Katika blogu hii, tutachunguza njia mbalimbali za kuimarisha ufahamu wetu wa Biblia. Tutajadili mbinu za kusoma Biblia kwa ufanisi, vidokezo vya kukariri maandiko matakatifu, na mikakati ya kutumia somo la Biblia katika maisha yetu ya kila siku. Iwe wewe ni mtaalam wa Biblia mzoefu au unaanza tu safari yako ya imani, "Jifunze Biblia Zaidi" ni rasilimali kamili ya kukusaidia kuongeza ufahamu wako wa Maandiko Matakatifu na kumkaribia Mungu zaidi.

VIJANA NA HATARI INAYOWAKABILI.

 



VIJANA NA HATARI INAYOWAKABILI.

Katika somo hili tutajifunza mambo yafuatayo:-

1.   Wito wa MUNGU kwa vijana

2.   Ni nini kinachoweza kuwafanya vijana wamshinde shetani?

3.   Maovu na makosa katika siku za ujana

Katika siku hizi za mwisho ni vijana wachache sana waliojitoa kikamilifu kumtumikia MUNGU. Wengi wa vijana hata wale walio makanisani wanaishi kwa unafiki, machoni pa watu wakionekana kama watu wa dini, lakini machoni pa MUNGU wakiwa wameoza na kunuka, sababu ya matendo na tabia zao chafu, ingawa si wote. Ningali kijana mdogo niliwahi kuwasikia watu wakidai kuwa dini ni ya wazee. Usemi huu ulimaanisha kuwa,hakuna kijana anaeweza kuwa mcha MUNGU katika siku za ujana,kwamba amewahi kushika dini mno na lazima ataasi tu. Huu ni usemi unaotoka katika kinywa cha shetani mwenyewe. Na kwa ajili hiyo vijana wengi wanaamua kuishi kwa tamaa za mwili wakifanya zinaa wapendavyo na kudhani kuwa wataweza kubadili mielekeo yao pale watakapotaka, maskini watu hawa wamenaswa wavuni mwa shetani na shetani amewamiliki kikamilifu.

Yafuatayo ni baadhi ya matendo mabaya ya vijana wa kizazi hiki.

1.   Utumiaji wa madawa ya kulevya

2.   Tamaa za uasherati

3.   Kuiga na kuvaa nguo na mitindo ya ajabu ya kidunia (vimini,vibode,modo)

4.   Kutowaheshimu wazazi wao.

5.   Kunyoa denge

6.   Kutazama picha chafu

7.   Kula vyakula na vinywaji vya ovyo.

8.   Kupenda miziki na mpira kana kwamba wanashindania uzima wa milele nk.

Vijana wengi wanaishi kana kwamba hakuna MUNGU, na kwa wengi hawamjui MUNGU wala na madai yake kwao. Lakini MUNGU anawaita Vijana;

1.   Wito wa MUNGU kwa Vijana.

“Mkumbuke Muumba wako siku za ujana wako,kabla hazijaja siku zilizo mbaya,wala haijakaribia miaka utakaposema,mimi sina furaha katika hiyo” Mhubiri 12:1.

MUNGU muumbaji anawataka vijana wajitoe kumtumikia; anataka aabudiwe, akumbukwe, ajaliwe, katika siku za ujana, bado una nguvu. Lakini pia fungu hili linataka tuelewe kuwa, baada ya ujana kuna siku zinakuja zilizo mbaya, siku za kukosa furaha.

“Wewe kijana, uufurahie ujana wako, na moyo wako ukuchangamshe siku za ujana wako, ukaziendee njia za moyo wako , na katika maono ya macho yako, lakini ujue wewe ya kwamba kwa ajili ya hayo yote MUNGU atakuleta hukumuni. Kwa hiyo ondoa majonzi moyoni mwako, nawe uondoe ubaya mwilini mwako,kwa maana ujana ni ubatili na utu uzima pia”. Mhubiri 11:9

MUNGU muumbaji anataka kila kijana afurahie ujana wake. Lakini ili ujana upite vizuri-ondoa ubaya mwilini mwako, je ni ubaya gani ulionao? Na utambue ujana ni kama maji ya moto ujana ni ubatili. Na ya kwamba mambo yote ya ujana na utu uzima pia yataletwa hukumuni. Ufanye unalotaka lakini usisahau kuwa katika hayo yote ipo hukumu ya MUNGU inakuja, Jiandae.

 

 

“Vijana rafiki wapendwa, kila mnachopanda mtakivuna pia.sasa ni wakati wenu wa kupanda. Mavuno yatakuwaje? mwapanda nini? Kila neno msemalo, kila tendo mtendalo ni mbegu ambayo itazaa matunda mema au mabaya, nayo italeta furaha au huzuni  kwa mpandaji. Kama ilivyo mbegu iliyopandwa.Ndivyo yatakavyokuwa mavuno. MUNGU amewapa nuru kubwa na mibaraka mingi. Baada ya nuru hiyo kutolewa baada ya hatari kuonyeshwa dhahiri mbele yenu, mambo yanabaki juu yenu. Namna mnavyofaya na nuru ambayo mnapewa na MUNGU italeta furaha ama huzuni. Ninyi wenyewe mnajitayarishaia mwisho wenu wenyewe”. EG White- 1 kutayarisha njia sura ya 35:1 uk.212.

Kila neno msemalo kila tendo mtendalo ni mbegu ambayo itazaa matunda mema au mabaya. Nayo italeta furaha au huzuni kwa mpandaji. Nataka  uelewe kuwa kutowaza sahihi tu kwa dakika moja, kutenda jambo dogo tu ambalo si la haki, kunaweza kubadiri mkondo wa maisha yako yote; Ninyi wenyewe mnajitayarishia mwisho wenu.

“Muda mfupi unaotumika katika kupiga maisha ujanani, rafiki zangu vijana wapendwa, utatoa mazao ambayo yatafanya maisha yako yote yawe machungu, saa moja ya kutowaza sahihi, mara unapokubali kuingia katika jaribu, waweza kubadilisha mkondo mzima wa maisha kwenda mwelekeo usio sahihi. Unao ujana mmoja tu, hebu ufanye kuwa wenye manufaa. Upitapo katika eneo moja huwezi kurejea na kurekebisha makosa yako. Shetani huwa anajigeuza na kuwa mfano wa malaika wa nuru ajapo kwa vijana na majaribu yake yanayohadaa na huwa anafanikiwa kuwashinda, hatua kwa hatua kutoka katika wajibu wao”. EG.White – 1 Maranatha uk 82:1-2.

Ni kweli shetani ajapo kwa vijana na majaribu yake tena yanayohadaa anafanikiwa kuwashinda. Ni wengi ambao shetani amewashinda kwa tamaa za mwili, kwa ulevi wa pombe, ulafi, na kwa kutowatii wazazi wao. Vijana hawa ambao ndio hufanya familia, taifa na kisha mataifa, wengi wao wamearibika kiasi kikubwa. Katika Mataifa mbalimbali hata vijana wanavyoongea tu ushuhudia jambo hili na wengine wanaongea kama mazezeta, wenyewe wakijiita kuwa ni masela; huu wote ni upotevu wa maadili.

MUNGU anahitaji maisha ya ujana juu ya vijana tulio nao katika nyumba zetu na kanisani, maisha yao yawe kielelezo:     - Kielelezo katika usemi

-      Kielelezo katika mwenendo

-      Kielelezo katika upendo

-      Kielelezo katika imani

-      Kielelezo katika mavazi, uvae kwa kujistiri. Maandiko yanaendelea  kuonya ifuatavyo:-

“Mtu awaye yote asiudharau ujana wako,bali uwe kielelezo kwao waaminio,katika usemi na mwenendo na katika upendo na imani na usafi”. 1 Timotheo 4:12.

Ili ujana wako usidharauliwe uwe kielelezo katika mwenendo, usemi, upendo, kielelezo katika imani, utakuwa na ujana wenye manufaa. Lakini kama mwenendo wako ni wa ovyo, usemi ni waovyo, watu hawataacha kukudharau. Je wewe kijana unaesoma kitabu hiki ulichonacho mkononi mwako, mwenendo wako ukoje? Je, watu wanavyo kutazama wanaona kielelezo katika imani na usafi? Habari gani juu ya usemi wako, Maana katika siku hizi za mwisho kuna lugha zinazotumika mitaani ambazo zinaonyesha upotovu wa maadili. Zifuatazo ni baadhi ya lugha zinazotumiwa na vijana lakini ni upotofu wa maadili cha ajabu hata vijana Wakristo nao wamepotoka.

(i)          Shilingi elfu moja- inaitwa buku, sijui hii nitafasiri ya lugha gani duniani.

(ii)        Shilingi mia tano – inatwa jero.

 

(iii)       Baba – anaitwa dingi, lakini ukweli dingi ni mdudu ambae husukuma mavi kinyume nyume, Maajabu kabisa.

(iv)       Masela, demu, nisepe, sharobaro, mshikaji, ganja nk.

Lakini vijana Wakristo siyo kwamba wanapaswa kuepuka kutumia lugha hizi tu, bali wao watabaki kuwa vielelezo katika usemi safi.Lakini kumbukumbu zinaonyeshaje? Hata vijana wakristo wengi wao wamepotoka. MUNGU kupitia nabii wake akuacha kuonya;

“Katika mazungumzo ya siku hizi kuna lugha zisizofaa zenye kutia hofu (masela, demu, dingi, jero, nisepe, mshikaji). Lugha hizi zinaonyesha hali duni ya mawazo na hali duni ya maadili.Heshima ya kweli katika tabia ni nadra sana.Wapo watu wachache tu ambao ni safi na wasiotiwa unajisi. Hatari za kimaadili ambazo zinawakabili wote wazee kwa vijana, zinaongezeka kila siku.Kuharibika kwa maadili,ambako tunakuita upotovu unapata nafasi ya kutosha kutenda kazi na wanaume, wanawake, na vijana ambao wanadai kuwa Wakristo, wataacha mvuto ambao ni duni, wa kupenda anasa, na wa kishetani”. EG. White - 1 Maranatha 153: 1,4.

·         Hizi ni lugha zisizofaa

·         Zinaonyesha upotovu wa maadili

·         Zinaonyesha hali duni ya mawazo ya wanaume na wanawake.

·         Wote wale wanaozitumia wanaacha mvuto wa kishetani.

·         Wote wale wanaozitumia ni wapenda anasa

·         Wamebaki watu wachache ambao ni safi katika usemi na ambao hawajatiwa unajisi.

Neno linaendelea kuonya.

“Wala aibu wala maneno ya upuuzi wala ubishi hayo hayapendezi, bali afadhali kushukuru. Mtu asiwadanganye kwa maneno yasiyokuwa na maana kwa sababu ya hayo hasira ya MUNGU huwajia wana wa uasi  Waefeso 5:4,6.

“Neno lolote lililo ovu lisitoke kinywani mwenu, bali lililo jema la kumfaa mwenye kuitaji ili liwape neema wanaosikia Waefeso 4:29.

Maneno maovu:

(i)          Lugha zisizofaa (upotevu wa maadili)

(ii)        Maneno ya upuuzi

(iii)       Maneno yasiyo na maana

(iv)       Maneno ya aibu.

(v)         Maneno ya ubishi

(vi)       Maneno ya utani (hata na mashemeji na binamu).

Maneno maovu mengine; masela, demu, dingi, buku, nisepe, jero, mshikaji, sharobaro, lugha hizi zinaonyesha hali duni ya mawazo na hali duni ya maadili. Na wanaume kwa wanawake na vijana wanaojidai kuwa wakristo lakini wanazungumza maneno maovu kama haya; neno linasema, wanaacha mvuto wa kishetani.Hata hivyo neno linaendelea kuonya ifuatavyo:-

“Basi nawaambia, kila nemo lisilo na maana watakalolinena wanadamu, watatoa hesabu ya neno hilo siku ya hukumu. Kwa kuwa kwa maneno yako utahesabiwa haki na kwa maneno yako utahukumiwa”.  Mathayo 12:36-37.

 

 

 

2.   Nini kinachoweza kuwafanya vijana wamshinde shetani.

Je, vijana wanauwezo wa kumshinda shetani? Ndiyo. Yafuatayo ni makundi mbalimbali ya watu waliomo kanisani wenye uwezo wa kumshinda shetani, wakiwemo na vijana.

“Nawaandikia ninyi akina baba, kwa sababu mmemjua yeye aliye tangu mwanzo. Nawaandikia ninyi vijana kwa sababu mmemshinda yule mwovu.Nimewaandikia ninyi watoto kwa sababu mmemjua

baba.Nimewandikia ninyi vijana kwa sababu mna nguvu na neno la MUNGU inakaa ndani yenu, nanyi mmemshinda yule mwovu”. 1 Yohana 2:13-14.

Kuna watu wengi sana wanaogelea katika maovu siku za ujana wao.Wanatenda maovu mpaka yanakera katika siku za ujana, wakidhani wataweza kubadili mambo watakavyotaka, na wengine kwa unyoge wanadhani hawawezi kumshinda Ibilisi katika siku za ujana, huo ni uongo. Neno la MUNGU linathibitisha kuwa vijana wanao uwezo wa kumshinda shetani. Lakini ili wapate kumshinda shetani ni mpaka neno la MUNGU likae kwa wingi ndani yao. Hii ndiyo siri ya kushinda dhambi katika siku za ujana.

“Kutokana na yale niliyoonyeshwa, si zaidi ya nusu ya vijana wanaodai kuamini dini na kweli ambao wameongoka kwelikweli. Majina yameandikwa katika vitabu vya Kanisa hapa duniani, lakini sio katika kitabu cha uzima. Naliona kuwa katika vijana hakuna hata mmoja kati ya ishirini anayejua hasa maisha ya dini yalivyo hasa”. EG. White - 1T 504; MYP 384 [1867] Dhiki kuu uk 51:2-3

Narudia tena; ni nini kinachomfanya mtu asitende dhambi?

“Moyoni mwangu nimeliweka neno lako nisije (mimi) nikakutenda dhambi”. Zaburi 119:11.

Kwa kutojua haya vijana wengi wanaishi kwa unafiki, machoni pa watu wakionekana kama watu wema. Lakini machoni pa MUNGU wakiwa wameoza na hata kunuka.Kama kuna kijana ananuka kwa vitendo viovu, ifuatayo ndio njia ya kujisafisha; liko tumaini la kunukia tena. “Jinsi gani kijana aisafishe njia yake? Kwa kutii akilifuata neno la MUNGU”. Zaburi 119:9.

“Usiogope maana hutatahayarika wala usifadhaike maana hutaaibishwa kwa kuwa utaisahau aibu ya ujana wako” Isaya 54:4.

Kama unanuka kwa tabia na matendo mabaya, kanisani, nyumbani, mtaani, pengine umekuwa mvuta bangi, mwizi, usiyeheshimu hata wazazi wako, mara ngapi umetembea nusu uchi mabarabarani, pengine umewai hata kujiuza na kufanya viungo vya mwili wako kuwa kiwanda cha kuchapisha hela; umetumia madawa ya kulevya, nguo zenyewe hata sasa unavaa modo, Kata kei, nguo zingine unavaa zimetobolewa matundu, unatembea viungo vya mwili wako viko nje, haujisitiri tena kama Biblia inavyofundisha. Kwa haya yote na mengine mengi ingawa waweza kujipaka marashi ukitembea unanukia; lakini ukweli katika haki unanuka. Machoni pa watu waliopotoka pia waweza kuonekana maridadi na hata wakakusifu, lakini machoni pa MUNGU mkuu, unakaribia hukumu yako, sababu ya vitendo vyako viovu.

Pamoja na hayo liko tumaini kwa vijana wale watakaoona imetosha waishie hapo kunuka kwa tabia mbaya; Namna ya kujisafisha ni kwa kutii na kulifuata neno la MUNGU, utakuwa umepata ushindi mkuu dhidi ya Ibilisi. Na MUNGU wetu atakusafisha hata uweze kunukia kwa tabia njema na wala siyo kwa malashi. Umebarikiwa sana kuijua siri ya ushindi wa dhambi katika siku za ujana.

 

“Hebu vijana wafundishwe kujifunza kwa makini neno la MUNGU. Likipokelewa rohoni litakuwa kizuizi kikubwa dhidi ya majaribu. Mtunga Zaburi anasema; “Moyoni mwangu nimeliweka neno lako, nisije nikakutenda dhambi; kwa neno la midomo yako nimejiepusha na njia za wenye jeuri” (Zaburi 119:11, 17:4).Kama mashauri ya neno la MUNGU yakifuatwa kwa uaminifu, neema ya Kristo inayookoa italetwa kwa vijana wetu; Kwani watoto wanaofundishwa kupenda na kumtii MUNGU na wanaojitoa wenyewe kwa

uwezo wake wenye nguvu wa neno lake linalounda ndiyo shabaha ya uangalizi maalumu na Baraka za MUNGU”. EG.White - 2 katika Ulimwengu wa Roho Uk 34:4-5.

Umebarikiwa sana kuijua siri ya ushindi wa dhambi katika siku za ujana. Hebu sasa nakusii umgeukie MUNGU na neno lake, utakuwa umebadili kabisa maisha yako toka mwelekeo usio sahihi, kwenda mwelekeo ulio sahihi, na ukijiandaa kuishi maisha ya milele katika mji wa MUNGU. Neno linaendelea kuwaita vijana:-

“Ni vema mwanadamu aichukue nira wakati wa ujana wake” Maombolezo 3:27.

Je, Nira ambayo vijana wanapaswa kuichukua wakati wa ujana ni nini?

“Nira hiyo ni sheria za MUNGU ,ambazo zimeandikwa ndani ya mioyo.Humuunganisha mtenda kazi wa MUNGU na mapenzi ya MUNGU.Kama tungaliachwa kuenenda jinsi tupendavyo,tungelitumbukia katika mashimo ya shetani.Kwa hiyo MUNGU hutufunga katika mapenzi yake”. EG.White - Tumaini la Vizazi Vyote Sura 34.Uk.180.

Mojawapo ya neno, ama maandiko ambayo kijana anapaswa kuyashika ni sheria ya MUNGU. Ifuatayo ndiyo nira ama sheria ya MUNGU ambayo itiiwe siku za ujana.

