayo, kamwe hamtaingia katika Ufalme wa Mbinguni”.MATHAYO 5:17-19
Ø  Watu wengi leo ,hutoa udhuru wa kuzishika Amri kumi za Mungu,kwa madai ya kumwamini na kumpenda Yesu.Husema “Ukimwamini Yesu tu,inatosha,hakuna haja ya kuzishika amri”.je, udhuru huo Yesu aliukubali katika maandiko matakatifu?
Yesu mwenyewe alisema;-
Mkizishika amri Zangu mtakaa katika pendo Langu, kama Mimi nilivyozishika amri za Baba Yangu na kukaa katika pendo Lake.”YOHANA 15:10
“Kama mnanipenda, mtazishika amri Zangu.”YOHANA 14:15
Kwa kuwa huu ndio upendo wa Mungu, kwamba tuzitii amri Zake. Nazo amri Zake si nzito”.1YOHANA 5:3
Ø  Je amri za Mungu kila mtu anapaswa kuzijua na kuzishika? Au kwa ajili ya watu Fulani tu,au dhehebu Fulani tu?
Biblia Inasema:-
“Hii ndiyo ya maneno ;yote yamekwesha sikiwa,mche mche Mungu, nawe uzishike amri zake maana kwa jumla ndiyo impasavyo mtu “MHUBIRI 12:13
Hivyo tunaona kuwa biblia inasema kuzishika amri za mungu kunampasa kila mtu yeyote anayejifahamu kuwa yeye ni mtu ‘ anapaswa kuzishika amri za mungu. Hata kama mtu angesema’Mima nampenda mungu’ au mimi nimeokoka; kama bado hataki kuzishika Amri za mungu ;madai yake huyo hayaungwi mkono na Biblia kwan maandiko yanasema”
Wokovu u mbali na wasio haki’ kwa maana hawajifunzi amri zako ZABURI 119:115
‘’Umewakataa wote wazikosao amri zako ,kwa maana hila zao ni uongo’’ZABURI 119:118
‘’Na katika hili twajua ya kuwa tumemjua yeye ikiwa tunashika amri zake.Yeye asemaye nimemjua ,wala hazishiki amri zake,ni uongo wala wala kweli haimo ndani yake’’YOHANA2:34.MITHALI28:9
Ø  Kwa hiyo hapana maandiko yatwambia kuwa,kutozitii amri za mungu nab ado huku tukijiita wakristo,Watu wa mungu Wanaompenda Mungu ,Walio okoka, Washika ibada na majina mengine kama hayo ya kujisifia uumini Huku tunapinga na kuvunja amri za mungu Maandiko yanasema watu wa namna hiyo ni ‘’WAONGO’’NA tunajua kuwa mwongo hawezi kwenda mbingni (soma ufunuo 21;8,22;15)Maana uongo bado ni uvunjaji wa amri ya tisa (KUTOKA 20;16)Katika amri kumi za MUNGU                                            
Wengi wamefundishwa kuzishika amri baadhi na zingine kuziacha,na kutoa mafundisho kuwa eti hizi hazituhusu,maana ziliondolewa na yesu pale msalabani n.k kwa mfano,amri ya pili inayokataza ibada ya sanamu (KUTOKA 20:4-6)NA amri ya nne inayo waigiza watu waitunze sabato siku ya saba ya juma (KUTOKA 20:8-11)amri hizi zimevunjwa wazi na kuondolewa na watu mamilion wanafundishwa na viongozi wao wa makanisa kuwa amri hizo kwa sasa haziwahusu.Huu ni mpango mkuu wa Yule adui (SHETANI)kuwafanya watu wamwasi Mungu kwa kuzivunja amri zake.                         
BIBLIA YENYEWE ANATOA ANGALIZO HILI:-                                                  
“Maana mtu awe yote atakaye shika sheria yote ila akajikwaa katika neon moja amekosa juu ya yote kwa maana yeye alisema,usizini,pia alisema usiue.Basi ijapokuwa hakuzini lakini umeua umekuwa mvunja sheria. Semeni ninyi na kutenda kama watu watakao hukumiwa kwa sheria ya uhuru’’YAKOBO 2:10-12, SOMA PIA, MATHAYO 5:19      
Kwa  nini watu wengi wachague kuvunja amri za mungu na hali ya kuwa amri ziko wazi katika neon lake –maandiko matakatifu.?                       
Biblia ainatoa sababu ya uvunjaj I wa sheria hizo za mungu kauli ya yesu iliyo sema:-   
Akawambia ,isaya alitabiri vema juu yenu ninyi wanafiki kama ilivyo andikwa,watu hawa huniheshimu kwa midomo ,ila mioyo iko mbali name:Nao waniabudu bure wakifundisha mafundisho yalio maagizo ya wanadamu.       
Ninyimwaiacha amri ya mungu na kuyasniks mapokeo ya wanadamu .Akawaambia vema mwaikataa amri ya mungu mpate kuyashika mapokeo yenu’’ MARKO 7:6-9
Ø  Biblia inatwambia sababu ya wengi kuvunja amri za mungu ni mapokeo ya wazee(VIONGOZI)wengi leo wanafundishwa mapokeo ya wanadamu na kuyatii kwa uaminifu kuliko amri za mungu ,hata kama mapokeo hayo hawayapatii ushindi wa maandiko hutetea kwa msimamo mkali wa kulinda itikadi za madhehebu kwa hiyo Miongozo,kanuni,katiba,desturi na heshima kwa viongozi wanadamu vimechukua nafasi kuliko maandiko matakatifu yaliyo neon laMungu.   
Ø  Ndugu msomaji mpaka haoa utakuwa umegundua umuhimu wa kuzijua na kuzitii amri kumi za mungu amua kuishi kulingana na matakwa ya mungu katika amri zake. Kwani kuna mbaraka mkubwa katika kuzishika amri maana Neno la MUNGU lasema,   
“Aishikaye amri hatajua neon baya na moyo wa mwenye hekima hujua wakati na hukumu MHUBIRI 8:5         
Ø  Tena watu wa mungu waaminifu watatambuliwa tu kwa kuzishika amri za mungu na si vinginevyo hivi ndivyo neon la Mungu linavyothibitisha kwa kusema    
   ’’Na waende kwa sheria na ushuda ikiwa hawasemi sawasawa na neon hili bila shaka kwa hao hapana asubuhi  ASAYA 8:20             
 ’’Hapa ndipo penye subira ya watakatifu hao wazishikao amri za Mungu na imani ya Yesu’’UFUNUO 14:12                      
                                      HITIMISHO  
Katika kuzishika amri za  Mungu ,mwanadamu anaweza kuishi kwanzo.Ndivyo nenola mungu linavyosema ,    
“Naye akanifundisha ,akaniambia ,moyo wako uyahifadhi maneno yangu shika amri zangu ukaishi”  MITHALI 4:4        
“ Nikawapa amri zangu na kuwaonyesha hukumu zangu ambazo mwanadamu ataishi kwazo. Kama akizitenda” EZEKIEL 20:11      
“Naye akaandika juu ya mbao mfano ya maandiko ya kwanza zile amri kumi alizo waambia bwana huko mlimani toka kati ya moto siku ya mkutano ; Bwana akanipa”KUMBUKUMBU LA  TORATI  10:4   
“Bali agano hili ndilo natakalo fanya na nyumba ya Israeli,baada ya siku zile,asema Bwana;nitatia sheria yangu ndani yao na katika mioyo yao nitaiandika;name nitakuwa Mungu wao,nao watakuwa watu wangu.”YEREMIA 31:33
“Mwanangu, shika maneno yangu na kuyahifadhi maagizo yangu ndani yako.Shika maagizo yangu nawe utaishi, linda mafundisho yangu kama mboni ya jicho lako. Yafunge katika vidole vyako,yaandike katika kibao cha moyo wako.”MITHALI 7:1-3

Mungu awabariki AMINA 
Kwa mawasiliano zaidi piga simu namba,0756959525
0756959525,0752164685
Share:

MFANO WA NGANO NA MAGUGU

MFANO WA NGANO NA MAGUGU
Mfano huu unapatikana katika Mathayo 13:24-30 na 36-43. Ni mashuhuri kwa watu wengiambao aidha 
wameusoma au wameusikia ukihubiriwa kwa kurudiwarudiwa. Unaweza ukawa wazikiasi kwamba tukafikiri tayari tunaufahamu na kuweza kuwa na tabia ya kusoma kwa haraka bila kujaribu kutafuta kweli zilizofichwa ambazo zimezikwa chini ya dunia.

