Katika blogu hii, tutachunguza njia mbalimbali za kuimarisha ufahamu wetu wa Biblia. Tutajadili mbinu za kusoma Biblia kwa ufanisi, vidokezo vya kukariri maandiko matakatifu, na mikakati ya kutumia somo la Biblia katika maisha yetu ya kila siku. Iwe wewe ni mtaalam wa Biblia mzoefu au unaanza tu safari yako ya imani, "Jifunze Biblia Zaidi" ni rasilimali kamili ya kukusaidia kuongeza ufahamu wako wa Maandiko Matakatifu na kumkaribia Mungu zaidi.

USIJIFANYIE SANAMU YA KUCHONGA "Kutoka 20:4-6"

AMRI YA PILI

 “Usijifanyie sanamu ya kuchonga, wala mfano wa kitu chochote kilicho juu mbinguni, wala kilicho chini duniani, wala kilicho majini chini ya dunia. Usivisujudie wala kuvitumikia; kwakuwa mimi, BWANA MUNGU wako, ni MUNGU mwenye wivu; nawapatiliza wana maovu ya baba zao, hata kizazi cha tatu na cha nne cha wanichukiao, nami nawarehemu maelfu elfu wanipendao, na kuzishika amri zangu. Kutoka 20:4-6

 

Ndugu msomaji amri ya pili inayo makatazo matatu

1.       Dhambi ya kwanza ni kuchonga sanamu

2.       Dhambi ya pili ni kusujudia sanamu

3.       Dhambi ya tatu ni kutumikia sanamu

 

   Kufanya kitendo chochote kati ya haya matatu, ni uvunjaji wa amri ya pili, inayokataza ibada ya sanamu. Zifuatazo ni aina za sanamu zilizokatazwa kuchongwa, kusujudiwa na kutumikiwa;

 

1.       Usichonge sanamu mfano wa sura yoyote

2.       Usichonge sanamu mfano wa mwanaume

3.       Usichonge sanamu mfano wa mwanamke

4.       Usichonge sanamu mfano wa mnyama yeyote aliye duniani

5.       Usichonge sanamu mfano wa ndege yeyote arukaye mbinguni

6.       Usichonge sanamu mfano wa kitu chochote kitambaacho juu ya ardhi

7.       Usichonge sanamu mfano wa samaki yeyote aliye majini duniani

8.       Usichonge sanamu mfano wa umbo la kitu chochote. K/Torati 4:16-18, 23

 

1. Wachonga sanamu wanavyoanza

          “Huchagua mti usiooza, kujitafutia fundi msitadi wa kusimamisha sanamu ya kuchonga isiyoweza  kutikisika” Isaya 40:20

   “Wachongao sanamu, wote ni ubatili, wala mambo yao yawapendezao hayatawafaa kitu; wala mashahidi wao wenyewe hawaoni, wala hawajui; ili watahayarike. Ni nani aliyejichongea mungu mmoja, au aliyesubu sanamu isiyofaa kitu? Tazama wenziwe wote watatahayari; na mafundi; hao ni wanadamu; na wakusanyike pamoja, wakasimame; wataogopa na kutahayari pamoja.

 

Mfua chuma hufanza shoka, hufanya kwa makaa, huitengeneza sanamu kwa nyundo, huifanyiza kwa nguvu za mkono wake; naam, huona njaa, nguvu zake zikampungukia; asipokunywa maji huzimia. Seremala hunyosha uzi; huiandika kwa kalamu ya mate; huitengeneza kwa randa, huiandika kwa bikari, huifanza kwamfano wa mwanadamu, sawasawa na uzuri wa mwanadamu, ili ikae nyumbani. Yeye hujikatia mierezi, hutwaa mtiliza, na mwaloni, hujichaghulia mti mmoja katika miti ya msituni; hupanda mvinje,mvua ikaustawisha. Kisha utamfaa mwanadamu kwa kuni; hutwaa kipande, akaota Moto; naam, huufanya mungu akauabudu; huifanya sanamu ya kuchonga akaisujudia. Sehemu moja huiteketeza; kwa sehemu nyingine hula nyama; huokwa kwa chakula kiokwacho, akashiba, naam, huota moto, akasema, ah, nimeota moto, nimeona moto. Na kwa sehemu iliyobakia hufanya mungu, yaani, sanamu yake ya kuchonga; husujudu mbele yake akaiabudu, akaiomba akasema, uniokoe, maana wewe u mungu wangu. Hawajui wala hawafikiri; maana amewafumba macho, wasione, na mioyo yao, wasiweze kufahamu. Wala hapana atiaye moyoni, wala hapana maarifa, wala fahamu kusema, nimeteketeza sehemu motoni, naam, pia nimeoka mkate juu ya makaa yake; nimeoka nyama nikaila; nami je! kilichobaki nikifanye kuwa chukizo? Je! nisujudie shina la mti? Isaya 44:9-19

 

                 Uchambuzi wa mafungu haya

1.       Sanamu ni ubatili, haitikisiki, haifai kitu

2.       Mafundi wa sanamu ni wanadamu ni maseremala

3.       Sanamu huetengenezwa kwa nyundo na randa

4.       Mafundi wa sanamu huona njaa wasipokunywa maji huzimia nguvu zao

          zikawapunguka.  Lakini hutengeneza sanamu mfano wa mwanadamu

5.       Watu huichukua hiyo sanamu ili ikae nyumbani, Je unayo?

6.       Sanamu ni mti unaomfaa mwanadamu kwa kuni

7.       Na bahati mbaya sehemu iliyobakia katika mti, aidha wamvinje,   

          huufanya MUNGU, yaani sanamu  yake ya kuchonga.

8.       Husujudu mbele ya sanamu iliyotokana na mti - akaiomba

9.       Husujudu mbele ya sanamu akisema - niokoe

10.     Husujudu mbele ya sanamu akisema wewe u Mungu wangu.

11.     Waabudu sanamu hawana maarifa, hawana fahamu, hawafikiri kusema,

          nimeteketeza sehemu ya kuni motoni, nimeoka mkate juu ya kuni,            nimeoka nyama juu ya makaa yake nikaila. Nami e! kilichobaki nikifanye

          kuwa chukizo?