Kutoka 20:1-17

1.   Usiwe na Miungu mingine ila mimi

2.   Usijifanyie sanamu ya kuchonga

3.   Usilitaje bure jina la BWANA MUNGU wako.

4.   Ikumbuke siku ya sabato uitakase

5.   Waheshimu baba yako na mama yako

6.   Usiue

7.   Usizini

8.   Usiibe

9.   Usimshuhudie jirani yako uongo.

10.     Usitamani nyumba ya jirani yako, usimtamani mke wa jirani yako.

Nimeiandika kwa ufupi hebu soma Kutoka 20:1-17.

Amri kumi ndiyo Nira ambayo kila kijana anapaswa kuichukua na kwa njia hiyo atakuwa amefungwa katika mapenzi ya MUNGU na kujihepusha na maisha machungu ya baadaye.Neno la MUNGU likipokelewa rohoni katika siku za ujana litakuwa kizuizi kikubwa dhidi ya majaribu, na litakuvika ustiri mtakatifu.

“Mioyo ya vijana ikiachwa bila kuzuiwa inaelekezwa kwenye mkondo unaopatana na tabia yao iliyoharibika, wanaacha kuwa macho na kujihadhari na kupeana upendo kila mmoja na mwenzake, kuwa na marafiki maalumu watu maalumu wa kuwatunzia siri na wakati marafiki hawa wanapokuwa pamoja,Yesu hatajwi sana kati yao.mazungumzo yao hayahusu maisha ya Kikristo, hayamhusu Kristo, hayahusu mbinguni bali yako katika mambo ya upuuzi.Hawafahamu hila za mwovu na wakiwa

 

kwenye umri wa miaka kumi na mbili,kumi na nne,kumi na tano, na kumi na sita,wanajifikiria kuwa ni vijana wakubwa wa kike na wakiume na kwamba wanauwezo wa kuchagua mwelekeo wao wenyewe na kujiongoza wenyewe kwa adabu na uangalifu”. EG. White – 2 Katika Ulimwengu wa Roho 38:4-5.

3.   Makosa na Maovu katika siku za ujana.

Wale wote wanaojiona wana uwezo wa kujiongoza wenyewe kwa sababu wamesoma elimu ya ulimwengu, ama kwa kuwa wana uchumi, au kwa vile, wanatoka katika ukoo ulio bora, wataishia katika maovu makuu. Neno la MUNGU ndio kizuizi kikubwa dhidi ya dhambi,si kwa vijana tu bali na kwa watu wote duniani. Hebu ufanye ujana wako kuwa wenye manufaa kwa kutii neno, utakuwa unaishi kwa viwango vya mbinguni na siyo kwa viwango vya ulimwengu.

Lakini kwa kutoyajua haya, kwa wengi miaka ya ujana ni siku za kupiga maisha. Wengine kwa kutazama picha chafu kwenye mitandao, tamaa za uasherati, kucheza mziki, kula na kunywa vyakula vya ovyo na vya kianasa, kunyoa denge, kuvaa nguo za mitindo ya ajabu ya kidunia (modo, kata keyi, vimini, vibode) utumiaji wa madawa ya kulevya, kujikoboa, kutowaheshimu wazazi wao, na hata wizi; haya ni baadhi tu ya maovu yanayotendeka katika siku za ujana.

“Tunaishi katika kipindi cha upotovu na Wanaume kwa vijana ni jasiri katika dhambi. Vijana wetu wasipolindwa kwa utakatifu, wasipolindwa kwa kanuni thabiti, uangalizi mkubwa usipodhihirishwa katika kuchagua rafiki zao pamoja na machapisho yanayolisha akili, watakuwa wameachiliwa kwa jamii ambayo maadili yao yamechafuka kama yalivyokuwa ya wakazi wa Sodoma. Vijana wetu watakutana na majaribu kila upande na ni lazima waelimishwe kwamba itawapasa wategemee nguvu itokayo juu, kuliko yale yatolewayo na binadamu”. EG. White – 2 Wana na Binti za Mungu uk 47:1.

Ni kwambie ndugu msomaji; ni vigumu kuyaandika maasi yote ya ujana katika somo hili. Kwani makosa na dhambi nyingi watu wengi hutenda wakati wa ujana, na hii ni kwa sababu wamemkataa MUNGU. Mtumishi wa MUNGU Daudi alipojua haya akasema ifuatavyo:

“Usiyakumbuke makosa ya ujana wangu, wala maasi yangu, unikumbuke kwa kadiri ya fadhili zako, Ee BWANA kwa ajili ya wema wako” Zaburi 25:7.

Ndugu msomaji kama si wema wa MUNGU, na kama si fadhili za MUNGU tu, kama akiyakumbuka maovu na maasi ya ujana wako nani angesimama? Hata na mimi kwa kuyaandika haya ni kwa wema wa MUNGU tu sistahili. Hebu ombi la Daudi na liwe ombi letu, tumlilie MUNGU afute dhambi zetu na asiyakumbuke maovu na maasi ya ujana wetu. Ingawa vijana wengi wanajipaka marashi nakutembea wananukia lakini kwa ajili ya maovu na maasi yao machoni pa haki wananuka, je, wewe unayesoma haya kwa tabia yako unadhani unanukia ama unanuka, tafakari. Yafuatayo ni baadhi tu ya makosa mengine ya ujana ambayo vijana wa kiume na wa kike wanapaswa kuyashinda.

(i)                  Tamaa.

“Lakini uzikimbie tamaa za ujanani, ukafuate haki, na imani, na upendo na amani, pamoja na wale wamwitao BWANA kwa moyo safi” 2 Timotheo 2:22.

Nataka uelewe kuwa kwenye ujana kuna tamaa. Na vijana mnapaswa kuzikimbia tamaa za ujanani. Na hili uzikimbie ni mpaka uwe mwenye imani, upendo safi, mwenye haki, na ufuatane pamoja na wale wamwitao BWANA kwa moyo safi. Kuna watu wengi hata

 

makanisani wanamtaja BWANA kwa kuimba, Kwa kuhubiri, lakini si kwa moyo safi. Uwe macho, usije ukarudia tabia za kishenzi wakati uko kanisani.

“Wengine wanahubiri habari za kristo kwa sababu ya husuda na fitina ,wengine kwa nia njema. Hawa wana mhubiri kwa pendo,wakijua ya kuwa nimewekwa ili niitetee injili,bali wengine wanamhubiri kristo kwa fitina,wala si kwa moyo mweupe”. Wafilipi 1:15-17. Soma pia Mathayo 7:21,

Lakini uzikimbie tamaa za ujanani; ni tamaa gani? “Msiipende dunia, wala mambo yaliyomo katika dunia. Mtu akiipenda dunia kumpenda Baba hakumo ndani yake. Maana kila kilichomo duniani, yaani tamaa ya mwili, na tamaa ya macho, na kiburi cha uzima, havitokani na Baba, bali vyatokana na dunia, na dunia inapita, pamoja na tamaa zake, bali yeye afanyaye mapenzi ya MUNGU adumu hata milele”. 1Yohana 2:15 -17.

Tamaa ambazo vijana wanapaswa kuzikimbia.

(i)   Tamaa ya mwili

(ii)  Tamaa ya macho

(iii) Na kiburi cha uzima

Wote watakao yang’anga’nia haya wataangamia na tamaa zao. Ishi kwa kutenda mapenzi ya MUNGU na utadumu milele ukiwa katika mji wa MUNGU.

“Vivyo hivyo na vijana waume uwaonye kuwa na kiasi Tito 2:6.

 Maonyo:

“Wapenzi, nawasihi kama wapitaji na wasafiri, ziepukeni tamaa za mwili zipinganazo na roho” 1 Petro 2:11.

Na mabinti nao; “Nawasihi, enyi binti za Yerusalemu kwa paa na kwa ayala wa porini, msiyachochee mapenzi, wala kuyaamusha, hata yatakapoona vema yenyewe” Wimbo bora 3:5

(i)          Kuacha wazi sehemu nyeti za mwili, mfano, kitovu, mapaja, matiti tumbo, ni kutangaza kuyaamsha mapenzi

(ii)        Kuvaa nguo fupi za kubana, zinaamsha mapenzi

(iii)       Kujipamba kwa kujikoboa. Vijana wote wa kiume na wa kike, na kama mapenzi unaona yanajichochea mwilini kwa tamaa ujizuie. Na kama unashindwa kujizuia ni aibu. “Bali yeye asiyejizuia nafsi yake amekufa ingawa yu hai” 1Timotheo 5:6 kuishi kwa tamaa ni uovu mkuu. Hata hivyo mpango mwingine wa kupinga tamaa huu hapa chini:-

“Lakini nawaambia wale wasiooa bado, na wajane ni heri wakae kama mimi nilivyo. Lakini ikiwa hawawezi kujizuia, na waoe, maana ni afadhali kuoa kuliko kuwaka tamaa”. 1Wakoritho 7:8-9.

Vijana wengine hukwepa kuoa wakidai Maisha ni magumu na huku wakiendelea kufanya uzinzi, ingawa hakuna siku maisha yatakuwa rahisi. Wanabadilisha wanawake kama nguo wakidhani wanawakomesha kumbe wanajikomesha wenyewe. Wasichana wengine nao wanaona maisha ya ndoa ni ya utumwa na hawata kuwa na uhuru, na hivyo wanaonelea afadhali waishi wakibadilisha wanaume kama nguo, ilimradi anapata riziki

 

ya kuishi. Kwa ajili hiyo kitendo cha ndoa kilichotolewa na kubarikiwa kiwe furaha kwao waliooana leo kimegeuzwa kuwa mradi wa kutafutia fedha. Maajabu kabisa.

Ifuatayo ni dawa ya kutiisha tamaa za mwili.

“MUNGU anataka vijana kuwa watu wenye mioyo hodari, kutayarishwa kuitenda kazi yake bora,na kufanya wafae kuchukua madaraka. MUNGU anawaita vijana wenye mioyo safi wenye nguvu na hodari, na wenye kukusudia kupigana kiume katika vita vilivyo mbele yao, ili wapate kumtukuza MUNGU, na kuwanufaisha wanadamu. Ikiwa vijana wangeifanya Biblia kuwa somo lao, wangeweza kutuliza tamaa zao mbaya, na kusikiliza sauti ya muumbaji wao. Licha ya kuwa na amani na MUNGU, hata wangejiona kuwa wameadilishwa na kuzidishwa hadhi” EG. White -1 Kutayalisha njia Sura ya... uk 214:2.

Ufuatao ndio mpango wa MUNGU juu ya miili yetu;

”Maana haya ndiyo mapenzi ya MUNGU, kutakaswa kwenu, mwepukane na uasherati, kila mmoja wenu ajue kuuweza mwili wake katika utakatifu na heshima,si katika hali ya tamaa mbaya, kama Mataifa wasiomjua MUNGU. Maana MUNGU hakutuitia uchafu, bali tuwe katika utakaso”. 1 Watesalonike 4:3-5,7.

Je, mwili wako unakushinda kujizuia kwa tamaa? Basi wewe ni maiti unaetembea, maana andiko lasema” Bali yeye asiyejizuia nafsi yake amekufa ingawa yu hai” 1Timotheo 5:6.

Wale waliotakaswa na neno la MUNGU wazingatie yafuatayo:-

·                     Kila mmoja wetu ajue kuuweza mwili wake

·                     Mwili uwe katika hali ya heshima

·                     Mwili uwe katika hali ya utakatifu

·                     Mwili usiwe katika hali ya uchafu, Maana MUNGU hakutuitia uchafu

·                     Na mwili usiwe katika hali ya tamaa mbaya, kama watu wa mataifa wasiomju MUNGU, yaani wapagani. Kufaamu kwa kina zaidi juu ya jambo hili hebu nikuombe fanya kila unaloweza kupata kitabu kile cha amri kumi na usome amri ya saba inayosema usizini. Utabarikiwa sana na utakuwa umeongeza kina cha ujuzi wa kumjua MUNGU.

 

(ii)                Makosa ya ujana, lingine ni kutoheshimu wazazi

“Msikilize baba yako aliyekuzaa wala usimdharau mama yako akiwa mzee”. Mithali 23:22.

Wazazi wengi wanaombembeleza, wana huzuni, na wengine wanauchungu kwa sababu ya tabia na matendo ya vijana wao maana yanakera,unaweza kuishia kushangaa kumuona kijana wa miaka kumi na tano,  au hata miaka ishirini, anavuta sigara, bangi, anavaa nguo, lakini nguo ya ndani ndiyo iko nje, hata katika suruali zao ni kama ndani yake amebeba mzigo wa mavi. Matendo kama haya na mengine kwa mzazi makini yatamtia uchungu.

“Mwana mpumbavu ni huzuni kwa babaye, na uchungu kwa mamaye aliyemzaa”. Mithali 17:25.

   “Mwana mwenye hekima humfurahisha babaye bali mwana mpumbavu ni mzigo wa mamaye”. Mithali 10:1.

 

Ni kweli wapo watoto ambao wanawapa matunzo na heshima nzuri baba na mama zao,na hawa bila shaka hufurahisha wazazi wao. Lakini katika familia nyingi wapo watoto ambao ni mzigo. Wameharibu miili na akili zao sababu ya uvutaji wa bangi na sigara. Kila siku hawakosi vijiweni na kwenye makundi ya watu wahuni. Si hivyo tu wengine wamekuwa mzigo sababu hata kufanya kazi kwa mikono yao hawataki, ni wavivu. “Ikiwa mtu hataki kufanya kazi basi asile chakula”. 2 Watesalonike 3:10-11.

Watoto hawa ambao ndio hufanya taifa kisha mataifa wameharibika kiasi kikubwa, hivyo karibu ulimwengu wote umeharibika kimaadili, ingawa bado kuna watu wachache wenye Roho wa MUNGU. Watoto wa kike nao kuna wengine wanalaani kuolewa,wakidhani kuolewa ni utumwa. Wengi wao wamebadilisha viungo vyao vya uzazi na kuwa viwanda vya kutengeneza hela, na mwisho wao, wameambulia magonjwa mazito, na wengine kuzaa ovyo ovyo na hatimaye kuwa mzigo nyumbani mwao. Laiti ungekubali maonyo ya wazazi wako ungejiokoa na maovu.

Na alaaniwe amdharauye baba yake na mama yake na watu wote waseme amina”. Kumbukumbu la Torati 27:16 kufahamu vizuri jinsi ya kuwaheshimu wazazi, hebu tafuta kitabu kile cha amri kumi za MUNGU na usome amri ya tano, utabarikiwa sana.

TAMAA YA MACHO: Kutamani vitu vya watu kumewafanya vijana wengine kugeuka kuwa wezi. Wizi au kuiba ni kitendo cha kutamani mali ya mtu mwingine na hatimaye kuamua kuchukua, kuficha, kulagahai, au kunyang’anya, na kujitwalia bila ridhaa ya mwenyewe. Dhambi hii ya wizi ni tatizo kubwa katika jamii linatokana na tabia iliyojengwa zaidi katika msingi wa tamaa na ubinafsi. Na vijana wengi katika familia mbalimbali kwa sababu ya kutokupenda kufanya kazi na uvivu hugeuka kuwa wanyang’anyi ama wadokoaji.

“Maana adhulumuye atapata mapato ya udhalimu wake wala hakuna upendeleo” Wakolosai 3:25.

“Msiwe na tabia ya kupenda fedha, mwe radhi na vitu mlivyonavyo kwa kuwa yeye mwenyewe amesema, sitakupungukia kabisa, wala sitakuacha”. Waebrania 13:5.

“Si kwamba nasema haya kwa kuwa nina mahitaji; maana nimejifunza kuwa radhi na hali yoyote niliyo nayo. Najua kudhiliwa, tena najua kufanikiwa, katika hali yoyote, nimefundishwa kushiba na kuona njaa, kuwa na vingi na kupungukiwa. Nayaweza mambo yote katika yeye anitiaye nguvu”. Wafilipi 4:11-13.

“Maana shina moja la mabaya ya kila namna ni kupenda fedha; ambayo wengine hali wakiitamani hali hiyo wamefarakana na imani na kujichoma kwa maumivu mengi”. 1 Timotheo 6:10.

(iii)               Kosa lingine katika siku za ujana, ni kutazama picha chafu.

