Katika blogu hii, tutachunguza njia mbalimbali za kuimarisha ufahamu wetu wa Biblia. Tutajadili mbinu za kusoma Biblia kwa ufanisi, vidokezo vya kukariri maandiko matakatifu, na mikakati ya kutumia somo la Biblia katika maisha yetu ya kila siku. Iwe wewe ni mtaalam wa Biblia mzoefu au unaanza tu safari yako ya imani, "Jifunze Biblia Zaidi" ni rasilimali kamili ya kukusaidia kuongeza ufahamu wako wa Maandiko Matakatifu na kumkaribia Mungu zaidi.

Inaonyesha machapisho yaliyo na lebo MAHUBIRI. Onyesha machapisho yote
Inaonyesha machapisho yaliyo na lebo MAHUBIRI. Onyesha machapisho yote

MWILI WA ASILI CHANZO CHA UTUMWA WA DHAMBI!

MWILI WA ASILI CHANZO CHA UTUMWA WA
DHAMBI!

Amani ya Bwana iwe nanyi wapendwa!
Kama kilivyo kichwa cha habari hapo
juu,tuchangie kuangalia mojawapo ya sifa za
mwili wa asili ambacho ndicho chanzo cha
utumwa wa dhambi!
Paulo asema:«Ndivyo ilivyoandikwa, Mtu wa
kwanza, Adamu, akawa nafsi iliyo hai; Adamu
wa mwisho ni roho yenye kuhuisha.Lakini
hautangulii ule wa roho, bali ule wa asili;
baadaye huja ule wa roho.Mtu wa kwanza
atoka katika nchi, ni wa udongo. Mtu wa pili
atoka mbinguni.Kama alivyo yeye wa udongo,
ndivyo walivyo walio wa udongo; na kama
alivyo yeye wa mbinguni, ndivyo walivyo walio
wa mbinguni.Na kama tulivyoichukua sura
yake yule wa udongo, kadhalika tutaichukua
sura yake yeye aliye wa mbinguni.»1Kori
ntho15:45-49
Kakika mafungu haya tunaona akina Adamu
wa wili(Adamu wa Edeni na Adamu wa
mbingu)
*Adamu wa Edeni ni wa udongo,
*Adamu wa Mbinguni ni wa Roho,
★Anasema kuwa wote kwa kuazliwa
tulichukuwa asili ya baba yetu wa dunia,ila
kwa neema ya damu ya Yesu twaweza kuingia
katika muunganiko wa kuchukua asili ya
Adamu wa mbinguni!
Wapendwa baada ya dhambi kuingia
ulimwenguni,mwanadamu alijiunga na adui
wa Mungu kupinga makusudi ya mbingu,na
kadri alivyo kuwa na kuimarika katika asili
hiyo,aliendelea kuwa mbali na Mungu na
kuvumbua uasi mpya!!
Soma hapa:«Baada ya dhambi,sheteni
hakupumzika aliazimia atakao waangusha
kama yy alivyoanguka.Kama alivyowadangany
a malaika ili wamgomee Mungu ndivyo
alivyomshawishi Adamu(wa udongo) kukiuka
(violer) sheria ya Mungu.Hivyo Adamu akaasi
kama Lucifer.Zaidi ya hayo Shetani na Adamu
wakawa marafiki,na wakajipanga kushambulia
mbingu kwa pamoja!»GC chap30 uk503
Nasi tukazaliwa na huyo huyo na kwa asili
tukawa tu maadui wa mapenzi ya Mungu na
tukawa hatuna nguvu ya kutenda mema na
ndiyo sababu mnaona huwa :udokozi,wizi,k
utukana,kukasirika,kulipiza kisasi,kuzini,nk
hayo hayafundishwi bali ni asili ya kila
mwanadamu!!!!!!
Paulo asema:«Kwa hiyo, kama kwa mtu
mmoja dhambi iliingia ulimwenguni, na kwa
dhambi hiyo mauti; na hivyo mauti ikawafikia
watu wote kwa sababu wote wamefanya
dhambi»Rumi5:12
Kwa sababu hizo ndani yetu kupitia Adamu
tulipoteza uwezo wa kutii sheria ya Mungu,
(Rumi8:7) na hicho ndicho chanzo cha wengi
hawawezi kutulia ndani ya Haki ya Mungu!
Yesu alisema:«Yesu akawajibu, Amin, amin,
nawaambia, Kila atendaye dhambi ni mtumwa
wa dhambi.Wala mtumwa hakai nyumbani
sikuzote; mwana hukaa sikuzote.Basi Mwana
akiwaweka huru, mtakuwa huru kweli
kweli»Yohana8:34-
Hiyo ndiyo sababu unaona wengi hujidai_,oh
mimi ni mtumishi,oh mimi nineokoka
oh...kama mafarisayo walivyomjibu
Yesu,wakisema kuwa wao si watumwa wa
mtu,kwa usemi mwingine walimwambia sisi
tumeokoka Yesu, # swali la kujiuliza ni“mimi
nimtumwa au niko huru?”
# Kuwa huru nje ya dhambi,siyo kuwa:
*mhubiri,*mchungaji,*
mwinjilisti,*mzee wa
kanisa nk ni zaidi ya hayo!!
Maana mmekuwa mkishuhudia ninyi wenyewe
wenye vyeo hivyo lakini,wakiwa bado
wanalawiti wafanyakazi wao,kutembea nje ya
ndoa,wengine kupata ukimwi nje ya
ndoa,kusuka nywele,kuklimu,vimini,suluale
kwa wana-mama nk(Je kweli hawa
wameokoka?)
WAPI NIPATE MSAADA WA KUNIPONYA?
____________________________
Paul alipokuwa bado ni mtumwa aliguswa na
hali ya Kimungu hivyo akalia akisema:«Ole
wangu, maskini mimi! Ni nani atakayeniokoa
na mwili huu wa mauti?»Rumi7:24
Yesu alijibu na kuwaita wote waliojikuta ktk
hali hiyo akisema:"Njooni kwangu ninyi
nyote»Mathayo11:28
Hapa aliahidi kukupa nguvu na uwezo,uwezo
ule ulioupoteza ktk Adamu wa udongo
utaupokea ktk Adamu wa Roho kwa njia ya
imani!
Yesu asema:«Bali wote waliompokea aliwapa
uwezo wa kufanyika watoto wa Mungu, ndio
wale waliaminio jina lake»Yoh1:12
Ombi:Katika jina la Yedu na kupitia damu
yenye nguvu ya Kalvary,pokea nguvu,na uwezo
ili kushinda mwili wa asili,Kristo aanzishe vita
ndani yako akishindana na utu wa kale,ili
akupe nguvu za kuishi utu upya na kudumu
ktk Uhuru nje ya Dhambi»
Ninyi mmekuwa rafiki zangu, mkitenda
niwaamuruyo»Yoh15 :14


KWA MAWASILIANO ZAIDI WASILIANA NASI
0756959525,0752164685
Share:

Vipindi 7 Vya Kanisa Katika Michakato Minne

 
MUHIMU: Somo hili limeelekezwa zaidi kwa kaka zetu na dada wa imani ya Kisababto ambao wanajifunza unabii. Hata hivyo, hii haina maana ya kusema kuwa wale walio nje ya SDA hawataweza kuona huu Ukweli kama vile ulivyo kwa sababu ni tukio la unabii hakika, na linatokea kwa uhakika katika siku zetu!
     Katika historia yote ya watu wa Mungu tunaona tabia moja inayojirudia na iliyobarikiwa. Imesemwa wazi kwa vielelezo kwa muda kwamba siyo sifa tu, hata hivyo, lakini zaidi uhitaji. Bila shaka ninaongea kutoka katika uhitaji wa moyo kuwa “Tokeni kwake, enyi watu wangu” ili kumfuata Bwana vizuri zaidi popote anapoweza kuongoza.
     Kama tukichunguza njia ambayo Baba aliwaongoza watu wake kutoka Babeli, michakato mitatu ya  iliyopita ya Kanisa lake; tutaweza kuona vizuri zaidi mapenzi ya Roho Mtakatifu katika mchakato wa nne na wa mwisho wa Kanisa la Mungu.

     “Ninataka kusistiza ukweli, kwamba Makanisa ambayo Yohana aliambiwa kutuma maelekezo aliyopewa huwakilisha Makanisa yote katika ulimwengu wetu, na kwamba huu ufunuo kwake unapaswa kujifunzwa na kuaminiwa na kuhubiriwa na Kanisa la Waadventista Wasabato leo. Kristo alikuja binafsi kwa Yohana kumwambia, ‘Mambo hayo…yaliyopo, na yale yatakayokuwa baada ya hayo’ (Ufu 1:19). Na kisha akaniambia, ‘Haya uyaonayo uyaandike katika chuo, ukayapeleke kwa hayo makanisa saba’ (Ufu 1:11). Nuru haikutakiwa kufichwa chini ya pishi.”
     “Katika ufunuo ambao Kristo alitoa umeungwa pamoja katika mnyororo wa ukweli ujumbe muhimu wa onyo na kwa dhahiri unapaswa kutolewa kwa ulimwengu kabla ya ujio wa pili wa Kristo. Ujumbe wa mwisho wa rehema unapaswa kuhubiriwa mahali ambapo haujapata kusikiwa. Watenda kazi wanapaswa kufanya kazi kwa kujinyima nafsi, kwa namna hiyo ya kujitoa, kiasi kwamba ujumbe utapelekwa kwa wale ambao hawajapata kuusikia” (“Manuscript Releases,” 1:372).