12.     Je! nisujudie shina la mti?

          Mpendwa ndugu msomaji katika jambo hili la ibada ya sanamu watu

         wengi wamekoseshwa, sijui kama na wewe umepona. Nabii Isaya                        alionyeshwa katika siku za mwisho ulimwengu ulikuwa   

         umejaa sanam. Madukani kuna sanamu, makanisani kuna sanamu;

 

  “Tena nchi yao imejaa sanamu, huabudu kazi ya mikono yao, vitu vilivyofanywa kwa vidole vyao wenyewe. Mtu mnyonge huinama, na mtu mkubwa hujidhili, kwa hiyo usiwasamehe” Isaya 2:8-9

  “Jikusanyeni mje; na kukaribia pamoja, ninyi wa mataifa miliokoka; hawana maarifa wale wachukuao mti wa sanamu yao ya kuchonga; wamwombao mungu asiyeweza kuokoa” Isaya 45:20

 

   “Na alaaniwe mtu afanyaye sanamu ya kuchonga, au ya kusubu, machukizo kwa BWANA, kazi ya mikono ya fundi. Akaisimamisha kwa siri. Na watu wote wajibu, waseme, amina” K/torati 27:15

          2.  Usisujudie sanamu; usiabudu sanamu

   “Na waaibishwe wote waabuduo sanamu, wajivunao kwa vitu visivyofaa” Zaburi 97:7

 

   MUNGU hataki katika kanisa lake wawemo waabudu sanamu na ndio maana ameagiza kwamba akijulikana mshiriki yeyote kuwa anaabudu sanamu; aondolewe ushirika mara moja. Maana ibada ya sanamu ni dhambi ya wazi. Zifuatazo ni dhambi za wazi:-

  “Naliwaandikia katika waraka wangu, kwamba msichangamane na wazinzi. Si semi msichangamane kabisa na wazinzi wa dunia hii, au na wenye kutamani, au na wanyang’anyi, au na wenye kuabudu sanamu; maana hapo ingewalazimu kutoka katika dunia. Lakini mambo yalivyo, na waandikia kwamba msichangamane na mtu aitwaye ndugu, akiwa ni uzinzi au mwenye kutamani au mwenye kuabudu sanamu au mtukanaji au mlevi au mnyang’anyi; mtu wa namna hii msikubali hata kula naye, maana yanihusu mimi kuwahukumu wale walio nje?  Nyinyi hamuwahukumu hao waliondani? lakini hao walio nje (ya kanisa) MUNGU atawahukumu. Ninyi mwendoeni yule mbaya miongoni mwenu”. Wakoritho 5:9-13

 

Na mbaya (1) Mzinzi (2) Mwenye kutamani

(3) Mtukanaji (4) Mlevi      (5) Mnyang’anyi     

(6) Mwenye kuabudu sanamu. Hizi ni dhambi za wazi.

 

  Kanisa la MUNGU duniani linaloshika amri kumi; halina urafiki, halina uhusiano wowote na waabudu sanamu. Maana waabudu sanamu ni watu wasio amini. MUNGU ameagiza ifuatavyo:-

  “Msifungiwe nira pamoja na wasioamini kwa jinsi isivyo sawasawa; kwa maana pana urafiki gani kati ya haki na uasi? Tena pana shirika gani kati ya nuru na giza? Tena pana ulinganifu gani kati ya Kristo na Beliari? au yeye aaminiye ana sehemu gani pamoja na yeye asiyeamini? Tena pana mapatano gani kati ya hekalu la MUNGU na sanamu? Kwa maana sisi tu hekalu la MUNGU aliye hai; kama MUNGU alivyosema, kwamba, nitakaa ndani yao, na kati yao nitatembea nami nitakuwa MUNGU wao, nao watakuwa

watu wangu. Kwa hiyo tokeni kati yao, mkatengwe nao, asema BWANA. Msiguse kitu kilicho kichafu, nami nitawakaribisha. Nitakuwa baba kwenu, nanyi mtakuwa kwangu wanangu wa kiume na wa kike, asema BWANA MWENYEZI”. 2 Wakorintho 6:14-18

 

Hebu sasa tuiulize biblia, je, huko nyuma waabudu sanamu walikuwa ni watu wa dini?

 

   “Mwajua ya kuwa mlipokuwa watu wa mataifa (wapagani) mlichukuliwa kufuata sanamu zisizonena kama mlivyoongozwa” 1 Wakoritho 12:2

 

   Mpendwa ndugu msomaji; Biblia inatufundisha kuwa, huko nyuma; waabudu sanamu hawakuwa watu wa dini. Bali walikuwa watu wa mataifa, wapagani wasiomjua MUNGU. Lakini baati mbaya, eti leo waabudu sanamu ni watu wa dini. Maajabu kabisa, mojawapo ya watu wapagani waliokuwa wanaabudu sanamu walikuwa ni wafilisti. Nikwambie mahali sheria ya MUNGU ilipo hapawezi kuwepo sanamu. Hebu sikiliza:-

   “Basi Wafilisti walikuwa wamelichukua sanduku la MUNGU, wakaenda nalo kutoka Eben-ezeri hata Ashidodi. Wafilisti wakalichukua sanduku la MUNGU, wakalitia katika nyumba ya Dagoni, wakaliweka karibu na Dagoni (Sanamu). Na watu wa Ashidodi, walipoamka alfajiri siku ya pili kumbe!, Dagoni (sanamu) imeanguka chini kifudifudi, mbele ya sanduku la BWANA. Wakaitwaa Dagoni ( Sanamu) wakaisimamisha mahali pake tena. Hata walipoamka kesho yake asubuhi, kumbe! Dagoni (Sanamu) ilikuwa imeanguka chini kifudifudi, mbele ya sanduku la BWANA; na kichwa chake Dagoni (Sanamu) na vitanga vya mikono yake vyote viwili vimekatika, vipo vimelala kizingitini; Dagoni ikasalia kiwili wili chake tu”. 1 Samweli 5:1-4