Kwa kweli mfano huu unaweza kuwa ndiyo usioeleweka na unaotafsiriwa vibaya leo na hutumiwakuwachanganya watu wetu kanisani; tumetegemea wachungaji na viongozi wa makanisa, taasisi za kujitolea, na makundi mengine kuwa tayari kukubali mafundisho na mapokeo ya wazee, bila kujaribu kujitafutia ukweli sisi wenyewe chini ya uongozi wa Roho wa Mungu.Wengi wanaona bora kuamini hekima ya kibinadamu, kukubali hoja zinazoelekea kuwa na mantiki za marabi na mafarisayo wa kileo badala ya kuthibitisha na kuyapima mafundisho kwa kuhakikisha kuwa “hivi ndivyo asemavyo Bwana”, na “kwa sheria na ushuhuda”. Lakini Je, hii ni njia salama kufuata? Hapana! Yeremia 17:5 anasema “amelaaniwa mtu Yule amtegemeaye mwanadamu, amfanyaye mwanadamu kuwa kinga yake”.

“Kama Nathaniel angewategemea marabi wamuongoze, asingempata Yesu. Ilikuwa nikwakuona na kujiamulia mwenyewe kwamba alikuwa mwanafunzi. Hivyo kwa wale ambao leo chuki binafsi inawazuia kupata mema……….wakati wanatumainia mamlaka za kibinadamu, hakuna atakaye yafikia maarifa yaokoayo ya kweli. Kama Nathaniel, tunahitaji kijisomea neno la Mungu sisi wenyewe, na kuomba Roho mtakatifu atuongoze”. Desire of Ages pg 140-141

Kwahiyo hatuwezi kutegemea hekima ya wanadamu ituongoze katika njia salama, bali lazima kwa maombi na juhudi tuutafute ukweli sisi wenyewe. Tukipambanisha andiko kwa andiko, msitari kwa msitari, shuhuda kwa shuhuda, hapa kidogo na pale kidogo, ndipo machafuko yatakapo peperukia mbali, naye Mungu ataturuhusu tuone kweli zake dhahiri bila lundo la taka za desturi na mapokeo, ndipo tutaweza kuzifanyia kazi kweli zilizofunuliwa nasi tutajua kuwa msingi wetu umesimama imara. Katika kujaribu kuelewa mfano huu wa ngano na magugu haiwi vinginevyo. Mama White anaeleza mara baada ya kunukuu mfano huu: “Soma fundisho hili kwa umakini, ukifanya yote yaliyo ndani ya uwezo wako kuuelewa mfano huu. Roho mtakatifu ataziongoza akili za wale wanaotafuta ufahamu kamili wa mfano huu”.Review and Herald, vol 4, (4RH) uk 395, col 2.Basi kinyume cha ushuhuda huu pia ni kweli kwamba wale wasiosoma mfano huu kwa uangalifu na kujaribu kufanya vyovyote wanavyoweza kuelewa, hawatapokea maongozi kutoka kwa Roho wa Mungu. Watauelewa vibaya na kueneza machafuko na makosa kila mahali, hili ndilo jambo lililotokea na linaendelea kutokea. Hivyo hebu tusome mfano huu kwa uangalifu, tukichunguza na
kufafanua kila moja ya alama ambayo Kristo anaitumia ili tuone kama hatuwezi kuondoa sehemu ya machafuko yanayozidi kuongezeka leo.
“Akawatolea mfano mwingine, akisema, Ufalme wa mbinguni unafanana na mtu aliyepanda mbegu njema katika konde lake, lakini watu walipolala, akaja adui yake akapanda magugu katikati ya ngano, akaenda zake. Badae majani ya ngano yalipomea na kuzaa, yakaonekana na magugu. Watumwa wa mwenye nyumba wakaenda wakamwambia, Bwana, hukupanda mbegu njema katika konde lako? Limepata wapi basi magugu? Akawaambia adui ndiye aliyetenda hivi. Watumwa wakamwambia, Basi, wataka twende tuyakusanye? Akasema, La; msije mkakusanya maguu, na kuzing’oa ngano pamoja nayo. Viacheni vyote vikue hata wakati wa mavuno; na wakati wa mavuno nitawaambia wavunao, yakusanyeni kwanza magugu, myafunge matita matita
mkayachome; bali ngano ikusanyeni ghalani mwangu”. Mathayo 13:24-30,

Ni nini kinachowakilisha “ufalme wa mbinguni au wa Mungu”? Je, Kristo hapa anaongelea mahala anapoishi Mungu huko juu kwenye mbingu halisi ama anajaribu kulielezea hili katika mazingira ya kiroho au kwa maneno mengine, mahali anapoishi Mungu, kupitia neno lake lililoandikwa mioyoni na akilini mwetu? Je, Kristo anazungumza hapa kwa maana halisi au kwa maana ya kiroho? “Na alipoulizwa na mafarisayo, Ufalme wa Mungu utakuja lini? Aliwajibu akawaambia, Ufalme wa Mungu hauji kwa kuuchunguza; wala hawatasema, Tazama, upo huku, au kule, kwa maana, tazama, ufalme wa Mungu umo ndani yenu.” Luka 17:20-21 Hivyo Kristo anaongelea maana ya kiroho ya ufalme wa Mungu, uliomo ndani ya akili zetu kupitia kwenye neno lake! Oh, huoni umuhimu wa sisi kujifunza sisi wenyewe, tukichimba Biblia na shuhuda, tukila na kunywa maneno ya Mungu sisi wenyewe, tutawezaje basi kuthibitisha
tumaini lililomo ndani yetu, kama halimo? Tutawezaje basi kumuakisi Kristo, kung’aa kama nyota zinazong’aa sana katikati ya giza nene la dunia hii ya uovu, na kumpa heshima istahiliyo jina lake takatifu? Ili tuyaweze hayo yote, Ufalme wa Mungu lazima uwemo ndani yetu.