     Ujumbe kwa Makanisa saba, pasipo swali, ni lazima uhubiriwe katika karne zote. Leo, kikiwa ni kipindi wa Kanisa la mwisho, tumeitwa kupokea ujumbe wote kutokana na uharaka wa wakati tunaoishi ndani yake. Ni maarifa ya kawaida kwamba Ibilisi anajua kuwa ana muda mchache, kwa hiyo, kusema kweli, anazunguku kila mahali ulimwenguni akimmeza kila anayeweza. Haijapata kutoke katika historia ya Kanisa kabla tulipoona mchezo wa ushambuliaji uliopangwa kwa watu wa Mungu. Adui amejifunza kila somo kwa kusoma madhaifu ya watu wa Mungu zaidi ya miaka 6,000 na linatumiwa dhidi yetu.
     Unabii hauongelei Makanisa manane balisaba. Hivi vipindi saba vya unabii vilivyoongelewa katika Ufunuo sura ya pili na ya tatu vinaonyesha kile ambacho ingemchukua Roho Mtakatifu kuweka sawa tabia za wale “walioitwa kutoka” huko na kuingia katika ukamilifu huo uliotabiriwa. Masalio hawa humtukuza Baba kuliko yeyote anavyoweza. Hawa ni watu wa pekee, “wazao wake waliosalia,” (Ufu 12:17) ambao wanapokea muhuri wa Mungu aliye hai.
     Mchakato wa watu wa Mungu wakati wa kipindi cha Makanisa saba, bila shaka, ni wale walioitwa kutoka Babeli “kumfuata Mwana-Kondoo kila aendako” (Ufu 14:4). Michakato hii imepambanuliwa kuwa watoto wa Mungu wakitenda sawa na mapenzi yake makamilifu yalivyowataka watende. Michakato yao inaonekana kama bado ni njia ya kumthibitisha Bwana Yesu Kristo na ukweli wake kama wa juu. Kwa sababu pasipo mkono wake kuhusishwa, wasingechukua hata hatua moja katika sehemu ya kwanza. Na mahali pasipo na hatua, hakuna mchakato.
     “Kutoka karne hadi karne Kristo alikuwa ametoa hazina zake kwa Kanisa, na kutoka kizazi kimoja  hadi kingine watumishi wake waaminifu wameendeleza talanta walizopewa. Karama ambazo miaka  elfu moja mia nane iliyopita aliziweka katika mikono ya wahudumu wake waliochaguliwa, mitume kumi na wawili, zimeshuka kwa watenda kazi wake katika kizazi hiki. Na bado ni watu wachache kiasi gani kati yetu wanatambua bahati hii, na nafasi yetu kama wahudumu wa neema yake” (“Manuscipt Releases,” 5:358.).
Siku moja haitakiwi kuwa ya kipekee. Bwana alisema waziwazi: “Mimi nipo pamoja nanyi siku zote, hata ukamilifu wa dahari” (Mt 28:20). Yuko pamoja nasi! Hatupaswi kuwa na jicho lililopofuka, au mgongo uliopoa kwa wito tunaohisi ukivuta roho zetu kabisa. Kufanya hivyo kungekuwa udanganyifu kwa mioyo yetu.
     “Ulimwengu unajiandaa kwa pambano kuu la mwisho, taifa kuinuka dhidi ya taifa jingine. Jamii kubwa ya wanadamu wanachukua misimamo yao kinyume na Mungu. Lakini katika kila kizazi Bwana Yesu amekuwa na mashahidi wake—masalio waliotumaini katika neno la Mungu. Na leo, katika kila sehemu kuna wale wanaofanya ushirika na Mungu. Mvuto muhimu wa mfereji wa chini unawaongoza kwenye nuru, na wakati swali linapokuja kwao, ‘Nani aliye upande wa Bwana?’ watachukua nafasi zao upande wake. Tabia yao imebadilishwa kufanana na tabia ya uungu, kwa sababu wamesoma na wanatembea sawa na mafundisho ya Neno lake” (“Signs of the Times,” Novemba 23, 1904).
  Kwa nini michakato minne? Mungu ni Mungu wa utaratibu na kanuni. Kila kitu katika utendaji Wake kipo katika kanuni zake. Mungu hutenda kazi katika hatua nne ili kufikia kukomaa kwa kazi Yake na mavuno kupatikana.  Imeandikwa: “…..nawapatiliza wana maovu ya baba zao, hata kizazi cha tatu na cha nne……Bwana akamwambia Ibrahimu, Ujue hakika ya kwamba uzao wako utakuwa mgeni katika nchi isiyo yake, watawatumikia watu wake, nao watateswa muda wa miaka mia nne. Na kizazi cha nne kitarudi hapa, maana haujatimia uovu wa Waamori bado.” Kutoka 20:5; Mwanzo 15:13, 16.
Katika amri ya pili Mungu alimaanisha vizazi vinne kutoka kwa Adamu wa kwanza hadi Adamu wa pili yaani Kristo. Vizazi hivyo ni kama ifuatavyo: kwanza Adamu – Nuhu (Mwanzo 5); pili Nuhu – Ibrahimu (Mwanzo 11); tatu Ibrahimu hadi Yesu (Matthayo 1:2-16) na nne, Yesu hadi mwisho wa dunia (Matthayo 24:34.)
Kwa Ibrahimu, Mungu alimuambia kwamba kizazi chake cha nne ndicho kitarudi kwenye nchi ya ahadi baada kutumika kwa miaka mia nne katika nchi ya utumwa. Kizazi cha kwanza cha Ibrahimu ni Isaka, kizazi cha pili ni Yakobo, kizazi cha tatu ni watoto 12 wa Yakobo na kizazi cha nne ni watoto wa watoto 12 wa Yakobo. Tunatambua kwamba watoto 12 wa Yakobo walifia Misri na wakati Waisraeli wanatoka Misri walibeba mifupa ya Yusufu na kuondoka nayo (Mwanzo 50:25.)
Katika Maandiko hayo tunatambua kwamba haikuwa kwa kubahatisha kwamba Mungu alitoa Amri ya pili na kuielezea katika mpangilio wa vizazi vinne kwa wale watakaokwenda kinyume na matakwa yake. Pia alimwambia Ibrahimu kwamba uzao wake utakaa Misri kwa miaka mia nne katika hali ya utumwa ambapo sababu ya kuwa huko kwa kipindi hicho ni kusubiri uovu wa Waamori ufikie katika kipimo cha kujaa kikombe.
Akiwa hapa duniani, Yesu alifundisha “Akasema, Ufalme wa Mungu, mfano wake ni kama mtu aliyemwaga mbegu juu ya nchi; akawa akilala na kuondoka, usiku mchana, nayo mbegu ikamea na kukua asivyojua yeye. Maana nchi huzaa yenyewe; kwanza jani, tena suke, kisha ngano pevu katika suke. Hata matunda yakiiva, mara apeleka mundu, kwa kuwa mavuno yamefika.”
Hizi ndizo hatua nne katika kanuni ya utendaji wa Mungu ili kupata mavuno katika ufalme wa Mungu; yaani hatua ya kwanza ni jani, ya pili ni suke, tatu ni ngano pevu katika suke na nne ngano iliyokwisha kuiva au kukomaa tayari kwa mavuno. Je,  mavuno katika uharibifu yanapatikana kupitia hatua ngapi? “Lakini kila mmoja hujaribiwa na tamaa yake mwenyewe….Halafu ile tamaa ikiisha kuchukua mimba huzaa dhambi, na ile dhambi ikiisha kukomaa, huzaa mauti.” Yakobo 1:14,15. Hatua nne pia kuelekea kuvunwa katika uharibifu, kwanza tamaa, pili mimba, tatu dhambi na nne mauti.
Ilikuwa ni kupitia hatua nne pia kwamba Mungu aliwasafirisha Israeli wa kale kutoka Misri kwenda nchi ya ahadi ya Kanani. Hatua ya kwanza ilikuwa ni kutoka Misri hadi bahari ya Shamu; hatua ya pili ilikuwa ni kutoka bahari ya Shamu hadi Sinai; tatu kutoka Sinai hadi Kadesh na nne ni Kadesh hadi Kanani. Ndiyo maana Israeli wa leo, yaani kanisa la Mungu baada ya Israeli wa kale, lazima lisafirishwe na Mungu katika hatua nne ndipo wale watakaokuwa wamekomaa kama ngano safi watavunwa katika ufalme wa Mungu.
Ili kukamilisha safari ya Israeli wa leo, Mungu analiongoza kanisa Lake kupitia katika vipindi saba vilivyoonyeshwa kupitia nabii Yohana. Wengi kwa kutojifunza chini ya uongozi wa Mungu, wameshindwa kutambua jinsi Mungu anavyoliongoza kanisa Lake katika siku hizi za mwisho.
Kabla ya vipindi saba vya kanisa saba havijajapata kuwepo, wokovu ulikuwa ni wa Wayahudi, na pasipo shaka, hili ndilo lilikuwa Kanisa la Mungu. Lakini kwa sababu Wayahudi walimwasi Mungu, hawakuwa tena kanisa lake. Mungu ataendelea kutenda kazi kwa kutumia kanuni hii hadi kukomaa kwa mavuno ya kanisa lake.
Basi tuna Michakato Minne sambamba na vipindi Saba vya Kanisa la Yesu:
Kipindi cha kanisa            Jina                                             Hatua

Efeso
Smirna
Pergamo
Thiatira
Ukristo
1

 Sardi
Filadelfia
Uprotestanti
2

Laodikia
Uadventista
3

Masalio wa SDA
4


gray-tl

gray-tr


1. Efeso (31-100 B.K.) “…na ya kuwa huwezi kuchukuliana na watu wabaya” (Ufu 2:2, 3, 6, 7).
Mchakato wa Kikristo – Mitume wanahubiri ukweli kwa ulimwengu katika hali ya juhudi za umisionari uliobarikiwa sana uliojulikana kwa mwanadamu (Mdo 13:46; 17:6; 18:6)
2. Smirna (100-313 B.K.) “...Naijua dhiki yako na umaskini wako, (lakini u tajiri)” (Ufu 2:9, 10).
3. Pergamo (313-538 B.K.) “...nawe walishika sana jina langu, wala hukuikana imani yangu” (Ufu 2:13, 17)
4. Thiatira (538-1517 B.K.) “...wowote wasio na mafundisho hayo…sitaweka mzigo mwingine” (Ufu 2:24-26).
5. Sardi (1517-1798 B.K) “Lakini unayo majina machache...watu wasioyatia mavazi yao uchafu” (Ufu 3:4, 5). 
Mchakato wa Kiprotestanti – Matengenezo ya Kiprotestanti na mashahidi wake wengi (Ufu 7:13-17).
6. Filadelfia (1798-Ujio wa pili wa Kristo) “Yeye ashindaye…nitaandika juu yake…jina langu mwenyewe” (Ufu 3:7-13, angalia dondoo Na. 1).
7. Laodikia (1844-Ujio wa pili wa Kristo) “Nayajua matendo yako, ya kuwa hu baridi wala hu moto” (Ufu 3:14-21).
Mchakato wa Waadventista – Uamso mkuu ambao ulitoka ulimwenguni kote sawasawa na unabii wa siku 2300 wa Danieli 8:14 na ulihubiriwa kuonyesha kuwa saa ya hukumu ilikuwa imekuja (Ufu 10:1-11; 14:6-8; angalia pia Dondoo Na. 2).
Mchakato wa Masalio wa Siku ya Saba – “Joka akamkasirikia yule mwanamke (kanisa la SDA), akaenda zake afanye vita juu ya wazao wake waliosalia (Masalio wa SDA), wazishikao Amri za Mungu, na kuwa na ushuhuda wa Yesu. Hapa ndipo penye subira ya watakatifu, hao wazishikao amri za Mungu, na imani ya Yesu.” (Ufu 12:17; 14:10-12, 17; 15:2, 3).


gray-bl

gray-br







Joka alifanya vita na wazao wa kanisa waliosalia (Masalio) ambao walidumu katika kuzishika Amri za Mungu na ushuhuda wa Yesu (Roho ya Unabii).
“Mungu ana Kanisa duniani, ambao ndiyo watu wake waliochaguliwa, wanaotunza amri zake.Anaongoza, siyo kundi la waliopotoka [machotara], siyo mmoja hapa na mwingine kule, lakini watu” (“Faith I Live By,” ukr. 2).
     Mungu amekuwa siku zote na Kanisa duniani. Michakato iliyopita ya Kanisa la Kikristo ni uthibitisho wa matunda yanayonena kwa ujasiri juu ya mioyo bikira ya watoto wa masalio waliopata kuwepo katika vizazi vyote. Ni kile tu “kisemwacho na Bwana” kinachoweza kushika kamba za moyo wa kitu hiki, watu wake. Hata kama wale wanaowazunguka wakitafuta kuua miili yao, njia yao pekee ni kwenda popote Mwana-Kondoo aendapo. Hata kama hii inamaanisha kuacha familia na marafiki, masalio wanapaswa kutembea na Bwana na kufanya sawa na walivyoumbwa kufanya. Wateule hawawezi kufanya zaidi ya hili.
“Kwa kukataa njia za Mungu na kufuata njia za wanadamu, anguko la Israeli lilianza. Hivyo basi liliendelea, mpaka Wayahudi walipokuwa mawindo hasa kwa mataifa ambayo matendo yao walikuwa wamechagua kufuata.
“Kama taifa, wana wa Israeli walishindwa kupokea bahati ambayo Mungu alitamani kuwapatia.Wa kuthamini kusudi lake au kushirikiana naye katika kulitekeleza. Lakini hata kama watu binafsi na watu wanaweza basi kujitenga wenyewe kutoka kwake, Kusudi lake kwa hao wamtumainio halibadiliki. ‘Najua ya kwamba kila kazi aifanyayo Mungu itadumu milele’ (Mhu 3:14).
     “Wakati kuna viwango tofauti vya maendeleo na udhihirisho tofauti wa nguvu yake kukidhi mahitaji ya watu katika vizazi tofauti, Kazi ya Mungu kwa wakati wote ni ile ile. Mwalimu ni yule yule. Tabia ya Mungu na mpango wake ni ile ile. Kwake yeye ‘hakuna kubadilika, wala kivuli cha kugeuka-geuka’ (Yak 1:17).
     “Mapitio ya Israeli yaliandikwa ili kutuelekeza sisi. Basi mambo hayo yaliwapata wao kwa jinsi ya mifano, yakaandikwa ili kutuonya sisi, tuliofikiliwa na miisho ya zamani’ (1 Kor. 10:11). Kwetu sisi, kama ilivyokuwa kwa Israeli ya zamani, mafanikio katika elimu hutegemeana na uaminifu katika kutekeleza mpango wa Mwumbaji. Utii kwakanuni za Neno la Mungu kutatuletea mibaraka mikubwa kama ambavyo ungeleta mibaraka mikubwa kwa Wayahudi” (“Education,” ukr. 50).

