Mfano huu unapatikana katika Mathayo
13:24-30 na 36-43. Ni mashuhuri kwa watu wengiambao aidha
wameusoma au
wameusikia ukihubiriwa kwa kurudiwarudiwa. Unaweza ukawa wazikiasi kwamba
tukafikiri tayari tunaufahamu na kuweza kuwa na tabia ya kusoma kwa haraka bila
kujaribu kutafuta kweli zilizofichwa ambazo zimezikwa chini ya dunia.
Kwa kweli mfano huu unaweza kuwa
ndiyo usioeleweka na unaotafsiriwa vibaya leo na hutumiwakuwachanganya watu
wetu kanisani; tumetegemea wachungaji na viongozi wa makanisa, taasisi za
kujitolea, na makundi mengine kuwa tayari kukubali mafundisho na mapokeo ya
wazee, bila kujaribu kujitafutia ukweli sisi wenyewe chini ya uongozi wa Roho
wa Mungu.Wengi wanaona bora kuamini hekima ya kibinadamu, kukubali hoja
zinazoelekea kuwa na mantiki za marabi na mafarisayo wa kileo badala ya
kuthibitisha na kuyapima mafundisho kwa kuhakikisha kuwa “hivi ndivyo asemavyo
Bwana”, na “kwa sheria na ushuhuda”. Lakini Je, hii ni njia salama kufuata?
Hapana! Yeremia 17:5 anasema “amelaaniwa mtu Yule amtegemeaye
mwanadamu, amfanyaye mwanadamu kuwa kinga yake”.
“Kama Nathaniel angewategemea
marabi wamuongoze, asingempata Yesu. Ilikuwa nikwakuona na
kujiamulia mwenyewe kwamba alikuwa mwanafunzi. Hivyo kwa wale ambao leo chuki
binafsi inawazuia kupata mema……….wakati wanatumainia mamlaka za kibinadamu,
hakuna atakaye yafikia maarifa yaokoayo ya kweli. Kama Nathaniel, tunahitaji
kijisomea neno la Mungu sisi wenyewe, na kuomba Roho mtakatifu atuongoze”. Desire
of Ages pg 140-141
Kwahiyo hatuwezi kutegemea hekima
ya wanadamu ituongoze katika njia salama, bali lazima kwa maombi na juhudi
tuutafute ukweli sisi wenyewe. Tukipambanisha andiko kwa andiko, msitari kwa
msitari, shuhuda kwa shuhuda, hapa kidogo na pale kidogo, ndipo machafuko
yatakapo peperukia mbali, naye Mungu ataturuhusu tuone kweli zake dhahiri bila
lundo la taka za desturi na mapokeo, ndipo tutaweza kuzifanyia kazi kweli
zilizofunuliwa nasi tutajua kuwa msingi wetu umesimama imara. Katika kujaribu
kuelewa mfano huu wa ngano na magugu haiwi vinginevyo. Mama White anaeleza mara
baada ya kunukuu mfano huu: “Soma fundisho hili kwa umakini, ukifanya yote
yaliyo ndani ya uwezo wako kuuelewa mfano huu. Roho mtakatifu ataziongoza akili
za wale wanaotafuta ufahamu kamili wa mfano huu”.Review and Herald, vol
4, (4RH) uk 395, col 2.Basi kinyume cha ushuhuda huu pia ni kweli
kwamba wale wasiosoma mfano huu kwa uangalifu na kujaribu kufanya vyovyote
wanavyoweza kuelewa, hawatapokea maongozi kutoka kwa Roho wa Mungu. Watauelewa
vibaya na kueneza machafuko na makosa kila mahali, hili ndilo jambo lililotokea
na linaendelea kutokea. Hivyo hebu tusome mfano huu kwa uangalifu, tukichunguza
na
kufafanua kila moja ya alama
ambayo Kristo anaitumia ili tuone kama hatuwezi kuondoa sehemu ya machafuko
yanayozidi kuongezeka leo.