Tafadhali usisahau wazo hili kwa sababu ni wazo moja la muhimu kukumbuka unapojaribu kuelewa mfano wowote wa Kristo unaohusiana na ufalme wa mbinguni.Nani katika mfano huu, mtu anayepanda mbegu njema au ngano? Ni Kristo (mathayo.13:37).Kwa hiyo ni nani anakuwa adui wa Yesu aliyepanda mbegu au magugu katika shamba la Yesu?Ni Shetani (Mathayo13:39). Kristo alipanda mbegu za ngano shambani mwake ikionyesha kwamba Kristo alikuwa amelinunua shamba lake kwa gharama.Sasa ni nani wanawakilisha shamba? Ni sisi! Linawakilisha roho zetu au akili zetu:“Adui anayepanda mbegu mbaya, ni mfano wa kazi ya shetani kwenye akili za wanadamu.Kristo ndiye mpanzi anayepanda mbegu ya thamani katika ardhi yenye rutuba ya moyo.”SPIRIT OF PROPHECY, VOL 2 (2sop), uk 248
Lakini inamaanisha kitu Fulani tena. Kristo anasema katika (Mathayo 13:38) kwamba shamba linamaanisha ulimwengu. Neno la kigiriki linalomaanisha “ulimwengu” lililotumika hapa ni“kosmos” likimaanisha mpangilio unofaa wa vitu duniani.
Naye Ellen White analibainisha hili: “Shamba, Kristo alilosema, ni ulimwengu. Lakini lazima tuelewe hili kwamba linamaanisha kanisa la Kristo duniani”.
CHRIST OBJECT LESSONS (COL), UK 70

Kwa hiyo shamba linamaanisha kanisa, lakini pia lina maana ya kina ya kiroho na
Inayomaanisha mioyo au akili zetu.Nani anawakilisha mbegu njema au ngano iliyopandwa katika shamba lake? Ingemaanisha vitu viwili. Kristo anasema katika Mathayo 13:38 kwamba lile konde ni ulimwengu; zile mbegu
njema ni wana wa ufalme au wanafunzi wa kweli kwenye kanisa la Mungu. Inawakilisha pia mafundisho safi ya Mungu au kweli zilizopandwa ndani ya mioyo yetu. Au neno la Mungu ndani ya mioyoNa huo mfano, maana yake ni hii; mbegu ni neno la Mungu” Luka 8:11 Mbegu hii (au neno la Mungu) inapandwa kwenye shamba (au mioyoni na akilini mwetu); ikimaanisha mafundisho ya neno la Mungu kwa upande wa ngano na mafundisho ya Shetani kwa upande wa magugu.Nani anawakilisha mbegu mbaya au magugu? Magugu ni wana wa mwovu au wafuasi wa kweliwa shetani. Inawakilisha pia mafundisho machafu ya shetani au makosa yaliyopandwa ndani ya mioyo yetu.

1. Sasa tuzirudie aya tena na kuweka maana sehemu ya alama, halafu tutumie maana ya kina ya kiroho.Ufalme wa mbinguni (au wokovu unaopatikana kwa kuishi ndani ya neno la Mungu linaloandikwa mioyoni na akilini mwetu), unafananishwa (au ni sawa) na Mtu (au Kristo Yesu) aliyepanda mbegu njema (au aliyetawanya kweli safi za Mungu) Katika shamba lake (au katika akili na mioyo ya watoto wa Baba yake ambao Mungu aliowanunua kwa gharama kuu za mwana wake mpendwa.). Lakini watu walipolala (au watu w N a Mungu walipoacha milango ya mioyoni na akilini bila ulinzi; [maana Biblia inasema: ‘Linda sana moyo wako kuliko yote uyalindayo’ Mith 4:23]) adui yake alikuja akapanda magugu katikati ya ngano akaenda zake
(au shetani aliingia akapanda makosa na mafundisho ya uongo katikati ya kweli safi za Mungu, kwa kuvichanganya pamoja, akaondoka zake bila kugundulika.)
2. Hebu sasa tuzichunguze aya zilezile na kutumia maana nyingine ya sisi wenyewe badala ya alama za kiroho.
Ufalme wa mbinguni (au maana ileile iliyotumika hapo kwanza au mchakato wa kuupatawokovu); unafananishwa na (au ni sawa na) mtu (au Kristo) aliyepanda mbegu njema katika shamba lake( au aliyewaweka Masalio wake katika kanisa duniani) Watu walipolala (au viongozi au waangalizi wa Masalio wa Mungu wakipoteza wivu na kuacha mlango wa kuingilia kanisani bila ulinzi) adui yake alikuja akapanda magugu katikati ya ngano akaenda zake (au shetani aliingia akawaweka watu wake na mawakala katikati ya kanisa akiwachanganya na Masalio naye akaondoka bila kugundulika.).

Je, inawezekana kuwa na neno moja lenye maana mbili kwenye Biblia? Ndiyo,
“….vile vichwa saba ni milima saba anayokalia mwanamke huyo. Navyo ni wafalme saba…”Ufun. 17:9,10
Hapo tunaona vichwa vikibeba maana mbili kwa wakati mmoja, yaani milima na wafalme.Hivyo basi katika mfano wa Yesu hapo juu tunaona neno moja likimaanisha maana mbili kama tulivyoonyesha hapo juu shamba likimaanisha kanisa la Mungu duniani au mioyo na akili za wanafunzi wa kweli wa Yesu. Na pia tumeona kuwa ngano inamaanisha watu wa Mungu duniani au mafundisho safi ya Yesu, yaani neno la Mungu. Lakini pia tumeona magugu kuwakilisha wafuasi wa Shetani au mafundisho ya Shetani ndani ya kanisa. Sasa ni nani wanawakilisha shamba au kanisa? Ni Kanisa la SDA. Kwa vile Kristo alianza kwa shamba safi na mbegu safi, kwa hiyo alianzisha kanisa hili kwa usafi na watu waliochaguliwa walikuwa ni watu wa Masalio na kanisa. Lakini ni nini kilichotokea katika mfano? Watu, au
waangalizi wa shamba walilala na kumruhusu adui kuingia, kujaribu na kuharibu shamba lote kwakueneza na kuchanganya magugu na ngano.
Je, hili limetokea katika kanisa la SDA? Je, kanisa na viongozi wake walilala? Wakipoteza wivu wa kumfanyia kazi mwenye kanisa? Ndiyo!
“Kama Kusudi la Mungu lingetekelezwa na watu wake kwa kuipatia dunia ujumbe wa rehema, Kristo angekuwa amerudi duniani, nao watakatifu wangekuwa wamekaribishwa katika jiji la Mungu.” Testimonies, vol 6 (6T), uk 450
“Kama kila askari wa Yesu angekuwa ametimiza wajibu, kama kila mlinzi kwenye kuta za sayuni angeipiga mbiu yake kikamilifu, dunia ingekuwa imesikia ujumbe na onyo mapema. Lakini kazi imechelewa kwa miaka mingi. Shetani ametuvizia wakati WATU WAMELALA, akaifanya kazi yake.” 9T 29
Hivyo uongozi wa kanisa na walinzi wake walipoteza wivu, wakasinzia. Lakini je, walimruhusu shetani kuingia kanisani akawatawanya wafuasi na mawakala wake au magugu katika ngazi zote ili kujaribu kuiharibu ngano? Ndiyo!
Watu wanoshikilia nafasi kubwa kwenye kitovu cha kazi WAMELALA. Wamepoozwa na Shetani ili kwamba mipango na hila zake zisigunduliwe, wakati anafanya kazi ya kunasa, kudanganya, na kuangamiza”.