     Ushauri wa upendo Bwana wetu anaoutoa kwa Kanisa la Laodikia unaongelea waziwazi kuwa kinachotakiwa ni toba ya kweli kwa wote walionaswa katika fikra hizi za upofu. Hakuna tofauti yoyote kuliko ya viongozi wa Kiyahudu wa wakati wa Yesu, sawa na tunayoiona kwa viongozi wenye majivuno wa Kanisa la Waadventista wa leo wakikataa ushauri wa wazi ulio katika Maneno ya Bwana wetu. Miaka mingi Bwana ametuma watoto wake waaminifu wengi kuwaonya wale anaowapenda. Lakini maonyo mengi yamedharauliwa na wengi. Hata wakati ukweli uliothibitishwa umeletwa machoni pao, wamegueza kisogo. Rehema kwa kiasi kikubwa imefungwa kwa Kanisa hili, sawa tu na rehema ilivyofungwa kwa taifa la Wayahudi muda mrefu uliopita na Waprotestanti mwaka 1844. kama ilivyo, rehema imefungwa kwa Kanisa zima lakini si kwa watu walio ndani yake.
     Wakati wa unabii wa miaka 490 ulipotimia, Mungu aliwaita watu kutoka katika makosa na kuanza mchakato wa Kikristo kwa kutumia wale walioitwa. Kusema kweli Paulo aliingia katika Makanisa ambayo kiunabii yalikuwa yamefungwa ili apate kuwatoa. Leo, Bwana anafanya kitu hicho hicho. Watoto wake watakwenda popote Mwana-Kondoo anapoongoza, na kama wote tunavyojua, hawezi kuwaongoza kupokea uasi wa wazi.

     “Njozi ambayo Kristo alimwonyesha Yohana, ikionyesha amri za Mungu na imani ya Yesu, inatakiwa kuhubiriwa waziwazi kwa mataifa yote, watu, na lugha. Makanisa, yanayowakilishwa na Babeli, yanaonyeshwa kuwa yameanguka kutoka katika hali yao ya kiroho na kugeuka kuwa mamlaka ya kutesa wale wanaotunza amri za Mungu na wana ushuhuda wa Yesu Kristo. Kwa Yohana hii mamlaka itesayo inawakilishwa kuwa ina pembe kama mwanakondoo, lakini inanena kama joka” (“Testimonies to Ministers and Gospel Workers,” ukr. 117; “Evangelism,” ukr. 197).
     “Kama Kanisa la Mungu likiwa vuguvugu, halisimami katika kupendwa na Mungu tena kama Makanisa ambayo yanawakilishwa kuwa yameanguka na kuwa maskani ya mashetani na ngome ya kila roho mchafu, na ngome ya kila ndege mchafu mwenye kuchukiza” (“Manuscript Releases,” 19:176).
     “Ulimwengu usiingizwe kamwe Kanisani, na kuolewa na Kanisa, ukifanya muungano wa umoja. Kwa njia hii Kanisa litapotoka kweli, na, kama ilivyoelezwa katika Ufunuo, kuwa ‘Ngome ya kila ndege mchafu mwenye kuchukiza’” (“Testimonies to Ministers and Gospel Workers,” ukr. 265).
     Hali ya Kanisa la Waadventista Wasabato leo kwa uhakika imekuwa ni Babeli. Kila aina ya uasi na mafundisho ya uongo yamepokelewa na viongozi wake, na wamefanya hivyo kwa miongo kadhaa. Uchunguzi wa kina wa fungu lifuatalo utakuongoza kuona kwamba hii ni hali iliyokuwa imetabiriwa kwa Kanisa hili. “Mwanamke sasa amefikia hatua ya kujikinai, na wakati huo huo, masalio ya uzao wake wamesimama imara.
     “Joka akamkasilikia yule mwanamke, akaenda zake afanye vita juu ya wazao wake waliosalia, wazishikao amri za Mungu, na kuwa na ushuhuda wa Yesu Kristo” (Ufu 12:17).
     Imetabiriwa waziwazi kwamba joka litazidisha mashambulizi yake na kufanya vita kwa masalio ya wazao wake, na siyo uzao wenyewe. Awali ya yote uzao wa mwanamke, Kanisa mama [SDA], lilishikilia sheria na kujua unabii. Ndiyo, Shetani ana hasira na hili Kanisa. Hata hivyo, hasira yake imelifanya kumwinamia. Ni masalio ya uzao wake wanaomfanya aende vitani sasa, kwa sababu hawako tayari kumsujudia. Masalio wanaotunza siku ya saba wanathibitishwa kuwa ni wale wanaoshinda.
     “Hata kama sheria ya Bwana itadharauliwa karibu ulimwenguni kote, kutakuwepo na masalio wa haki ambao watakuwa watiifu kwa matakwa ya Mungu. Hasira ya joka itaelekezwa dhidi ya watumishi waaminifu wa mbinguni. Nabii anasema, ‘Joka akamkasilikia yule mwanamke, akaenda zake afanye vita juu ya wazao wake waliosalia, wazishikao amri za Mungu, na kuwa na ushuhuda wa Yesu Kristo’ (Ufu 12:17). Tunaweza kuona kutoka kwenye andiko hili kuwa siyo Kanisa la kweli la Mungu ambalo linafanya vita na wale wazishikao amri za Mungu na kuwa na ushuhuda wa Yesu Kristo. Ni wale wanaoidharau na kuitangua sheria, wanaojiweka wenyewe upande wa joka, na kuwatesa wale wanaoithibitisha sheria ya Mungu” (“Signs of the Times,” April 22, 1889).



Joka akaenda zake afanye vita juu ya wazao wake waliosalia.
 gray-tl

gray-tr

           Waaminifu
         Watesaji
1.     Wakristo waliteswa na Wayahudi. (Viongozi wa Kanisa la Kiyahudi waliwatafuta Wakristo ili kuwafunga na kuwaua)
  1. Waprotestanti waliteswa na Upapa. (Mamilioni ya Wakristo waliuawa kama wazushi na Rumi ya Kipapa)
  2. Waadventista waliteswa na Waprotestanti. (Waprotestanti walidhihaki, na kuwakejeli Waadventista wakati wa Kilele cha Kukatishwa Tamaa)
  3. Masalio wanateswa na Waadventista. (Masalio wanachukuliwa kotini, na hali kadhalika kudhihakiwa, kukejeliwa, na kufutwa ushirika kinyume na sheria na Kanisa la SDA. Nabii anasema Wa SDA watawasaliti Masalio kwa Wakatoliki na kusaidia kupatikana kwao ili wauawe.)
  1. Wakristo

  1. Waprotestanti  

  1. Waadventista   


  1. Masalio      
  1. Wayahudi

  1. Wakatoliki

  1. Waprotestanti


  1. Waadventista



gray-bl

gray-br
“Niliona kanisa kwa jina na Waadventista kwa jina, kama Yuda, watatusaliti kwa Wakatoliki ili wapate nafasi ya kuwa kinyume na ukweli. Kisha watakatifu hawataeleweka, wakijulikana kidogo kwa Wakatoliki; lakini makanisa na waadventisata kwa jina wanaojua imani yetu (maana walituchukia kwa sababu ya Sabato), watawasaliti watakatifu na kupeleka taarifa kwa Wakatoliki kuwashitaki watakatifu kama watu wasiojali taasisi za wanadamu; yaani, wanaitunza siku ya Sabato na kutokuijali siku ya jua, jumapili.” [Ellen G. White, SpM 1.5]
Hata leo, wengi wetu ambao tunapeleka ukweli kwa moyo mzuri kwa wale wanaoanguka katika uasi, tumeona aina zote za uovu zikibambikizwa juu yetu. Dada White alieleza hili kwa uyakinifu, “Ahabu alimhesabu Eliya kama adui yake kwa sababu nabii alikuwa mwaminifu kukemea maovu yake ya siri. Kwa hiyo leo mtumishi wa Kristo, mkemeaji wa dhambi, hukumbana na dharau na kukataliwa makusudi” (“Spirit of Prophecy,” 3:12; “The Desire of Ages,” ukr. 589).
     Kama tunavyojua, kwa njia ya kujifunza unabii, mchakato wa Ki-ekumene tunaouona ukienea kila mahali katika ulimwengu wa leo, hatimaye utakusanya wale wote walio wa Babeli kufanya vita dhidi ya Masalio waaminifu wa Siku ya saba. Tunayaona haya katika michakato ya Upapa kupitia katika Kanisa moja la ulimwengu, na tunaona mshikamano wa Kikristo ukitenda kazi kwa ushirikiano na Roma ili kufikia mwisho ule ule hapa hapa Marekani. Muda si mrefu siku itawadia wakati ambapo tutashuhudia kile ambacho Wakristo wote wa zamani waliona wakati wa zama za mateso makali. Wale wote wanaochukia ukweli watawazunguka wana wa masalio wanaochukiwa ulimwenguni kote.
     Ni wakati muafaka wa kuwakaribia ndugu zetu na kaka katika Bwana na kujaribu kuwambia ukaribu wa mambo katika siku zetu. Kitu cha kusikitisha ni kwamba, hii si kazi nyepesi kuifanya. Shetani ameshawadanganya wengi tayari na utaratibu wa aina hiyo hiyo wa kuchanganya alioutumia kipindi cha nyuma. Wengi wao sasa wanapokea kuwa Kanisa la Waadventista Wasabato litapita hadi mwisho bila kujali ukweli kwamba kuna ushahidi mwingi uliokusanywa dhidi yake kulifunua kama dada kwa Babeli iliyoanguka. Kama wakipokea uongo ni namna gani wanaweza kusimama upande wa ukweli? Bado, baadhi wataruhusu dhambi ya wazi kutamalaki kwa kile wanachokiona kuwa “kizuri zaidi.” Kuchanganyikiwa huku tu kunatosha kutambulisha kuwa hii niishara mojawapo ya kutangaza kwamba mkono wa Bwana uko upande wa mchakato wa Masalio wa Siku ya saba.
gray-tl

gray-tr

Kujitenga kunaitwa Uzushi
  1. Kanisa la Kiyahudi lilitangaza kujitenga kuwa ni uzushi.
  2. Kanisa la awali la Kikristo ambalo lilikuwa Wakatoliki lilitangaza pia kuwa ni wazushi wale waliojitenga kutoka ndani yake.
  3. Kanisa la Kiprotestanti mpaka leo hii, wakati halijajitenga kabisa kutoka Roma, hudai kuwa ndiyo njia pekee kwenda mbinguni.
  4. Na sasa Kanisa la Waadventista Wasabato linatoa kilio kile kile kwa kutangaza kwamba ni vema kukaa na meli inayozama, kuliko kuiacha. Wanaojitenga na kanisa hilo wanaitwa wazushi na waasi.
  1. Wayahudi