Shetani ambaye hapendi maadili mema ameingiza uharibifu katika baadhi ya vyombo vya habari. Vitabu vya hadithi za mapenzi, video, magazeti, TV, Internate, Simu nk. Vitu hivi vimebeba uchafu unaochafua mawazo ya vijana wengi. Asilimia kubwa ya yale yaliyomo katika vitu hivi ni shule inayoelekeza wengi kwenda kwenye umalaya. Mengi yaliyopitia machoni na kusikia kwa masikio yamekuwa chanzo cha watu wengi kuharibika. Wale wanaopenda maisha yao watachaghua vile vya kuona, kusoma na kusikiliza. Kuingia katika shule ya umalaya kwa kuangalia na kusoma visivyofaa kutaharibu afya yako, akili yako. Na mwisho ni kuangamia milele. MUNGU muumbaji kupitia kwa Nabii wake.  E.G.White, anaandika ifuatavyo juu ya jambo hili;

 

“Hata hivyo bado tunayokazi ya kufanya ili kupinga majaribu. Wale ambao hawataanguka katika mbinu za shetani wanapaswa kulinda vizuri maeneo ya nafsi; wanapaswa kujizuia kusoma, kuona, au

kusikia kile kitakacholeta mawazo machafu. Akili haipaswi kuachwa itangetange huku na huko katika kila kitakachopendekezwa na adui wa roho. E.G.White - 1W/Manabii 465:3 pp 460:2

Hata hivyo mtumishi wa MUNGU Daudi akiwa katika njozi takatifu MUNGU alimwambia aandike ifuatavyo; “Unigeuze macho yangu nisitazame visivyofaa, unihuishe katika njia yako” Zaburi 119:37

 

Watu wengi katika simu zao wanapicha za wanawake walio uchi, na Wasichana wengine nao hupiga picha za ajabu kabisa na kuzituma kwenye mtandao wao wenyewe, ili wanaume wawaone walivyoumbika. Hata saluni nyingi zimepambwa ukutani na picha za hivyo, hakika hiki ni kizazi kilichopotoka sana, kizazi cha zinaa. Unaweza kushangaa kuona baba mzima tena na kitambi chake anaangalia picha za ngono, hili ni janga. Wasomi wengi nao ni wahanga wa janga hili, unaweza kuishia kushangaa kuwaona watu wanaodaiwa kuwa wameelimika kwa kupata elimu ya ulimwengu, na kumbe ndio wamepotoka kabisa, ingawa sio wote. Nikwambie ndugu msomaji elimu kuu kuliko elimu zote ni ya Biblia. Kama haujapata elimu ya Biblia, basi bado una ulemavu katika mambo ya elimu. Kutazama dhambi, yaani, kutazama picha za ngono kwenye mitandao na kusoma hadithi za mapenzi - ni uzinzi; ni uvunjaji wa amri ya saba. Hebu sasa nikuombe usome hapa chini kwa makini sana;

 

“Vijana wengi wana shauku ya vitabu. Wanasoma kila kitu wanachoweza kukipata. Hadithi za kusisimua za mapenzi na picha chafu zina mvuto wenye kupotosha. Vitabu vya hadithi za kubuni vinasomwa na wengi, na matokeo yake ni kwamba fikra za  wengi zinanajisika. Ndani ya magari, picha za wanawake ambao wako uchi zinasambazwa kwa ajili ya kuuzwa. Picha hizi zenye kuchukiza zinaninginizwa kwenye kuta za wale wanaofanya biashara ya kutia nakshi. Hiki ni kizazi ambacho upotovu unaenea kila mahali. Tamaa ya macho na ya mwili inaamushwa kwa kutazama na kusoma. Moyo unachafuliwa kwa njia ya fikra. Akili inapendezwa kufikiria matukio yanayoamusha tamaa mbaya. Picha hizi zenye kutia aibu, ambazo zinatazamwa kupitia fikra zilizonajisiwa, zinaharibu tabia na kumwandaa mtu ambaye amedanganyika na kupumbazwa na upendo, ashindwe kujizuia katika tamaa za mwili. Ndipo inafuata dhambi na uhalifu ambavyo vinawavuta wanadamu ambao wameumbwa kwa mfano wa MUNGU, kwenda chini kabisa hadi kufikia kiwango sawa na mnyama, na katimaye kuwazamisha katika uangamivu. Epuka  kusoma na kuangalia mambo ambayo yataleta mawazo mabaya. Hebu akili zetu zisidhoofishwe na kupotoshwa hata kwa kusoma vitabu vya hadithi.”  E.G.White - 1 Maranatha 143:1

Hatima ya Vijana na watu wote watakaodumu kutenda maovu;

“Mimi nalisema nawe wakati wa kufanikiwa kwako, lakini ulisema, sitaki kusikia. Hii ndiyo iliyokuwa desturi yako tangu ujana wako, kutokutii sauti yangu”Yeremia 22:21.

“Na tulale kwa aibu yetu, haya yetu na itufunike; kwa maana tumemwasi BWANA, MUNGU wetu, sisi na baba zetu tangu ujana wetu hata leo. Wala hatukutii sauti ya BWANA, MUNGU wetu”. Yeremia 3:25.

Wito

“Hakika baada ya kugeuzwa kwangu nalitubu; na baada ya kufundishwa kwangu, nalijipiga pajani; nalitahayarika, naam, nalifadhaika, kwa sababu naliichukua aibu ya ujana wanguYeremiah 31:19.

“Maana ujapojiosha kwa magadi, na kujipatia sabuni nyingi, lakini uovu wako umeandikwa mbele zangu, asema BWANA MUNGU”. Yeremia 2:22.

 

Fanya maamuzi sasa ya kuishi kwa mpango wa MUNGU, ukitii neno lake na amri kumi zake, na utakuwa umepata ushindi mkuu dhidi ya Ibilisi katika siku za ujana. Kumbuka,

ukimgeukia MUNGU katika siku za ujana, utakuwa umejiandaa vyema kubeba majukumu ya kazi ya MUNGU. Ukiwa na utambuzi na maarifa, tofauti na mtu aliyearibu ujana kwa kupiga maisha.

 

“Historia ya Mfalme wa kwanza wa Israeli inaonyesha mfano wenye huzuni wa nguvu za awali katika mazoea. Wakati wa ujana wake Sauli hakumpenda wala kumcha Mungu; na Roho ya kutokuwa na subira, akiwa hakufundishwa mapema kujitoa, alikuwa tayari kuasi mamlaka ya Mbinguni. Wale ambao wakati wa ujana wao hujali mambo matakatifu kwa ajili ya mapenzi ya Mungu, na ambao wanatekeleza Wajibu katika nafasi zao kwa uaminifu, wataandaliwa kushika majukumu makubwa baadaye. Lakini wanadamu hawawezi kwa miaka mingi kupotosha nguvu ambazo Mungu amewapa, na kisha, wanapochagua kubadilika, wanazikuta nguvu hizi zikiwa mpya na huru kwa ajili ya kuzifanyia kazi iliyo kinyume na iliyokusudiwa”. EG. White – PP 622;2, 2 Wazee na Manabii uk 686:2.

BWANA akubariki na karibu katika Kanisa la Mungu.

Share:

UJUMBE WA SHAHIDI MWAMINIFU KWA WALAODIKIA

 

      Mungu amekusudia kuwaamsha watu wake, ili waone hali yao ya kiroho, Ujumbe huu unamhusu kila mtu ndani ya kanisa.  Mtu au watu watakao ukubali ushuhuda huu wa shahidi Mwaminifu watatakaswa kwa ile kweli na watakuwa tayari kusimama peke yao na kuutangaza ukweli bila kuupindisha. “Niliuliza maana ya mpepeto niliokuwa nimeuona na nikaonyweshwa kuwa umesababishwa na ushuhuda yakinifu (wazi usiopinda) wa shahidi Mwaminifu kwa walaodiakia.Huu utakuwa na mvutano kwa yule aupokeae, na utamuongoza kuinua kiwango chake  cha kusambaza ukweli bila kuupindisha . Wengine hawatakuwa tayari kuusambaza ushuhuda huu watainuka kinyume chake na jambo hili litasabisha mpepeto. MATUKIO SURA 12 UK 162”

   Wengine hawatakuwa tayari kuupokea ushuhuda huu wa shahidi   Mwaminifu watachukua Msimamo wao kinyume na ushuhuda huu kwa kuukataa na kuupinga, huku wakiendelea kushikilia nadharia na mapokeo ya watu, Migawawanyiko itatokea kanisani. Makundi mawili yatatokea. Wakati wa hatari kuu upo mbele yetu. Kila mmoja anayejua kweli angeamka, na kuweka mwili wake, Mawazo, Moyo na roho chini ya uongozi wa MUNGU. Adui yukatika njia yetu, Yatupasa tukeshe tukimpinga. Yatupasa tuvae silaha zote za Mungu. Yatupasa tufuate maagizo tuliopewa kwa njia ya Roho ya unabii. Yatupasa tumtii na kuupenda ukweli wa wakati huu. Kwa njia hii tutaokolewa katika kuupokea udanganyifu ambao MUNGU amezungungumza nasi kwa njia ya Maonyo kwa kanisa, na kwanjia ya vitabu ambavyo vilisaidia kuufanya wazi wajibu wetu wa sasa na hali ambayo tungekuwa nayo. Onyo ambalo limetolewa Mstari kwa Mstari, amri kwa amri lingefuatwa, tusipojali, tutatoa udhuru gani? 8T UK 298, 2K/NJIA SURA 8 UK 51.

      “Nilionyeshwa kuwa ushuhuda kwa walaodikia unafaa kwa watu wa MUNGU katika wakati huu… umeazimiwa kuamusha watu wa MUNGU, kuwafunulia kuasi kwao, na kuwaongoza katika bidii ya toba ili wapate kibali kwa kuwamo kwa Yesu, na kufaa kuutangaza ujumbe wa Malaika watatu” 1T UK 186 UFUNUO  3:17-19.

       Kwa namna ya pekee Waadventista Wasabato wamewekwa ulimwenguni kama walinzi na wachukua nuru kwao limekabidhiwa onyo la mwisho kwa ulimwengu unao potea. Juu yao inag’aa nuru ya ajabu kutoka katika Neno la MUNGU. Wamepewa kazi muhimu na nzito sana utangazaji wa jumbe za malaika wa kwanza, wapili, na watatu. Hakuna kazi nyingine yenye umuhimu mkubwa kama hiyo. Hawapaswi kuruhusu jambo lingine lolote kuingilia kati kuwatenga na jukumu hili. 9T UK 19(1909) MATUKIO YA SIKU ZA MWISHO SURA YA 4 UK 41 P.3

      Shetani anajitahidi kwa nguvu zake zote, kuwatenga watu wa Mungu na wajibu wao wa kutangaza ujumbe wa Malaika watatu. Kwa kutumia viongozi wa kanisa wasiojitakasa kwa kutii ile kweli wanaingiza nadharia na mafundisho ya uongo ndani ya kanisa, kwa njia hiyo kanisa litachafuliwa na kunajisiwa.

     Wakati upepetaji utakapoanza kwa uingizwaji wa nadharia za uongo, hawa wasomaji wa juu juu, ambao hawakuweka nanga mahali popote (Maandiko Matakatifu) wako kama mchanga upeperushwao huko na huko. Wanateleza kuingia katika nafasi yeyote ili kuupendeza mwenendo wa hisia zao. MATUKIO UK 162 p.2 SURA YA 12,” “Adui ataingiza nadharia za uongo kama vile kuwa huduma za Yesu. Katika patakatifu hili ni moja wapo ya mafundisho ambayo yatasababisha wengi kujitenga na Imani. MATUKIO SURA 12 UK 63 p.4, EV 224(1905)”

      “Wakiwa hawakuupokea upendo wa ukweli, watachukuliwa katika madanganyifu ya adui, watasikiliza roho zidanganyazo na mafundisho ya mashetani na watajitenga na Imani MATUKIO SURA 12 UK 163 p.3, 6T 401(1900)” YEREMIA 17:12-13.

        “Wengi watasimama katika Mimbari zetu wakiwa wamenyanyua Mienge ya unabii wa uongo mikononi mwao, iliyowashwa kutoka kwenye Mwenge wa shetani ambao ni Mwenge wa jehanamu MATUKIO SURA YA 12 UK 165 p.4, TM UK 409,411(1898)”.

        “Adui amedhamilia kuingiza dhana za uongo ndani ya kanisa la Waadventista Wasabato. Mabadiliko makubwa yatafanyika itakuwa ni pamoja na kuachana na misingi ya Imani yetu, iliyosimama kama nguzo ya kanisa, uasi huu utapelekea kanisa kupangwa upya. Matengenezo haya ya bandia yatakapoanza yataleta matokeo gani? Kanuni za ukweli ambazo MUNGU kwa hekima yake alizitoa kwa kanisa la masalio zitatupwa chini, dini yetu itabadilika. 1SM UK 204 p.2. ”

         Mambo mbalimbali ambayo yamepelekea kanisa la Waadventista Wasabato kupangwa upya ni kuingizwa kwa mafundisho ya kikatoliki na sera za ulimwengu ambazo ni;

IDARA YA WANA WA KIKE NA HUDUMA MIMBARINI

        Haki sawa ni sera ya kiulimwengu iliyojajadiliwa mnamo Mwaka 1995 Beijing China na Getruda Mongela aliyekuwa katibu wa mkutano huo Mkuu wa nne (4) ulimwenguni juu ya habari za Wanawake. Fouth World Conference on Women Beijing China 1995-UNITED NATIONS (4-15 September 1995 Beijing China)

        Baada ya hapo harakati za kuwainua wanawake kuwa na nafasi za madaraka sawa na wanaume zilianza katika mataifa na makanisa. Na shetani kwa sasa amefaulu katika jambo hili maana ulimwengu umekwisha piga hatua na kuiweka siku maalumu katika juma la kwanza la Mwezi watatu kwa kila Mwaka, katika juma hilo Serikali zote na makinisa yote husheerekea likiwemo na kanisa la SDA-GC, wao wamejificha wakiita huduma za wana wa kike, na sabato ya juma hilo huitwa Sabato ya Wanawake Ulimwenguni na wanawake huhubiri Mimbarini.

       Idara hii imetoka ulimwenguni na huenzi Miungu ya kike ya kipagani ambayo wao walikuwa wakiifukizia uvumba Miungu hiyo ya kike. Haki za wana wa kike kanisani zimekuja na sera ya kuhubiri kwenye Mimbari mbele ya wanaume kinyume kabisa na neno la MUNGU. Kama ilivyokuwa siku za Makuhani leo wanaume wanaagizwa na neno la MUNGU”Nataka wanaume wasalishe kila mahali… Wanawake na wajifunze kwa utulivu wakitii kwa kila namna, simpi ruhusa Mwanamke kufundisha wala kumtawala Mwanaume” 1T:2:8:11, 12. Tunapoona wanahubiri na kushika nafasi za utawala ni uasi sawa ni ule uliofanywa na Wanawake wa yuda waliofukizia uvumba Miungu ya kike. “YEREMIA 44:15-30”                                                        

         Shetani kupitia wanawake aliingiza ibada ya kufukiza uvumba kwa Miungu Mingine yaani Malkia wa Mbinguni (Mungu Mke). Katika historia ya Biblia huduma za hekaluni ziliendeshwa na Makuhani waliochaguliwa na MUNGU nao walikuwa ni wanaume M/Walawi 7:35, 8:12, 21:10, Kutoka 40:13-15. siku zetu leo tunaona wanawake wakifanya yaleyale yaliofanywa na wale wanawake wa zamani katika yuda. Kitendo tu cha kufukiza uvumba kilikuwa ni kinyume na maagizo ya MUNGU, na hakuna sehemu yeyote katika Biblia iliyomruhusu Mwanamke kufundisha au kutoa huduma Mimbarini.

     “Nilionyeshwa kwamba roho ya ulimwengu kwa kasi inatia chachu kanisa. Mnafuata njia ile ile waliyoifuata Israeli ya kale. Kuna kuanguka kule kule kwa Mwito wenu Mtakatifu kama watu wa pekee wa MUNGU. Mwashikamana na Matunda ya kazi zisizofaa za giza. Makubaliano yenu ya kuungana kidini na wasio amini yameleta hasira ya Bwana. Huyajui mambo ya Amani yako na kwa haraka yamefichwa usiyaone. Maneno yale yale yalitumiwa kuwaonya Israel iliyoanguka, kukataa kwako kuifuata nuru kutakuweka katika nafasi mbaya Zaidi kuliko Wayahudi “5T PAGE 75-76 (75 p.3)”.

         “Kama Israeli ya kale kanisa limemdharau MUNGU wake kwa kuondoka kwenye nuru likiacha wajibu wake likitumia vibaya upendeleo wake Mkuu kwa kuwa wapekee na safi kwa tabia. Washiriki wake wamevunja Agano la kuishi kwa ajili ya mungu na kwa yeye tu. Wameungana na wabinafsi wanaopenda dunia, kiburi, wanaopenda anasa na vimendelezwa, na KRISTO AMEONDOKA. Roho wake amezimwa katika kanisa.Shetani anafanya kazi bega kwa bega na wakristo wanaokiri Imani lakini ni Maskini wa utambuzi wa kiroho kiasi kwamba hawamgundui” 2T UK 441-442. (441 p.3)

A. MWANAMKE KUFUNDISHA KANISA

    1TIMOTHEO 2:11, 12, 1KORITHO 11:31-35. “Watu wengi hujiona kuwa hawafai eti kwasababu hawana kazi Maalumu kanisani, kwamba hawana kazi inayoonekana wazi ya kuendesha Injili… Mama anaye walea watoto wake na kuwafundisha ukweli, MUNGU humuhesabu kuwa Muhubiri Mkuu kama vile Mchungaji anaye hubiri Mimbarini. MANABII NA WAFALME UK 124 P.2 SURA YA 17, PROPHET AND KING (PK) UK 119 P.1

         Yampasa Mwanamke kushika Madaraka ambayo MUNGU alimwekea tangu zamani sawa na yale ya Mumewe. Ulimwengu unahitaji hakina Mama ambao ni Mama siyo kwa jina tu, bali kwa kweli kama ilivyo maana ya neno lenyewe. Twaweza kusema kuwa kazi zimuhusuzo Mwanamke ni Takatifu Zaidi ya zile za Mwanaume. Basi Mwanamke na afahamu uwakifu wa kazi yake na kwa nguvu na Kicho cha Mungu ashike kazi yake ya Maisha. Hebu awafundishe watoto kwa ajili ya manufaa katika ulimwengu huu na kwaajili ya makao katika ule ulimwengu bora Zaidi… Yampasa kuona kuwa anahaki sawa na Mumewe kusimama karibu naye, akiwa Mwaminifu kwa kazi na wajibu umpasao. Kazi yake katika mafundisho ya watoto wake ni yenye kukuza hali kwa kila jambo na yenye kuadilisha sawa na kazi iwayo yeyote awezayo kufanyia Mumewe… Malaika asingeweza kuomba kazi ya cheo kikubwa Zaidi ya hiyo maana kwa kufanya kazi hii (Mama) humtumikia MUNGU. 1k/NJIA UK 163 p.2, 3, 4.