“Akawatolea mfano mwingine,
akisema, Ufalme wa mbinguni unafanana na mtu aliyepanda mbegu njema
katika konde lake, lakini watu walipolala, akaja adui yake akapanda
magugu katikati ya ngano, akaenda zake. Badae majani ya ngano yalipomea na
kuzaa, yakaonekana na magugu. Watumwa wa mwenye nyumba wakaenda wakamwambia,
Bwana, hukupanda mbegu njema katika konde lako? Limepata wapi basi magugu? Akawaambia
adui ndiye aliyetenda hivi. Watumwa wakamwambia, Basi, wataka twende
tuyakusanye? Akasema, La; msije mkakusanya maguu, na kuzing’oa ngano pamoja
nayo. Viacheni vyote vikue hata wakati wa mavuno; na wakati wa mavuno
nitawaambia wavunao, yakusanyeni kwanza magugu, myafunge matita matita
mkayachome; bali ngano ikusanyeni
ghalani mwangu”. Mathayo 13:24-30,
Ni nini kinachowakilisha “ufalme
wa mbinguni au wa Mungu”? Je, Kristo hapa anaongelea mahala anapoishi Mungu
huko juu kwenye mbingu halisi ama anajaribu kulielezea hili katika mazingira ya
kiroho au kwa maneno mengine, mahali anapoishi Mungu, kupitia neno lake
lililoandikwa mioyoni na akilini mwetu? Je, Kristo anazungumza hapa kwa maana
halisi au kwa maana ya kiroho? “Na alipoulizwa na mafarisayo, Ufalme wa Mungu
utakuja lini? Aliwajibu akawaambia, Ufalme wa Mungu hauji kwa kuuchunguza; wala
hawatasema, Tazama, upo huku, au kule, kwa maana, tazama, ufalme wa Mungu
umo ndani yenu.” Luka 17:20-21 Hivyo Kristo anaongelea maana
ya kiroho ya ufalme wa Mungu, uliomo ndani ya akili zetu kupitia kwenye neno
lake! Oh, huoni umuhimu wa sisi kujifunza sisi wenyewe, tukichimba Biblia na
shuhuda, tukila na kunywa maneno ya Mungu sisi wenyewe, tutawezaje basi
kuthibitisha
tumaini lililomo ndani yetu, kama
halimo? Tutawezaje basi kumuakisi Kristo, kung’aa kama nyota zinazong’aa sana
katikati ya giza nene la dunia hii ya uovu, na kumpa heshima istahiliyo jina
lake takatifu? Ili tuyaweze hayo yote, Ufalme wa Mungu lazima uwemo ndani yetu.
Tafadhali usisahau wazo hili kwa
sababu ni wazo moja la muhimu kukumbuka unapojaribu kuelewa mfano wowote wa
Kristo unaohusiana na ufalme wa mbinguni.Nani katika mfano huu, mtu anayepanda
mbegu njema au ngano? Ni Kristo (mathayo.13:37).Kwa hiyo
ni nani anakuwa adui wa Yesu aliyepanda mbegu au magugu katika shamba la Yesu?Ni
Shetani (Mathayo13:39). Kristo alipanda mbegu za ngano shambani
mwake ikionyesha kwamba Kristo alikuwa amelinunua shamba lake kwa gharama.Sasa
ni nani wanawakilisha shamba? Ni sisi! Linawakilisha roho zetu au
akili zetu:“Adui anayepanda mbegu mbaya, ni mfano wa kazi ya shetani
kwenye akili za wanadamu.Kristo ndiye mpanzi anayepanda mbegu ya thamani
katika ardhi yenye rutuba ya moyo.”SPIRIT OF PROPHECY, VOL 2 (2sop), uk
248
Lakini inamaanisha kitu Fulani
tena. Kristo anasema katika (Mathayo 13:38) kwamba shamba linamaanisha
ulimwengu. Neno la kigiriki linalomaanisha “ulimwengu” lililotumika hapa ni“kosmos”
likimaanisha mpangilio unofaa wa vitu duniani.