 

   Hawa walikuwa ni watu wa mataifa wapagani wasiomjua MUNGU waliabudu Dagoni - waliabudu Sanamu. Ingawa sanamu za leo zimepambwa kwa majina ya watakatifu, lakini sanamu ni sanamu tu, Dagoni ni Dagoni tu. Na wanaozichonga, na wanaozisujudia, na wanaozitumikia, ni watu wa mataifa, ni wapagani, ni Wafilisti. Wengi mpaka leo wanafanya ibada za kifilisti, rafiki yangu toroka kutoka katika ibada za Wafilisti wa leo. Neno linaendelea kusema;

   “Paulo alipokuwa akiwangojea huko Athene na kuona jinsi mji ule ulivyojaa sanamu, roho yake ilichukizwa sana ndani yake”. Matendo 17:16

 

   Umesikia ndugu yangu neno takatifu linavyoonya. Manabii na Mitume hakuna aliyewahi kufurahia ibada ya sanamu. Paulo alipoenda kwa watu wa mataifa wapagani wasiomjua MUNGU kule Athene, kwa waabudu sanamu, na akakuta mji wa Athene umejaa sanamu, Biblia inashuhudia wazi roho yake mtume Paulo, ilichukizwa sana ndani yake. Lakini leo wanao mwabudu MUNGU wa Paulo, wao wanapendezwa na ibada ya sanamu, tena baadhi wanavaa shingoni.

 

   “Paulo akiwa ndani ya hekalu lililojaa sanamu za kila namna, alinyoosha mkono wake akieleza kwamba ibada hiyo ya kuabudu Miungu ni ibada ya uongo, ambayo wenyeji wa Athene wanayo abudu. Wasikilizaji wake walishangaa kabisa. Alijionyesha kuwa anafahamu ufundi huo na michoro hiyo ya sanamu, na hali hiyo ya kimizimu. Alionyesha mikono yake kueleleza kwa sanamu hizo, alitamka kuwa MUNGU hawezi kufananishwa na vitu kama hivyo. Sanamu hizo hazina uzima, wala hazijisogezi huko na huko, isipokuwa zisogezwe na mikono ya wanadamu, na kwamba wanaoziabudu ni wakuu kuliko zenyewe” E.G. White - Maonjo hadi ushindi 102:2 Sura 23

 

   Waisraeli walipokengeuka wakaacha ibada kwa MUNGU. Walitengeneza sanamu ya ndama wa dhahabu wakaisujudia. Hebu sikiliza nabii Musa naye 

 

alivyoshughulikia jambo hilo, kuonyesha kuwa ibada ya sanamu ni chukizo.  Manabii na Mitume walikemea vikubwa sana juu ya ibada ya sanamu. Na hakuna mwandishi wa biblia hata mmoja ambaye hajaonya juu ya  ubaya wa ibada ya sanamu.

 

   “Hata alipoyakaribia marago akaiona ile ndama, na ile Michezo. Hasira ya Musa ikawaka, akazitupa zile mbao mikononi mwake, akazivunja chini ya mlima. Akaitwaa ile ndama (Sanamu) waliyoifanya akaichoma moto, akaisaga hata ikawa mavumbi, akainyunyuza juu ya maji, akawanywesha wana wa Israeli. Musa akamwambia Haruni watu hawa wamekufanyia nini hata ukaleta dhambi hii kuu juu yao?” Kutoka 32:15-21

 

   Hivi ndivyo mtumishi wa MUNGU Musa alivyoondoa upagani kwa watu wanaoelekea mbinguni. Manabii na Mitume hawakuwa na mzaa na ibada ya sanamu. Paulo alipoenda kule Athene na akakuta mji umejaa sanamu roho yake ilichukizwa sana ndani yake. Musa naye alipoiona ile sanamu, hasira ya Musa ikawaka. Ni jambo lilelile.

1.       A kaitwaa ile sanamu waliofanya akaichoma moto

2.       Akaisaga hata ikawa mavumbi

3.       Akainyunyuzia maji

4.       Akawanywesha wale wote walioleta upagani kwa taifa la MUNGU.

Hivi ndivyo Musa alivyowashughulikia waabudu sanamu. Je wewe msomaji  unapoona sanamu roho yako inafurahia au inachukizwa. Tafakari sana, swala la kwenda mbinguni siyo la kuchezewa.

5. Musa akamwambia Haruni watu hawa wamekufanyia nini hata ukaleta dhambi hii kuu juu yao? Na Paulo katika agano jipya akinukuu jambo lile lile anasema ifuatavyo:-

 

 “Waka mwambia Haruni, tufanyie miungu, watakaotutangulia, maana huyo Musa, aliyetutoa katika nchi ya Misri, hatujui lililompata. Wakafanya ndama siku zile, wakaleta dhabihu kwa sanamu ile wakafurahia kazi za mikono yao. Basi MUNGU akaghairi, akawaacha” Matendo 7:40-42

   “Lakini wote pia huwa kama wanyama, ni wapumbavu. Haya ni maelezo ya sanamu, ni shina la mti tu”  Yeremia 10:8

 

Zingatia yafuatayo:-

1.       Ibada ya sanamu ni dhambi kuu

2.       Haruni alitengeneza miungu

3.       Sanamu ni shina la mti tu

4.       Sanamu ni kazi ya mikono ya binadamu

5.       Na waabudu sanamu ni wakuu kuliko sanamu.

 

Sasa kwanini MUNGU ametukataza kuchonga sanamu, kusujudia sanamu, kutumikia sanamu




 


Sanamu “Zina vinywa lakini hazisemi

Zina macho lakini hazioni

Zina masikio lakini hazisikii                     

Zina pua lakini hazisikii harufu                                   Zaburi 115:5-8             

