Katika blogu hii, tutachunguza njia mbalimbali za kuimarisha ufahamu wetu wa Biblia. Tutajadili mbinu za kusoma Biblia kwa ufanisi, vidokezo vya kukariri maandiko matakatifu, na mikakati ya kutumia somo la Biblia katika maisha yetu ya kila siku. Iwe wewe ni mtaalam wa Biblia mzoefu au unaanza tu safari yako ya imani, "Jifunze Biblia Zaidi" ni rasilimali kamili ya kukusaidia kuongeza ufahamu wako wa Maandiko Matakatifu na kumkaribia Mungu zaidi.

2.IFUATAYO NDIYO NJIA YA KUMTAMBUA NABII WA KWELI NA NABII WA UONGO.

1.   IFUATAYO NDIYO NJIA YA KUMTAMBUA NABII WA KWELI NA NABII WA UONGO.

SOMO:MIUJIZA INAENDELEA................................


Na katika hili twajua ya kuwa tumemjua yeye ikiwa tunashika amri zake. Yeye asemaye, nimemjua, wala hazishiki amri zake, ni muongo, wala kweli haimo ndani yake” 1YOHANA 2:3-4

“kwa maana watu hawa ni watu waasi, watoto wasemao uongo, watoto wasiotaka kuisikia sheria ya BWANA”ISAYA 30: 9

          Kipimo cha kumtambua nabii wa kweli na nabii wa uongo kiko katika Biblia yenyewe, usiulize mchungaji wako, usiulize wazazi wako, wala mke au mume wako,usiulize mwanao.Na kipimo hicho ni ikiwa anazishika amri. Na kama anadai kumjua MUNGU na huku hazishiki amri ndiye nabii wa uongo;wala kweli (neno la Mungu) halimo ndani yake (Yohana17:17) Kwa maana wasio taka kuitii sheria ya MUNGU ni waasi, na wanamafundisho ya uongo. Hata maombi yao ni udanganyifu tu maana MUNGU ameangiza ifuatavyo juu ya maombi;

“Na lolote tuombalo tutalipokea kwake, kwakuwa twazishika amri zake; na kuyatenda yapendezayo machoni pake”1YOHANA 3:22

           Mpenzi msomaji ili kumjua nabii wa uongo Biblia hapa inachofundisha ni kuwa wanakataa amri kumi za MUNGU.Na mojawapo ya amri kumi ni amri ya nne, yaani amri ya sabato, na huo ndio mpango wa shetani leo kuwafanya watu wawe wanasali lakini wanavunja amri angalau moja tu, basi huwa makusudi yake yametimia.Maana katika hesabu ya mbinguni amri kumi ukitoa amri moja jawabu ni sifuri.Divyo neno la MUNGU linavyotufundisha katika kitabu cha Yakobo;Neno linasema;

“Maana mtu awaye yote atakayeshika sheria yote, ila akajikwaa katika neno moja (amri moja) amekosa juu ya yote. Kwa maana yeye aliyesema, usizini, pia alisema, usiue. Basi ijapokuwa hukuzini, lakini umeua, umekuwa mvunja sheria”YAKOBO 2;10-11

 

Hiki ndicho kipimo

1.   Nabiiwa kweli anashika amri kumi

2.   Nabii wa uongo anakataa amri kumi

Uchaguzi ni wako utaenda wapi? MUNGU anawatumishi wanashika amri.

Shetani naye anawatumishi hawataki amri, ila wanafanya miujiza, na wakiwa na majina makubwa makubwa.Mara utasikia matangazo huyu anayekuja ni nabii na mtume. Lakini wao wenyewe hawakubaliani, kila mtu anakanisa lake.Kwanini hawapatani, kwanini hawakubaliani, wakati mitume na manabii wa MUNGU hawakupingana?Kupitia manabii hawa injili makanisani imebadilika;

·         Kila kanisa njoo uponywe

·         Kilakanisa njoo utajirike

·         Kila kanisa njoo upandishwe cheo

·         Kila kanisa njoo upate mchumba

Manabii wa uongo wanaibada,wanasali, wanamakanisa na wangeitumia biblia, na wengetumia jina la Yesu.Lakini wakiwa na lengo la kupoteza hata wateule.