  1. Wakatoliki


  1. Waprotestanti


  1. Waadventista






Hata hivyo kujitenga ni kanuni ya Mungu. Musa aliwaambia waisraeli wajitenge na waasi kule jangwani kabla Mungu hajawaangamiza kwa kufunua kinywa cha ardhi na kuwafunika waasi wote.  “Kulikuwepo na kutoka nje, utengano wa kujitenga na waovu uliotolewa maamuzi, kukimbia ili kuokoa maisha. Ndivyo ilivyokuwa katika siku za Nuhu; ndivyo ilivyokuwa kwa Lutu; ndivyo ilivyokuwa kwa wanafunzi muda mfupi kabla ya angamizo la Yerusalemu; na ndivyo itakavyokuwa katika siku za mwisho. Sauti ya Mungu inasikika tena ikiwa na ujumbe wa onyo, ikiwataka watu wake wajitenge kutoka katika wimbi la uovu.” [E.G. White, Wazee na Manabii uk. 167, kurasa za ndani.]

 Kwa kuangalia neno lake, mtu anaweza kuona waumini wakimfuata Bwana wao kwa uaminifu kufanya kazi aliyowaitia kuifanya. Mwanzoni kabisa tulikuwa na Kanisa la Kiyahudi ambalo lilikuwa limechaguliwa na Baba kutangaza ukweli wake kwa Ulimwengu. Lakini uovu uliingizwa na hatimaye walikutwa hawastahili kupata uzima wa milele. Kwa hiyo watu wa Bwana walitoka kati yao kufanya kazi ya Bwana na kuanza mchakato wa Kikristo. Baada ya hapo tunaona tena Kanisa likiingiliwa na uovu wakati Ukatoliki wa Kirumi uliporuhusiwa kuchanganyika na Upagani na Ukristo.

Tena watu wa Bwana walitoka kwenye uovu ili kufanya kazi katika matengenezo ya Kiprotestanti. Hatimaye tena uovu ulikumbatiwa na sauti ya Bwana wetu ilisikika kwa Waadventista waaminifu kutoka Babeli na kufanya kazi yake. Bila shaka, historia ilirekodi hili kama mchakato wa Waadventista Wasabato. Mwishoni, leo katika saa ya kumi na moja tunaona Kanisa la Waadventista Wasabato likikumbatia uovu kama ukweli. Kwa hiyo Bwana kwa mara nyingine tena anatangaza kwa Masalio wake waaminifu kutoka kati yake na kufanya kazi ambayo ni ya haraka sana katika siku zetu. Je, unaweza kuona uhakika wa unabii wa matukio haya? Je, hii yote haijaonyeshwa kwa vielelezo kamili katika mfano wa wakulima katika shamba la mizabibu uliotolewa na Bwana Yesu mwenyewe?

“Kwa maana ufalme wa mbinguni umefanana na mtu mwenye nyumba, aliyetoka alfajiri kwenda kuajiri wakulima awapeleke katika shamba lake la mizabibu. Naye alipokwisha kupatana na wakulima kuwapa kutwa dinari, aliwapeleka katika shamba lake la mizabibu. Akatoka mnamo saa tatu, akaona wengine wamesimama sokoni wasio na kazi; na hao nao akawaambia, Enendeni nanyi katika shamba langu la mizabibu, na iliyo haki nitawapa. Wakaenda.Akatoka tena mnamo saa sita na saa kenda, akafanya vile vile. Hata kama saa kumi na moja akatoka, akakuta wamesimama, akawaambia, Mbona mmesimama hapa hapa mchana kutwa bila kazi? Wakamwambia, Kwa sababu hakuna mtu aliyetuajiri. Akawaambia, enendeni nanyi katika shamba la mizabibu” (Mt. 20:1-7).

gray-tl

gray-tr

Asubuhi na mapema sana = Taifa la Kiyahudi
Saa 3 = Wakristo
Saa 6 = Waprotestanti
Saa 9 = Waadventista
Saa 11 = Masalio Wanaotunza Sabato

gray-bl

gray-br

     Ukweli ni kwamba waumini wa kweli walijitenga kutoka kwenye sinagogi la Shetani la taifa la Kiyahudi, kwamba walitoka pia kutoka katika Upagani wa Ukatoliki wa Kirumi, na kwamba hata walitoka pia kutoka katika uovu wa Kiprotestanti. Na sasa tunaona Masalio tena wakielekea katika mwelekeo wa kweli tu ambao mtoto wa Mungu anaweza kuufuata. Tunaweza kuongozwa tu na Mwana-Kondoo wa Mungu. Hatutakiwi kunajisiwa na wanawake hawa (au Makanisa yaliyoasi—angalia Ufu 14:4).

     Wateule wa Mungu hawawezi kudanganywa. Tunapaswa kufuata popote anapoongoza! Tunafanya hivyo tu kwa sababu sisi tu kondoo wake, na tunaisikia kwa uhakika sauti yake. Wakati viongozi wa Kanisa wanapokumbatia uovu hadharani na kukataa kila onyo la kutubu, masalio hawawezi kusimama nao tena. Hasa baada ya mambo mengi kuwa yamefanyika kujaribu kuwajulisha uasi ambao hawaukumbatii tu bali pia wanauhamasisha.

Je, sisi siyo watu wanaoelewa kanuni ya unabii? Je, hatuvutwi sana katika mioyo yetu kutafuta makimbilio mahali ambapo tunaweza kuabudu katika kweli sawa na mioyo yetu inavyotusukuma kufanya? Wateule hawawezi kusimama na uovu, sawa na ambavyo Shetani hawezi kusimama katika kweli. Haiwezekani kabisa kutokea.

     Hivi karibuni nilitoa swali hadharani kuhusiana na “kutoka” katika Kanisa la Waadventista Wasabato. Nilitaka kujua kama kila mtu alikuwa analiona. Kwa muda mfupi tu, nimepokea mamia ya barua pepe zikieleza ukweli katika ukweli huu, na kuomba ushauri juu ya nini cha kufanya hatimaye. Watu kutoka ulimwenguni kote wanatafuta wale wanaoweza kuwaamini na kumwabudu Bwana pamoja nao katika roho na kweli. Wana njaa ya ukweli tunaoutoa. Hauhubiriwi katika mimbari ya Makanisa yao tena. Kondoo hawalishwi tena katika Makanisa haya. Wametoka, kwa sababu hakuna nafasi kwa ajili yao tena katika Makanisa haya. Ni wazi kuwa sauti ya Bwana inasikika. Watoto wake wanaitikia wito wake “Tokeni kwake, enyi watu wangu.”
     Litunze hilo mawazoni. Watoto wake ni kweli huisikia sauti yake. Wanatoka kabisa kati yake.Hili siyo jambo ambalo yeyote anahitaji kushurutishwa tena zaidi. Kutoka kwa watu wengi kunatokea ulimwenguni kote. Kwa baadhi yetu tulio na huduma duniani kote, ukweli huu unajirudia kila siku mbele za macho yetu kutoka katika kila sehemu ya maisha. Watu nje na ndani ya Kanisa wanaona hili waziwazi.
     Wale wanaokubali au kupinga utengano wanakiri, kuna mchakato mwingine unaoonekana leo! Hii tu iko wazi kabisa. Kama nilivyosema mapema, mkono wa Bwana unaonekana hapa. Kwa sababu pasipo mkono wake kuhusika, Wafuasi wa Mungu wasingechukua hata hatua moja kutoka katika Kanisa lililoanguka. Mahali popote pasipokuwa na hatua, hakuna mchakato. Na kwa yakini kuna mchakato wa watu wa Mungu siku hizi kabisa. Je, usingependa kuwa sehemu ya Mchakato wa
Masalio?
KUMBUKA 1: Wengi wanaamini kwamba Filadelfia iliishia mwaka 1844, lakini mlango ule uliofunguliwa kwa Filadelfia ulikuwa ni mlango wa Patakatifu pa Patakatifu kule mbinguni (angalia “Spirit of Prophecy,” 4:268-269). Hivyo hali ya Filadelfia inazidi baada ya Oktoba 22, 1844 mpaka kazi ya huduma ya Kristo imekamilika.
KUMBUKA 2:Kristo ameauacha mchakato wa Kiadvenista na hali kadhalika Kanisa la SDA (“Testimonies for the Church,” 8:250) kwa sababu ya uasi kama vile alivyofanya kwa Kanisa la Kiyahudi (Mwa 49:10; Mt 21:43; 23:12-24:2; 27:50, 51). Roho Mtakatifu anagusa mioyo ya watoto wake kutoka katika Makanisa yaliyoanguka ili kupokea ukweli wake. (Ufu 3:15-17; 16:9, 11; 18:1-5).
Fanya uamuzi wa kujitenga sasa kutoka katika mifumo ya madhehebu yaliyopotoka madamu Mungu anapataikana na mlango ukingali wazi.

MUNGU akubari.

KWA MAWASILIANO ZAIDI WASILIANA NASI
0756959525,0752164685
Share:

SHERIA YA JUMAPILI NA UNABII WA SIKU 2300, 1260, 1290, 1335 KATIKA DANIEL 8 NA 12 NA UFUNUO 13.

SHERIA YA JUMAPILI NA UNABII WA SIKU 2300, 1260, 1290, 1335 KATIKA DANIEL 8 NA 12 NA UFUNUO 13.



Ni unabii unaopaswa kujifunza kwa kina tukizingatia kwamba unalo fundisho kubwa kwetu sisi tunaoishi katika siku hizi za mwisho.

Nabii anasema: “Kuna ukweli mwingi muhimu katika Neno la Mungu, ‘Lakini ukweli wa leo’ ndio unahitajika kundini sasa. Niliona hatari ya wajumbe wanaoweka kando mada muhimu za ukweli wa leo na kukawia juu ya masomo ambayo hayalengi kuunganisha kundi na kutakasa moyo. Hapo Shetani atapata kila nafasi iwezekanayo ili kuharibu kazi ya Mungu.” {Maandiko ya Awali uk. 60}

 

Kwa bahati mbaya kabisa makundi mengi lilipo kanisa la Mungu (Masalio Watengenezaji wa kanisa la Waadventista Wa siku ya Saba –Sabato) wajumbe wa Mungu wamekuwa wakitilia mkazo masomo ambayo hayalengi kuunganisha kundi la Mungu na badala yake masomo hayo yanatenganisha zaidi na kusababisha mgawanyiko mkubwa ndani ya kanisa la Mungu. Upo ukweli wa leo ambao ukifundishwa katika uongozi wa Roho Mtakatifu, hitilafu na tofauti zinazoonekana katika kanisa la Mungu zitafutiliwa mbali na tutaona umoja na upendo ukitawala na kuwaweka watu tayari kwa kupokea mvua ya masika.