      Kama watu walio-oa wanakwenda kazini, wakawaacha wake zao kuwatunza watoto nyumbani, Mke na Mama anafanya kazi kamili na kubwa anayoifanya Mume na Baba. Ingawa mmoja yupo katika shamba la umishonari, mwingine ni mishonari wa nyumbani ambaye kujali kwake, shauku na mizigo yake mara kwa mara huzidi ile ya Mume na baba. kazi yake ni kubwa na muhimu, kutengeneza tabia za watoto wake kuwafundisha wawe watumishi hapa, na kuwafanya wafae wakati ujao kuwa na maisha milele. Mume akiwa katika shamba la umishonari linaloonekana anaweza kupata heshima ya watu wakati anayeangaika akiwa nyumbani anaweza asipate sifa yeyote ya kidunia katika kazi. Lakini kama atafanya kazi yake kwa ajili ya mafanikio ya Familia yake, akitafuta kutengeneza tabia zao kwa mfano wa mbinguni Malaika anayetunza kumbukumbu huandika jina lake kama mmoja wa wamishonari wa kuu katika ulimwengu. Mungu atazami vitu kama Mwanadamu mwenye kikomo cha kuona vitu. HUDUMA YA KIKRISTO UK 175 p.1 SURA 21, 5T UK 594, 1K/NJIA UK 165 p.5

B.MWANAMKE KUWA SHEMASI, MZEE WA KANISA (MCHUNGAJI)

  1TIMOTHEO 3:12-13, 3:1-7, TITO 1:5. “Uangalifu katika kuchagua viongozi wa kanisa hebu Bwana awaangazie nia na mioyo ya wale, waliojiungamanisha na kazi takatifu ya Mungu, waone Umuhimu wa wale wanaopaswa kutumika kama Mashemasi na Wazee kuwa wanapaswa kuwa Wanaume safi walioaminiwa na kundi la MUNGU. Yesu anajiita mwenyewe kuwa mchungaji mwema. EG WHITE COMMENTS ON 1TIMOTHEO 3:1-13, SPIRIT OF PROPHET VOL. 3 PAGE 2123, 7BC UK 914 P.11 SURA 17. ”MWANZO 3:16, 1TIMOTHEO 2:12- 1

“…..Lakini baada ya Hawa kutenda dhambi, kama alivyokuwa wa kwanza katika kukosa, Bwana alimwambia kuwa Adamu atakutawala. Aliwekwa chini ya mamlaka ya mume wake, na hii ilikuwa ni sehemu ya Laana. Katika matatizo mengi; Laana imefanya uzao wa mwanamke kuwa na machungu na maisha yake kuwa mzigo….” 3T, 484.1 

“Hawa alikuwa mwenye furaha kamili kuwa kando ya Mme wake katika nyumba yake ya Edeni, lakini, kama akina Hawa wa Kisasa alijisifu kwa kuwa na matumaini ya kuwa juu Zaidi ya nafasi aliyowekewa na MUNGU katika kujaribu kupanda Zaidi ya nafasi yake ya Asili alishushwa chini Zaidi ya nafasi yake ya Asili. Matokeo kama hayo yatafikiwa na wale wasiopenda kwa hiari yao na kwa furaha kushika Majukumu yao katika mpango wa Mungu katika juhudi za kutaka kuwa katika nafasi ambazo Mungu hakuwapangia, wengi wanaacha nafasi wazi ambapo wangekuwa Mbaraka katika kutamani nafasi za juu. Wengi wametoa kafara heshima na hadhi ya kweli kama Mwanamke, na wameacha kile mbingu ilicho wapangia.” WAZEE NA MANABII UK 31p.1 SURA 3, PP (PATRIACHES AND PROPHET) UK 59 p.1

   WAJIBU AMBAO MUNGU ALIMPANGIA MWANAMKE: CHS: UK 25

         i). Kuwalea watoto na kuwafundisha Maadili Mema ya kumcha MUNGU.

    “Mwalimu wa kwanza wa watoto ni mama, katika kipindi ambacho ni rahisi sana kuathiriwa na ushawishi na ambacho ni cha kukuwa haraka elimu yake kwa sehemu kubwa Imo Mikononi Mwa Mama yake. Mama amepewa fursa ya kwanza ya kufinyanga tabia kwa wema ama kwa ubaya anapaswa kuelewa thamani ya fursa hiyo na Zaidi ya Mwalimu Mwingine yeyote yule yafaa awe amestahili kutumia kwa ubora Zaidi. Na bado hakuna mwingine ambaye Mafunzo yake hufikiriwa kwa kiwango kidogo sana huyu ambaye Mvuto wake katika elimu ni Muhimu sana na wenye kwenda mbali sana, ndiye ambaye Msaada wake umepewa jitihada ndogo kabisa.” HELIMU YA KWELI SURA 12 UK 222 p.1, 201 p.1, EDUCATION 275 p.1

“Yokobedi alikuwa mwanamke mtumwa. sehemu ya maisha yake ilikuwa duni, na mzigo mzito lakini hajapatikana Mwanamke Mwingine yeyote ukimuondoa Mariamu wa Nazareti aliyeupatia ulimwengu baraka kubwa Zaidi akijua kuwa lazima mototo wake angekuwa mbali na malezi yake, kwenye malezi ya wale wasiyo mjua MUNGU kwa moyo wake wote alijitahidi kuunganisha nafsi ya Musa na mbingu alitafuta kujenga Moyoni Mwake upendo na utii kwa MUNGU. Na kwa uaminifu kazi ilimalizika, zile kanuni za ukweli ambazo zilikuwa Mzigo wa mafundisho ya mamaye, somo la maisha yake, hakuna mvuto wa baadaye ambao ungemfanya Musa azikane.” HELIMU YA KWELI UK 46 p.3, 42 p.5, EDUCATION 61 p.3, WAZEE NA MANABII UK 228 p.4, PP 243 p.4

        II). KUSHUHUDIA NENO LA MUNGU NYUMBA KWA NYUMBA

“Wengi wanaitwa kuingia shambani na kufanya kazi ya nyumba kwa nyumba, wakitoa Masomo ya Biblia, na kuomba pamoja na walio na shauku. 9T 172”. “Wanawake walio jitoa kweli kweli wanapaswa kufanya kazi ya Biblia nyumba kwa nyumba. 9T 120

     

 

 III). KUSAMBAZA UKWELI KWA NJIA YA VITABU, MAJARIDA, VITINI NA VIJIZUU VILIVYOBEBA UKWELI WA LEO.

“Akina dada wanaweza kufanya kazi kwa ufasaha kwa kutafuta wale watakaoweza kusambaza vijuzuu na majarida, nuru itasambazwa kwenye akili za wengi kwa njia hii. Wapo Wanawake ambao wanajua siri kwa kutaka ukweli uenee kutokana na uzito wa ushuhuda wao. Wamekubali ukweli kwa dhati. Wanazo mbinu, muono na uwezo mzuri, na Watakuwa watenda kazi wenye Mafanikio kwa Bwana wao. Wanawake wakristo wanaitwa kwa ajili hiyo. RH DEC 19, 1878”

“Dada zetu wanaweza kuwa watenda kazi wakubwa katika kuandikia na kuwavuta Rafiki wote wenye hisia za ukweli ambao wamepokea karatasi na vijizuu vyetu… Wanawake walio imara katika utendaji na tabia nzuri wanahitajika, wanawake wanao amini kwamba hakika tunaishi katika siku za Mwisho na kwamba tuna ujumbe Muhimu wa onyo la Mwisho unaotakiwa kutolewa ulimwenguni… hawa ndio wale wanaoweza kutumiwa na Mungu. Kufanya kazi ya vijizuu na umishionari hawa wanaweza kufanya kazi ya thamani kwa namna mbalimbali kwa kusambaza vijizuu na jarida la Sign of times (Alama za nyakati). RH DEC 19 1878

      IV). KUWAHESHIMU WAUME ZAO NA KUVAA KWA HESHIMA NA ADABU: IK/NJIA UK 205.

Mke anapaswa kumheshimu mumewe. Mme anapaswa kumpenda na kumtunza mkewe; na kadri        viapo vya ndoa vinavyowaunganisha kuwa kitu kimoja, kwa hivyo Imani yao kwa Kristo inapaswa kuwafanya wawe mmoja ndani yake: ADVENTIST HOME 114:2, 1PETRO 3:1-6, EFESO 5:22,1KORINTHO 11:3, AH UK 114 P.2, 115 P.3, MATUKIO SURA 6 UK 81 P.2 (3SM 242(1856)), ELIMU YA KWELI SURA 27 UK 202 P.4, IK/NJIA UK 210 SURA 34.

  V). KUFUNDISHA ELIMU YA UPISHI, UKARIMU NA KARAMA YA UNABII.

Tangu zamani wanawake wamekuwa wakimtumikia MUNGU kwa namna mbalimbali, walikuwa watumishi kwenye hekalu kutoka 38:8, Wakati wa yesu walimuhudumia kwa mali zao Luka 8:3, Wakati wa Mitume waliendeleza karama ya kumtumikia MUNGU. Matendo 9:35-40, Warumi 16:1-2, Kwa karama ya unabii walitumika. Waamuzi 4:4 Debora aliwaamuru watu chini ya mtende kutoka 15:20, Miriam aliongoza wanawake kuimba, na Musa aliongoza taifa zima kuimba kutoka 15:1-19, Ana alitoa Unabii Luka 2:36, wakati wa Mfalme Yosia, Hulda alitoa Unabii 2falme 22:14-19, Mabinti wa Filipo walikuwa Manabii Matendo 21:9-14. Hata wakati za Wa-adventista Wasabato MUNGU alimtumia E.G.W kwa karama ya unabii kwa ajili ya kulielekeza kanisa, kulionya na alitabiri mambo mengi yatakayo tokea kanisani na ulmwenguni. Mengi yamekwisha timia na yataendelaekutimia. Kati ya Wanawake wote hao hakuna hata mmoja aliyefanya kazi ya Ukuhani, uongozi, Kuwa mzee wa kanisa, Shemasi au wadhifa wowote wa utawala kanisani.

WANAWAKE KUWEKEWA MIKONO YA KUWA MASHEMASI NA WACHUNGAJI

    Hakuna jambo la hatar kama hili la kuwawekea Mikono Wanawake Kushika nyadhifa hizi kanisani, Ni UASI wa kupindua Mpango wa MUNGU. NI kuwakosesha watu na kuharibu njia ya mapito ya zamani ya watu wa MUNGU “MWANZO 3:16, 18:19, YEREMIA 6:16, WAEBRANIA 13:7

    Katika historia ya kanisa la MUNGU hakuna sehemu yeyote katika Maandiko Matakatifu ambayo wanawake waliwekewa Mikono yakuwa Viongozi. UASI huu wa kuwawekea Wanawake Mikono ulijadiliwa na kupitishwa na viongozi wa General Conference (GC) Mwaka 2010 nakuingizwa ndani ya kanisa, Soma kanuni ya kanisa TOLEO LA 18 SAHIHISHO LA 2010.

   “Huduma ya kuwawekea Mikono Mashemasi Wakike. Huduma hiyo haina budi kufanywa na Mchungaji aliyewekewa Mikono Mwenye cheti hai kutoka Conference. Huduma ya kuweka Mikono haina budi kuwa sahihi na ifanywe mbele ya kanisa. Kanuni ya Kanisa UK 86.” Maelekezo haya ya GC  ya kuwawekea Wanawake mikono yanapingana na ushuhuda wa roho ya unabii na Biblia

  “Sipendekezi kwamba Mwanamke atafute kuwa mpiga kura wala kushika wadhifa wa Ofisi; lakini akiwa kama Mmishonari, akifundisha ukweli kwa njia ya Majarida, kwa kusambaza Vijuzuu na Majarida yaliyobeba ukweli wa leo anaweza kufanya kazi kubwa Zaidi. HUDUMA YA KIKRISTO UK 19 P.4, CHS 28 P.4 SURA 1” MATENDO 6:5-6, 14:23.

    “Wale wanaofikiria kwamba wameitwa kutetea harakati za kutafuta haki za wanawake na kile kinachoitwa Matengenezo ya Mavazi hawataweza kuunganika katika utangazwaji wa ujumbe wa Malaika watatu. 1T UK 421 p.4

    “Kuna umuhimu wa kutosha na ulazima wa kazi katika ulimwengu huu wenye uhitaji na kuteseka pasipo kupungukiwa na thamani kwa Uzuri na kujionyesha… Wakati MUNGU alipomuumba Eva hakupanga Eva awe chini au juu ya Adam kimamlaka bali katika mambo yote atakuwa sawa naye. Wazazi wetu wa kwanza wasingekuwa na Mipango inayojitegemea kila mmoja wala kila mmoja asingekuwa na mawazo binafsi na kutenda kwa Ubinafsi; lakini baada ya Eva kutenda dhambi, kama alivyokuwa wakwanza kukosa Bwana alimwambia kuwa Adam atakutawala. Aliwekwa chini ya mamlaka ya mume wake na hii ilikuwa ni sehemu ya laana. 3T 484 P.1”

    “Mstari unaotofautisha kati ya wanaodai kuwa wakristo na Makafiri sasa haiwezekani kutofautisha. Washiriki wa kanisa wanapenda yale ambayo ulimwengu unayapenda na wako tayari kujiunga nao, na shetani anadhamiria kuwaunganisha katika kundi moja na kwa kufanyia hivyo anaimarisha kazi yake kwa kuwaswaga wote katika safu za UMIZIMU. Wakatholiki ambao wanajivuna Miujiza kama Ishara Maalumu ya kanisa la kweli watadanganyika kwa urahisi na uwezo wa utendaji huu wa ajabu; na Waprotestant wakiwa wameshatupa tayari ngao ya ukweli nao pia watadanganyika. Wakatholiki, Waprotestant na Wapagani wote kwa pamoja watakubali kuwa na mfano wa utauwa tu bila nguvu na wataona katika Muungano  Maendeleo Makubwa ya kubadilika kwa ulimwengu na kuanzisha milenia iliyo tarajiwa kwa muda mrefu. PAMBANO KUU UK 588(KINGEREZA) UK 481(KISWAHILI P.2)”

Bima ya maisha ni  sera ya ulimwengu inayoondoa utegemezi wa Mwanadamu kwa MUNGU wake juu ya ulinzi wa maisha yake, utendaji wa kazi yake ya Injili, Na kuweka kikwazo kikubwa, kinacho kwamisha kazi ya MUNGU  kwa kujiungamanisha pamoja katika biashara na ulimwengu.SPIRIT OF PROPHECY VOL 2550

     Nilionyeshwa kwamba Wa-adventista Wasabato hawapaswi kujiunga na bima ya maisha. Hii ni biashara ya ulimwengu ambao Mungu hakuithibitisha. Wale wote wanaojiingiza katika biashara hii wamejiunga na ulimwengu wakati Mungu anawaita watu wake watoke na kujitenga nao, Malaika alisema “Kristo amewanunua ninyi kwa kafara ya maisha yake, vipi? Hamjui yakuwa miili yenu ni hekalu la Roho Mtakatifu aliye ndani yenu ambaye ni Wa mungu, na sio wenu! Kwa maana mlinunuliwa kwa thamani kwa hiyo mpeni utukufu Mungu katika miili yenu, na ndani ya roho zenu ambavyo ni vya Mungu. Kwa maana mmekufa na maisha yamefichwa katika kristo ndani ya Mungu. Wakati kristo ambaye ni uhai wenu atatokea, ndipo mtatokea pia pamoja naye katika utukufu. Hii ndiyo bima pekee ya maisha ambayo mbingu inakusudia. 1T 176-177, LIFE INSURANCE, 1T 550 SURA 96, Warumi 14:7-8, 1PETRO 1:17-19, 1KORITHO 6:19-20, 1KORITHO 7:23” warumi 14:7-8  1 petro 1:17-19  1 korintho 6:19-20, 7:23, 1T 549.2, 1T 176-177 p.1-3, 1T 550 p.1-3 SURA 96. “Wanafunzi walipaswa kuendele kazi yao mbele kwa jina la Kristo. Kila neno na tendo lao lilikuwa kuzingatia jina Lake, kama kuwa na nguvu hiyo muhimu ambayo wenye dhambi wanaweza kuokolewa. Imani yao ilikuwa kwa kuzingatia yeye ambaye ndiye chanzo cha rehema na nguvu. Kwa jina lake walipaswa kuwasilisha maombi yao kwa Baba na wangepokea jibu.walipaswa kubatiza kwa jina la Baba,Mwana na Roho Mtakatifu.Jina la kristo lilikuwa liwe neno lao la kutazama alama yao ya kutofautisha, kifungo chao cha umoja, mamlaka ya mwenendo wao, na chanzo cha mafanikio yao.hakuna kitu ambacho kilitambulika katika ufalme wake ambacho hakikuchukua jina lake na chapa yake.”ACTS OF THE APOSTLES 28p.2        

Bima ya maisha ni sera ya ulimwengu ambayo imeingizwa kanisani na ni sera inayo haribu utaratibu wa Injili. Mtu hawezi kufanyia kazi ya kupeleka injili kutoka sehemu moja kwenda nyingine bila kulipia bima, hakuna sehemu yeyote katika historia ya maandiko Matakatifu ambapo watu wa MUNGU walipeleka injili kwa kulipa Bima, kulipa Bima ni kinyume na mpango wa MUNGU. 1T 550 P.1, 1PETRO 2:9-10, YAKOBO 4:4

Bima ya Maisha ni Mpango wa shetani wa kuondoa unyenyekevu na upekee wa Wa-adventista Wasabato na kuungana na Ulimwengu 1T550 p.2

Ni mpango wa shetani kuleta udanganyifu na kuweka watu katika hali ya mzubao ili washindwe kufahamu nini kinacho ukumba ulimwengu, na wao wenyewe kushindwa kujiandaa kwa ajili ya marejeo ya Kristo 1T 550 p.3

MFUMO WA KANISA LA MUNGU.

  Kanisa la Mungu duniani ni chombo kiteule kwa ajili ya Maisha Matakatifu. MUNGU amelipa Kanisa Mamlaka ya kutenda na kuamua kwa ajili ya utukufu wake. Tangu kupaa kwa Kristo kwenda mbinguni Kanisa limekuwa likitenda kwa niaba yake hapa duniani.kanisa ni jumuiya ya watu wawili au watatu wanapopatana katika neno  la MUNGU na kukusanyika pamoja na kumwamini yesu na kushika amri zake, hao ndio Kanisa la MUNGU Duniani hata kama ni wachache ndilo kanisa la MUNGU.

“Mitume walikuwa waangalifu sana kuwazunguka waumini wapya na ulizi wa utaratibu wa Injili. Makanisa yalipangwa na kufunguliwa mahali pote waumini walipotokea. Maofisa wa kanisa walichaguliwa, na mpango kamili wa Kanisa uliimarishwa kwa ajili ya Mambo ya Kiroho ya waumini….PAULO alikuwa mwangalifu sana kuendesha mpango bora wa utaratibu wa kanisa mahali popote makanisa yalipofunguliwa, na yote yaliambatanishwa katika Kristo aliye kichwa cha wote. Hata pale palipo kuwa na waumini wachache tu palifunguliwa kanisa pia na walifundishwa kusaidiana wao kwa wao wakikumbuka ahadi kwamba “Wakusanyika watu wawili au watatu kwa jina langu mimi nipo kati yao” Mathayo 18:20, MAONJO HADI USHINDI UK 79 p.3-4 sura 18

“MUNGU aliweka juu kanisa lake uwezo na hali ya juu kabisa chini ya mbingu. Ni sauti ya MUNGU kupitia watu wake walio na Umoja katika mamlaka ya kanisa ambayo yapaswa kuheshimiwa.” 3T 451 p.1 sura 36.