“Baadhi ya wale wanaoshikilia nafasi za walinzi ili kuwaonya watu juu ya hatari, wameacha kazi yao na kubweteka. Si walinzi waaminifu.Wanatulia wakati adui yao mwerevu anaingia katika ngome na kufanya kazi kwa ukamilifu kando yao na kuvunja kile ambacho Mungu ameamuru kijengwe.Wanaona kwamba shetani anawadanganya wale wasio na uzoefu na wasio
makini; bado wanakaa kimya, kana kwamba hawana jukumu maalumu, kana kwamba mambo haya hayakuwahusu. Hawaoni hatari yoyote, hawaoni sababu ya kutangaza hatari. Na shetani anashangilia kufanikiwa kwake kuzitawala akili za watu wengi wanaodai kuwa ni wakristo. Amewadanganya, amezitia ganzi fahamu zao, akapanda bendera ya kuzimu (mafundisho ya uongo) katikati yao, nao wamedanganyika kiasi kwamba hawajui kuwa ni yeye….” “Washiriki wake wamevunja agano lao la kuishi kwa ajili ya Mungu, naamu yeye tu…naye Kristo ameondoka. Roho wake amenyamazishwa ndani ya kanisa. Shetani hufanya kazi bega kwa bega na wakristo kwa jina; lakini wanakosa utambuzi wa kiroho kiasi kwamba hawamgundui. Kweli kuu wanazodai kuziamini haziwasaidii…Nilishangaa nilipotazama giza la kutisha la washiriki wengi wa makanisa yetu. Kukosekana kwa uchaji wa kweli kulikuwa ni kwa
kiwango kikubwa kiasi kwamba waligeuka chanzo cha uovu na mauti, bila ya kuwa nuru kwa  ulimwengu. Wengi walidai kumpenda Mungu, lakini kwa matendo walimkana…Uchafu wao utawatisha katika siku ile ambayo inatujia upesi sana”. 2T 439-446 Kwa kusema kitovu cha kazi ingemaanisha nini kama si General Conference? Hakika uongozi na walinzi wa kanisa la SDA wamelala wakamruhusu shetani aingie kanisani. Shetani kwa ustadi amepanda bendera yake ya kuzimu akapanda magugu maovu katikati ya ngano na sasa mbegu ya thamani na mbaya zimechanganyika pamoja ndani ya kanisa. Sasa gugu ni nini? Kwa kweli gugu ni mbegu chungu inayosababisha kichefuchefu na kutapika. Pia ni mbegu yenye sumu kali yenye kulewesha inayosababisha usingizi na ikiwa nyingi imetumiwa, husababisha kifo. Kwa hiyo kwa maneno mengine inasababisha usingizi wa kifo. Ni hali gani ambayo punde nimeifafanua? Hali ya Laudikia hali ya usingizi ya Laudikia.na ikibaki kama ilivyo kwa muda mrefu zaidi itasababisha usingizi wa kifo. Sasa je, hali ya walaudikia
inawakilisha magugu? “Tunao ushahidi tele kwamba magugu yanaota pamoja na ngano katika kanisa la Mungu. Kuna wakristo waaminifu katika kanisa la Mungu na kuna wakristo wa uvuguvugu pia.Waadventista wa uvuguvugu.” Ellen G white Upward look, p. 35 Je, hawa walaudikia wanamsababishia nani kichefuchefu na kutapika? KRISTO.. “Basi kwa sababu una uvuguvugu, wala hu baridi wala moto, nitakutapika utoke katika kinywa changu.” Ufunuo3:16
Kwa hiyo Kanisa la laodikia la SDA ndilo linalomsababisha Kristo kulitapika kwa sababu ya uvuguvugu wake na bado wanafikiria wanamtumikia Kristo kwa hali hiyo na wanaamini wataokolewa. Ina maana gani kwa Kristo kuwatapika watoke kinywani mwake? “Kitendo cha kutapikwa na Kristo ina maana kwamba Hawezi kuwakilisha maombi yao na maelezo yake kwa Mungu. Hawezi kukubaliana na mafundisho yenu ya neno Lake au kazi yenu ya kiroho kwa namna yoyote. Hawezi kuwakilisha mazoea yenu ya kidini na maombi ambayo angewapa neema” 6T 408.
Je, Ni lini ambapo kwa ishara Kristo anawatapika kutoka katika kinywa chake walaodikia? Je Ni wakati wanapodidimia kikamilifu katika hali hii ya uvuguvugu? Au ni wakati wa badae wa kukaribia kufungwa kwa mlango wa rehema?
“Kwa wale ambao hawaweki kivitendo neno la Mungu, ni barua iliyokufa. Kristo anasema kwa hao; ‘Heri ungekuwa baridi au moto. Kwa hiyo, kwa kuwa u vuguvugu, hu baridi wala moto,nitakutapika utoke kinywani mwangu’. Hawezi kupeleka mahitaji yao kwa Baba. Kama watatambua kuwa ni wadhambi, angeweza kuwaombea, na Bwana angewanyanyua kwa Roho mtakatifu wake. Lakini ni wabaya kuliko wafu kwa makosa na dhambi. Wanasikia neno, lakini hawalifanyii kazi; badala yake wanalifanyia kazi neno kwa majirani zao.” 7BC 96 col 2& 964 col 1.
“Shahidi mwaminifu asema kuhusu ubaridi, maisha hafifu, kanisa lisilo na Kristo, ‘nayajua matendo yako, kwamba hu baridi wala hu moto… Kwa hiyo kwa kuwa u vuguvugu, hu baridi wala hu moto, nitawatapika watoke kinywani mwangu,’ (Ufun.3:15-16). Kwa kuwa wasema, mimi ni tajiri, na mwenye kila kitu, na sihitaji chochote….Kristo hawezi kuchukua majina ya wale ambao wameridhika kwa namna walivyojitosheleza. Hawezi kuwaombea watu wasiohisi hitaji la msaada wake, wanaodai kujiona kuwa na kila kitu.” 1SM p. 357- 358
Je, neno importune lina maana gani? Lina maana ya kujibu maombi na matakwa. Hivyo mara kanisa au mtu anapoangukia kabisa katika hali ya uvuguvugu ya kujitosheleza, ya ulaudikia,Kristo hawezi kujibu sala au maombi ya baraka .Hawezi kupeleka maombi yao kwa Baba, ambayo humaanisha kwamba wameshatapikwa! kabla hawajapata nafasi ya kuokolewa, lazima watubu na kutoka kwenye hali hii. Mama White alisema kwamba kanisa la SDA lilikuwa katika hali hii ya kuhuzunisha.
Lakini je, Mungu aliliacha kanisa katika hali hii ya kutapikwa lipotee? Hapana! Mungu
alituma jumbe za kweli za kujaribu ambazo zingewaamsha watu wake na kanisa, akiwasababisha kudhihirisha Roho wa kweli katika mioyo yao ama kwa maneno mengine kuzaa matunda. Kweli hizi za kujaribu zingeonyesha nani alikuwa ngano na nani alikuwa gugu ama kwa kukubali na kuzifanyia kazi AU kwa kukataa kuzipokea na kuzikana kweli hizi au kuzipinga hivyo kutapikwa! Unaweza kuniambia kwamba jumbe hizi za moja kwa moja na zakujaribu ambazo ndizo zimebeba
majaliwa ya watu wa Mungu ni nini? Ni ujumbe kwa Laudikia au kweli za karipio kali. Ellen White anasema katika Early writings EW p. 270, Kwamba kwa kweli hatua ya kanisa inategemea ushuhuda wa moja kwa moja wa shahidi mwaminifu (Kristo) kwa walaudikia. “…Huu utaubadilisha moyo wa mpokeaji, nao utamfanya ainue bendera na kumwaga ukweli usiopinda...Ushuhuda huu lazima umbadilishe kwa ungamo la dhati; kwa kweli wote watakaoupokea watautii na kutakaswa. Baadhi hawatauvumilia ushuhuda huu usiopinda, wataupinga, na hili ndilo litakalosababisha pepeto miongoni mwa watu wa Mungu.” EW 270; Kwa hiyo wanaoukubali na kuutii ukweli huu usiopinda wenye kujaribu watazaa tunda au kujidhihirisha wazi kwamba ni ngano halisi, na wale wanaoukataa na kuupinga watazaa tunda au kujidhihirisha kuwa magugu halisi.
Je, ni lini ushuhuda huu usiopinda kwa laodikia na washiriki wake ulianza?
“Watu wa Mungu lazima wayaone makosa yao na kuamka kufanya toba ya dhati, na kuachana na dhambi zile ambazo zimewaweka kwenye hali ile yakusikitisha ya umasikini, upofu, unyonge, na udanganyifu wa kutisha. Nilionyeshwa kwamba ushuhuda mkali lazima udumu kanisani. Hili peke yake litajibu ushuhuda unaofaa kwa walaodikia. Makosa lazima yakemewe, dhambi lazima iitwe dhambi, na uovu lazima ushughulikiwe mara moja na kwa dhati na kuondolewa mbali na sisi kama watu.”
“Wale wenye roho ya upinzani kwa kazi ambayo kwa miaka ishirini na sita sisi (yeye na mume wake ) tumesukumwa na Roho wa Mungu kuifanya, ambao wangeuvunja ushuhuda wetu, niliona hawapigani na sisi, bali na Mungu…” 3T 260
Hivyo kwa miaka 26 yeye na James walikuwa wakitoa ushuhuda usiopinda wenye karipio kali kwa kanisa na washiriki wake. Ushuhuda huu uliandikwa lini basi? Mwaka 1873.Hivyo 1873 ukitoa miaka 26 unaweza kupata mwaka 1846-47 ambapo ujumbe wa kweli kwa Walaodikia ulipoanza kuhubiriwa kwa watu wake. Hakika walinzi wa kanisa waliwahi kulala, wakiruhusu magugu ya shetani yaingie, yote haya yalitokea miaka miwili tu baada ya1844.