“Umizimu sasa unababdilisha mfumo wake, ukiwa umeficha baadhi ya sehemu zake muhimu zinazochukiza, sasa umejivika vazi la Kikristo …. Wakati zamani ulimkana Kristo na Biblia, sasa unakiri kukubali vyote viwili” (Biblia na Ukristo) E.G White – Dhiki kuu uk,61:1

 

3.   KIAPO CHA SHETANI

“Nawe ulisema moyoni mwako, nitapanda mpaka mbinguni, nitakiinua kiti changu juu kuliko nyota za MUNGU; nami nitaketi juu ya mlima wa mkutano, katika pande za mwisho za kaskazini.Nitapaa kupita vimo vya mawingu, nitafanana na yeye aliye juu. Lakini utashushwa mpaka kuzimu; mpaka pande za mwisho za shimo. Wao wakuonao watakukazia macho, watakuangalia sana, wakisema je! huyu ndiye aliyeitetemesha dunia, huyu ndiye aliyetikisa falme; aliyeufanya ulimwengu ukiwa akaipindua miji yake; asiyewafungua wafungwa wake waende kwao?”ISAYA 14;13

 

 

Hiki ndicho kiapo cha shetani; ingawa na angamizo lake linatajwa hapo hapo. Aliapa kuwa angefanana na yeye aliye juu.

1.   Aliye juu anakanisa – shetani naye ana makanisa

2.   Aliye juu anaabudiwa – shetani naye anaabudiwa

3.   Aliye juu anamanabii – shetani naye ana manabii

4.   Aliye juu ana mitume – shetani naye ana mitume

Ila cha ajabu watumishi wa shetani wangefanyaibada, miujiza, siyo kwa jina la shetani, bali kwa jina Yesu; ndipo ulimwengu ungewapokea na kuwaamini. Ndugu msomaji katika jambo hili umepona?

“Watu wangu wamekuwa kondoo waliopotea, wachungaji wao wamewapoteza; wamewapotosha milimani;(makanisani) wamekwenda toka mlima hata mlima (kanisa hadi kanisa)wamesahau mahali pao pa kupumzika”.                 YEREMIA 50: 6

Mpaka leo ni watu wengi wanaohama kanisa hadi kanisa wakitafuta miujiza, wengine wakitafuta ukweli; sababu ya kukoseshwa na wachungaji. Na watu wamesahau mahali pao pa kuabudu yaani kwa wanao shika amri.

“Na ishara hizi zitafuatana na hao waaminio; kwa jina langu watatoa pepo; watasema kwa lugha mpya;watashika nyoka; hata wakinywa kitu cha kufisha, hakitawadhuru kabisa; wataweka mikono yao juu wagonjwa, nao watapata afya”MARKO 16:17

          Shetani akalidaka hilo maana aliazimu kufanana na yeye aliye juu. Swali,je, watumishi wa shetani wanao uwezo wa kufanya miujiza? Ndio; mtumishi wa Mungu Paulo anajibu swali hili;

“Maana watu kama hao ni mitume wa uongo, watendao kazi kwa hila, wanaojigeuza wawe mfano wa mitume wa Kristo.Wala si ajabu.Maana shetani mwenyewe hujigeuza awe mfano wa malaika wa nuru.Basi si neno kubwa watumishi wake nao wakijigeuza wawe mfano wa watumushi wa haki ambao mwisho wao utakuwa sawasawana kazi zao’’2 KORINTHO 11;13-15.