 

MFUMO WA KANISA LA AWALI (MITUME)

   Baada ya kifo cha Sitefano wanafunzi walisambaa na kukimbia mateso wakaanza kuubiri Injili kwa nguvu na kutii agizo la Yesu, “Enendeni ulimwenguni kote mkahubiri injili”. MATHAYO 28:19-20, MARKO 16:15-16. Makanisa yalianza kufunguliwa na kila mahali na kuongezeka katika idadi ya waumini, na makanisa. Na wote walikuwa na umoja wa Imani, na Mafundisho. WAEFESO 4:1-6. Na mfumo uliendelea kuimarishwa sambamba na utaratibu wa Injili. “EW sura 23”

“Mfumo wa Kanisa kule Yerusalemu ulitakiwa uwe mfano wa mfumo wa kanisa kila mahali ambapo wajumbe wa kweli watakapo ongoa roho katika Injili baadaye katika historia ya Kanisa la awali wakati katika maeneo mbalimbali ya ulimwengu ambapo makundi ya waumini yalipopatikana na kutengeneza makanisa, Mfumo wa kanisa ulizidi kufanywa kuwa kamili kiasi kwamba utaratibu na matendo yenye ulinganifu yaweza kudumishwa. Kila mshiriki alifundishwa kufanya sehemu yake. Kila mmoja alitakiwa kutumia talanta zake kwa hekima.”AA (Act of Apostles) sura 9 UK 91 p.2,Maonjo ushindi UK 29 P.sura9.

  Baraza la makanisa yote ulimwengunii lilikaa Yerusalemu kujadili mada zote za mafundisho na hasa juu ya swala la tohara. Wajumbe walitoka Makanisa mbalimbali yaliyokwishwa funguliwa na Mitume ili kuwakilisha Makanisa yote.

“Sehemu mbalimbali zilisemwa ili kuleta matatizo Barazani, baada ya majadiliano mengi sana, Petro alisimama akasema “ndugu zangu mnajua kwamba mwanzo MUNGU alinichagua kwamba watu wa mataifa wasikie neno la Injili kwa kinywa changu na kuamini.”” MAONJO HADI USHINDI UK 82 P.6 SURA 19, MATENDO15:7

“Roho matakatifu hakuona kuwa inafaa kuwalazimisha waumini wa kimataifa kushika sharia ya Musa kwa hiyo mawazo ya mitume juu ya jambo hili alikuwa tusiwataabishe waumini wakimataifa …… uamuzi huu ulikomesha majadiliano juu ya jambo hili katika jambo hili tunakanusha wazo la kusema kuwa Petro alikuwa ndiye wanayemfuata katika uongozi wa kanisa, Hawana uthibitisho wowote wa maandiko matakatifu kupatana na madai wao. Petro hakuwa mkuu kuliko ndugu zake. Kama wale wanaodai wanamfuata petro, kila mara wengekuwa na ndugu zake, wakibaki kayika hali ya ulinganifu na engine.” MAONJO HADI USHINDI UK 83 P.5, 6 SURA 19

Yakobo alikuwa Mwenyekiti wa kikao hiko cha mjadala huo na hakuna Mwenyekiti wa makanisa kama walivyo wengi leo. Mwenyekiti wa kikao hawezi kuwa Mwenyekiti wamakanisa. Makanisa yalikuwa na viongozi wake ambao n wazee wa Makanisa na Mashemasi. Walipokuwa wakikutana kwenye vikao walikuwa wanamchagua Mwenyekiti wa Barazaa na baada ya kikao kuisha wenyekiti wake. Ulishia hapo hapo utekelezaji wa mipango yote ulibaki kwa mitume na wazee na Mashemasi.

Utaratibu uliofuatwa katika kanisa la kwanza, uliwawezesha kuwa jeshi Imara lisiloshindwa. Waumini ingawa walitawanyika katika sehemu mbalimbali walikuwa na Umoja. Matatizo yalipoteikea mahali pa kanisa Fulani hakuachiwa yaligawe kanisa zima mitume na wazee waliliongoza kanisa kwa ukamilifu.”Maonjo hadi Ushindi UK 42 p.2 Sura 19, Act of Apostles (AA) 95 P.3

“Baraza lililoamua kesi hii lilikuwa la mitume na waalimu waliokuwa nguzo za taifa la wayahudi, na wakristo kutoka makanisa yote kama walivyochaguliwa, kutoka mahali mbalimbali. Makanisa makubwa yote yalikilishwa. Baraza liliendeshwaa kwa utulivu kutoka katika makanisa yaliyofunguliwa kwa Utukufu wa MUNGU. Wote waliona kuwa MUNGU amejibu hoja hiyo kwa njia ya kumwaga roho mtakatifu kwa watu wa mataifa. Sasa ilikuwa sehemu yao kufuata maongozi ya roho.” MAONJO HADI USHINDI UK 84 P.4

Kanisa la Yerusalemu lilikuwa ndio kanisa pekee lililopokea utume  wa injili, na kufungua  makanisa kila mahali ulimwenguni Matendo 1:6-26, Mathayo 28:16-21 katika historia ya kanisa tunaona Umoja wa hali ya juu utaratibu wa kanisa kuwa na amaamuzi ya pamoja. Mfumo huo ndio uliotumiwa na Wa-adventista Wasabato kabla ya kuiga Mfumo wa Ulimwengu yaani utawala wa Msonge. Utawala wa kanisa la MUNGU mamlaka ya maamuzi imo mkononi mwa washiriki wa kanisa huu ndio muundo wa la kanisa la siku za mitume, na Wa-adventista Wasabato wa mwnzo “Wakati Mmlaka ambayo MUNGU amelikabidhi kanisa, yanapotelewa kwa jumla. Kwa mtu mmoja na atakuwa mamlaka ya kuwa mwamuzi kwa niaba ya watu wengine basi utaratibu wa kweli wa Biblia umekiukwa. Juhudi za shetani mawazoni mwa mtu kama huyo zitakuwa za hila nyingi na wakati mwingine karibu zenye kutisha kwa sababu adui atatumaini kwamba kupitia kwa mawazo ya mtu huyo ataweza kuwageuza wengine wengi. Hebu tuto kwa mamlaka ya juu kabisa katika kanisa. Kile ambacho tunataka kumpa my mmoja au kikundi ha watu.” 9T UK 261 P.1

 Ni kwa jinsi gani kanisa la Wa-adventista Wasabato leo limegeukia mbali na kuacha mfumo aliounzaisha MUNGU kupitia kanisa la Mitume utakao dumisha kazi yake hata mwisho? Kanisa kwa sasa limekuwa taasisi mpya, Shirika jipya la dini ambalo utaratibu wa zamani (Mfumo) ulioliwezesha kanisa kusimama imara na kulifanya kuwa la pekee ulimwenguni umeachwa.

“Adui amedhamiria kuingiza dhana za uongo ndani ya kanisa la Wa-adventista Wasabato. Mabadiliko makubwa yalifanyika itakuwa ni pamoja na kuachana na misingi ya Imani yetu, iliyosimama kama nguzo ya kanisa.uasi huu utapelekea kanisa kupagwa upya. Matengenezo haya bandia yatakapoanza yataleta maokeo gani? Kanuni za ukweli ambazo MUNGU kwa hekima yake alizitoa kwa kanisa la masalio zitatupwa chini. Dini yetu itabadilika kanuni kuu ambazo zimeendimisha kazi ya MUNGU kwa Zaidi ya miaka 50 zitaonekana kama zilikosewa. Shirika jipya la dini litaanzishwa.vitabu vyenye mabadiliko mapya vitaandikwa na mfumo wenye falsafa ya kisomi utaanzishwa. Waanzilishi wa mfumo mpya watakwenda kwenye mji na kufanyia kazi ya kutisha. Sabato haitachukuliwa katika uzito wake na hata yule aliyeitoa. Hakuna mambo ya zamani yatakayo simama katika mfumo huu mpya. Viongozi hawa watawatazimisha waumini kwa watu badala ya MUNGU, watajenga mfumo wao katika mchanga na tufani na dhoruba itafagilia mbali nyumba zao.” 1SM 204 P.2 SURA 29

  Moja ya mambo yaliyopelekea kanisa kupangwa upya ni pamoja na kuweka mfumo wa msonge na kuweka makao makuu ya kanisa ulimwenguni. “Imani ambayo kwa muda karne nyingi ilishikiliwa na kufundishwa na wakristo wakialdensis ulitofautiana kabisa na mafundisho ya uongo yaliyotoka rumi. Imani ya dini yao ilipatikana katika neon la MUNGU lililoandikwa, ambao ni mfumo wa kweli wa kikisto. Lakini hawo wakulima  wanyenyekevu, katika makimbilio yao ya faragha, wakiwa wamejitenga mbali na ulimwengu na kulazimaka kila siku kufanyia kazi za taabu katika makundi ya mifugo yao na katika mashamba yao wao hakuweza kufikiwa na upinzani uliotokana na  Dogma na uzushi wa kanisa liloasi. Imani yao haikuwa Imani mpya iliyopokelewa.imani ya dini yao ilikuwa urithi kutoka kwa baba zao. Walipambana kwa ajili ya Imani ya kanisa la mitume, Imani waliyo kabidhiwa watakatifu mara moja tu.  “Yuda 1:3” kanisa lililoko jangwani lilikuwa ndio kanisa la kweli la kristo, Mlinzi wa hazina za ukweli ambao MUNGU amewakabidhi watu wake kwa ajili ya kuzitoa kwa ulimwengu, wala sio lile lenye mfumo msonge wa utawala wakiburi na majivunio lililoweka makao yake makuu ulimwenguni.” PAMBANO KUU UK 51 P.3 SURA 4 GC UK 64 P.2

“Roho ya kuyaunganisha na ulimwengu inavamia makanisa mahali pote katika ulimwengu wa kikristo. Robert Atkins, katika hotuba yake iliyohubiriwa London, Kuhusu picha ya giza la kiroho linaloenea uingereza: “Haki ya kweli imetoweka duniani, na hakuna mtu anayelitia moyoni. Maprofesa wa leo wa dini katika kila kanisa, ni wapenda ulimwengu, wanafuata ulimwengu, wanapenda faraja za watu, na watafutaji wa heshima. Wanaitwa kuteseka pamoja na kristo, lakini wananywea kwa kushutumiwa tu…. UASI, UASI, UASI unachongwa kwenye makao makuu kabisa ya kila kanisa, Na kama wangelijua hilo, na kama wangeliona hilo, kungekuwepo na tumaini, lakini loh!  Wanapiga kilele, tumetajiri, tuna mali nyingi na hatuna haja ya chochote. ” PAMBANO KUU UK 370 P.3 SURA 21 GC 388 P.1

“Kadri moyo wa mwanadamu unavyo sukuma damu katika kila sehemu ya mwili ndivyo uongozi wa mahali hapa, Makao Makuu ya kanisa letu unavyo athiri jamii nzima ya washiriki, ikiwa Moyo una afya njema basi na damu inayozunguka mwili wote ni safi, lakni iwapo chemichemi ni; chafu viungo vyote vitaugua kwa ajili ya sumu iliyo katika damu, ndivyo ilivyo kwetu pia kama chanzo cha Makao Makuu ya kazi yetu kitachafuka; kanisa zima katika matawi yake mbalimbali na mipango iliyo enea katika uso wa dunia itaathirika hatimaye.” 4T 210 P.4 SURA18, “4T 210 P.5””. “Kazi kubwa ya shetani ipo katika makao makuu ya Imaniyetu.”

Kitendo cha kuanzisha makao makuu Duniani, kanisa lilifungua mlango kwa shetani kuingia na kuanza kufanyia mabadiliko makubwa kupitia sauti ya kiongozi aliyepewa mamlaka ya kuwa msemaji Mkuu na kwa njia hiyo tunayaona mambo mengi yeingizwa kanisani yakiwemo hayo ambayo tumeyaorodhesha.

“Watawala, Wanasiasa, Madaktari, Wanasheria, Wafanyabiashara, wote walijiunga na kanisa kama washirika, ili iwe njia ya kuendeleza mambo yao ya kiulimwengu. Halmashauri za kanisa zilikuwa zikiongozwa na makafiri hao ambao walifanya kana kwamba ni waongofu wa kweli hukuwakitafuta anasa za ulimwengu. Makanisa makubwa, maridadi sana yaliyojengwa Wachungaji hodari ambao amabo kazi yao hasa ilikuwa kuwaburudisha watu, walikuwa wakilipwa mishahara mikubwa sana. Mahubiri yao yalikuwa ya kuwaburudisha tu wasikilizaji. Hivyo dhambia zilifichika chini ya uonngofu wa mfumo tu.”PAMBANO KUU UK 223 P.1 SURA 21, PAMBANO KUU UK 322 P.2, GC 88 P.1 SURA 21

  “Kama misingi ikiharibika, Mwenye haki atafanya nini?” Zaburi 11:3

     Wakati kanisa linapoacha kutii Neno la MUNGU na kushikilia mapokeo na desturi; Waaminifu huitwa kujitenga na mfumo wa kanisa Asi.Kama vile ambavyo tumeona kanisa la Wa adventista wasabato wa chini ya taasisi ya General Conference (GC) wameshikilia mafundisho potofu yaliyo kinyume na neno la MUNGU “YUDA 1:3-4, 17-19”

        “Bwana yesu daima atakuwa na watu wake wateule kumtumikia yeye, wakati wayahudi walipomkataa kristo Mfalme wa uzima, aliuondoa ufalme wa MUNGU kutoka kwao na kuwapa watu wa Mataifa. MUNGU ataendelea kutenda kazi kwa kutumia kanuni hii kwa kila tawi la kazi kwa yake, wakati kanisa linapodhihirika kutokuwa na uaminifu. Kwa neno la Bwana; Ijapokuwa msimamo wao uweje, ijapokuwa wito wao uwe wajuu na mtakatifu Kiasi gani, Bwana hawezi kuendelea kutenda kazi pamoja nao. Wengine huchaguliwa kushika majukumu haya muhimu Lakini na Kama hao nao hawajasafisha maisha yao kuondokana na kila tendo baya. Kama hawakuzi kanuni safi na takatifu katika mipaka yao yote ndipo Bwana kwa masikitiko atawapa mateso na kuwanyekeza na wasipotubu atawaondoa kutoka katika mahali pao na kuwafanya kuwa karipio na aibu.”  MATUKIO SURA 4 UK 54 P.2, 3MR.VOL 14 UK 102 P.1, MR (MANUSCRIPT RELEASE), WARUMI 11:17-21,1SAMWELI 2:30

“Baada ya mda mrefu na Mapambano makali waaminifu wachache waliamua kuvunja umoja wote na kanisa Asi kama linaendelea kukataa kujiondoa lenyewe kutoka kwenye uongo, na Ibada ya Sanamu.Waliona kwamba hutengano ulikuwa lazima ufanyike kama wangetaka kulitii neon la MUNGU. Hawakuthubutu na kuweka Mfano ambao ungehatarisha Imani ya watoto wao na wajukuu wao. Ili kupata amani na umoja walikuwa tayari kukubali kufanya Mapatano yeyote kwa unyoofu na MUNGU; Lakini waliona kwamba hata amani ni ya thamani ndogo mno kununuliwa kwa kutoa mhanga kanuni. Kama umoja ungeweza kupatikana tu Kwa kuhasatarisha ukweli na haki, Hebu kuwepo utengano na hata kwa Vita. PAMBANO KUU SURA 2 UK 36P.3, PAMBANO KUU SURA 2 UK28 P.1 GREAT- CONTROVERSY UK 45 P.3”

“Miongoni mwa wale waliopinga ujitwaliaji usio halali wa utawala wa upapa, waldense walikuwa mstari wa mbele…. Hata hivyo walikuwepo baadhi waliokataa kusalimu amri Kwa mamlaka ya upapa, au ya Maaskofu. Walidhamiria kudumisha uaminifu wao Kwa MUNGU na kulinda usafi na unyofu wa Imani yao. Ndipo utengano ukatokea. Wale walioshikilia Imani ya awali sasa walijitenga; baadhi walihamia kwao katika milima ALPS, wakainua bendera ya ukweli katika nchi za kigeni; wengine wakakimbilia sehemu za faragha za mabonde membamba na katika majabali imara kabisa ya milima, na huko walitunza uhuru wao wa kumwabudu MUNGU. PAMBANO KUU, UK 51 P.2, UK 39 P. GREAT CONTROVERSY UK 64 P.1

Mwenyewe kwamba inapaswa kuthubutu kusimama peke yangu kupingana na upapa na kumhubiri kuwa ni Mpinga KRISTO…. Pambano kuu UK 118 P.1, UK 84 P.6, Great Contro versy UK 143 P.1 Sura 7.” “Luther alifanya Uamuzi wake wa mwisho wakutengana na kanisa kwa mashindano ya kutisha. Ulikuwa wakati huu alipoandika kwamba: ”Kila siku ninaona jinsi ilivyo vigumu kabisa kuacha aibu ambazo mtu amezihifadhi akilini katika utoto.Lo! ni Mamivu kiasi gani niliyopata ingawa nilikuwa na Maandiko yakiniunga Mkono, kuutetea uamuzi huo na kujithibitishia

Wakati wapritan kwa mara ya kwanza taifa lalazimika kujitenga kutoka kwenye kanisa la kingereza (Angilikana), walijiunganisha pamoja wao wenyewe kwa Agano Kuu la “kutembea pamoja katika njia zote za Bwana zilizo funuliwa au zitakazofunuliwa kwao kama watu wa Bwana walio huru.Pambano Kuu UK 247 P.1, UK 171 P.3 Sura16, Great Controversy uk 291 p.3”