Naye Ellen White analibainisha
hili: “Shamba, Kristo alilosema, ni ulimwengu. Lakini lazima tuelewe hili
kwamba linamaanisha kanisa la Kristo duniani”.
CHRIST OBJECT
LESSONS (COL), UK 70
Kwa hiyo shamba
linamaanisha kanisa, lakini
pia lina maana ya kina ya kiroho na
Inayomaanisha mioyo au akili
zetu.Nani anawakilisha mbegu njema au ngano iliyopandwa katika shamba lake?
Ingemaanisha vitu viwili. Kristo anasema katika Mathayo 13:38 kwamba
lile konde ni ulimwengu; zile mbegu
njema ni wana wa
ufalme au wanafunzi wa kweli kwenye kanisa la Mungu. Inawakilisha pia mafundisho
safi ya Mungu au kweli zilizopandwa ndani ya mioyo yetu. Au neno la Mungu ndani
ya mioyoNa
huo mfano, maana yake ni hii; mbegu ni neno la Mungu” Luka 8:11 Mbegu
hii (au neno la Mungu) inapandwa kwenye shamba (au mioyoni na akilini
mwetu); ikimaanisha mafundisho ya neno la Mungu kwa upande wa ngano na
mafundisho ya Shetani kwa upande wa magugu.Nani anawakilisha mbegu mbaya
au magugu? Magugu ni wana wa mwovu au wafuasi wa kweliwa shetani. Inawakilisha
pia mafundisho machafu ya shetani au makosa yaliyopandwa ndani ya mioyo
yetu.
1. Sasa tuzirudie
aya tena na kuweka maana sehemu ya alama, halafu tutumie maana ya kina ya kiroho.Ufalme
wa mbinguni (au wokovu unaopatikana kwa kuishi ndani ya neno la Mungu linaloandikwa
mioyoni na akilini mwetu), unafananishwa (au ni sawa) na Mtu (au
Kristo Yesu) aliyepanda mbegu njema (au aliyetawanya kweli safi za
Mungu) Katika shamba lake (au katika akili na mioyo ya watoto wa Baba
yake ambao Mungu aliowanunua kwa gharama kuu za mwana wake mpendwa.). Lakini
watu walipolala (au watu w N a Mungu walipoacha milango ya mioyoni na
akilini bila ulinzi; [maana Biblia inasema: ‘Linda sana moyo wako kuliko
yote uyalindayo’ Mith 4:23]) adui yake alikuja
akapanda magugu katikati ya ngano akaenda zake
(au shetani aliingia akapanda
makosa na mafundisho ya uongo katikati ya kweli safi za Mungu, kwa
kuvichanganya pamoja, akaondoka zake bila kugundulika.)
2. Hebu sasa
tuzichunguze aya zilezile na kutumia maana nyingine ya sisi wenyewe badala ya alama
za kiroho.
Ufalme wa
mbinguni (au
maana ileile iliyotumika hapo kwanza au mchakato wa kuupatawokovu); unafananishwa
na (au ni sawa na) mtu (au Kristo) aliyepanda mbegu njema katika
shamba lake( au aliyewaweka Masalio wake katika kanisa duniani) Watu
walipolala (au viongozi au waangalizi wa Masalio wa Mungu wakipoteza wivu
na kuacha mlango wa kuingilia kanisani bila ulinzi) adui yake alikuja
akapanda magugu katikati ya ngano akaenda zake (au shetani aliingia
akawaweka watu wake na mawakala katikati ya kanisa akiwachanganya na Masalio
naye akaondoka bila kugundulika.).
Je, inawezekana kuwa na neno moja
lenye maana mbili kwenye Biblia? Ndiyo,
“….vile vichwa saba ni milima
saba anayokalia mwanamke huyo. Navyo ni wafalme saba…”Ufun.