Lakini ukweli wa leo ni upi?  Nabii anaendelea kusema: “Lakini masomo kama hema takatifu pamoja na siku 2300, Amri za Mungu na imani ya Yesu, vinaeleza kwa usahihi mwamko uliopita wa wanamarejeo na kuonyesha msimamo wetu wa leo, kuimarisha imani ya mwenye mashaka na kuweka wazi utukufu ujao. Mara nyingi nilionyeshwa kuwa haya ndiyo masomo ya msingi ambayo wajumbe wa Mungu wanapaswa kukawia juu yake.” {E.G. White,Maandiko ya Awali uk. 60.}

 

Basi kwa sababu ya ushuhuda huu wa Mungu, kama tunahitaji kuwa na umoja na kutakaswa mioyo, hatuna budi kukawika juu ya masomo ya hema takatifu, unabii wa siku 2300 na Amri za Mungu na imani ya Yesu ambapo katika somo hili tutajikita zaidi kuhusu utimilifu wa unabii wa siku 2300.

 

“Nuru ile aliyoipokea Daniel kutoka kwa Mungu ilitolewa zaidi kwa ajili ya siku hizi za mwisho. Njozi alizoziona akiwa kwenye mto Ulai na Hiddekel, mito ile mikubwa ya Shinar, kwa sasa zipo kwenye mchakato wa utimilifu, na matukio yote yaliyoelezewa yatatimilika na kupita.” {E.G. White,TM 112. 3, 113.}

Njozi alizoona Danieli akiwa kwenye mto Ulai na Hidekkel ni njozi zinazohusu unabii wa siku 2300. Nabii anasema nuru hiyo ilitolewa zaidi kwa ajili ya siku hizi za mwisho na kwamba ‘kwa sasa njozi hizo zipo kwenye mchakato wa utimilifu, na matukio yote yaliyoelezewa yatatimia na kupita’, hii ikimaanisha kwamba ingawa unabii wa siku 2300 ulifikia mwisho mwaka 1844 kwa maana ya kutimia katika siku moja kwa mwaka, lakini matukio YOTE yaliyotimia kipindi hicho, yatatimia tena hadi mwisho wa wakati.

 

Siku 1260, 1290 na 1335 za unabii wa Danieli 12.

Unabii wa siku 2300 umetajwa katika mgawanyiko wa siku 1260, siku 1290 na siku 1335. Upo uhusiano mkubwa wa siku 1335 na watu 144,000 kwa sababu wale watakaofanikiwa kufika katika siku 1335 ndiyo watakaokuwa sehemu ya 144,000 na watajua kuwa ni sehemu ya 144,000 baada kipindi hiki kupita. Ufafanuzi wa hili utatolewa mbele ya fundisho hili.

Nabii anasema: “Ujumbe wa malaika wa kwanza na wa pili ulitangazwa, lakini pasingetolewa nuru zaidi hadi pale jumbe hizi zingekuwa zimefanya kazi yake iliyokusudiwa. Jambo hili linawakilishwa na malaika aliyesimama na kuweka mguu wake mmoja juu ya bahari akisema kwamba hapana wakati tena. Wakati huu unaotajwa na malaika kwa sauti kuu, siyo mwisho wa historia ya ulimwengu, wala siyo wakati wa kufungwa kwa mlango wa rehema, bali wa unabii wa siku moja kwa mwaka, ambao utatangulia marejeo ya Bwana wetu. Hii inamaanisha, watu hawatakuwa na ujumbe mwingine kuhusu wakati maalumu. Baada ya kupita kwa wakati huu, kufikia mwaka 1842 hadi 1844, hakutakuwepo na muda wa kufuatilia unabii wa nyakati (siku moja kwa mwaka). Ufuatiliaji mrefu kabisa unafikia mwaka 1844.” {E.G. White, SDA BC vol. 7 p. 971.}

 

Hii inamaanisha kwamba unabii huu utajirudia siyo katika utimilifu wa siku moja ya unabii sawa na mwaka mmoja halisi bali katika kujirudia kwa matukio. Hata hivyo hadi pale nuru ya ujumbe wa malaika wa kwanza na wa pili itakapofanya kazi ndani ya mioyo ya watu wa Mungu ndipo nuru zaidi itatolewa. Nuru inayotakiwa kufanya kazi mioyoni mwetu ili tupate nuru zaidi ni ujumbe wa kuhesabiwa haki kwa imani kwa maana ya kumruhusu Yesu akae na kutawala ndani yetu na kutegemea uongozi, msaada na ulinzi wake katika maisha yetu yote tukijua kwamba hatuwezi kutenda wema wowote kwa uwezo wetu isipokuwa kama Yesu anakaa ndani yetu. Je, umeuruhusu ujumbe wa malaika wa kwanza na wa pili kufanya kazi ndani yako ili Mungu akufunulie nuru zaidi ikiwa ni pamoja na unabii wa siku 2300? Hebu mruhusu Roho wa Mungu akusaidie katika kutimiza mapenzi ya Mungu kama ilivyo kwenye jumbe hizi za malaika wa kwanza na wa pili.
Unabii wa siku 2300 umegawanyika katika sehemu kuu mbili za utimilifu wake. Sehemu ya kwanza niutimilifu kuanzia mwaka 457KK hadi mwaka 1844BK na sehemu ya pili ni kuanzia mwaka 1844 hadi marejeo ya pili ya Bwana wetu Yesu Kristo.

1.     UTIMILIFU WA UNABII WA SIKU 2300 SEHEMU YA KWANZA.
Nini yalikuwa matukio katika kutimia kwa unabii wa siku 2300? “Ndipo nikamsikia mtakatifu mmoja akinena, na mtakatifu mwingine akamwuliza huyo aliyenena, Haya maono katika habari ya sadaka ya kutekezwa ya daima, na lile kosa lifanyalo ukiwa, yataendelea hata lini, kukanyagisha patakatifu na jeshi?” {Danieli 8:13.} Basi tukitafakari Andiko hili tunaona mambo makubwa mawili yaliyojenga msingi wa swali hili. Kwanza nisadaka ya daima ya kutekezwa na pili ni lile kosa lifanyalo ukiwa. Haya ndiyo matukio makubwa tunayohitaji kuyajifunza ili kupata kujua mantiki ya jibu lililotolewa katika swali hilo, yaani: “Hata nyakati za jioni na asubuhi elfu mbili na mia tatu; ndipo patakatifu patakapotakaswa.” {Daniel 8:14.} Jibu hili linatuonyesha pia kwamba upo uhisiano mkubwa kati ya siku 2300 na patakatifu (hema takatifu) lakini haya ni masomo mawili yanayotakiwa kujifunza kila moja kwa wakati wake.

Nabii Daniel anaendelea kutuambia kile alichoambiwa na mtakatifu katika habari ya siku 2300, anasema: “Muda wa majuma sabini umeamuriwa juu ya watu wako, na juu ya mji wako mtakatifu ili kukomesha makosa, na kuishiliza dhambi, na kufanya upatanisho kwa ajili ya uovu, na kuleta haki ya milele, na kutia muhuri maono na ubaii, na kumtia mafuta yeye aliye Mtakatifu. Naye atafanya agano thabiti na watu wengi kwa muda wa juma moja; na kwa nusu ya juma hiyo ataikomesha sadaka na dhabihu; na mahali pake litasimama chukizo la uharibifu; na hivyo hata ukomo, na ghadhabu iliyokusudiwa imemwagwa juu yake mwenye kuharibu.” {Daniel9:24; 27}

Waisraeli walipewa muda wa majuma 70 ili wajitakase na kuacha dhambi na kwamba kipindi hicho kilikuwa ni kipindi cha rehema kwao ambapo baada ya muda huo kupita, mlango wa rehema kwao ungekuwa umefungwa.Unabii wa siku 2300 ulianza kutimia mwaka 457KK na hapa ndio mwanzo wa majuma sabini. Majuma 70 ni sawa na siku 490 na katika unabii wa siku moja kwa mwaka mmoja, hii ni miaka 490. Ukichukua miaka 490 na kutoa miaka 457 jibu ni miaka 33 ambapo Masihi alikatiliwa mbali (alikufa juu ya mti wa mateso). Maandiko yanatuambia kwamba wakati huo mlango wa rehema kwa taifa la Israeli ulifungwa rasmi. Hivyo kipindi cha majuma 70 sawa na miaka 490 kilikuwa ni kipindi cha rehema kwa taifa la Israeli.
Katika Matthayo 18:22 Yesu alisema: “……Sikuambii hata mara saba, bali hata saba mara sabini.” Je, Yesu alimaanisha mwisho wa kusamehe ni 7x70 = 490 au alimaanisha nini? Hapa Yesu alikuwa na maana ya kiroho zaidi na siyo katika mtazamo wa hesabu. Ieleweke kwamba Mungu hufanya kazi katika namba na kwamba namba anazotumia ni 1 hadi 12 na kila namba ina maana yake ya kiroho. Namba 490 katika maana ya kiroho humaanisha kipindi cha rehema kabla ya kufungwa kwa rehema. Kwa vile Waisraeli walipewa muda wa majuma 70 yaani 7x70 = 490 kama kipindi cha rehema, Yesu alimaanisha pia kuwa tunapaswa kusamehe siku zote hadi wakati mlango wa rehema utakapofungwa. Kwa ufupi matukio makubwa tunayoyapata ndani ya majuma 70 ni kusulubishwa kwa Yesu na kufungwa kwa mlango wa rehema kwa taifa la Israeli. Nini kilitokea baada ya mlango wa rehema kufungwa kwa taifa la Israeli? Walichaguliwa wamataifa ili kushika nafasi ya Israeli ya zamani. Zingatia: Hitimisho hili lina maana kubwa katika kurudiwa kwa utimilifu wa unabii huu siku za mwisho.