JE, PEPETO LILIANZA LINI BASI?
“ Pepeto kali limeanza na litaendelea, na wote watapeperushiwa nje wasiotaka kuchukua msimamo wa ujasiri na usio tetereka kwa ajili ya kweli, na kujitoa mhanga kwaajili ya Mungu nakazi yake.” EW 50
Nini maana ya ‘msimamo wa ujasiri usio tetereka’? ni wazi kwamba huo si kitu kingine bali ujasiri wa kufanya maamuzi magumu ya kujitenga na mfumo unaopendelea magugu au mafundisho ya Uongo.

HII ILIANDIKWA LINI? January 26,1850. Kwa hiyo pepeto tayari limeanza kabla ya mwaka 1850, na pepeto hili lilikuwa linasababishwa na ushuhuda usiopinda wa ukweli wa kuwajaribu uliokuwa unamwagwa kwa watu wa Mungu na watu wake. Kwa hiyo watu walikuwa tayari wakijidhihirisha kuwa magugu na ngano halisi kufikia mwaka 1850, ama kwa kupokea onyo kali wakijitakasa na kutangaza ujumbe huo huo au kwa kuukataa na kuupinga ujumbe na wale walio uhubiri.
Basi ni muhimu kukumbuka kwamba Kristo alianza kanisa lake la Masalio kwa usafi, lakini kwa vile uongozi uliruhusu magugu kuingia kanisani na kwenye mfumo, na kuzaa matunda ya uovu, kanisa na mfumo wote, unakoma kuitwa kanisa la “Masalio” kwa sababu ya magugu yaliyo ndani yake. Sasa nini kinafuata? Mungu anawaita watu wake waaminifu na kuwafanya kuwa ‘masalio’ wake. Watu wanaoendelea kuzaa matunda ya haki na kutimiza maelezo na masharti ya ufunuo12:17 wangali wanachukuliwa kama Masalio (Watu watiifu ndio wanaitwa Masalio na si mfumo unaoitwa Masalio). Ni kwa vile tu kanisa la Masalio haliwezi kutumiwa kutaja kanisa lote na
mfumo, kama ilivyokuwa mwanzoni, kwa sababu uongozi ulilala na kuruhusu mawakala wa shetani kuingia kanisani.

Ndiyo maana katika Mathayo 13:26-28, watumishi waaminifu wanahamu ya kujaribu kuliepusha kanisa na magugu haya, au mawakala na watoto wa shetani, ili waweze kulirudisha kanisa na mfumo wake katika usafi wake halisi.
Lakini Kristo anasema katika Mathayo 13:29-30 kwamba hawapaswi kulifanya hili, wasijaribu kuyatenga magugu na ngano, kwa sababu anayo njia bora zaidi; “Acha vyote vikue pamoja mpaka wakati wa mavuno, na katika wakati wa mavuno nitawaambia wavunaji, yakusanyeni kwanza magugu myafunge matita matita mkayachome, bali leteni ngano safi ghalani.” Katika Mathayo 3:12 anaongeza zaidi na kusema “ambaye pepeto lake li mkononi mwake, naye atausafisha sana uwanda wake; na kuikusanya ngano yake ghalani, bali makapi atayateketeza kwa moto usiozimika”.

Tunazo alama nyingine chache tunazohitaji kuzifafanua na tutaanza na MAVUNO. Naamini hii nimoja ya alama zinazofafanuliwa vibaya katika mfano huu wote, nao wanaoutafsiri vibaya namna kwamba hawataweza kuona na kutambua kile ambacho Bwana anawataka wakifanye. Kabla yayote hebu tupitie mchakato mzima wa uvunaji na hatua mbalimbali zinazohusika, ndipo tutaona ni lini kipindi cha mavuno kitaanza.
Mara matunda yanapozaliwa na kukomaa, uvunaji unaweza kuanza, tena kuna hatua mbili za mavuno.

HATUA YA KWANZA YA MAVUNO INAHUSISHA MAMBO HAYA.
-Wavunaji wanaajiriwa kuvuna ama kukata vichala vya ngano au vichala vya magugu ambavyo vimezaa matunda.
-Wavunaji wanaanza kutenganisha vichala vya ngano na vichala vya magugu
-Vichala vya ngano vinakusanywa katika matita matita na kufungwa pamoja kwa kamba.
-Hayo yanafanyika hata kwa vichala vya magugu.

HATUA YA PILI YA MAVUNO INAHUSISHA MAMBO YAFUATAYO.
-Wavunaji wanaovuna shambani au kukusanya matita ya ngano zilizofungwa huiondoa Shambani kupeleka mahali pa kupepetea, ambayo kwa kawaida ilikuwa juu ya shamba.
-Matita matita ya magugu yaliyofungwa hurundikwa katika rundo kubwa yachomwe.
-Uputaji wa ngano zilizovunwa shambani unafanyika ili kutenga ngano na makapi.
-Upepetaji unafanyika pale makapi yanapokuwa yametengwa na mbegu za ngano.
-Mbegu za thamani za ngano zinaondolewa toka kwenye uwanja wa kupepetea na
kuwekwa ghalani ambapo zinalindwa dhidi ya dhoruba.