Zina mikono lakini hazishiki

Zina miguu lakini haziendi

Wala hazitoi sauti kwa koo zake

Wazifanyao watafanana nazo, na kila mmoja

anayezitumainia”

 

   “Basi niseme nini? ya kwamba kile kilochotolewa sadaka kwa sanamu ni kitu? Au ya kwamba sanamu ni kitu?  1 Wakorintho 10:19

 

“Sanamu si kitu katika ulimwengu” 1 Wakoritho 8:4

 

   “Mimi ni BWANA ndilo jina langu; na utukufu wangu sitampa  mwingine, wala sitawapa sanamu sifa zangu”. Isaya 42:8

 

    “Kila mtu amekuwa kama mnyama, hana maarifa; kila mfua dhahabu amefedheheshwa na sanamu yake ya kuchonga; maana sanamu yake ya kuyeyuka ni uongo, wala hamna pumzi ndani yake. Ni ubatili tu, ni kazi za udanganyifu; wakati wa kujiliwa kwao watapotea”. Yeremia 10:14-15

  “Huajiri mfua dhahabu, akaifanya mungu; huanguka, naam, huabudu. Humchukua begani, humchukua, wakamsimamisha mahali pake, akasimama; hataondoka katika mahali pake, naam, mmoja atamwita, lakini hawezi kujibu, wala kumwokoa na taabu yake”. Isaya 46:6-7

 

   “Hata hivyo ingawa uasi umeenea jinsi hiyo, si kwamba umewakumba watu wote. Sio watu wote waliomo ulimwenguni, kwamba ni wafedhuli na waovu; si wote wanaomwunga mkono shetani. MUNGU anao watu maelfu ambao hawakumsujudia Baali; ni wengi wanaotamani kuelewa habari za Kristo na sheria ya MUNGU; Ni wengi wanaotamani kabisa kabisa kwamba Yesu atakuja tena karibuni, ili kukomesha utawala wa dhambi na mauti. Pia wako wengi ambao wamekuwa wakimwabudu Baali kwa kutojua, ambao Roho wa MUNGU anawashughulikia.

 

Watu kama hawa wanahitaji msaada kutoka kwa wale waliomjua MUNGU na uwezo wa neno lake. Wakati kama huu, kila mtoto wa MUNGU hana budi kujitahidi kuwasaidia wale waliomo gizani. Watu ambao wanaifahamu kweli ya Biblia, wanaposhughulika kuwasaidia wale wasiojua kitu, Malaika wa BWANA hushirikiana nao katika kazi hiyo.

 

Na ikiwa malaika kufuatana nao hakuna hofu yoyote. Matokeo ya kazi ya watu hawa waaminifu, yatakuwa mazuri sana, maana watawageuza watu waliokuwa wakiabudu sanamu, wapate kumwabudu MUNGU aliye hai. Wengi wataacha kufuata mafundisho ya kibinadamu, na kumgeukia MUNGU na sheria yake”. E.G. White - Manabii na wafalme 95:3-4  ni sura ya 13

 

   Ushauri wa kiroho kwa wale waliokuwa wakitumikia sanamu na wale waliokuwa wamedanganywa, hata na wale waliokuwa hawajui na wanaohitaji kumgeukia MUNGU;

   “Kwa ajili ya hayo, wapenzi wangu, ikimbieni ibada ya sanamu”. 1 Wakoritho 10:14

 

Baada ya kukimbia hatua nyingine hii hapa “ watoto wadogo, jilindeni nafsi zenu na sanamu” 1 Yohana 5:21 yaani, usiabudu sanamu tena.

 

Ifuatayo ndiyo hatima ya waabudu sanamu wote na wadhambi wengine

 

   “Bali waoga, na wasioamini, na wachukizao, na wauwaji, na wazinzi, na wachawi, na hao waabuduo sanamu, na waongo wote, sehemu yao ni katika lile ziwa liwakalo moto na kiberiti. Hii ndiyo mauti ya pili” Ufunuo 21:8

 

   “Nami nitakatilia mbali sanamu zako na nguzo zako. Zitoke kati yako; wala hutaiabudu tena kazi ya mikono yako. Nami nitayang’oa maashera yenu, yasiwe kati yako; nami nitaiangamiza miji yako. Nami nitajilipiza kisasi katika hasira ya ghadhabu juu ya mataifa waliosikiliza” Mika 5:13-15

 

  “Au hamjui ya kuwa wadhalimu hawataurithi ufalme wa MUNGU? Msidanganyike; waasherati hawataurithi ufalme wa MUNGU, wala wabudu sanamu, wala wazinzi, wala wafilaji, wala walawiti, wala wevi, wala watamanio, wala walevi, wala watukanaji, wala wanyang’anyi”. 1 Wakoritho 6:9-10 

 

   Ndugu msomaji nataka uelewe kuwa, MUNGU muumbaji kupitia Manabii na Mitume wake, alishatangaza waziwazi hatima ya wote wanaoabudu sanamu. Hawataurithi ufame wa MUNGU, na sehemu yao ni katika ziwa la Moto. Elewa kuwa mahali watu wana abudu kuna sanamu, ni udhalimu. Na nabii Yeremia ametwambia ni ubariri tu, ni kazi za udanganyifu, na wakati wa mwisho waabudu sanamu watapotea Yeremia 10:15 Uchaghuzi ni wako. Hata hivyo nabii Isaya anatueleza jinsi itakavyokuwa siku ya mwisho juu ya wale watakaong’ang’ania sanamu;

 

   “Na majivuno ya mwanadamu yatainamishwa, na kiburi cha watu kitashushwa; naye BWANA yeye peke yake, atatukuzwa siku hiyo. Nazo sanamu zitatoweka kabisa. Na watu wataingia ndani ya pango za majabali, na ndani ya mashimo ya nchi, mbele za utisho wa BWANA na utukufu wa enzi yake, atakapoondoka ili aitetemeshe mno dunia.  Siku hiyo kila mtu atazitupilia mbali sanamu zake za fedha na sanamu zake za dhahabu, walizojifanyia ili kuziabudu, kwa fuko na popo; ili aingie ndani ya pango za majabali, na ndani ya tundu za miamba iliyopasuka, mbele za utisho wa BWANA na utukufu wa enzi yake, atakapoondoka ili aitetemeshe mno dunia”. Isaya 2:17-21