Siku 1260, 1290 naChukizo la Uharibifu
Baada ya kuangalia matukio ya kusulubishwa kwa Yesu yaani ‘kukomesha Sadaka ya daima ya kutekezwa’, pamoja na kufungwa kwa mlango wa rehema kwa taifa la Israeli, yaani ‘muda wa majuma 70 umeamuliwa juu ya watu wako’ sasa tuangalie tukio la ‘Chukizo la uharibifu.’ Nabii Daniel anasema: “Na tangu wakati ule ambapo sadaka ya kutekezwa ya daima itaondolewa, na hilo chukizo la uharibifu litakaposimamishwa, itapita siku elfu na mia mbili na tisini.” {Daniel 12:11.}
Kuondoa sadaka ya daima ya kuteketezwa inamaanisha kukomesha sheria za kusamehewa dhambi kwa njia ya kutoa kafara za wanyama na kuziteketeza juu ya madhabahu ya kutolea kafara. Je, ni kwa njia gani mwanadamu angesamehewa dhambi baada ya kuondoa sheria za kutoa kafara kwa ajili ya ondoleo la dhambi? Ni nani mwenye haki ya kusamehe dhambi? Imeandikwa: “Naye YESU alipoiona imani yao, akamwambia yule mwenye kupooza, Mwanangu, umesamehewa dhambi zako. Na baadhi ya waandishi walikuwa huko, wameketi wakifikiri mioyoni mwao, Mbona huyu anasema hivi?, anakufuru. Ni nani awezaye kusamehe dhambi isipokuwa mmoja, ndiye Mungu?” {Marko 2:5,6}
Nabii anasema tukio la kuondoa sadaka ya kuteketezwa ya daima lilifuatiwa na‘kusimamishwa kwa chukizo la uharibifu.’Je, ni wakati gani ambapo chukizo la uharibifu’ lilisimamishwa kwa mara ya kwanza? Ni wakati ule ambapo kanisa lilidhamiria kuwa na mamlaka ya kiserikali na kidini na kwamba kiongozi wa kanisa (Papa) na maaskofu na mapadri wa kanisa ndiyo wenye mamlaka na haki ya kusamehe dhambi kwa kutumia kimakosa kauli ya Yesu aliposema: “Amini nawaambieni, yoyote mtakayoyafunga duniani yatakuwa yamefungwa mbinguni; na yoyote mtakayoyafungua duniani yatakuwa yamefunguliwa mbingu.” Matthayo 18:18.
Je, hayo yalitendekea lini? Mwaka 508BK. Hivyo kwa kusema:“Na tangu wakati ule ambapo sadaka ya kutekezwa ya daima itaondolewa, na hilo chukizo la uharibifu litakaposimamishwa, itapita siku elfu na mia mbili na tisini” unabii huu ulimaanisha baada ya siku 1290 kutakuwa na tukio jingine muhimu katika mfululizo wa matukio ya utimilifu wa unabii wa siku 2300. Kwa ufupi tunaweza kusema kwambamwanzo wa siku 1290 ni mwaka 508BK wakati wa kutumizwa kwa tukio la chukizo la uharibifu (mamlaka ya kusamehe dhambi kuwekwa mikononi mwa wanadamu)baada ya sadaka ya kutekezwa ya daima kuondolewa mwaka 33 kwa kafara ya Yesu kutimiliza sheria ya kafara za wanyama. Ni tukio gani lilifuata mwishoni mwa siku 1290? Mwisho wa siku 1290 ni mwaka 1798 na tukio lililotimilizwa mwaka huo ni ‘kimoja cha vichwa vya mnyama kupatwa na jeraha la mauti’.
Lakini pia tunatambua kwamba mateso dhidi ya watu wa Mungu yalianza rasmi mwaka 538 na kudumu kwa miaka 1260. Kuna tofauti ya siku 30 kati ya siku 1290 na siku 1260. Hii inamaanisha kwamba kulikuwa na kipindi cha miaka 30 kwa watu wa Mungu kujiandaa kwa ajili ya mateso kutokana na kutokuamini juu ya msamaha wa dhambi uliotolewa na wanadamu. Tutaona pia kwamba wakati unabii huu unajirudia katika siku za mwisho kutakuwa na kipindi cha kujiandaa kwa watu wa Mungu tangu siku ya tangazo la sheria ya jumapili hadi wakati wa ulazimishwaji na kuwekwa sheria ya kutokuuza wala kununua kwa wale watakaokataa kutii sheria ya kuitunza sabato bandia ya siku ya kwanza ya juma tofauti na Sabato halisi ya siku ya saba.

Uheri wa kuzifikia siku 1335
“Heri angojaye, na kuzifikilia siku hizo elfu na mia tatu na thelathini na tano.” {Daniel 12:12.}
Je, siku 1335 zilianza lini? Katika Daniel 12:11 tunapewa mwanzo wa siku 1290 ikiwa ni sawa na mwanzo wa siku 1335 kwa sababu mstari wa 12 ni muendelezo wa kile kilichoanza kuelezewa kwenye mstari wa 11. Ukichukua mwaka 508BK na kujumlisha siku sawa na miaka 1335 utapata mwaka 1843. Maandiko yanatuambia kwamba William Miller alianza kuhubiri ujumbe wa utimilifu wa unabii wa siku 2300 mwaka 1843. Kwa nini HERI YULE ANGOJAYE na kuzifikia siku 1335? Kuna sababu kubwa mbili za uheri huu. Sababu ya kwanza ni kwamba mwisho wa siku 1335 ulikuwa ni wakati wa kuanza rasmi kuhubiri ujumbe wa malaika watatu katika utimilifu wa siku 2300 na kutakaswa kwa patakatifu. Ulikuwani wakati wa malaika wasaba kupiga baragumu yake. Nabii Yohana anasema: “isipokuwa katika siku za sauti ya malaika wa saba atakapokuwa tayari kupiga baragumu; hapo ndipo siri ya Mungu itakapotimizwa; kama alivyowaambia watumishi wake hao manabii.” {Ufunuo 10:7.}Kwa miaka mingi Sabato ilikuwa imetupiliwa mbali, mashahidi wawili (Neno la Mungu katika agano la kale na agano jipya) walikuwa wameuawa wakati wa mapinduzi ya Ufaransa kwa kuichoma moto Biblia na kuzuia watu kusoma Neno la Mungu. Lakini Mungu alikusudia kwamba mwisho wa siku 1335, siri yake iliyokuwa imetiwa muhuri katika unabii wa siku 2300 sasa ifunuliwe kwa ulimwengu na watu wake wajue huduma inayofanywa na kuhani wao Mkuu katika patakatifu pa mbinguni. Yule aliyengoja kwa uvumilivu aliitwa mwenye heri maana alipata nafasi ya kushuhudia siri ya Mungu ikifunuliwa. Sababu ya pili ya uheri ni kwamba wakati huo ulikuwa ni wakati wa kufungwa kwa mlango wa rehema kwa watumishi walioitwa shambani mwa Bwana mnamo saa 6 (Matthayo 22:1-14). Maandiko yanasema ujumbe wa malaika wa pili uliotangaza anguko la Babeli ulihubiriwa mwaka 1844 na kwamba wale waliokataa kutii ujumbe wa kutoka Babeli kama mfumo wa kanisa, mlango wa rehema kwao ulifungwa. Waprotestant waliokuwa waaminifu katika kupinga mafundisho ya kanisa la Rumi lakini wakakataa nuru ya Sabato, kwao mlango wa rehema ulifungwa mwaka 1844 na ilipofika saa 9 Mungu akawaita Waadventisa wa Sabato kuchukua nafasi yao.Katika kuwaita watumwa wake, Yesu alisema watumwa wa kwanza waliitwa ‘alfajiri’ ikiwakilisha kuitwa kwa taifa la Israeli kama taifa teule la Mungu. Hata hivyo wahakuwa waaminifu na ilipofika saa 3, mitume waliitwa kuchukua nafasi hiyo. Lakini pia mitume waliuacha upendo wao wa kwanza na kuruhusu Upapa kuinuka ambapo ilipofika saa 6 Waprotestant waliitwa ili kupinga madanganyo ya kanisa la Rumi. Kwa sababu ya kukataa ujumbe wa malaika wa kwanza na wa pili, tangazo la anguko kwa Waprotestant lilitolewa mwaka 1844 na ilipofika saa 9 Waadventista wa Sabato (SDA) waliitwa. WaSDA walifanya kazi kwa uaminifu kwa muda wa chini ya saa mbili maana ilipofika saa 11, watumishi wengine waliitwa ili watoke ndani ya kanisa asi la SDA wakiwa ni masalio waaminifu wazishikao amri za Mungu na imani ya Yesu.
Mpaka hapa tumeona kwamba mwisho wa majuma 70 ulikuwa ni mwisho wa rehema kwa taifa la kiyahudi kuitwa kama watu wa Mungu. Wayahudi walifungiwa mlango wa rehema baada ya mumkataa Yesu kama Masihi. Tumeona pia kwamba mwisho wa siku 1335 ulikuwa ni wakati wa kufungwa kwa rehema kwa mfumo wa Uprotestant kama taifa la Mungu na hili lilitokea baada ya Uprotestant kuikataa Sabato kama siku iliyowekwa na Mungu kwa ajili ya kumuabudu. Lakini yule aliyengoja akimtumaini Yesu alikuwa na heri maana huyo ndiye aliyefunuliwa nuru ya Sabato na kukubali kuhama na Kristo kutoka chumba cha pili cha patakatifu na kuingia naye kwa imani katika chumba cha pili cha patakatifu pa patakatifu kwenye hema iliyoko mbinguni isiyotengenezwa kwa mikono ya mwanadamu.

Lakini nini kilitokea wakati unabii wa siku 2300 unaendelea kutimia? Lipo tukio jingine muhimu ambalo limewekwa kwetu kama fundisho kuu. Tukio hili niangamizo la Yerusalemu lililotokea mwaka 70.

2.     Angamizo la Yerusalemu mwaka 66na70 na kukimbilia milimani.
Nabii Ellen White aliandika akisema kwamba kipindi cha mwaka 27 hadi 70 katika taifa la Israeli kilikuwa ni kipindi kinachofananishwa na angamizo la ulimwengu wote lakini uangamivu huu utaanzia katika Hekalu na nyumba ya Mungu, Ezekieli 9:6. Hakuna shaka kwamba historia ya Wayahudi kuanzia mwaka 27 hadi 70 ilikuwa ni utimilifu wa kujirudia kwa unabii wa Ezekieli 9.
Sura ya kwanza ya kitabu cha Pambano kuu inaelezea kile kitakachotokea katika siku za mwisho. Angamizo hili litaanza katika nyumba ya Mungu, yaani kanisa asi la SDA ambalo Mungu alilipatia upendeleo wa nuru kubwa katika nyumba ya Yakobo. {5T 211; Ezekieli 9:6}
“Wakati ujio wa majeshi ya Rumi ulikuwa ni ishara kwa wanafunzi juu ya angamizo la Yerusalemu, hivi ndivyo ilivyo kwamba uasi huu [sheria ya jumapili] ni ishara kwetu ya kufikia ukomo wa uvumilivu wa Mungu, kwamba kipimo cha uovu wa taifa letu [Marekani] kimejaa, na kwamba malaika wa rehema amekaribia kupaa na kamwe asirudi tena. Kisha watu wa Mungu watapitia katika kipindi kigumu na mateso ambayo nabii ameyaelezea kama taabu ya Yakobo. Kilio cha waaminifu na wanaoteswa kitafika mbinguni. Na kama damu ya Habili ilivyotoa kilio kutoa ardhini, sauti pia zinazotoa kilio kwa Mungu kutoka kwenye makaburi ya wafia dini, kutoka kwenye maiti zilizomo baharini, kutoka kwenye mapango ya milimani: ‘mpaka lini Bwana, Mtakatifu na wa kweli, hutahukumu na kulipa kisasi cha damu yetu kwa wale wakaao katika nchi’”? {5T 451.2}
“Sasa siyo wakati kwa watu wa Mungu kudumisha mapenzi yao au kuweka hazina zao katika ulimwengu. Muda si mwingi wakati, kama ilivyokuwa kwa wanafunzi wa awali, tutalazimishwa kutafuta makao kwenye maeneo yasiyokaliwa na watu. Kama ilivyokuwa kuzungukwa kwa Yerusalemu na majeshi ya Rumi kuwa ishara kwa wakristo wa Judea, kujipatia mamlaka kwa taifa letu katika kutangaza sabato ya Papa itakuwa ni onyo kwetu. Utakuwa ni wakati wa kuondoka kwenye miji mikubwa, maandalizi ya kuondoka kwenye miji midogo tayari kukimbilia milimani. Na sasa badala ya kutafuta makazi ya thamani kubwa hapa, tunapaswa kujiandaa kuondoka na kwenda kwenye nchi nzuri ya mbinguni. Badala ya kutumia mali zetu katika kujifurahisha, tunapaswa kujifunza jinsi ya kubana matumizi.” {5T 464-5}

Angamizo la Yerusalemu ni kielelezo cha kile kitakachotokea wakati wa kutangazwa kwa sheria ya jumapili. Wakati majeshi ya Rumi yalipouzunguka mji wa Yerusalemu mwaka 66 ilikuwa ni dalili na muda wa kuanza kuondoka mjini Yerusalemu na kukimbilia kwenye milima ya Pella, tangazo la sheria ya jumapili itakuwa ni ishara ya kuanza kuondoka kwenye miji mikubwa na kukimbilia kwenye miji midogo tayari kwa kukimbilia milimani. Ni wazi kwamba hatutakimbilia milimani wakati tangazo la sheria ya Jumapili litakapotolewa. Mwanzoni hakutakuwa na ulazimishwaji wa kuitunza Jumapili wala adhabu kwa wale wasioitii sheria ya jumapili. Kama sheria hii ingeanza moja kwa moja na kutokuruhusu kuuza na kununua, kufungwa gerezani na kukabiliwa na kifo, basi tusingepata muda wa kufanya maandalizi ya kukimbilia milimani.Kadri hukumu za Mungu zitakavyozidi kuwa kubwa kwa sababu ya kutangaza sabato bandia kinyume na Sabato ya kweli, sababu za hukumu hizi zitapelekwa kwa wale wasiokubali kuitunza sheria ya jumapili.