Hivyo tunaona kwamba hatua mbili za mavuno zinafanyika katika maeneo mawili tofauti naya pekee!
1. -Hatua ya kwanza ni shambani
2. -Hatua ya pili ni nje ya shamba
Pia tuliona kwamba mwanzo wa kila moja ya hatua hizi mbili huitwa “mavuno”. Mwanzo wa hatua ya kwanza, au wa ukataji wa nafaka ngano isiyozaa matunda unaitwa “mavuno” na ya pili inapoanza, au yakukusanya ngano iliyofungwa, kuiondoa shambani inaitwa pia “mavuno”.Tazama katika dictionary yako kama huamini.
Websters inaliorodhesha neno mavuno kama lenye sehemu au mfuatano wa sehemu mbili. Harvest:
1. The time when farmers gather in the corn, fruit, or vegetables they have grown.
2 The crop that is gathered in Mavuno:

1. Wakati wakulima wanapokusanya nafaka, matunda au mboga walizolima.
2. mazao yaliyokwisha kusanywa toka shambani na kuwekwa ghalani.
Matukio haya mawili tofauti kila moja linaitwa mavuno nayo lazima yote yafanyike ili mwenye shamba aweze kupata nafaka bora za ngano na kuzitunza katika ghala lake.
Sasa ingekuwaje kama mavuno ya kwanza yangefanyika na hatua zake, na ngano iliyofungwa isingeondolewa shambani; Je, ungekuwepo uwezekano wa matita haya ya ngano kutoka shambani? Hapana! Zingepotea kwa sababu zingebaki shambani, nao msimu wa mavuno ungepita na kukoma. Ndipo dhoruba na pepo zingevuma ghafla nazo zingeoza na kuharibiwa na mvua nyingi. Au zingeharibiwa na moto uleule unaochoma magugu. Aidha matita hayo ya ngano yangepotea kwa sababu yalibaki shambani kwa muda mrefu sana bila kuvunwa.

Hatua ya pili ya mavuno, ya kuondoa ngano shambani, ni ya lazima sana ili kwamba michakato ya kuputa na kupepeta ianze kutenga makapi na mbegu safi za ngano. Katika hatua hii ngano yote huzungukwa na maganda yaitwayo makapi, nayo hujulikana kama machipukizi ya ngano. Sasa tazama ngano hii iliyodumaa, kila moja ina uwezekano wa kuwa na mbegu za ngano ndani.
Lakini usingeweza kujua kama zote zilikuwa na ngano ndani, au kama baadhi zilikuwa tu zinaonesha lakini hazikuwa nazo, kwa sababu zote zilikuwa zinafanana kwa nje. Mdudu anaweza kuwa aliingia ndani ya baadhi yake na kuharibu mbegu au labda mbegu haikuweza kuumbika hata kidogo. Hivyo hizi zingekuwa makapi ambayo mwenye shamba hazihitaji hata kidogo.Machipukizi yote yanayokuja kwenye viwanja vya kupepetea yanauwezekano wa kuwa na mbegubora ya ngano ndani na kuokolewa. Lakini haitafahamika ni kiasi gani cha mavuno kingepatikana mpaka makapi yasiyofaa yanapotengwa yasiwe pamoja na ngano ndipo ngano inatolewa kwenye
viwanja vya kupepetea na kuwekwa ghalani ambapo inalindwa dhidi ya dhoruba na upepovinavyotarajiwa punde. Lakini ngano hiyo iliyofungwa matita isipoondolewa shambani, ngano hiyo haina nafasi ya kuokolewa katika ghala la mwenye shamba.

Tumeona tayari mchakato wa mavuno hatua zote za ndani na nje ya shamba, na sasa tutautazama muda wa mavuno. Uvunaji unafanyika lini na ngano kutengwa na magugu? Watu wengi leo wanaamini tena wamefundishwa kwamba mavuno yanavunwa Kristo anaporudi mara ya pili katika mawingu ya mbinguni, ndipo wakati huu kutenganishwa ngano na magugu kutafanyika. Hivyo wanajenga hoja kwamba hakuna wanaopaswa kujitenga mpaka Kristo aje. Je, hii ni kweli? Hapana!
Hebu tuangalie Kristo anachosema kuhusu muda wa mavuno tuone kama tunaweza kuondoa kiasi fulani cha machafuko na ujinga wa uelewa katika mfano wa mpanzi ambao ni muhimu kuufahamu kama ilivyokusudiwa na Yesu Mwenyewe.
Kristo anasema katika Mathayo 13:39 kwamba “yule adui aliyepanda magugu ni Ibilisi; mavuno ni mwisho wa dunia; na wale wavunao ni malaika”.Neno la kiyunani linalo maanisha dunia lililotumika hapa ni “Aion” linalomaanisha “zama”. Lakini hasa linamaanisha “kipindi cha masihi kiwe cha wakati huu au ujao”.

Hivyo tunaona kwamba mwisho wa dunia unamaanisha mambo mawili.
1. katika wakati uliopo inamaanisha kukoma au kufungwa kipindi cha Masihi
2. katika wakati ujao inamaanisha kikomo kamili cha wakati unaomuhusisha Masihi.
Neno “Masihi” linamaanisha mwokozi na mfunguaji wa watu wake kutoka kwenye utumwa na kifungo. Je, ni nani Masihi na Mwokozi hasa? Kristo Yesu. Hivyo tukiweka maana zote hizi pamoja tunaona kwamba uvunaji wenyewe unafanyika katika kikomo au kufungwa kwa kipindi cha wakati ambacho Kristo anawahudumia watu wake. Pia tunaona kwamba mavuno kamili yanafanyika baada ya kipindi cha wakati ambapo Kristo amemaliza kabisa kuwahudumia watu wake milele. Mavuno katika vipindi vyote yanahusisha Kristo kuwaokoa na kuwafungua toka kwenye utumwa na kifungo.
Je, tunaishi katika kipindi gani cha wakati sasa? Tunaishi katika siku zilizotabiriwa za upatanisho.

Katika huduma ya patakatifu, siku ya upatanisho ilikuwa huduma ya mwisho iliyoendeshwa na kuhani mkuu kwa ajili ya watu wake. Hivyo leo tunaishi katika kipindi cha huduma ya Yesu kwa watu wake au wakati wa Mavuno.
Je, kipindi hiki kilianza lini? 1844. Hivyo tangu 1844 tumekuwa katika wakati na mchakato wa mavuno. Hatua ya kwanza ya mchakato wa mavuno ni kukata au kuvuna nafaka yenye matunda, kutenga ngano na magugu, kuzikusanya katika matita na kuzifunga kwa kamba. Je, Ellen White analiunga mkono hili? Ndiyo!
“Kisha nikaona malaika. Alisema malaika anayeniongoza, ‘Kazi yake ni ya kutisha. Utume wake ni wa ajabu. Ni malaika atakaye tenga ngano na magugu, na kutia muhuri, au kufunga ngano kwa ajili ya ghala ya mbinguni. Mambo haya yanapaswa kutawala akili yote, fikra zote.” EW p. 118

Hapa tunaona kuwa Malaika ndiye anayetenga ngano na magugu, na kama tulivyoona hapo awali,hatutarajii kuwa kitendo hiki ni cha kimwili, bali ni cha kiroho maana tuliona kuwa “….mbegu ni neno la Mungu” Luka 8:11 na kwa hiyo mbegu chafu ni neno au mafundisho ya shetani. Vyote vinapandwa katika shamba la Mungu, au katika Kanisa la Mungu. Lakini pia tumeona kuwa mwenye shamba au Kristo anaporudi mara ya pili haji kuvuna bali anakuja kuchukua ngano safi iliyovunwa tayari na malaika na kuipeleka Mbinguni. Na kwa hiyo wale wanaoelewa kuwa mwisho wa dunia aliosema Yesu kwamba mavuno yatafanyika inamaanisha siku atakayokuja Yesu mara ya pili wanaelewa kimakosa fundisho hili kwa sababu mwisho wa dunia yanapofanyika
mavuno ni tofauti na siku ya Bwana anayokuja Yesu kuchukua mavuno yaliyokwisha kuvunwa tayari ili ayapeleke ghalani – yaani mbinguni.