“Ee Yerusalem, Yerusalem, Uwauae Manabii na kuwapiga kwa mawe wale waliotumwa kwako! ni mara ngapi nimetaka kuwakusanya pamoja watoto wako kama vile kuku avikusanyavyo pamoja vifaranga vyake chini ya mbawa zake, lakini hamkutaka.”katika maombolezo ya kristo moyo wa  MUNGU uliguswa. hivyo ulikuwa Kwa heri ya kisirisiri ya uvimilivu wa upendo wa MUNGU.Mafarisayo na masadukayo walinyamazishwa kimya.Yesu aliwakusanya wanafunzi wake wakatoka hekaluni, akiwa sio kama mtu aliyeshindwa, bali kama ambaye ametimiza kazi yake. Aliondoka akiwa Mshindi toka katika mapambano .Katika siku hiyo ya ajabu katika mioyo mingi mawazo mapya yalichipuka, na historia mpya ikaanza baada ya kusurubishwa na kufufuka. Watu hawa walijokeza mbele wakiwa na hekima na bidii ….. Lakini Israeli Kama taifa lilikuwa limejitenga toka Kwa MUNGU akiangalia ndani ya hekalu Kwa mara ya mwisho, yesu alisema Kwa huruma na kuomboleza angalieni nyumba yenu mmeachiwa hali ya ukiwa.Kama vile mwana wa Mungu alivyo zitoka zile kuta utukufu wa kuwepo MUNGU Utaondolewa milele kutoka katika hekalu lililojengwa kwa ajili ya utukufu wake”. TUMAINI LA VIZAZI VYOTE UK 348 P.1-4 UK 310 P.1-4 DA 620 P.1-4 SURA 67. ”

“Wakati kazi yake ilipolenga kujenga Makanisa kwa mda kitambo ilipendwa. Lakini wakati wachungaji na viongozi wa dini walipokataa fundisho la Marejeo na kunuia kukomesha na kuzima hamasa na majadiliano yote ya mada hii, hawakuipinga kwenye Mimbari tu, bali waliwanyima washiriki wao furusa ya kuudhuria Mahubiri juu ya kuja mara ya pili au hata kuzungumzia tumaini lao katika Mikutano ya Jumuiya za kanisa hivyo ndivyo wahumini walivyojikuta katika jaribu la mfadhaiko, mkanganyiko na upinzani mkali. Waliyapenda makanisa yao na hawakutaka kutengana nayo; Lakini walipoona ushuhuda wa neno la MUNGU ukinyamazishwa na haki yao yakuchunguza unabii ikizuiwa waliona kwamba uaminifu wao kwa MUNGU unawazuia kutii, wale waliotafuta kufungia nje ushuhuda wa neno la MUNGU hawawezi kuhesabiwa kuwa Miongoni Mwa wanao lifanya kanisa la kristo kuwa nguzo na umoja wa ukweli.Hivyo walijiona kuwa na sababu ya kujitenga kutoka kwenye Mathehebu yao ya Zamani. Katika Majira ya joto ya Mwaka 1844 karibu waumini 50 elfu waliondoka kutoka Makanisani.” PAMBANO KUU UK 314 P.3, UK 217 P. 3, GREAT CONTROVERSY UK 376 P.1 SURA 21

“Kwa kila kizazi historia ya kristo kujitenga na yuda zilitangazwa. Wakati watengenezaji wa dini walipohubiri neno la MUNGU, hawakuwa na wazo la kujitengana na yuda lakini viongozi wa kanisa hawakukubaliana na nuru hiyo mpya; na hao waliokuwa na nuru hiyo walipaswa kutafuta. Watu wanao kubaliana na ukweli huo. Siku zetu hizi ni watu wachache tu baina ya wafuasi watenganezaji wa kanisa yaani reformers, husikia sauti ya MUNGU, na kuwatayari kukubaliana na neno linalo hubiriwa.kila mara wale wanaofuata hatua za watengenezaji hulazimishwa la MUNGU; Wengi hutoka na kutengana na Makanisa ya Baba zao, hili wapate kumtii MUNGU: TUMAINI LA VIZAZI VYOTE UK 123 P.3, UK 108 P.5 DA UK 232 P.2 SURA 23.”

“Kulikwepo na kutoka nje, utengano wa kujitenga na waovu uliotolewa Maamuzi, kukimbia ilikuokoa Maisha.Ndivyo ilivyokuwa katika siku za Nuhu; ndivyo ilivyokuwa kwa Luthu; ndivyo ilivyokuwa kwa wanafunzi muda mfupi kabla ya angamizo la Yerusalemu; Na ndivyo itakavyokuwa katika siku za Mwisho. Sauti ya MUNGU inasikika tena ikiwa na ujumbe wa onyo ikiwataka watu wake wajitenge kutoka katika Wimbi la uovu”. WAZEE NA MANABII UK 145 P.1. PATRIACHS AND PROPHET (PP) UK 166 P.4. RH JULY 24 1894 P.2-3

“Nilionyeshwa Masalio wa MUNGU wakilichukua jina Makundi Mawili yalipitishwa mbele yangu. Kundi moja ilikumbatia jamii kubwa ya kikristo. Waliokuwa wakikanyaga sharia ya MUNGU na kutukuza taasisi ya kipapa.Waliokuwa wakitunza siku ya kwanza ya juma kama sabato ya Bwana. Kundi lingine ambao walikuwa wachache kwa idadi, walikuwa wakimsujudia mtoa Sheria Mkuu. Wao walikuwa wakitunza amri ya nne. Upekee na Muonekano wa tabia ya Imani yao ulikuwa utunzaji wa siku ya saba, na kutazamia muonekano wa Bwana wetu kutoka Mbinguni”1 T 223 P.1 SURA 42.

 

Kundi la kwanza seveth day Adventista of General Conference GC

Kundi la pili seventh day Adventista church masalio.

i)Makao Makuu yao yako duniani

“ MUNGU amewakabidhi watu wake kwaajili ya kuzitoa kwa ulimwengu wala sio lile lenye mfumo msonge wa utawala wakiburi na majivuno lililoweka makao yake Makuu ulimwenguni” PAMBANO KUU UK 51 P.1 GC 64 P.2

ii)” Roho ya kufungamanisha na ulimwengu inavamia makanisa mahali pote katika ulimwengu wa kristo…….. Uasi, uasi, uasi unachongwa kwenye makuu kabisa ya kila kanisa” PAMBANO KUU UK 388 P.1 SURA 21.

Kanuni ya kanisa inayobadilika kila baada ya miaka mitano                                                                      

“Kuna wajenzi wa mnara katika wakati wetu….. Katika ulimwengu wa kikristo wengi ugeuka na kuwa mbali na mafundisho ya Biblia yaliyo wazi na kutegemea kanuni kutokana na hadithi zinazo wapendekeza” WAZEE NA MANABII UK 98 P.2, 3 PATRIACHS AND PROPHET UK 124 P.1, 2 SURA 10.

i) Makao Makuu yao yako Mbinguni: 2NYAKATI 30:27 EFESO 2:18-20

“Hebu wote wanaoteswa ama kutendewa hiana wamlilie MUNGU…. Tunamwaga yale maitaji yetu ya moyo katika chumba chetu cha ndani, twayatoa Maombi ya kimya tunapotyembea, na maneno yetu yanafikia kiti, cha Kifalme cha mtawala wa malimwengu. Sala zetu zinaweza kuwa azisikilizani kwa masikio ya wanadamu. Yanapanda juu ya makelele mpaka kufikia makao makuu Mbinguni VIELELEZO VYA MAFUNDISHO YA KIKRISTO UK 124 P.2 SURA 14”.

ii) Kanuni yao ni Biblia na Roho ya unabii

     ISAYA 8:20 UF, 19:9-10, ZABURI 119:129-130, 2

     NYAKATI 20:20

    “ Lakini MUNGU atakuwa na watu wenye kush

      Ika Biblia na mafundisho yake peke kuwa ndio”

     Kanuni ya maisha na msingi wa Matengenezo

     Yote…. PAMBANO KUU UK 339 P.1 SURA 37.

iii)Muongozo wa kujifunza Biblia ( Lesson)

“Kama ingewezekana sehsmu kubwa ya vitabu vilivyokwisha kuchapishwa kutumiwa, baalinaloogofya sana. Watu akilini na Moyoni lingezuiwa hadithi za mahaba, hadithi zisizo na mahana zenye kusisimua pia hadi vitabu vya jamii ile iitwayo hadithi za riwaya za kidini vitabu ambavyo ndani yake. Mwandishi hutia kwenye hadithi yake fundisho la wema na ubaya maneno ya dini yaweza kuchanganywa katika kitabu cha riwaya lakini Mara nyingi shetani hujivika, Mavazi ya Malaika Wema apate kudanganya Zaidi. Hakuna walioimarika katika Mafundisho mazuri wala hakuna wanaosalimika Majaribuni hata wasiweze kuwa hatarini kwa uovu unao haribu hali ya kiroho wenye kuitagiza uzuri wa Biblia huanzisha fadhaa, hitiwa wasiwasi Akilini, hudhofisha Akilini za moyoni zisiweze kuwa na manufaa, huiachisha roho ya mtu Maombi, na kuiharamisha roho kwa ibada yeyote ya kiroho. 1 1 k 191 p.4, uk 192 p.4 CCH UK 168 P.4.”

*kwa mfano angalia Lesson ya Robo ya tatu ya Mwaka 2007: ambayo inanjia: kwa wema au kwa ubaya; Ni laana kwa msomaji.

iii) Muongozo wa kujifunza ni Biblia ni Roho ya Unabii: YOHANA 14:25, YOHANA 16:13, ZABURI 119:167-168, ZABURI 119:129

“Shuhuda hizi zingeingizwa kwa kila watu wa nyumbani washikao sabato, na yapaswa ndugu kujua thamani yao na kuombwa kuzisoma. Haukuwa mpango wa busara sana kuviweka vitabu hivi hesabu ya chini na kuwa na seti moja tu. Kanisa yapasa pawepo katika jamii vitabu (maktaba) ya kila watu nyumbani na kusomwa mara kwa mara. Hebu viweke mahali viwezapo kusomwa na wengi ”1K/NJIA UK 109 P.3, CCH ( COUNCIL TO THE CHURCH) UK 94P.5,5T 681P.2

“Naliitwaa Biblia na kuizinga na hizi shuhuda kwa kanisa, ambazo zilitolewa kwaajili ya watu wa Mungu hapa nikasema habari za watu karibu wote zaguswa. Mashauri mema ambayo hayatamani huweza kupatikana hapa, yametolewa kwa ajili ya mambo ya wengine yakiwa na hali ya kuwafaa wao wenyewe pia. Mungu amependezwa kuwapa amri juu ya amri kanuni juu ya kanuni. 1K/NJIA UK 1164P.4,

 

UKATAAJI NA SHUHUDA

“Jambo moja ni hakika: Wale Wa-adventista wasabato wanaochukua msimamo wa chini ya shetani wataanza kwanza kuikataa Imani inayohusu maonyo na shutuma zilizomo katika shuhuda za roho wa Mungu”MATUKIO YA SIKU ZA MWISHO UK 164 P.1 SURA 12.

“Eleni white alifanya madai kuhusu huduma yake ambayo hayatuachi njia panda, alidaikuona mambo ambayo yangalitokea tu katika muujiza wa uvuvio. Iwe madai yake ni kweli ama alikuwa amechanganyikiwa au muongo mkuu aliweza kudumisha mafundisho yake tangu katikati ya karne ya 19 hadi muongo wa wa pili wa karne 20 (yaani 1844-1915). Nimaelezo gani ya kiakili mtu awezayo kutoa Iwapo atadai kuona Mama White aliyoyaona, akiwa njozini? Alidai kuona watu waishio katika sayari nyingine; na pia wakiwaona malaika wakiwalinda watu wa MUNGU alidai kuona, njozini akiwa yesu katika Patakatifu pa Mbinguni, na uzuri aliokuwa nao shetani kaua ajaanguka alidai kuwaona Malaika wakimtembelea Adam na Hawa bustanini edeni, alidai kuuona uso wa yesu, njozini mara baada ya uzoefu wa kufunga nyikani siku 40 alidai kuona ufufuo wa yesu akitoka kaburini na pia kumuona malaika akiwafungulia Paulo na Sila kutoka gerezani. Mtu hufanyeje na madai hayo? Vipi Kwa wale wanao linganisha huduma yake na ile ya Martin Luther, hakika wanaishi katika ulimwengu wa ndoto yapasa tuwe tunamchukulia kutokana na vile alivyojielekeza (ambapo Hakuzuki Maswali) au tumkatae kama Muongo, aliyechanganyikiwa, au kuvuviwa na yule Muovu. Hizo ndizo baadhi ya hoja za kiakili” LESSON YA ROBO 1 UK 2000, KWA WATU WAZIMA UK 67 P.1-3.

Wa-adventista Wasabato wamechaguliwa na MUNGU kama watu wapekee, waliotengwa na ulimwengu. Kwa kutumia upanga Mkali wa kweli ukatao kuwili amewakata na kuwatenga kutoka kwenye Mafungamano na ulimwengu na kuwaunganisha na yeye mwenyewe.” MATUKIO YA SIKU ZA MWISHO UK 41 P.2 SURA 4, 7T UK 138 (1902), IK/NJIA SURA 7 UK 67 P.4, KUMB 7:6-7

Lesson inataka kuwa sio wa pekee soma “LESSON YA INJILI NA HUKUMU YA 1844 JULY ROBO 3 MWAK 2006 UK 3 P.1. “Kama Wa-adventista, mengi ya mafundisho yetu ya pekee, sio ya pekee, tuliipata hata hivyo, sabato ya siku ya Saba kutoka Kwa Baptist watunza sabato, na isitoshe wapo wakristo wengine, japo siyo wengi wenye kutunza sabato ya siku ya saba ya juma Kutoka 20:20.”

“Sabato ya siku ya Saba ulitolewa na MUNGU Mwenyewe na siyo wabaptist kama wanavyo sema kwenye lesson.”

KANISA KUUNGANA NA MATHEHEBU MENGI

“Kamwe atupaswi kuwa na mapatano na watu.Waabuduo sabato ya Miungu (Jumapili) 2SM 35 P.1. Mstari wa kutenganisha kati ya wanafunzi wa yesu na wa shetani usifutwe’’.5T UK 502P.

    Lessoni ya dini ya mahusiano Robo 3 Mwaka 2oo4 UK 54p.2 Lesson inasema kuwa “Hatatuwe tunawajbika kiasi gani kwa utume wetu, hatupaswi kuelewe ujumbe wetu Zaidi kile unavyoelezea kama kukumbatia Imani kuwa sisi wa-adventista ndio pekee ambao tutaokolewa.Mtazamo huu kamwe haujawahi kuwepo, na wala sasa haupo katika misingi ya Imani kanisa la wa-adventista wasabato:

“Tunayatambua mashirika yenye kumuinua kristo machoni mwa wanadamu Kama sehemu ya mpango wa kimbinguni wa kupeleka habari njema ya injili kwa ulimwengu, natunawaheshimu sana wanaume kwa wanawake katika mathehebu mengine ambao wanashiriki katika kazi njema yakuleta roho kwa kristo” GC WORKING POLICY 1999-2000 UK494 POLICY 0.100 AKTICLE1.

IBADA YA SANAMU NDANI YA KANISA LA WASABATO WA GC

Kanisa kuchora picha za Watakatifu ni kuenzi Ibada za sanamu na machukizo machoni pa Mungu, angalia vitabu vilivyo na upagani wa mapicha ya Watakatifu, Kanisa limefikia hali mbaya na kuharibu mafundisho ya Imani kwa kuingiza Ibada ya Sanamu Kanisani na sasa ni sehemu ya mafundisho ya Kanisa.

Mikutano mbalimbali utaona wanaonyesha picha ya Yesu ya uongo, picha za Watakatifu hata akina Musa, Nuhu, Adam, Eva, Maria, Petro, na Senema za Mitume, Mnabii na watu hawashtuki au kuuliza swali wakati maandiko matakatifu yanakataza kuchonga sanamu na kuchora.

“Sanamu ya kuchora yafaa nini, hata yeye aliyeifanya ameichora? Sanamu ya kuyeyuka, nayo ni mwalimu wa uongo, yafaa nini hata yeye aliyeifanya aiwekee tumaini lake, na kufanyia sanamu zisizoweza kusema? HABAKUKI 2:18-19, KUTOKA 20:4-6, ZABURI 115:2-9. Kwa kitendo hiki Kanisa la Wasabato chini ya GC na Viongozi, Wachungaji, Wainjilisti, Wazee wa Makanisa na Washiriki wote wameungana kuvunja Amri ya pili “KUTOKA 20:4-6” na kushuhudia uongo kwa kusema picha hiyo ni Yesu na mapicha mbalimbali na kuvunja Amri ya tisa “Usimshuhudie jirani yako uongo” KUTOKA 20:16.”

“Wakristo wengi sana hatimaye walikubali kushusha kiwango cha Ukristo wao na Muungano ukafanyika kati ya Ukristo na Upagani. Ingawa waabudu sanamu walijifanya kushilia na kugandama kwenye Sanamu zao, walibadilisha tu vielelezo vyao vya Ibada zao kwa Sanamu za Yesu na hata za Maria, na Watakatifu wengine, chachu mbaya sana ya Sanamu iliingizwa Kanisani kwa njia hiyo, iliendeleza kazi yake ya uovu. Mafundisho ya uongo, desturi za kishirikina na taratibu za vitendo maalumu vinavyoambatana na Ibada ya Sanamu ziliunganishwa katika Ibada za Kanisani”. PAMBANO KUU 34(42-43)

Kanisa la Wasabato chini ya GC         limejiunga na Romani Katoliki kwa kuendeleza Ibada za Sanamu, Sanamu za Kisasa za kupiga picha, kuchora na kunakshi. Ni nani alimpiga picha Yesu, picha Adamu, Ibrahimu, Musa, Isaka na kutunza picha zao huo ni uongo. Yesu mwenyewe alisema “waheri wale watakaoamini bila kuona” YOHANA 20:29, 1PETRO 1:8, 2WAKORINTHO 5:7. Kuchora, kutengeneza senema za mkanda wa maigizo ya Yesu n.k, ni uongo na kumzarau Mungu na kumvunjia heshima. Nani ataondoa uovu na takataka hizi za uchafu? Nabii wa Mungu Ellen G. White anasemaje kuhusu mapicha yanayochorwa kwenye vitabu, picha za Ukatili wa Kirumi na mateso. Ondoa picha za Kikatoliki kwenye vitabu vyetu “CW 172:1”

Picha ya Yesu-CW 171:2-3, 175:4 “Hakuna maonyesho ya kutisha, weka nje vitabu vyenye vielezo vya picha za Kikatoliki za Mateso na kuchomwa moto. Inatosha kusoma juu ya matendo haya maovu bila kujaribu kuyaleta katika maelezo yao yote mabaya mbele ya macho”. Barua 28, 1897 CW UK. 172 aya 1.