 

  “Basi matendo ya mwili ni dhahiri, ndiyo haya, uasherati, uchafu, ufisadi, ibada ya sanamu, uchawi, uadui, ugomvi, wivu, hasira, fitina, faraka, uzushi, husuda, ulevi, ulafi; na mambo yanayofanana na hayo. Katika hayo nawaambia mapema, kama nilivyokwisha kuwaambia, ya kwamba watu watendao mambo ya jinsi hiyo, hawataurithi ufalme wa MUNGU”. Wagalatia 5:19-21

 

  “Amri ya pili hukataza ibada ya MUNGU wa kweli kwa sanamu au mifano. Mataifa mengi ya kipagani yalidai kwamba sanamu zao zilikuwa ni mfano au alama tu ambazo hupitia hizo MUNGU aliabudiwa, lakini MUNGU amesema kuwa ibada kama hiyo ni dhambi. Kujaribu kumwakilisha aliye wa milele kwa vitu kutashusha dhana ya mwanadamu kwa MUNGU. Akili ikitolewa mbali na ukamilifu wa Yehova, itavutwa ielekee kwa viumbe badala ya kwa Muumba. Na kadri dhana yake kumhusu MUNGU itakavyoshushwa, ndivyo mwanadamu pia atakavyodhoofika”. E.G. White - 1Wazee na Manabii 294:2 pp 306:1

 

YAFUATAYO NI MAKUNDI MBALIMBALI YA WAABUDU SANAMU

 

1.Uchawi

   “Na wakati watakapokuambia tafuta habari kwa watu wenye mapepo na kwa wachawi; waliao kama ndege na kunong’ona; Je! haiwapasi watu kutafuta habari kwa MUNGU wao? Je! waende kwa watu waliokufa kwa ajili ya watu walio hai? Isaya 8:19

   “Walipokwisha kupita katikati ya kisiwa chote mpaka pafo, wakaona mtu mmoja mchawi, nabii wa uongo, myahudi jina lake Bar-Yesu; mtu huyu alikuwa pamoja na Liwali Sergio Paulo, mtu mwenye akili. Yeye Liwali akawaita Barnaba na Sauli waje kwake akataka kulisikia neno la MUNGU. Lakini Elima, yule mchawi (maana ndio tafasiri ya jina lake,) akashindana nao, akitaka kumtia yule Liwali moyo wa kuiacha ile imani. Lakini Sauli, ambaye ndiye Paulo, akijaa Roho mtakatifu, akamkazia macho akasema, Ewe mwenye kujaa hila na uovu wote, mwana wa Ibilisi, adui wa haki yote, huachi kuzipotoa njia za BWANA zilizonyooka? Basi angalia mkono wa BWANA u juu yako, nawe utakuwa kipofu, usilione jua kwa mda. Mara kiwi kikamwangukia na giza, akazunguka zunguka na kumtafuta mtu wa kumshika mkono na kumwongoza. Ndipo yule Liwali, alipoyaona yaliyotendeka, akaamini, akiyastaajabia mafundisho ya BWANA”Matendo 13:6-12

 

   Mpendwa msomaji ikiwa haujachonga sanamu, lakini kwa kwenda kupiga ramli kwa waganga na wachawi, ni kufanya mawasiliano na mapepo, na mizimu. Kufanya hivyo ni kuwa na uhusiano na shetani mwenyewe, ni uvunjaji wa amri ya Pili, ni ibada ya sanamu. Zingatia wachawi, mbele za MUNGU ni wafu, je uende kwa watu waliokufa kutafuta habari kwao, badala ya kutafuta habari kwa MUNGU? Ukweli kuhusu wachawi.

1.       Ni manabii wa uongo

2.       Wanashindana  na watu wa MUNGU

3.       Wamejaa hila na uovu wote

4.       Wachawi ni maadui wa haki yote

5.       Wachawi ni wana wa  Ibilisi

6.       Wachawi ni wapotoshaji wa njia za BWANA zilizonyooka.

   Hata hivyo leo kuna uchawi wa zamani na uchawi wa kisasa, hebu tuendelee na uchawi wazamani. Maana huu uchawi wa kisasa tutauzungumza katika sura za mbele, na kwa sehemu kubwa ndio wamekosesha ulimwengu kwa kufanya miujiza ya uongo - ni uchawi uleule, ila waleo umeboreshwa. Hebu tuendelea na uchawi wa zamani abalogi, abarozi, abhaturutumbi.

  “Msiwaendee wenye pepo, wala wachawi, msiwatafute; ili kutiwa unajisi na wao; mimi ndimi BWANA, MUNGU wenu” M/walawi 19:31

 

   “Asionekane kwako mtu ampitishaye mwanawe au biti yake kati ya moto, wala asionekane mtu atazamaye bao, wala mtu atazamaye nyakati mbaya, wala mwenye kubashiri, wala msihiri, wala mtu alogaye kwa kupiga mafundo, wala mtu apandishaye pepo, wala mchawi, wala mtu awaombaye wafu. K/torati 18:10-11

 

2. Wanaofanya matambiko kwa ajili ya wafu

A:Mtambiko wa kwanza kunyoa nywele (kipara) kwa          ajili ya aliyekufa.   

 “Ninyi mmekuwa wana wa BWANA MUNGU wenu; msijitoje miili yenu, wala       

msifanye upaa katikati ya macho yenu kwa ajili ya wafu” K/torati 14:

 

B: Wanaomaliza msiba kwa kuchanjwa eti anatakasika “ Msichanje chale yoyote katika nyama ya miili yenu kwa ajili ya wafu, wala msiandike alama miilini mwenu; mimi ndimi BWANA”. M/walawi 19:28

 

C:      Mtambiko mwingine ni ujenzi wa makaburi;

“Ole wenu waandishi na mafarisayo,wanafiki! kwa kuwa mmefanana namakaburi yaliyopakwa chokaa, nayo kwa nje yaonekana kuwa mazuri, bali ndani yamejaa mifupa ya wafu, na uchafu wote”. Mathayo 23:27 .