Ni lini malaika wa tatu alianza kufanya kazi hii kwa kutoa jumbe hizi zenye kweli za kujaribu? Mwaka 1844. Hivyo tangu mwaka 1844 tumekuwa katika muda wa mchakato wa mavuno. Tangu octoba 22,1844 hadi mnamo 1846-47 Kweli hizi zenye kujaribu zilitolewa kwa watu wetu. Mwaka 1844 unatokana na unabii wa Daniel 8:14 kuhusu siku 2300 za kiunabii sawa na miaka 2300 halisi iliyoanza mwaka 456 KK na kuishia mwaka 1844 BK. Alama au neno lingine ni MWISHO WA DUNIA.
Watu wengi wameelewa visivyo maana ya ‘mwisho wa dunia’ wakidhani kuwa ni siku Yesu anaporudi mara ya pili.
“ …mavuno ni mwisho wa dunia; na wale wavunao ni malaika” Math. 13:39
“Basi kama vile magugu yakusanywavyo na kuchomwa motoni; ndivyo itakavyokuwa katika mwisho wa dunia...” “Ndivyo itakavyokuwa katika mwisho wa dunia; malaika watatokea, watawatenga waovu mbali na wenye haki na kuwatupa katika tanuru ya moto; ndiko kutakuwepo kilio na kusaga meno” Math 13:40, 49,50
Je, mwisho wa dunia uliosemwa hapa unamaanisha kurudi kwa Yesu mara ya pili? Hapana! Wengi wamekuwa wakifikiri kuwa Yesu alimaanisha mwisho wa dunia kuwa ni siku ile atakaporudi, ndio maanaYesu akifahamu kuwa watu watatafsiri tofauti mfano huu kama hawatasoma kwa uangalifu na kwa uongozi wa Roho wake, alisisitiza mara baada ya kufafanua mfano huu, akisema: “…mwenye masikio na asikie” Math. 13:43. Kama tulivyoona hapo juu kuwa mavuno yanafanyika kwa hatua kadhaa kabla ya kupelekwa ghalani na si mara moja kama itakavyokuwa ile siku ya Bwana atakapokuja Yesu mara ya pili ambayo ni siku moja. Mwisho wa dunia unapotajwa kwenye Biblia una maana ya tangu siku za mwisho wa dunia zianze, yaani
tangu mwaka 1844 hadi waovu watakapoangamizwa pamoja na shetani na kuwa mwisho wa dhambi. Kwa hiyo, hivi sasa tunaishi katika mwisho wa dunia au siku za mwisho wa dunia.

Tunasema hivyo kwa sababu tunatambua kuwa waovu au magugu hayatachomwa siku Yesu atakaporudi duniani mara ya pili. Siku Yesu atakaporudi anakuja kuchukua watu wake au ngano safi na waovu watakufa na kukaa makaburini hata baada ya miaka elfu moja wakati watakatifu na mji mtakatifu watakaposhuka, ndipo waovu watafufuliwa na kuchomwa moto pamoja na shetani.Je, ungeulizwa uelezee kuhusu siku ya Sabato ungesemaje? Ungesema “Sabato inaanza tangu kuzama kwa jua siku ya sita hadi kuzama kwa jua siku ya saba”; kadhalika ndivyo mwisho wa dunia unavyoanza mwaka 1844 hadi shetani, malaika zake na waovu (magugu) watakapotupwa katika tanuru iwakayo moto.

Je, Biblia inaiitaje siku ya kuja Yesu mara ya pili? Siku Yesu anapokuja imetambulika katika Maandiko kama Siku ya Bwana. na si mwisho wa dunia, [japo pia siku ya Bwana ni siku ya Sabato: “Nalikuwa katika Roho, siku ya Bwana…” Ufun.1:10; kumbuka kuwa neno moja kwenye Biblia laweza kuwa na maana mbili]; “Jua litageuzwa kuwa giza, na mwezi kuwa damu,kabla haijaja hiyo siku ya Bwana iliyo kuu na itishayo.” Yoeli 2:31. Hii ndiyo siku ya kuja kwa Yesu mara ya pili anayoisema Yoeli ambayo ni tofauti na siku za mwisho wa dunia.
“Walakini habari ya siku ile na saa ile hakuna aijuaye, hata malaika walio mbinguni, ila Baba”.Marko 13:32. Yesu akiwa hapa duniani anaitaja siku ya kuja kwake mara ya pili kama “Siku” na wala hasemi “walakini habari ya ‘mwisho wa dunia’…” maana siku za mwisho wa dunia zimefunuliwa kwetu ila siku ya kuja Yesu ndio hatuijui.
Huoni faida ya kusoma mwenyewe kwa uongozi wa Roho wa Mungu badala ya kutegemea wanadamu wakufundishe? Umeona namna ambayo Yesu alimaanisha katika mfano huu?

JE, MWISHO WA MAVUNO NI LINI KAMA YALIANZA TANGU MWAKA 1844?
“Ngano na magugu vinakuwa pamoja hadi wakati wa mavuno; na mwisho wa mavuno ni kufungwa kipindi cha rehema” (au mwisho wa mavuno ni kufungwa kwa mlango wa rehema) Christ Object Lesson p. 72
Yohana yeye anaelezea mwisho wa mavuno kwa kusema, “Mwenye kudhulumu na azidi kudhulumu; na mwenye uchafu na azidi kuwa mchafu; na mwenye haki na azidi kufanya haki; na mtakatifu na azidi kutakaswa”. Ufun. 22:11. likimaanisha kuwa malaika wameshamaliza kazi ya kuvuna na mavuno yako tayri. Tangazo hilo litatolewa mara Kristo atakapomaliza kazi ya upatanisho kule mbinguni. Mara baada ya maelezo hayo, tangazo la kuja kwa Yesu linafuatia,
“Tazama, naja upesi, na ujira wangu u pamoja nami, kumlipa kila mtu kama kazi ilivyo”.
Ufun 22:12. hapa Krsito anakuja kuchukua mavuno na kuyapeleka kwa Baba mbinguni.
Ukweli ni kwamba, tangu mwaka 1844 mavuno yanaendelea, na mlango wa rehema
utakapofungwa ndio itakuwa mwisho wa mavuno.
Kwa hiyo ndugu, kama ulifikiri kuwa mwisho wa dunia ni siku Yesu anaporudi na ndio wakati wa kufanyika mavuno, hivyo sivyo maana Mama White anatuambia kuwa mwisho wa mavuno ni wakati wa kufungwa mlango wa rehema na tunatambua kuwa mlango wa rehema utafungwa kabla hata ya kuja kwa Yesu mara ya pili; hivyo ina maana pia kuwa mavuno yanafanyika kabla ya kurudi Yesu mara ya pili. Kwa hakika malaika wanaendelea kuvuna ngano katika shamba la Bwana.

Kuna wanosema kuwa wafuasi wa kweli wa Kristo wasitengwe na mifumo iliyoasi kwa kusema kuwa ngano na magugu vinakuwa pamoja hadi wakati wa mavuno, hawajui kuwa kazi inayofanyika ni mchakato wa mavuno, wanafikiri kuwa wokovu unapatikana kwa kujiita wakristoau kujiita kwa jina fulani la kanisa; roho ya unabii inatuambia nini juu ya wokovu?Mungu analitaka kanisa hili lifanye mabadiliko. Walikuwa na jina la kudumishwa, lakini kazi zao hazikuwa na upendo wa Yesu. Ah, ni wangapi wameanguka kwa kutegemea sifa zao kwa wokovu! Ni wangapi wamepotea kwa kufanya juhudi za kuenzi jina. Kama kuna mtumwenye sifa ya kuwa muinjilisti, mwenye mafanikio, Mhubiri mwenye karama, mwenye imani, mtu mwenye kicho cha pekee, Kuna hatari ya wazi kwamba ataharibu imani atakapojaribiwa na majaribu madogomadogo ambayo Mungu angependa yaje’’ – Ellen white – 7 BC, 958.