“Usahihishaji ni muhimu, je hatupaswi kufanyia uchunguzi kuhusu suala la kuonyesha vitabu vyetu kwa kaisi kikubwa? Je, akili haingekuwa na maono wazi kikamilifu Zaidi ya Malaika, Kristo au kitu chochote cha Kiroho, ikiwa hakuna picha zilizotengenezwa kuwakilisha vitu vya mbinguni? Picha nyingi zilizotengenezwa ni za uongo kabisa. Je, picha ambao zipo mbali na ukweli hazitoi sauti ya uongo? Tunatakiwa kuwa wa kweli katika uwakilishi wetu wote wa Yesu Kristo lakini maandishi mengi ya kusikitisha yaliyowekwa kwenye vitabu vyetu na majarida ni mashtaka kwa umma”. BARUA YA 145, 1899-CW 171.2.

“Mifano inayofaa, mawazo ya wengi katika kurejea mambo yanayohusu kazi ya Mungu ni ya bei rahisi sana. Katika uteuzi wa picha kuonyesha mambo matakatifu ni upungufu wa hekima umeonyeshwa kuwa Mungu hawezi kuubali”. Barua ya 39, 1899 CW 171 aya 3.

“Ndugu zangu, je hamtalipa kundi la Mungu mkate, na sio jiwe? Kamwe usichapishe katika majarida yetu neni ambalo litashusha kiwango ambacho Mungu anatarajia watu wake wakutane. Msimwite mtu yeyote mwenye kipaji ambaye hana hekima ya kumchagua Bwana Yesu Kristo, mwanga na uzima wa ulimwengu, ubora wa mtu huamuliwa na umiliki wake na fadila za Kristo kwa wanadamuwenye dhambi. Ukweli lazima uwekwe mbele ya watu. Kiwango cha usafi, kiasi cha utakatifu lazima kiinuliwe CW, UK 175 aya 4.”

Ondoeni mapicha ya sanamu za kikatoliki kwenye vitabu “2WAFALME 21:1-6, 11-15”, matengenezo yanahitajika kwenye kila msimamo wetu wa Imani “2WAFALME 23:1-14”. Kwani hasira ya Bwana imewaka juu ya watu wake waabuduo sanamu. MATENDO 17:16 “Paulo alipokuwa akiwangojea huko Athene na kuona jinsi mji ule ulivyo jaa sanamu roho yake ilichukizwa sana ndani yake.” “KUTOKA 32:19 Hata alipo yakaribia yale malango akaiona ile ndama na ile michezo. Hasira ya Musa ikawaka, akazitupa zile mbao mikononi mwake akazivunja chini ya mlima. Akaitwaa ile ndama waliyoifanya akaichoma moto, akaisaga hata ikawa mavumbi, akinyunyuzia juu ya maji akawanywesha wana wa Israeli.”

MJADARA KUHUSU KANUNI YA KANISA

Loughborough alipendekeza kwamba kama ndivyo ilikuwa, walikuwa wakifuatisha makanisa mengine kwa kujenga nyumba za mikutano. Alisema, “Tunayaita makanisa Babelii sio kwa sababu wamefanya agano ili kumtii Mungu.” Alirejea nakala ambayo alikuwa ameandika kwa tathmini ambayo aliitangaza: 1BIO 453.1

   Hatua ya kwanza ya uasi ni kuwa na kanuni ya Imani, ikituambia tuamini nini. Hatua ya pili ni kuifanya kanuni hiyo kuwa kipimo cha ushirika. Hatua ya tatu nikuwajaribu washirika kwa kanuni hiyo. Hatua ya nne kuwashutumu kama wazushi wale ambao hawa amini kanuni hiyo. Na hatua ya tano, kuanza mateso dhidi yao.  1BIO 453.2

     Ninahisi kwamba hatufanyi kulingana na makanisa kwa maana yoyote isiyo na sababu katika hatua iliyopendekezwa.-Ibid.1BIO 453.3

    Cornell hakuona kwamba kukubali agano kama hilo ilikuwa nikufanana makanisa Kisha James White alitoa taarifa ya kina na muhimu:

    Nathibitisha, si kwa yale ambayo ndugu wasema, kwa maana nilikuwa nimeshawishika hapo awali. Ningependa kusema nao sasa kuunga mkono azimio hilo. Napendelea kwamba ndugu wanapaswa kuwa kitu kimoja katika jambo hili. Hii ingeleta umoja katika kanisa. Hebu tuweke mfano sahihi hapa, na tuache uende nje ya mkutano huu. Hii ndio sababu moja kwanini nitapigia kura azimio hili 1BIO 453.3

    Kuhusu mada ya kanuni za Imani, nakubaliana na ndugu loughborough. Sikupima vidokezo ambavyo amewasilisha, kama vile nilivyoanza kuchunguza mada hiyo mwenyewe. Katika WAEFESO 4:11-13, tunasoma, “Naye alitoa wengine kuwa mitume, na wengine kuwa manabii, nakadhalika.” Hapa tunakarama za kanisa zilizotolewa. 1BIO 453.6

    Sasa ninachukua msingi kwamba kanuni za Imani zinasimama kinyume kabisa na karama. Hebu tufikirie: Tunapata kanuni, ikisema tutakavyoamini juu ya jambo hili na lile, na tutafanya nini kwa kuzingatia jambo hili na lile, na tuseme tutaamini karama hizo pia. 1BIO 454.1

    Chukulia Bwana, kupitia karama ametupatia nuru mpya haikuendana na kanuni yetu, basi, ikiwa tunabaki thabiti katika karama, inapinga kanuni yetu mara moja. Kufanya kanuni ni kuweka vigingi na kuzuia njia ya maendeleo yote ya baadaye. Mungu aliweka karama kanisani kwa lengo kubwa na zuri, lakini watu ambao wamemiliki makanisa yao, wamefunga njia au wamejiweka nje ya njia za…        Mwenyezi. Sawa nakuwa wanasema kwamba Bwana asifanye chochote Zaidi ya kile ambacho kimewekwa kwenye kanuni. 1BIO 454.2

    Kanuni na karama zinapingana moja kwa moja. Sasa msimamo wetu kama watu ni upi? Biblia ndio kanuni yetu. Tunakataa kila kitu chenye kanuni za kibinadamu. Tunachukua Biblia na karama za Roho; tukishilia Imani kwamba Bwana atatufundisha mara kwa mara. Na katika hili tunachukua msimamo dhidi ya utengenezaji wa kanuni. Hatuchukui hatua moja, katika kile tunacho kifanya, kulekea kuwa Babeli.-1BIO 554.3

Hakuna kosa kama hili la Kanisa la Wasabato chini ya General Conference kuunda kanunu ya Imani kinyume kabisa na Biblia na Roho ya Unabii. Kanuni au muongozo ni mawazo ya nadharia ya viongozi wa juu na huwa zinasahihishwa au kuboreshwa kila baada ya miaka mitano. Neno la Mungu limejitosheleza na hakuna mwanadamu mwenye ruhusa kuliboresha au kulirekebisha, kanuni za Kanisa au makanisa huwa zinaborehswa kulingana na mitazamo ya viongozi wa kanisa kulingana na matakwa yao. “Kila neno la Mungu limehakikishwa; yeye ni ngao yao wamwaminio. Usiliongeze neno katika maneno yake; asije akakulaumu, ukaonekana u mwongo. METHALI 30:5-6, UFUNUO 22:18, K/TORATI 4:2”

“Katika ulimwengu unaodaiwa kuwa wa kikristo wengi hukataa mafundisho ya wazi ya Biblia na kujenga Imani kutoka katika kanuni za mawazo ya kibinadamu na hadithi za kupendeza, na wanaelekeza kwenye mnara wao kama njia ya kupanda juu mbinguni… IKIWA WALE WANAODAIWA KUWA WAFUASI WA KRISTO wengekubali kiwango cha Mungu, ingewaleta katika umoja; lakini maadamu hekima ya mwanadamu imeinuliwa juu ya neno lake takatifu, kutakuwa na mafarakano. Machafuko yalipo ya Imani na madhebu yanayopingana yanawakilishwa vyema na neno Babeli, Ambayo ni unabii (Ufunuo 14:8; 18:2) inatumika kwa makanisa yanayopenda ulimwengu wa mwisho.” Patriarchs and Prophets UK 124 aya 1

 WACHUNGAJI WA MISHAHARA.

“Mtu wa mshahara wala si mchungaji ambaye kondoo si mali yake humwoma mbwa mwitu anakuja akawaacha kondoo na kukimbia, na mbwa mwitu huwakamata na kuwatawanya. Yule hukimbia kwa kuwa ni mtu wa mshahara; wala mambo ya kondoo si kitu kwake”. YOHANA 10:12-13, EZEKIELI 34:1-10, YEREMIA 23:1-4, ZEKARIA 11:15-17, MALAKI 2:1-3.

“Kristo mchungaji mkuu amewaachia watumishi wake waangalizi wa kundi lake kama wachungaji wasaidizi; na anawataka kuwa na majukumu matakatifu kwa kazi aliyowaachia amewaamuru wawe waaminifu, kulinda kundi, kuwatia nguvu wanyonge, kuwaamsha waliozimia na kuwakinga wasiliwe na mbwa mwitu. Ili kuwaokoa kondoo hawa Kristo aliutoa uhai wake na anawaelekeza wachungaji wake katika upendo aliowaonyesha kama mfano kwao. Lakini “aliye wa mshahara; ambaye kondoo siyo mali yake,” hana nia ya kweli kwa kondoo. Anatumika kwa ajili yakupata faida na anajijali yeye mwenyewe, anaangalia matwakwa yake tu. Badala ya kuangalia matwaka ya kundi na wakati wa hatari, atakimbia na kuliacha kundi.” WAZEE NA MANABII UK 172-173 (191P.1-4):1 PETRO 5:2-3. TIMOTHEO 3:3 TITO 1:7, KUTOKA 18-21.  Kwa wale wote walioitwa na kristo kumtumikia yeye katika kazi yake ya wokovu. Hakuwa ahidi mshahara wa aina yeyote kama malipo.

   “Kristo alipowaita wanafunzi wake wamfuate, hakuwatumainisha kwamba watapata cheo na sifa katika maisha haya. Hakuwahidi mapato wala heshima, wala wao hawakuweka masharti juu ya mambo ambayo walitaka kuyapata. Mathayo alipoketi forodhani, mwokozi alimwambia;

  “Nifuate. Akaacha vyote, akaondoka, akamfuata.” (MATHAYO 9:9, LUKA 5:27-28) Mathayo hakungoja na kudai mshahara kadri ya ule alioupata katika kazi yake kama mtoza ushuru, ndipo amfuate yesu, mara moja pasipo kuuliza neno lolote wala kusitasita. Kuwa pamoja na mwokozi apate kuyasikia maneno yake na kushirikiana naye katika kazi yake, ndiyo mambo yaliyomtosha. Vivyo hivyo na wale wanafunzi walioitwa mwanzoni. Yesu alipomwambia petro na wenzake ili wamfuate wakaviacha vyombo na nyavu zao mara.  Wengine walikuwa na jamaa waliowatazamia kwa riziki zao; lakini waliposikia mwito wa mwokozi, hawakusitasita na kuuliza nipateje riziki na nitawezaje kuwasaidia jamaa zangu? Waliitikia mwito huo na baadaye Yesu alipowauliza, “Je? Nalipowatuma hamna mfuko wala mkoba, wala viatu, mlipungukiwa na kitu?” Waliweza kusema “LA?” LUKA 22:35, WAJUMBE WA KRISTO UK 31P.1-2, HUDUMA YA UPONYAJI UK 479 P.3-4: SURA 40, TUMAINI LA VIZAZI VYOTE UK 147P.4-5 SURA 28 DA (DESIRE OF AGES) UK 273P. 2-6 SURA 28

    Wachungaji wote wanaofanya kazi na huku wanalipwa mishahara, Hawamtumikii MUNGU. Bali MUNGU wao ni tumbo: WAFILIPI 3:18-19 “Maana wengi huenenda, ambao nimewaambieni mara nyingi habari zao, na sasa nawaambia hata wa machozi, kuwa ni adui za msalaba wa kristo; mwisho wao ni uharibifu mungu wao ni tumbo, utukufu wao u katika fedheha yao waniao mambo ya duniani. ”, WARUMI 16:17-18, MIKA 3:5 “Bwama asema hivi katika habari za manabii wanaowakosesha watu wangu; hawa waumao kwa meno yao, na kulia, Amani; na mtu awaye yeyote asiyetia kitu kinywani mwao, wao humwandalia vita.”

   “Tofauti kubwa kati ya roho ya watu waliotengeneza maskani jangwani na wale waliojenga hekalu la sulemani, inatufundisha fundisho muhimu watu waliojenga hekalu ambao walikuwa wakitufuta faida yao wenyewe walikuwa na tabia iliyo ya watu wengi leo, ambao hujipenda nafsi zao tu, wenye kutafuta vyeo na mishahara mikubwa. Roho yakujitolea kwa hiari kufanya kazi kama ile iliyoonekana wakati wakutengeneza maskani imeadimika mno hasa. Lakini roho ya namna hiyo ndiyo inayotakiwa wafuasi… wa wakristo kuwa nayo. Bwana wetu ametuonyesha mfano wa jinsi ipasavyo wanafunzi wake kufanya kazi. Kwa wale wanaowaita na kusema kwamba: “nifuateni, naminitawafanya kuwa wavuvi wa watu,” Hakuwa ahidi mshahara wa aina yeyote kwa ajili ya kazi yao. Yawapasa kushiriki kijikana kwake na kujinyima.” MANABII NA WAFALME UK 32P.3, SURA 4, UK 29P.3, PROPHETS AND KING UK 64P.3 SURA

Hiramu alikuwa mfalme wa Tiro na alikuwa mjuzi wa kazi ya ufundi stadi za kuchora. Hiramu alizaliwa na wazazi mchanganyiko (mama yake alikuwa mwisraeli wa kabila la dani, Baba yake alikuwa mtu wa Tiro) Hakuwa na sifa njema ndiyo sababu ya yeye kufanya kazi kwa kudai mshahara. Kitendo cha kuchanganya mafundi wa Israeli na mafundi wa kutoka Tiro kulileta chachu mbaya kwa wajenzi kutaka mshahara, walidai mishahara mikubwa. 1FALME 5:1-2, 6

   “Hivyo, aliyekuwa msimamizi wa wafanyakazi wa Sulemani, alikuwa mtu aliyekuwa akifanya kazi kwa kujitumikia mwenyewe. Hakumtumikia Mungu. Kwa moyo ya kujinyima.Yeye alimtumikia mungu wa dunia hii, yaani mali. Makusudi ya maisha yake yote yaliongozwa na kujipenda nafsi. Kwa ajili ya ufundi wake mkubwa, Hiramu alidai mshahara mkubwa sana mwishowe hali yake ya uroho wa fedha iliwaambukiza wenzake pia. Kwa vile walivyokuwa wakifanya kazi pamoja kila siku na kulinganisha mshahara wake na mishahara wao, mwisho hata wao wakapotoka, wala hawakuhesabu kazi yao kuwa ni kazi takatifu. Roho ya kujinyima ikawatoka na badala yake wakawa na roho ya uroho wa fedha. Matokeo yakawa kudai mishahara mikubwa, ambayo walipewa. Hivyo basi mvuto mbaya huo ulienea katika sehemu zote za kazi ya Bwana, hata kuenea popote katika ufalme wake. Mishahara mikubwa uliyodaiwa na kupeana iliwafanya watu wengi waishi maisha ya anasa sana na starehe. Watu maskini walionewa na matajiri; na roho ya kujinyima ilitoweka kabisa haki hii ya upotevu, iliyoenea pengi sana; mtu ambaye apo mwanzo alikuwa miongoni mwa wenye hekima yakutisha, aliyewapita wote, na sasa amekuwa Mwaasi”. MANABII NA WAFALME UK 31P.4-3 2P.1-2 UK 28P.3-5, ISAYA 56:10-12, PROPHETS AND KINGS UK 63P.3-64P.2 SURA 4

Wale wanaolipwa leo na kudai mishahara wanafuata roho ile ile ya Hiramu. Badala ya kufuata tabia ya Yesu na mitume wake na ile ya wale waliojenga hema Kule jangwani. Mungu anaitaji watumishi waliojitoa wakfu na kujikana nafsi. MATHAYO 16:24-29, 10-38, LUKA 9:23. “Akawaambia wote, mtu yeyote akitaka kunifuata, na ajikane mwenyewe, ajitwike msalaba wake kila siku, anifuate

    “leo mwokozi anatuita sisi pia, kama vile alivyomuita Mathayo, Yohana, na Petro. Naikiwa tumeguswa moyoni na upendo wake, hatutafikiri sana jambo la malipo na ridhaa.  Tutafurahi kuwa watendakazi pamoja na kristo, na tutatumaini ulinzi wake bila hofu. Tukimfanya Mungu kuwa nguvu zetu, tukifahamu dhairi wajibu wetu utupasao tutakuwa na moyo wa kuwapendelea wengine kuliko mwenyewe tutaongozwa na nia iliyo bora ambayo itatuinua hali ya moyoni tusiwe na nia yakutaka mambo afifu ya dunia hii.” WAJUMBE WA KRISTO UK 31P.3 SURA 8

      “Wachungaji wa leo wanalipwa mishahara kwa zaka wakisema wao ni makuhani. Makuhani na wachungaji ni huduma mbili tofauti. HESABU 18:21-24 makuhani walikaa hekaluni siku zote na hawakuwa na urithi wala mashamba wao walihudumu hekaluni, wakati wachungaji wanamiliki nyumba na wengine ni wafanya biashara na wanamiliki mashamba na magari n.k. Wakati wa huduma ya kikuhani makuhani walikula zaka na matoleo yaliyotoka kwa waisraeli. Pia wale waliohudumu kwenye madhabahu walikula vya madhabahuni. 1NYAKATI 9:32, KUTOKA 40:23 MARKO 2:25-6, LUKA 6:3-4, WALAWI 24:8-9.