 Mpendwa msomaji endelea kufuatilia makala hii na Mungu akubariki AMINAAA!!!!!!
                               ITAENDELEA....
Share:

MIUJIZA, MANABII WA UONGO



 MIUJIZA
Katika somo hili tutajifunza mambo yafuatayo:
1.   Manabii wa uongo
2.   Njia ya kumfahamu nabii wa kweli na nabii wa uongo
3.   Kiapo cha shetani
4.   Je shetani, ama watumishi wa shetani, wanaouwezo wa kufufua?
5.   Uchawi wa zamani na uchawi wa kisasa
6.   Je, uko nyuma shetani aliwahi kufanya miujiza?
7.   Ni jinsi manabii wa uongo wanavyotafuta hela
8.   Tutajifunza ibada za manabiii wauongo jinsi wananvyoomba
9.   Je, wacha MUNGU wanaombaje?
10.  Miujiza ya uongo ni ubunifu kutoka taifa gani na toka makanisa gani?
11.  Ni roho za mashetani
12.  Jambo la mwisho tutakalo jifunza. Je, waatumishi wa MUNGU waaminifu leo wanaweza kufanya kazi kwa njia ya miujiza?
Katika ulimwengu wa Kikristo wa siku hizi za mwisho tunashuhudia matangazo makubwaya miujiza, tunasikia na kuona kwenye vyombo vya habari mahubiri ya uponyaji, mahubiri ya utajirisho; mara utasikia matangazo kwenye redio au kwenye television au gari mtaani au vipeperushi;
1.   Viwete watatembea
2.   Matumbo yaliyofungwa yatafunguliwa
3.   Utapandishwa cheo kazini
4.   Njoo uponywe
5.   Njoo utajirike
Je, haya yote yanayofanyika sasa ni kweli? Hebu fungua moyo wako Roho wa MUNGU azungumze na wewe na sasa ukweli halisi unaomkononi. Somo hili hakikisha usilipoteze maana ni ufunguo wa kukutoa gizani bali zalisha uwagawie na wengine.
          Mpenzi wangu msomaji miujiza ya uongo ni miongoni mwa dalili za kurudi kwa Yesu. Hebu sikiliza Yesu mwenyewe alivyosema;

1.   MANABII WA UONGO
“Kwa maana watatokea makristo wa uongo na manabii wa uongo nao watatoa ishara kubwa na maajabu (miujiza) wapate kuwapoteza kama yamkini hata walio wateule”MATHAYO 24:24.
Umesikia ndugu msomaji kutokea kwa makristo wa uongo, manabii wa uongo, wanaofanya miujiza na maajabu; ni lengo la shetani kuwatumia hawa ili kuwapoteza hata walio wateule. Je, watapoteaje?  Wataamini uongo sababu ya ishara, sababu ya miujiza.Jambo hili limeshatimia katika siku zetu. Leo tunashuhudia watu wanaojiita wenyewe kuwa ni manabii na mitume, wenye majina ambayo hatuyasomi katika maandiko.  Hayamo, mfano:
1.   Mungu wa bendera
2.   Mungu wa upako
3.   Mungu wa epafa
4.   Mungu wa ngurumo
5.   Mungu wa yawe
6.   Baba Godi – yaani yeye ni baba yake na Mungu.Maajabu kabisa. Ni kwambie ndugu msomaji haya ni majina yanayotukuza miungu siyo MUNGUmuumbaji.
MUNGU anao manabii na mitume. Na manabii na mitume wa MUNGU hatuko nao kimwili maana walikwisha toweka.Ila tunao kupitia maandishi yao, lakini shetani anamanabii na mitume ambao wanaonekana na wanaofanya ishara.
JE, MANABII WA UONGO NI NINI?
“Jiadharini na manabii wa uongo watu wanaowajia wamevaa mavazi ya kondoo walakini kwa ndani ni umbwa mwitu wakali.Mtawatambua kwa matunda yao” MATHAYO 7:15
          AH – manabii wa uongo ni watu.Je, kuja wamevaa mavazi ya kondoo maana yake ni nini? Wanakuja wakijifanya kuamini ukristo; kuamini Biblia,ila kwa ndani ni mbwa mwitu na si mbwa mwitu tu, bali mbwa mwitu wakali. Andiko hilo mwishoni linamaliza kwa kusema kuwa mtawatambua kwa matunda yao.
 

                                 Mpendwa msomaji endelea kufuatilia makala hii na Mungu akubariki AMINAAA!!!!!!
                               ITAENDELEA.

 KWA MAWASILIANO ZAIDI WASILIANA NASI

0756959525,0752164685 
Share:

Popular Posts

Lebo

Recent Posts

Pages