“Si kwa jina lake, bali kwa tunda lake thamani ya mti hutambulika. Kama tunda halifai, jina haliwezi kuuokoa mti kwa uangamivu” DA, pg. 107
Hatuokolewi kwa kundi:, Hakuna jina la dhehebu lenye uwezo wa kutupatia upendeleo kwa Mungu. Tunaokolewa mmoja mmoja kama waumini wa YESU Kristo.” – E.G.W. RH 02/ 1891 Ukweli ni kwamba, Maandiko yanaelezea tatizo hili kama hivi: Kama unajisikia kujiita mu SDA,fikiria ni nini unachokifanya. Jiulize swali hili: Ni nini kinachomfanya mtu awe mu SDA wa kweli? Tazama jibu hapa chini.
Paulo asema: “Bali ni Myahudi aliye myahudi kwa ndani; na tohara ni ya moyo, katika roho, si katika andiko; ambaye sifa yake haitoki kwa mwanadamu, bali kwa Mungu”.
Warumi 2: 29, Nami nasema: “Bali ni Muadventista msabato aliye muadventista msabato kwa ndani; na tohara ni ya moyo, katika roho, si katika andiko; ambaye sifa yake haitoki kwa mwanadamu, bali kwa Mungu”.

Ufafanuzi wa hatua mbili zinazoitwa ‘mavuno’ katika mfano wa ngano na magugu ni huu: Kama tulivyoona kwamba hatua ya kwanza inafanyikia ndani ya shamba, hii inamaanisha kwamba watu wa Mungu wamekuwa wakivunwa ndani ya kanisa tangu mwaka 1844. Tuliona pia kwamba hatua ya pili ya mavuno ilifanyika nje ya shamba ambapo ngano safi huandaliwa kwa ajili ya kupepetwa na kuondoa makapi. Wakati huo huo magugu hufungwa katika matita matita tayari kwa kuchomwa moto. Hii inamaanisha kwamba wale waliojitenga kutoka kwenye kanisa potofu (shamba) wamechangamana na magugu na huko ndipo panapofanyika hatua ya mwisho ya
kupepeta ngano na kuwekwa ghalani wakati magugu yanafungwa pamoja ili kusubiri moto. Je, wale waliobaki ndani ya kanisa (shamba) potofu ni akina nani? Hao ni miiba na sio ngano safi wala magugu tena. Kumbuka mfano wa Yesu kuhusu mpanzi aliyepanda mbegu zingine zikaanguka penye miiba na hazikuweza kuzaa matunda. Kwa ufupi, ngano na magugu (Wakristo safi na Wakristo kwa jina) wamejitenga na kanisa potofu ikimaanisha hatua ya pili ya mavuno wakati miiba (Wakristo wanaofanya dhambi za wazi na kumkufuru Roho Mtakatifu) wanaendelea kubaki ndani ya kanisa asi na kamwe hawatazaa matunda safi.

JE; UNATAKA KUZAA MATUNDA YA SDA?, Yesu anasema “Kaeni ndani yangu, namindani yenu.Kama vile tawi lisivyoweza kuzaa peke yake, lisipokaa ndani ya mzabibu; kadhalika nanyi msipokaa ndani yangu”. Yohana 15:4.
Yesu hasemi tutafute kwanza kanisa au dhehebu, ila anasema tukae ndani yake, naye
Atatuwezesha kuzaa matunda safi ya SDA maana Yeye ndiye kanisa na kanisa sio mfumo wawatu. Ellen White Acts of Apostles p. 11

“Hakuna kanisa jingine la Mungu zaidi ya mkusanyiko wa wale walio na neno la Mungu, na ambao wamesafishwa nalo” Sprit of Prophecy Vol. 4, p237.
“Wale wanaotunza Amri za Mungu, wale wanaoishi si kwa mkate pekee, lakini kwa kila neon kutoka kwenye kinywa cha Mungu, wanaunda kanisa la Mungu anayeishi”.
7BC 949 “Mungu analo kanisa.Sio majengo makubwa, wala sio lililoundwa kitaifa, (au sio mfumo ulioundwa kidunia) wala si madhehebu mbalimbali; ni watu wanaompenda Mungu na kushika Amri zake, ‘wakutanapo wawili au watatu kwa ajili ya jina Langu, nipo kati yao’ (Mat 18:20). Pale Kristo anapokuwepo kati ya wachache wenye unyenyekevu, Hilo ni kanisa la Kristo, Kwa maana uwepo wa Mtakatifu aliye Juu ambaye ana umilele ndio tu unaounda kanisa lake” Ellen White: The Upward Look p 315. Je, ninahusikaje na dhambi wanazozifanya viongozi wa kanisa langu wakiwa wanatekeleza majukumu ya kanisa wakati mimi sizifanyi? Ninahusikaje na mafundisho ya uongo yanayotolewa na viongozi wa kanisa langu kama mimi siyaamini ingawa nimo ndani ya kanisa hilo au mfumo wa kanisa? Upo uwajibikaji wa pamoja (collective responsibility) kutokana na dhambi zinazofanywa na viongozi wa kanisa wakiwa wanatekeleza majukumu ya kanisa. Kisa cha Akani ni kielelezo kizuri. Akani alifanya dhambi yeye mwenyewe kama anavyosema ‘Kweli nimefanya dhambi juu ya Bwana, Mungu wa Israeli’ Yosh. 7:20. Lakini Bwna alisema nini juu ya dhambi ya Akani?
Israeli WAMEFANYA dhambi, wamelivunja agano langu…. Kitu kilichowekwa wakfu kiko katikati yako Ee Israeli; huwezi kusimama mbele ya adui zako hata mtakapokiondoa kitu mlichonacho’.Yosh. 7:11-13. Kwa vile Akani alikuwa ni kiongozi wa kanisa na alifanya dhambi akiwa katika kazi za kanisa, Mungu aliwahesabia hatia washiriki wote wa kanisa na hata kusababisha vifo vya watu waliodhaniwa kuwa hawakuwa na hatia!

Hivyo basi unapokuwa ndani ya mfumo wa kanisa unaoliongoza kanisa katika makosa, wewe pia unashiriki makosa hayo. Yesu alisema ‘Kipofu akimuongoza kipofu, wote wataangukia shimoni.’Tena imeandikwa ‘Wawaongozao ndip wawapotoshao’ hivyo ‘watu wangu wanaangamizwa kwa kukosa maarifa.’ Sasa nifanye nini Kama viongozi wangu wanafundisha uongo na kuufanya kuwa msingi wa imani?
Tokeni kwake enyi watu wangu, msishiriki dhambi zake (dhambi za kanisa), wala msipokee mapigo yake’. Ufu. 18:4. Dawa ni kujitenga na mfumo mzima wa kanisa kwa lengo la kuokoa roho yako!

Sambaza ujumbe huu kwa watu wengi kadri uwezavyo!
Mungu akubariki unapoendelea kutafakari neno lake!.

KWA MAWASILIANO ZAIDI WASILIANA NASI
0756959525,0752164685
Share:

Popular Posts

Lebo

Recent Posts

Pages