 

Kaburini kuna uchafu namifupa “Ole wenu, waandishi na mafarisayo wanafiki! kwa kuwa mnayajenga makaburi ya manabii na kuyapamba maziara ya wenye haki”. Mathayo 23:29  “Makaburi meupe yaliyopambwa yalificha maozea yaliyomo ndani yao. Ndivyo ilivyokuwa kwa Makuhani na wazee waliokuwa wakionekana kwa nje kama wanyofu, walificha uovu ndani yao...Ushirikina wa kuheshimu makaburi ya watakatifu ulidumishwa na fedha nyingi zilitumika katika kuyapamba. Machoni pa MUNGU hii ilikuwa ibada ya sanamu. Ilionyesha kuwa hawakumpenda MUNGU hata kidogo, wala jirani zao kama nafsi zao. Leo watu wengi hawawajali wajane, na yatima, wagonjwa na masikini, ili kutoa gharama ya kujenga minara ya kumbukumbu kwa ajili ya wafu. Wajibu kwa walio hai, wajibu ambao Kristo ameuagiza kwa dhati umeachwa bila kutendeka”. E.G. White - Tumaini la vizazi vyote 346:2-4

 

3.  Wanaopiga magoti na kuungama dhambi kwa mwanadamu aliye kama  wao.

 

  Katika kundi hili hebu tuangalie kwani dhambi zinaungamwa kwa nani?

   “Watoto wangu wadogo na waandikia haya ili kwamba masitende dhambi. Na kama mtu akitenda dhambi tunaye mwombezi kwa Baba, Yesu Kristo mwenye haki, naye ndiye kipatanisho kwa dhambi zetu, wala si kwa dhambi zetu tu, bali na kwa dhambi za ulimwengu wote”. 1 Yohana 2:1-2

 

  “Kwasababu MUNGU ni mmoja, na mpatanishi kati ya MUNGU na wanadamu ni mmoja, Mwanadamu Kristo Yesu; 1 Timotheo 2:5

 

Huu ndio ukweli wa Biblia, anayesamehe dhambi ni mmoja tu; Yesu Kristo mwenye haki. Na mpatanishi kati ya MUNGU na wanadamu naye ni mmoja tu, Ni Yesu Kristo. Lakini pamoja na ukweli huu leo wapo watu wanadai kusamehe dhambi. Je! ni nani hao? Yafuatayo ndiyo madhara kumsujudia mwanadamu:-

 

  “Mtu anayepiga magoti mbele ya mwandamu mkosaji, na kuungama makosa yake, na kufunua siri za moyo wake kwa huyo (1) hujihafifisha yeye mwenyewe(2) hujiondolea uthamani wake (3) Hujitia unajisi (4) Mawazo yake hushuka chini na kumfananisha na mwanadamu mwenye dhambi. Maana kwa mtu huyo Padri huwa badala ya MUNGU. Maungamo haya yanayofanywa kwa binadamu mwenye dhambi sawa na yule anayeungama kwa MUNGU, ndiyo yamekuwa asili ya uovu uliojaa katika ulimwengu mzima, hata hivyo kwa mwenye kupenda anasa na ulimwengu, huonekana kuwa fahari kuliko kujidhili mbele za MUNGU na kumfunulia siri za moyo wake. Humfurahisha mtu kulipa malipo ya kitubio kuliko kuacha dhambi na kujitenga nayo. Mtu anaona urahisi wa kujitesa yeye mwenyewe kwa njia mbalimbali, kuliko kuusulubisha mwili na tamaa zake”

E.G. White - 1 pambano kuu 323:2, GC 567:3

 

   “Rehema na msamaha ni kwa BWANA MUNGU wetu, ingawa tumemwasi” Danieli 9:9

 

Mitume na Manabii hawakuwai kudai kuwa na haki yoyote ya kusamehe dhambi, tena, walikiri wazi wazi kuwa wao ni wenye dhambi 1 Timotheo 1:15 Hata walikataa kusujudiwa.

 

  “Siku ya pili yake wakaingia Kaisaria. Na Kornelio alikuwa akiwangojea, hali amekusanya jamaa zake na rafiki zake. Petro alipokuwa akiingia Kornelio akatoka amlaki akamwangukia miguu, akamsujudia. Lakini Petro akamwinua, akasema, simama, mimi nami ni mwanadamu”. Matendo 10:24-25

 

Hata malaika alikataa kupigiwa magoti na Nabii Yohana:-

 

   “Nami Yohana ndimi niliyeyasikia na kuyaona mambo hayo. Na hapo nilipo yasikia na kuyaona nilianguka, ili nisujudu mbele ya Miguu ya Malaika yule mwenye kunionyesha hayo. Naye akaniambia, angalia, usifanye hivi; mimi ni mjoli wako, na wa ndugu zako manabii, na wa wale wayashikao maneno ya kitabu hiki. Msujudie MUNGU” Ufunuo 22:8-9

 

 

 Hata kama unacheo cha dini, huu ni udhalilishaji wa hali ya juu kabisa, kudai kupigiwa magoti. Maajabu kabisa.