3.     UTIMILIFU WA UNABII WA SIKU 2300 SEHEMU YA PILI.
Katika unabii wa siku 2300 sehemu ya kwanza tumeona matukio yaliyotukia katika siku 1260 na 1290. Wakati unabii huu unatimia kwa mara ya kwanza tuliona kwamba siku 1290 zilihusika kwa tukio la kukomesha sadaka ya kuteketezwa ya daima na mahli pake kusimamisha chukizo la uharibifu, ambapo unabii huu unapojirudia kwa mara ya pili tukio hili litakuwa sawa na tangazo la kukomesha ibada ya siku ya Saba, Sabato ya Mungu na mahali pake kuwekwasheria ya jumapili, yaani, chukizo la uharibifu. Wakati wa utimilifu wa unabii huu sehemu ya kwanza, kulikuwa na kipindi cha siku 30 za maandalizi kwa ajili ya mateso yaliyoanza katika siku ya kwanza ya siku 1260. Wakati wa kurudiwa kwa utimilifu wa unabii huu siku za mwisho tunajifunza kwamba kutakuwa na kipindi cha kufanya maandali ya dhati mara baada ya tangazo la sheria ya jumapili kutolewa. Watu wa Mungu watakuwa wakijiandaa kwa mateso makali ambayo hayajawahi kutokea tangu kuumbwa kwa msingi wa dunia. Baada ya kipindi hiki kupita, jeraha la mauti litakuwa limepona katika utimilifu wake na ndipo tutashuhudia mnyama akishika tena mamlaka aliyoyapoteza mwaka 1798. Kipindi hiki ni sawa na kipindi kilichosemwa na nabii Yohana katika Ufunuo 13:1-5 cha utawala wa mnyama kwa muda wa miezi 42 au miaka mitatu na nusu.
Lakini pia ipo tofauti ya siku 75 kati ya siku 1335 na siku 1260 ambapo tofauti ya kipindi hiki inawakilisha kipindi cha kujiandaa kukimbilia milimani pamoja na kipindi cha kukaa milimani. Tumeona kipindi cha maandalizi kikiwakilishwa na siku 30 tangu kutolewa kwa sadaka ya kuteketezwa ya daima na kusimamishwa kwa chukizo la uharibifu na unapochukua 75 – 30 = 45 ambapo kipindi cha siku 45 kinawakilisha kipindi cha kukaa milimani kumsubiri Bwana na Mwokozi wetu. Hii ndiyo sababu ya uheri kwa wale watakaozifikia siku 1335 kwa sababu watakutwa na Yesu wakiwa hai, yaani wale 144,000. Wakati wa angamizo la Yerusalemu wale waliokimbilia milimani waliponya nafsi zao kama ilivyokuwa kwa Lutu ambaye pia aliponya nafsi yake baada ya kutoka Sodoma na kukimbilia kwenye mapango. Nimeelezea zaidi kuhusu 144,000 kwenye somo jingine.

Chukizo la Uharibifu na Kosa liletalo ukiwa.
“Ndipo nikamsikia mtakatifu mmoja akinena, na mtakatifu mwingine akamwuliza huyo aliyenena, Haya maono katika habari ya sadaka ya kutekezwa ya daima, na lile kosa lifanyalo ukiwa, yataendelea hata lini, kukanyagisha patakatifu na jeshi?”Daniel 8:13
“Na tangu wakati ule ambapo sadaka ya kutekezwa ya daima itaondolewa, na hilo chukizo la uharibifulitakaposimamishwa, itapita siku elfu na mia mbili na tisini.” {Daniel 12:11.}
Kusimamishwa kwa chukizo la uharibifu kulikosemwa na Daniel katika sura ya 12:11 ni tofauti na lile kosa liletalo ukiwa katika sura ya 8:13. Wakati chukizo la uharibifu linasimamishwa na nguvu kutoka nje ya watu wa Mungu kama tulivyoona, kwa upande mwingine lile kosa liletalo ukiwa linasababishwa na watu wa Mungu ndani ya hekalu au nyumba ya Mungu. Tumeona kwamba katika utimilifu wa unabii wa siku 2300 sehemu ya kwanza chukizo la uharibifu lilisimamishwa na nguvu ya kanisa la Rumi kwa kudai kuwa na mamlaka ya kusamehe dhambi. Lakini pia katika Ezekiel 8:9-18 tunaambiwa habari ya machukizo yaliyokuwa yanafanyika ndani ya hekalu la Mungu chini ya uongozi wa wazee (viongozi wa kanisa). Tumeona kwamba katika siku za mwisho chukizo la uharibifu linamaanisha kusimamishwa kwa sheria ya jumapili.Na sasa swali linaulizwa, nini maana ya ‘lile kosa lifanyalo ukiwa?’ Jibu ni kwamba ‘lile kosa lifanyalo ukiwa’ inamaanisha viongozi wa kanisa asi la SDA watawalazimisha washiriki wao kuitunza siku ya Jumapili. Je, hili litatokea? NDIYO.
Nabii anasema: “Bwana na vita na watu wanaodai kuwa Wake katika siku hizi za mwisho. Katika vita hii watu walioshika nyazifa za juu watachukua masimamo kinyume na msimamo aliouchukua Nehemia. Siyo tu kwamba hawataijali Sabato, bali pia watajaribu kuitunza kwa kuizika chini ya takataka za desturi na mapokeo. Katika makanisa na katika mikusanyiko ya wazi, watendakazi watawaeleza watu umuhimu wa kuitunza siku ya kwanza ya juma. Kuna majanga kwenye bahari na nchi kavu: na majanga haya yataongezeka, janga moja likifuatiwa na jingine; na kundi dogo la watunza Sabato litasondwa kidole kama linalosababisha uwepo wa ghadhabu ya Mungu juu ya ulimwengu kwa sababu hawaijali Jumapili.” {E.G White, R&H 18-3-1884.} Ukweli ni kwamba viongozi wa kanisa asi la SDA wataungana na adui katika kusimamisha chukizo la uharibifu (sheria ya jumapili) katika kurudia kwa utimilifu wa unabii wa siku 2300 ikiwa ni mwanzo wa siku 1260 baada ya jeraha la mauti kupona kwa ukamilifu wake. Jeraha la mauti halitapona kikamilifu mwanzoni mwa siku 1290 wakati wa tangazo la sheria ya jumapili. Kwa nini ninasema hivyo? Kwa sababu Daniel 12:11 anasema kwamba chukizo la uharibifu (kupona kwa jeraha la Kanisa la Rumi na tangazo la sheria ya jumapili) litasimamishwa siku ya kwanza katika siku 1290 ikiwa ni badiliko la kisheria la kuondoa Sabato ya kweli na kusimamisha sabato bandia ikifuatiwa na kutolewa kwa adhabu, mateso na kifo katika siku ya kwanza ya siku 1260. Hivyo ‘lile kose lifanyalo ukiwa’ linafanyika ndani ya kanisa asi la SDA kwa kuungana na mnyama kushinikiza utunzaji wa siku ya kwanza ya juma. Kwa jinsi gani kutakuwepo na ‘ukiwa’?  Ni kwa sababu Mungu atakuwa ameliacha kanisa na kushikamana na uzao wa mwanamke (kanisa) hao waliosali, wazishikao amri za Mungu na imani ya Yesu (Tazama Ufunuo 12:17). Itakumbukwa kwamba wakati Yesu alipowaacha wayahudi na hekalu lao aliwaambia: “Angalieni, nyumba yenu imeachwa hali ya ukiwa.” {Matthayo 23:38}

Kwa nini kurudiwa kwa unabii wa siku 2300 ni Muhimu?
Tunatambua kwamba unabii wa siku 2300 ulifikia mwisho mwaka 1844. Je, unabii huu ulitolewa kwa jinsi gani? Nabii Daniel anasema: “Ndipo nikamsikia mtakatifu mmoja akinena, na mtakatifu mwingine akamwuliza huyo aliyenena, Haya maono katika habari ya sadaka ya kutekezwa ya daima, na lile kosa lifanyalo ukiwa, yataendelea hata lini, kukanyagisha patakatifu na jeshi?” {Danieli 8:13.}Majibu yakatolewa: “Hata nyakati za jioni na asubuhi elfu mbili na mia tatu; ndipo patakatifu patakapotakaswa.” {Daniel 8:14.}
Hivyo tunatambua kwamba siku 2300 zilikuwa ni kipindi cha kukanyagisha patakatifu na jeshi. Lakini kwa nini unabii huu uliendelea hadi mwaka 1844 wakati Papa alikamatwa mateka na kufa nchini Ufaransa mwaka 1798? Je, miaka 46 ilikuwa miaka ya nini wakati kukanyagisha patakatifu na jeshi kuliishia mwaka 1798? Ninakubaliana na sehemu ya utimilifu wa unabii wa siku 2300 lakini tunaona kwamba unabii huu haukutimia kwa ukamilifu wake. Je utimilifu wake kikamilifu ni wa jinsi gani? Mfalme Justinian alikabidhi mamlaka kwa Papa ambapo Papa alikaa karibia miaka minne kabla ya kutumia madaraka yake aliyokabidhiwa ili kukanyagisha patakatifu na jeshi. Kwa ilikuwepo miaka kadhaa iliyojumuishwa katika muda ulio ndani kati yam waka 1798 na 1844.Mwaka 66 BK Warumi walikanyaga ardhi ya wayahudi lakini hawakufanya mashambulizi yoyote wakati huo. Amiri jeshi wa Rumi, Celstius aliondoa majeshi yake na kurudi Roma. Kipindi hiki kilitabiriwa katika unabii kama kipindi cha wayahudi kuondoka Yerusalemu na kukimbia kwenye milima ya Pella. Walikimbia nje ya Yerusalemu miaka mitatu na nusu kabla ya uvamizi wa jeshi la Rumi mwaka 70. Miaka hii mitatu na nusu inawakilisha kipindi ambapo unabii huu unapojirudia watu wa Mungu watatakiwa kukimbia kutoka miji mikubwa na kufanya maandalizi ya kukimbilia milimani. Nabii Ellen White ameelezea kwa kina katika sura ya kwanza ya kitabu cha Pambano kuu. Wapo wanaofanya makosa wakisema kwamba wakati tangazo la sheria ya jumapili linatolewa, itakuwa ni kipindi cha kutoka ndani ya kanisa asi la SDA na makanisa mengine. Hili ni kosa kubwa maana wakisubiri kipindi hicho watakuwa wamechelewa kuokoa nafsi zao kwa sababu hukumu za Mungu zitaanza ndani ya kanisa lake kwa watu waliopewa upendeleo mkubwa wa nuru hivyo watapimwa katika mizani ya hekalu sawasawa na wingi wa nuru waliyopewa [Tazama 5T 211].
Sasa tunaweza kufupisha kama ifuatavyo:

1.     Sheria ya jumapili itatangazwa. Hakuna adhabu yoyote mwanzoni mwa tanganzo la sheria hii. Tangazo litatolewa siku ya kwanza ya siku 1290 katika kujirudia kwa matukio ya unabii wa siku 2300. Katika siku ya kwanza ya siku 1260 ndipo sheria ya kutokununua wala kuuza sambamba na adhabu za mateso, vifungo na kifo zitatolewa.
2.     Tofauti ya siku 30 kati ya siku 1290 na siku 1260 zinawakilisha kipindi cha kukimbia kutoka miji mikubwa na maandalizi ya kuhama kwenda milimani tangu tangazo la sheria ya jumapili kutokewa na kabla ya kuanza kwa mateso.
3.     Katika siku ya kwanza ya siku 1260, hukumu za Mungu zinaanza kwa sababu ya kupuuza sheria Yake. Hukumu zitaongezeka zaidi na watakatifu watalaumiwa kuwa wanasababisha hukumu hizo kwa sababu wamekataa kutii jumapili.
4.     Ellen White anafananisha sheria ya jumapili na ujio wa kwanza wa jeshi la Rumi katika ardhi ya wayahudi mwaka 66. Kipindi hiki kitakuwa ni kwa ajili ya kuondoka kwenye miji mikubwa na kukimbilia kwenye midogo kwa maandalizi ya kukimbilia milimani {Tazama 5T 464-5}
5.     Tunatambua kwamba kutakuwa na kipindi kinachowakilishwa na miezi 42 ya mateso baada ya jeraha la mauti kupona kimamilifu (Ufunuo 13:1-5). Wakati wa tangazo la sheria ya jumapili jeraha la mauti litakuwa limepona lakini siyo kikamilifu.
6.     Kipo kipindi cha ‘kukanyagisha patakatifu na jeshi’ kitakachotumiwa na viongozi wa kanisa asi la SDA kwa kuwalazimisha waumini wao kuitunza jumapili. Kipindi hiki kitaendelea hadi wakati wa kufungwa kwa mlango wa rehema baada ya patakatifu kutakaswa ambapo kujirudia kwa unabii wa Ezekiel 9 kutasababisha angamizo la kanisa asi ya SDA na mchakato wake mpya. Mapigo saba hayatamwagwa juu ya dunia hadi mlango wa rehema utakapofungwa.

Kutakuwepo na matangazo mawili. Tangazo la kwanza litatolewa siku ya kwanza ya siku 1290 na kutakuwepo na siku 30 za maandalizi ya watu wa Mungu kukimbilia milimani na siku ya kwanza ya siku 1260 litakuwa ni tangazo la kifo kwa wale watakaokaidi kuitunza jumapili. Tangazo la pili litatolewa baada ya kufungwa kwa mlango wa rehema na mapigo saba yataanza kumwangwa juu ya nchi. Nabii Ellen White anasema hakutakuwepo na wafia dini baada ya kufungwa kwa mlango wa rehema lakini kutatolewa tangazo la kifo kutaka kujaribu kuwaua wale 144,000 ambapo silaha za adui zitakuwa kama manyasi hivyo tangazo hilo halitapata mafanikio. Kwa hiyo tangazo moja la kifo linafanikiwa kusababisha vifo vya wafia dini waaminifu na tangazo la pili halifanikiwi kwa sababu mlango wa rehema utakuwa umefungwa duniani kote na wale waaminifu watakuwa hai wasionje kifo kama Henoko na Eliya walivyopaa mbinguni bila kuonja mauti.
‘Lile kosa liletalo ukiwa’ linalosababishwa na kanisa asi la SDA linaufanya unabii wa siku 2300 kuwa na umuhimu mkubwa wa kujirudia. Kisha kutakaswa kwa mwisho kwa patakatifu pa Mungu kutafanyika ikiwa siyo mwanzo wa kutakaswa kwa patakatifu kama ilivyokuwa katika historia ya utimilifu wa unabii huu uliofikiwa mwisho wake mwaka 1844.
Wale wanaongejea na kuzifikilia siku 1335 wana heri kwa sababu wanajua kwamba kama watakimbilia milimani, watakuwa salama. Wale wote wanaokimbilia milimani wataletwa katia agano na Mungu kama ilivyoandikwa na nabii Ezekieli 20:34-38. Wataendelea kutoa kilio kikuu wakiwa jangwani ambao wale waliopokea alama ya mnyama bila kujua na wanaposikia kilio kikuu na kutii, wataokolewa.
Toafuti ya siku 75 kati ya siku 1260 na 1335 inahusika na kipindi cha kukimbilia milimani (siku 30) pamoja na kipindi cha kusubiri tangazo la marejeo ya Yesu mara ya pili (siku 45). Kipindi hiki ni sawa na miaka mitatu na nusu iliyotumiwa na wayahudi wakiwa kwenye milima ya Pella tangu mwaka 66 hadi 70 kabla ya angamizo la Yerusalemu.
Baadhi hawataweza kukimbilia milimani hivyo watakuwa wahanga na mashahidi wa kufia dini wakiwa watiifu kwa Mungu. Tunapaswa kukesha na kuomba kwa bidii ili kukuza tabia zetu zitakazotuwezesha kuwa tayari kutoa miili yetu kuwa kafara ya kumpendeza Mungu. Wapo pia watakaofungwa magerezani na wengine watakutwa na Yesu wakiwa hai gerezani na kuokolewa bila kuonja mauti kama vile Paulo na Sila walivyookolewa.

Sasa tunaweza kuweka maana ya sasa kwenye utimilifu wa unabii huu kama ifuatavyo:
““Na tangu wakati ule ambapo sadaka ya kutekezwa ya daima (Sheria ya Sabato ya Kweli) itaondolewa, na hilo chukizo la uharibifu(Sheria ya jumapili) litakaposimamishwa, itapita siku elfu na mia mbili na tisini. Heri angojaye, na kuzifikilia siku hizo elfu na mia tatu na thelathini na tano, (angojaye kwa kipindi chote cha uvumilivu mkubwa tangu siku ya tangazo la sheria ya kutokuuza na kutokununu, sheria ya vifungo na kifo, hadi kufungwa kwa mlango wa rehema).”  {Daniel 12:11,12.}

Katika kipindi kinachowakilishwa na siku 30 ikiwa ni tofauti kati ya siku 1290 na siku 1260, Wale 144,000 watakimbilia milimani wakati wa sheria ya jumapili inapotangazwa. Hawa ndiyo wanaoitwa ‘Sayuni’ na watalindwa na Mungu kama wayahudi waaminifu walivyolindwa mwaka 66 hadi 70 wakati wa angamizo la Yerusalemu.[Tazama The Great Controversy p. 426-7).
Lakini pia kuna tofauti ya siku 75 kati ya siku 1335 na siku 1260 ambapo kipindi hiki kinajumuisha vipindi viwili kwa pamoja, mosi kipindi cha siku 30 za kuanza kutoka miji mikubwa, kujiandaa na kuondoa miji midogo kwenda milimani na siku 45 zinawakilisha kipindi cha watakatifu kukaa milimani sawa na miezi 42 ya mateso wakati wa utimilifu wa unabii wa siku 2300 sehemu ya kwanza na miaka mitatu na nusu ya kuishi milimani kusubiri angamizo la Yerusalemu.

Hitimisho.
Mwanzo wa utimilifu wa unabii wa siku 2300 ni mwaka 457KK na ulifikia mwisho mwaka 1844 katika hali ya utimilifu wa siku moja kwa mwaka mmoja. Unabii wa siku 2300 umetajwa katika matukio ya siku 1260, siku 1290 na siku 1335. Mwanzo wa utimilifu wa unabii wa siku 1260 ni mwaka 538 na ulifikia mwisho wake mwaka 1798 kwa tukio la jereha la mauti baada ya Papa kukamatwa mateka na kufia ufaransa. Siku 1260 zinahusika na kipindi cha miaka 1260 ya mateso kutoka kwa kanisa la Rumi lililokuwa na mamlaka kamili ya kiserikali na kidini. Tukio kubwa katika unabii wa siku 1260 ni kuwekwa kwa sheria ya kuwaua wale waliokuwa kinyume na kanisa la Rumi. Unabii huu utajirudia wakati jeraha la mauti litakapopona kikamilifu kwa kanisa la Rumi kurejea tena kwenye mamlaka kamili ya kidini na kiserikali na kuweka sheria ya kuwaangamiza wale watakaokataa kutii sheria ya jumapili. Mwanzo wa utimilifu wa unabii wa siku 1290 ndio mwanza wa utimilifu wa unabii wa siku 1335 ambapo tukio linaloashiria mwanzo huu ni kuondolewa kwa sadaka ya kutekezwa ya daima na kusimamishwa kwa chukizo la uharibifu. Kujirudi kwa utimilifu wa unabii huu ni wakati wa tangazo la kufutilia mbali sheria ya Sabato ya kweli na mahali pake kusimamisha sheria ya jumapili. Mwanzo wa kipindi hiki ni mwaka 508 ambapo mwisho wa kipindi cha siku 1290 ni mwaka 1798 na mwisho wa kipindi cha siku 1335 ni mwaka 1843 kuelekea 1844.
Wakati chukizo la uharibifu litasimamishwa na ndani ya kanisa kutokea nje, lile kosa lifanyalo ukiwa litafanyika ndani ya kanisa asi la SDA. Hii ni kwa sababu viongozi wa kanisa asi la SDA, siyo tu kwamba hawataijali Sabato, bali pia watawalazimisha waumini wa kanisa hili kuitunza na kuiheshimu siku ya kwanza ya juma, jumapili badala ya siku ya saba ya juma Sabato. Jambo hili litasababisha ghadhabu ya Mungu na hukumu zake kuanza katika nyumba yake. Wakati hukumu za Mungu zinashuka juu ya dunia, watunza Sabato wa kweli, yaani masalio wa kanisa asi la SDA ambao waliamua kutoka na kukimbia kwa kujitenga na kanisa hilo, watasondwa kidole kuwa ndio wanaosababisha hukumu za Mungu hivyo watatafutwa ili wauwawe. [Tazama The Great Controverdy p. 635.]

“Na kama Bwana asingalikatiza siku hizo, asingeokoka mtu yeyote; lakini kwa ajili ya wateule aliowateua amezikatiza siku hizo.” Marko 13:20.

“Usiogope mambo yatakayokupata; tazama huyo ibilisi atawatupa baadhi yenu gerezani ili mjaribiwe, nanyi mtakuwa na dhiki siku kumi. Uwe mwaminifu hata kufa, nami nitakupa taji ya uzima.” Ufunuo 2:10.

Somo linalofuata ni somo la “Hema Takatifu”.

kwa mawasiliano wasiliana na 0756959525/0752164685





Share:

Popular Posts

Lebo

Recent Posts

Pages