   Mtume Paulo aliposema watu wa madhabahuni hula vya madhabahuni na watu wa hekaluni hula vya hekaluni 1Korintho 9:13 alimaanisha hivi wale wahubirio injili watakula kutokana na hiyo injili yaani mtu yeyote anayeacha shughuli zake na kwenda kuhubiri injili ni haki yake kupewa fedha ya nauli pamoja na ya mahitaji yake mbalimbali. Na sivyo kama wengi wafanyavyo leo kwa kulipwa mishahara kila mwezi. “Mchungaji wa mshahahara si mchungaji” YOHANA 10:12,1KORINTHO 9:14-17, LUKA 10:14-7

“Bwana anatamani watoto wake kutenda kwa njia hiyo ya kujikana, ya kujitolea ambayo itakuletea kuridhika. Kwa kuwa tumetimiza wajibu wetu vizuri kwa sababu ulikuwa ni wajibu. Mwana pekee wa MUNGU alijitoa mwenyewe kwa kifo cha aibu pale msalabani, na je tunapaswa kulalamika kwa dhabihu ambazo tumeitwa kuzitoa? 2SM UK206P.1 SURA 25. “Maana japokuwa naihubiri injili, sina la kujisifia; maana nimewekewa sharti; tena ole wangu nisipoihubiri injili! Maana nikitenda kazi hii kwa hiari yangu ninathawabu; ila ikiwa si kwa hiari yangu, nimeaminiwa uwakili basi thawabu yangu ni nini? Ni hii, yakuwa nihubiripo, nitaitoa injili bila gharama bila kutumia kwa utimilifu uwezo wangu nilio nao katika injili 1WAKORITHO 16:19”.

Zaka ni ya Bwana kwaajili ya wale wahubirio injili, na siyo yakuwalipa mishahara wachungaji. Wote wanaopeleka injili kwa ulimwengu. MATHAYO 28:19-21 wanapaswa kuhudumiwa kwa zaka na michango mbalimbali. “Ni askari gani aendaye vitani wakati wowote kwa gharama zake mwenyewe?”1WAKORITHO 9:7. Ukuhani wa leo ni upelekaji wa injili. “Lakini nawaandikia kwa ujasiri Zaidi katika sehemu za waraka huu, kana kwamba kuwakumbusha, kwa neema ile niliyo pewa na mungu, ili niwe muhudumu wa kristo Yesu, katik ya watu wa mataifa, niifanyie injili ya Mungu kazi ya ukuhani kusudi mataifa wawe sadaka yenye kibali ikiisha kutakaswa na Roho mtakatifu.” WARUMI 15:15-16, 1PETRO 2:9-10

“Zaka ni ya Bwana, na wale wanaoiingilia kati wataadhibiwa kwa kupoteza hazina yao ya mbinguni kazi isizuiwe kwa sababu zaka…  Mungu hajabadilika; zaka bado inapaswa kutumika kwa wahubiri wa injili. TESTIMONIES FOR THE CHURCH VOL.9:247-250, CS 102aya 4. Sura 21”

     “Katika siku zijazo kazi yetu inapaswa kupelekwa mbele kwa njia ya kujikana na kujitolea hata zaidi ya ile ambayo tumeiona katika miaka iliyopita. Mungu anatutaka tukabidhi roho zetu kwake ili afanye kazi kupitia sisi kwa njia nyingi. Najisikia sana juu ya mambo haya. Ndugu zangu, natuenende kwa upole na unyenyekevu wa akili, nakuweka mbele ya washiriki wetu mfano wa kujitolea ikiwatutafanya sehemu yetu kwa Imani Mungu atafungua njia mbele zetu ambazo hazijatarajiwa.” 2SM 206P.3 SURA26        

MWONEKANO UNAOFAA KATIKA KUOMBA

“Njoni, tuabudu, tusujudu,Tupige magoti mbele za BWANA aliyetuumba” ZABURI 95:6 “Kwa nafsi yangu nimeapa neno hili limetoka kinywani mwangu katika haki, wala halitarudi, ya kwamba mbele zangu kila goti litapigwa, kila ulimi utaapa” ISAYA 45:23.

Katika jambo hili Mungu ametoa msimamo kwa kila mwanadamu anavyopaswa kuja mbele zake. Mfalme Daudi anatumia neno “Njoni tuabudu, tupige magoti mbele za BWANA” alielewa kuwa Mungu anapaswa kuabudiwa kwa unyenyekevu. Maana ndio msimamo wa wacha Mungu. Isaya naye amesema kile kile sawa na Daudi. Neno kupiga magoti ni agizo la Mungu, maana amesema kila goti litapigwa mbele zangu, na kwenda kinyume na utaratibu huo ni uasi.

Kielelezo hiki cha kupiga magoti, kiliendelezwa na watakatifu, kizazi hadi kizazi Mtume Paulo anasema. “Kumbukeni wale waliokuwa wakiwaongoza, waliowaambia neno la Mungu, tena kwa kuuchunguza sana mwisho wa mwenendo wao iigeni Imani yao.” WAEBRANIA 13:7. Tuone mifano michache ya watakatifu namna walivyo mwomba Mungu. Mtume Paulo anasema,

      “Kwa hiyo tena Mungu alimwadhimisha mno, akamkilimia jina lile lipitalo kila jina; Ili kwa jina la Yesu kila goti lipigwe na vitu vya mbinguni, na vya duniani, na chini ya nchi; na kila ulimi ukiri ya kuwa YESU KRISTO NI BWANA, kwa utukufu wa Mungu Baba” WAFILIPI 2:9-11. “YESU ambaye ni jiwe kuu la pembeni EFESO 2:20 alipiga magoti akaomba” LUKA 22:41. Nabii DANIELI “Alipiga magoti mara tatu kila siku akisali, akshukuru mbele za Mungu wake” DANIELI 6:10. EZRA kuhani “Na wakati wa sadaka ya joini, nikainuka baada ya kunyenyekea kwangu Nguo yangu na joho yangu zimeraruliwa, nikaanguka magotini nikainua juu Mikono yangu mbele za BWANA Mungu Wangu”. SULEMANI Kiongozi, “Akasemama mbele ya madhabahu ya BWANA, machoni pamkutano wote wa Israeli, akanyosha Mikono… akasimama juu yake, akapiga magoti mbele ya mkutano…. 2NYAKATI 6:12-13, 1WAFALME 8:54.” MTUME PETRO: “Petro akawatoa nje wote. Akapiga magoti akaomba” MATENDO 9:40. STEFANO: “Akapiga magoti, akalia kwa sauti kuu” MATENDO 7:60. MTUME PAULO. “Alipokwisha kunena haya akapiga magoti, akaomba pamoja nao wote.” MATENDO 20:36, 21:5

Linganisha jinsi watu wa Mungu walivyofanya na ujiulize kile kinacho fanywa na makanisa ya leo, na hata wewe mwenyewe. Swali wanaoomba hali wamesimama au kukaa agizo hilo wamelitoa wapi? Jibu kuomba watu wamesimama, walirithi desturi ya mafalisayo wapinzani wa Yesu. (Injili)  MATHAYO 6:5-23:1-30. LUKA 18:9-12. Nanyi mwaicha amri ya Mungu na kuyashika maagizo ya wanadamu. MATHAYO 15:6-12, MARKO 7:6-9, ISAYA 29:13

Hata viumbe vya mbiguni husujudu “Na hao wenye uhai wanapompa yeye aketiye juu ya kiti cha enzi utukufu… Ndipo hao wazee ishirini na nne… huanguka… nao humsujudia yeye aliye hai huta... Milele na milele”… UFUNUO 4:8-11, ISAYA 6:3 “Na malaika wote walikuwa wamesimama pande zote za kile kiti cha enzi, na za hao wazee na zale wenye uhai wane, nao wakaanguka kifulifuli mbele ya kile kiti cha enzi, wakamsujudu MUNGU” UFUNUO 7:11

“Na wale wazee ishirini na nne na wale wenye uhai wanne, wakusujudu wakamwabudu Mungu”... UFUNUO 19:4, 5:6-8, 5:11-14

           ROHO YA UNABII

“Tukisali katika chumba chetu, au kanisani, inatulazimu kupiga magoti. Mbele za Mungu. Popote tuombapo ni haki kupiga magoti” MANABII NAWAFALME UK 21

 “Nimaepokea Barua nyingi zikiniuliza kuhusiana na namna sahihi ya kuwa wakati wakutuo maombi kwa mkuu wa ulimwengu. Ni wapi ndugu zetu wamepata wazo yakuwa wanaweza kusimama kwa miguu yao wakimuomba Mungu? Mmoja amabaye alisoma kwa miaka takribani mitano katika Battle Greck aliomba kuongoza katika maombi kabla dada White hajaanza kuongea na watu. Lakini nilipo muona akisimama wima kwa miguu yake huku midomo yake ikiwa tayari kupanuliwa ili amuombe Mungu, moyo wangu uliwaka ndani yangu ili nimkemee kwa wazi. Nikimwita kwa jina lake nikisema” “Nenda chini katika mgoti yako.” Hii ndyo inayotakiwa daima. Kama moyo upo tayari Kupokea somo hili ni la thamani kujifunza.

    Kupiga magoti tunapo muomba Mungu, ndivyo tunavyopaswa kuwa wakati wote. Namna hii ya Ibada ilihitajika kwa mateka watatu Wakiebrania waliokuwa Babeli... Lakini namna hii ilikuwa heshima iliyopaswa kutolewa kwa mungu peke yake ambaye ni mkuu na mtawala wa dunia na hawa vijana watatu Wakiebrania waliokataa kutoa heshima kama hiyo kwa sanamu yoyote hata kama ilitengenezwa kwa dhahabu. Katika kufanyia hivi katika haki na makusudi wangempigia magoti mfalme wa Babeli kwa kukataa kutekeleza amri ya mfalme waliadhibiwa kwa kutupwa katika tanuru la moto. Lakini kristo alikuja mwenyewe na kutembea nao katika moto nao hawakupata madhara.  Iwe katika hadhara au katika Ibada za faragha nijukumu letu kupiga magoti mbele za mungu tunapopeleka maombia yetu kwake. Hii huonyesha utegemezi wetu kwake… 2SM 310-315

Mpendwa msomaji Mungu akusaidie, kufanya mabadiliko katika jambo hili usiendelee kufanya kinyume na utaratibu wa Mungu na kama utaendelea kuomba umesimama au kukaa, utambue kuwa hauna nafasi yoyote miongoni mwa wacha Mungu.

 

 

NEMBO MSALABA

Ishara au alama ya msalaba (mti) ulitumiwa na mataifa ya kipagani kwa ibada za Miungu. Historia inaonyosha jinsi makuhani wa Kimisri n.k walivyokuwa wakutoa heshima. Wakati wa utawala wa Waajemi mti (msalaba) uliutumia kwa kuwanyonga watu mfano ni ule wa Hamani kutaka kumnyonga Mordekai na kuwaangamiza Wayahudi wote waliokuwa kule utumwani. Soma ESTER 5:13-14, 7:7-10. An Expository Dictionary of New Testament Words (London 1962 W.E.Vine Uk 265). “Kuabudu msalaba ilikuwa ni sehemu ya ibada ya Mungu Tamuzi ukiwa katika umbo la T, au ya kifimbo ikiwakilisha herufi ya kwanza ya jina lake”

The worship of dead (LONDON 1904) Kanali J.Garnier UK 226

“Msalaba katika umbile la Crux Ansta... ulichukuliwa katika Mikono ya makuhani wa kimisri na walafme na maaskofu kuwa ufananisho wa mamlaka yao, wakiwa makuhani wa Mungu jua waliitwa ishara ya uhai.”

Kwa hiyo kuchora au kutumia ishara ya msalaba kwenye vitabu vyetu kwenye makanisa na kwenye nembo. Ni kuendeleza ibada za kipagani.

“Sasa yesu aliwaambia wanafunzi wake kuwa maisha yake ya kujinyima” na

kimasikini ni kielelezo cha maisha ambayo lazima waishi. Alisema: “Mtu yeyote atakaye kunifuata lazima ajikane nafsi yake, ajitwike msalaba wake kila siku anifuate.” Msalaba ulikuwa ikitumika katika utawala wa kirumi. Ulikuwa kitu cha uchungu sana, na kifo chake ki1ikuwa cha ukatili kuliko vyote. Wahalifu  walio husika kwa kifo cha msalaba iliwapasa kujichukulia msalaba mpaka mahali pa kusulubiwa. Kila mara walipobebeshwa misalaba walifurukuta sana na kutaka kuj iokoa. Maneno ya kristo kwa wanafunzi wake ingawa waliyafahamu kigizagiza yaliwaonyesha mauti ya kritso" “E.G. WHITE Tumaini uk. 236

 

“Msalaba  uliokuwa umetayarishwa kwa ajili  ya Baraba. ulitwishwa katika mabega ya yesu yaliyokuwa yakichuruzika damu. Wezi wa Baraba waliopaswa kusulubiwa pamoja naye nao walibebeshwa misalaba yao. Tangu alipokula pasaka pamoja na wanafunzi wake, yesu alikuwa hajala wala kunywa chochote. Alikuwa amevumilia uchungu wa kusalitiwa, na alishuhudia wanafunzi wake wakimwacha na kutawanyika. Alikuwa amepelekwa kwa Anasi. Kwa  Kayafa, Kwa pilato, Kwa Herode na kurudishwa kwa

Pilato tena. Usiku ule wote palikuwapo tukio baada ya tukio kiasi cha kuweza kudhoofisha roho ya mtu hadi kuzimia. Lakini  Kristo hakushindwa. Alikabili fadhaa zote kishujaa. Lakini badaa kupigwa mara ya pili na kutishwa msalaba hali ya kibinadamu haikuweza kustahimili zaidi. Alianguka na kuzimia chini ya mzigo huo” “E.G. WHITE TUMAINI UK. 420.

 

Desturi ya kuweka misalaba kama Nembo ilirithiwa na kanisa la Roma. Wao huvaa msalaba shingoni, madhabahuni, makaburini kila mahali wanautukuza msalaba (mti) pia na makanisa ya Kiprotestanti yamefuata mfano wa Roma kwa kuweka ishara ya msalaba kwenye makanisa yao n.k. “Kama mama ya mtu alivyo ndivyo alivyo na binti yake EZEKIELI 16: 44 wanatumia msalaba kama Nembo ya ukristo huo ni uongo ishara au alama ya ukristo ni tabia  MATHAYO 5:14-16, 2WAKORITHO 3:1-3 MATENDO 11: 24 -26

 

Wayahudi wakati wa kristo ... hali kadhalika warumi hujidai kuwa wanautukuza msalaba. Huweka msalaba kila mahali:makanisani, madhabauni, kwenye mavazi n.k. klla mahali wanautukuza msalaba kijuju. Lakini mafundisho ya kikristo wakiyazika chini na kuyainua mapokeo ya bure ya kibinadamu “E.G.WHITE PAMBANO  KUU  UK. 323 – 324”

 

Shetani hunasa watu wengi kwa njia ya kuwaunganisha pamoja na maadui za Mungu, au msalaba wa krisio. Muungano huu unaweza kuwa wa kuzaliwa, kuoana, au urafiki.

watu wa namna hii hawatamani kutimiza wajibu wao. E.G. WHITE PAMBANO KUU UK. 340”

 

Viongozi wa majeshi ya kirumi walikusudia kutoa kipimo kizito kwa wayahudi ambacho kingewafanya wasalimu amri mara moja. Mateka walipigwa, wakateswa sana na kutundikwa mtini, mbele ya kuta za mji. Kufuata bonde la Yehoshafati na kuendelea mapaka mlima wa Golgota, misalaba mingi sana, ambako watu walikuwa wametundikwa ilijazana tena. Hapakuwa na nafasi ya kupita kati yake. “E.G. WHITE PAMBANO KUU UK. 21 SURA 1.

Nabii “Ellen  G. White Alionyeshwa msalaba ukiingizwa ndani ya kanisa la Wasabato.

Usiku ule niliota kwamba nipo Battle Greek nikiwa nachungulia nje ya vioo mlangoni nikaona kundi linatembea kuja kwenye nyumba wawili wawili walionekana wakakamavu na vanaojielewa. Nilikuwa na wafahamu vizuri nikawa tayari kwa kuwapokea kwa kuwafungulia mlango. Lakini wazo likanijia nitazaine tena. Safari hii nikaona kitu kingine. Sasa nikaona kanisa katoliki katika maandamano, mmoja ameshikilia msalaba mkononi mwake na mwingine maagizo la kanisa lao. Nao walipo ikaribia wale waliobeba maagizo ya kanisa wakafanya duara kuizunguka nyumba yetu wakisema mara tatu nyumba hii haipaswi kuwepo mali zake zote lazima zichukuliwe wameongea na kupingana na Kanuni yetu ya imani. Nilia machozi na kufanya maombi nilipoona mali zetu zikichukuliwa.” 1T 578.

 

 

“Ulikumbuke kusanyiko lako, ulilolinunua zamani ulilolikomboa liwe kabila ya urithi wako, Mlimani Sayuni ulioufanya maskani yako. Adui ameufanya kila ubaya katika patakatifu. Watesi wako wamenguruma kati ya kusanyiko lako;wameweka bendera zao ziwe alama”. ZABURI 74:2-9

 

 “Kwahiyo tokeni kati yao, mkatengwe nao, asema Bwana, msiguse kitu kilicho kichafu, nami nitawakaribisha.”  2KORINTHO 6:17, ISAYA 52:11-12, EZEKIEL 12:1-5, YEREMIA 51:6 “Natoa mwito kwa wote ambao wameungana katika mwenendo wa kanuni hizi mbaya, hufanya maamuzi ya matengenezo na kutembea kwa unyenyekevu mbele za Mungu. Huu si upuuzi wala hadithi bali ni ukweli. Ninauliza tena ni upande gani unaosimama? 1WAFALME 18:21 ikiwa BWANA ndiye MUNGU mfuateni, bali ikiwa baali basi mfuate” 8T UK 68

 

 

 

KANISA LA WA-ADVENTISTA WA SABATO (WANA MATENGENEZO)

KISASA, DODOMA, TANZANIA

0756959525, 0768315787, 0624141001, 0682,773384

Share:

Popular Posts

Lebo

Recent Posts

Pages