“Bila shaka hakuna mwanadamu mwenye haki hapa duniani ambaye afanya mema, asifanye dhambi” Mhubiri 7:20

  Ndugu msomaji hakuna haja ya kwenda kuungama dhambi kwa mwanadamu. je! unataka kuungama dhambi zako? Fanya jambo lifuatalo;

 

  “Bali wewe usalipo, ingia katika chumba chako cha ndani, na ukiisha kufunga mlango wako, usali mbele za baba yako aliye sirini; na Baba yako aonaye sirini atakujazi” Mathayo 6:6

 

Hebu soma vitabu vifuatavyo 1 Yohana 1:9, saya 1:18

 

   “Mimi naam, Mimi, ndimi niyafuataye makosa yako kwa ajili yangu mwenyewe, wala sitazikumbuka dhambi zako. Unikumbushe, na tuhojiane; eleza mambo yako , upate kupewa haki yako” Isaya 43:25-26

 

Wale wote wanaowapigia wanadamu wenzao magoti eti kwa sababu tu anacheo cha dini, wale wanaowasujudia watu na wale wanaosujudiwa; ni zaidi ya ibada ya sanamu, bali ni makufuru.

 

   “Hebu soma mariko 2:1-10 “Naye Yesu, alipoiona imani yao, akamwambia yule mwenye kupooza, mwanangu, umesamehewa dhambi zako. Na baadhi ya waandishi walikuwako huko, wameketi, wakifikiri mioyoni mwao, mbona huyu anasema hivi? anakufuru. Ni nani awezaye kusamehe dhambi isipokuwa mmoja, ndiye MUNGU?...Lakini mpate kujua ya kwamba mwana wa Adamu anayo amri duniani ya kusamehe dhambi”. Marko 2:1-10

 

 

 

 

4: Ni sanamu za kuchora na maigizo

 

   “Sanamu ya kuchora yafaa nini, hata yeye aliyeifanya ameichora? sanamu ya kuyeyuka, nayo ni Mwalimu wa uongo, ya faa nini, hata yeye aliyeifanya aiwekee tumaini lake, na kufanya sanamu zisizoweza kusema? Habakuki 2:18

 

  “Tena BWANA ametoa amri katika habari zako,...toka nyumba ya miungu yako, nitakatilia mbali sanamu ya kuchora, na sanamu ya kuyeyusha; nitakufanyia kaburi lako; maana u mbovu”. Nahumu 1:14

 

Katika jambo la kuchora Mungu ameruhusu jambo lifuatalo:-

   “Ujumbe wa malaika wote watatu yapasa tuutawanye katika ulimwengu kwa njia ya uchapishaji (vitabu na magazeti) kwa njia ya mahubiri mbalimbali, tukionyesha kwa vielelezo, vyevye michoro ionyeshayo historia ya kiunabii mambo ambayo yalikwisha kutokea na yale yatakayotokea”.

E.G. White - Matukio ya siku za mwisho 82:1 Sura ya 6, Hosea 12:10.

 

   “Uchore historia ya unaubii tu, ukichora mengineyo ni sanamu. Sanamu ya kuyeyuka maandiko yanasema hii ni mwalimu wa uongo nayo ni- Maigizo na sanaa. Watu wamefikia mbali wametengeneza Yesu wa video. Maarifa ya kupiga picha (PHOTOGRAPHY) yalivumbuliwa mwaka 1839. Sinema zilivumbuliwa 1895. Na Yesu alibatizwa mwaka wa 27 na alikufa na kufufuka mwaka wa 31 na kupaa mbinguni soma (Pambano 315:1-3 kubwa) (Pambano 192:1-3 ndogo) Maarifa ya Photography 1839 toa 31 = 1808.

 

   Baada ya Yesu kupaa mbinguni ilipita miaka 1808 ndipo ulimwengu ukavumbua mtambo wa kupiga picha. Sasa hiyo ni sura ya Yesu wa wapi? Hata hivyo sura hiyo leo ziko picha zaidi ya tatu. Yesu mwingine anamadevu mengi, mwingine hana. Sasa ni yupi wa kweli? Tafakari; Hata hivyo Biblia kupitia Mtume Paulo ilisha tabiri jambo hilo. Kuweka sura ya mwanadamu wa kufa  na akafananishwa na sura ya mwana wa MUNGU, sikiliza;Wanadamu wote tuna dhambi.

 

   “Wakaubadili utukufu wa MUNGU asiye na uharibifu kwa mfano wa sura ya binadamu aliye na uharibifu,...kwa ajili ya hayo MUNGU aliwaacha katika tamaa za mioyo yao, wafuate uchafu, hata wakavunjiana heshima miili yao. Kwa maana waliibadili kweli ya MUNGU kuwa uongo, wakakisujudia kiumbe na kukiabudu badala ya muumba anaye himidiwa milele.Amina”. Warumi 1:23-25

 

   “Mtanifananisha na nani, na kunisawazisha naye, na kunilinganisha naye ili tuwe sawasawa? Isaya 46:5

 

  “Naye mwampenda, ijapokuwa hamkumwona; ambaye ijapokuwa hamwoni sasa, mnamwamini; na kufurahi sana,kwa furaha isiyoneneka, yenye utukufu”. 1 Petro 1:8

 Huyu Yesu anayeonekana ni Maigizo tu, hata hivyo ni ibada ya sanamu. Ni kusujudia kiumbe, ni kuabudu kiumbe, huo ndio mpango wa shetani. Hata hivyo kuweka sura ya binadamu akafananishwa na MUNGU ni kudharau utukufu wa MUNGU. Wapendwa MUNGU hafananishwi na binadamu wa kufa. Hata hivyo Biblia inasema; MUNGU aliwaacha katika tamaa za mioyo yao, ili wafuate uchafu. Yesu tunampenda, ijapokuwa hatumwoni, na tunamwamini na kufurahi sana. Lakini Yesu wa picha, Yesu aliye kwenye miti huyu ni mwingine kabisa.

 

  “Sanamu na picha ndivyo vilivyokuwa vya mwanzo kabisa kuingizwa makanisani, siyo kwa ajili ya kuabudiwa, bali ama kwa ajili ya kuchukua nafasi ya vitabu kuwapatia mafundisho kwa wale wasioweza kusoma au kuamsha na kuchochea upendo katika akili za watu wengine. Ni hakika kwamba ziko mbali sana kutimiza kusudi hilo, lakini hata kuzikubali tu lilikuwa ni suala la mda tu, lakini lilikoma kuwa hivyo mapema sana, na ikaoneka kwamba picha na sanamu zinaleta giza makanisani badala ya kuangazia akili za wale wasioelewa - ziliuwa upendo kwa anayeabudu badala ya kuinua upendo wake. Hivyo basi, hata kama zingelenga kuelekeza akili za watu wa MUNGU, zinaishia katika kuwageuza kutoka kwake na kuwafanya waabudu vitu vilivyoumbwa? E.G.White - Pambano kuu 645:2, GC 680:2       

 

5.  Sanamu za mafundisho ya uongo

 

 “Ni vyepesi kufanya sanamu ya mafundisho ya uongo, sawa sawa na kufanya sanamu ya kuchonga. Kwa wengi sanamu ya falsafa inasimikwa na kutawazwa mahali pa Yehova... Maelfu ya watu wanaaabudu viumbe huku wakimkataa MUNGU wa viumbe....hakika leo ipo ibada ya sanamu katika ulimwengu wa Kikristo katika mtindo tofauti kama ilivyokuwepo katika Israel ya zamani katika siku za Eliya. Mungu wa watu wengi wanaojidai kuwa na hekima, wanafalsafa, watungaji wa mashairi, wanasiasa, waandishi wa habari - ni mungu wa kutengenezwa na kunakishiwa, na vyuo vingi, na vyuo vikuu, hata na baadhi ya taasisi nyingi za thiolojia ni mungu anayezidi Baali kidogo tu, mungu jua wa Wafoeniki”. E.G. White - Pambano kuu 554:1 Kubwa 332:3 ndogo ni sura 36

 

6. Kundi la sita kupiga picha

   “Kupiga picha na kuweka ukutani, wanajaza Albam na kuweka sebuleni, kwenye fremu, mabankara na kwenye meza. Hii nayo ni ibada ya sanamu...fedha hizo:

          1.       Zingetumika kubariki watu.

          2.       Zingetumika kupunguza makali ya mateso katika maisha

          3.       Zingetumika kuvisha walio uchi

          4.       Zingetumika kulisha walio na njaa

          5.       Zingewekwa katika hazina ya BWANA ili kuokoa walio dhambini”.

                    E.G. White - 1 Maranatha 48:1

 

 

Ukutani ndani ya nyumba kwa mjibu wa maandiko upambe nini?

   “Sikiliza, Ee Israeli, BWANA, MUNGU wetu, BWANA ndiye mmoja. Nawe mpende BWANA MUNGU wako, kwa moyo wako wote, na kwa roho yako yote, na kwa nguvu zako zote. Na maneno haya ninayokuamuru leo, yatakuwa katika moyo wako; nawe uwafundishe watoto wako kwa bidii, na kuyanena uketipo katika nyumba yako, na utembeapo njiani, na ulalapo na uondokapo. Yafunge yawe dalili juu ya mkono wako, nayo yatakuwa kama utepe katikati ya macho yako. Tena yaandike juu ya miimo ya nyumba yako, na juu ya malango yako”. K/torati 6:4 - 9

 

“ Muumba wetu anadai uchaji wetu katika kiwango cha juu kabisa, na utiifu wetu wa kwanza. Chochote kinachoonekana kupunguza upendo wetu kwa MUNGU, au kuingilia utumishi ambao upo kwa ajili yake, kwa namna hiyo kinakuwa sanamu. Kwa baadhi ya watu, ardhi zao, nyumba zao, bidhaa zao, ni sanamu zao. Shughuli za biashara zinatekelezwa kwa ari na nguvu, hali utumishi kwa MUNGU ikifikiriwa kuwa ya pili. Ibada ya familia inaachwa, maombi ya siri yanasahaulika. Wengi wanadai kutendeana kwa haki na wenzao, na wanaonekana kuhisi kuwa kwa kutenda hivyo wanatekeleza wajibu wao wote. Lakini haitoshi kushika amri sita za mwisho za sheria ya MUNGU. Upungufu wowote katika kutii kila kanuni...nikigezo tosha kwetu kushidwa kukidhi madai ya sheria ya mbinguni.

 

  Wapo wengi ambao mali zimefanya mioyo yao kuwa migumu kiasi cha kumsahau MUNGU na kusahau matakwa ya wanadamu wenzao. Wale wajiitao Wakristo wanajipamba kwa vito, nguo zilizopambwa, mavazi ya gharama kubwa, hali maskini wa BWANA wakiteseka kwa kukosa mahitaji muhimu ya maisha. Wanaume kwa wanawake wanaodai kuwa wamekombolewa kwa njia ya damu ya mwokozi wanafuja mali ambayo wamekabidhiwa kwa ajili ya kuokoa roho, na halafu wanasita kutoa sehemu kwenye sadaka zao kwa ajili ya dini, huku wakitoa kwa ukarimu pale tu ambapo itawaletea heshima kwa kufanya hivyo. Hawa ni waabudu sanamu. Chochote ambacho kinachopotosha akili kutoka kwa MUNGU kinachukua nafasi ya sanamu na hiyo ndiyo sababu ya kuwa na nguvu ndogo kiasi hicho kanisani leo.

 

 Amri ya pili inakataza kumwabudu MUNGU wa kweli kupitia kwa sanamu au mifano... Akili zikiwa zimegeuzwa mbali na ukamilifu usio na mwisho wa Yehova, Zinaweza kuvutwa kwa kiumbe badala ya muumbaji. MUNGU ni mtafiti wa mioyo. Yeye hutambua tofauti kati ya utumishi wa kweli wa moyo na ibada ya sanamu”. E.G.White - 1Wana na Binti za mungu uk.55,

 

Umebarikiwa sana kupata somo hili mkononi mwako  na amini nimeujua ukweli  na sasa uwe tayari kuushikilia. Karibu katika kanisa la Mungu lenye kushika amri kumi, karibu katika ukweli.

Ni Waadventista Wasabato (Wanamatengenezo) Dodoma - Tanzania. 

Share:

Popular Posts

Lebo

Recent Posts

Pages