17:9,10
Hapo tunaona vichwa vikibeba
maana mbili kwa wakati mmoja, yaani milima na wafalme.Hivyo basi
katika mfano wa Yesu hapo juu tunaona neno moja likimaanisha maana mbili kama tulivyoonyesha
hapo juu shamba likimaanisha kanisa la Mungu duniani au mioyo
na akili za wanafunzi wa kweli wa Yesu. Na pia tumeona kuwa ngano inamaanisha
watu wa Mungu duniani au mafundisho safi ya Yesu, yaani neno la
Mungu. Lakini pia tumeona magugu kuwakilisha wafuasi wa Shetani au
mafundisho ya Shetani ndani ya kanisa. Sasa ni nani wanawakilisha shamba au
kanisa? Ni Kanisa la SDA. Kwa vile Kristo alianza kwa shamba safi na mbegu
safi, kwa hiyo alianzisha kanisa hili kwa usafi na watu waliochaguliwa walikuwa
ni watu wa Masalio na kanisa. Lakini ni nini kilichotokea katika mfano? Watu, au
waangalizi wa shamba walilala na
kumruhusu adui kuingia, kujaribu na kuharibu shamba lote kwakueneza na
kuchanganya magugu na ngano.
Je, hili limetokea katika kanisa
la SDA? Je, kanisa na viongozi wake walilala? Wakipoteza wivu wa kumfanyia kazi
mwenye kanisa? Ndiyo!
“Kama Kusudi la Mungu
lingetekelezwa na watu wake kwa kuipatia dunia ujumbe wa rehema, Kristo
angekuwa amerudi duniani, nao watakatifu wangekuwa wamekaribishwa katika
jiji la Mungu.” Testimonies, vol 6 (6T), uk 450
“Kama kila askari wa Yesu angekuwa
ametimiza wajibu, kama kila mlinzi kwenye kuta za sayuni angeipiga mbiu yake
kikamilifu, dunia ingekuwa imesikia ujumbe na onyo mapema. Lakini kazi imechelewa
kwa miaka mingi. Shetani ametuvizia wakati WATU WAMELALA, akaifanya kazi
yake.” 9T 29
Hivyo uongozi wa kanisa na
walinzi wake walipoteza wivu, wakasinzia. Lakini je, walimruhusu shetani
kuingia kanisani akawatawanya wafuasi na mawakala wake au magugu katika ngazi
zote ili kujaribu kuiharibu ngano? Ndiyo!
“Watu wanoshikilia nafasi
kubwa kwenye kitovu cha kazi WAMELALA. Wamepoozwa na Shetani ili kwamba
mipango na hila zake zisigunduliwe, wakati anafanya kazi ya kunasa, kudanganya,
na kuangamiza”.
“Baadhi ya wale wanaoshikilia
nafasi za walinzi ili kuwaonya watu juu ya hatari, wameacha kazi yao na
kubweteka. Si walinzi waaminifu.Wanatulia wakati adui yao mwerevu anaingia
katika ngome na kufanya kazi kwa ukamilifu kando yao na kuvunja kile
ambacho Mungu ameamuru kijengwe.Wanaona kwamba shetani anawadanganya
wale wasio na uzoefu na wasio
makini; bado wanakaa kimya, kana
kwamba hawana jukumu maalumu, kana kwamba mambo haya hayakuwahusu. Hawaoni
hatari yoyote, hawaoni sababu ya kutangaza hatari. Na shetani anashangilia
kufanikiwa kwake kuzitawala akili za watu wengi wanaodai kuwa ni wakristo. Amewadanganya,
amezitia ganzi fahamu zao, akapanda bendera ya kuzimu (mafundisho ya
uongo) katikati yao, nao wamedanganyika kiasi kwamba hawajui kuwa
ni yeye….” “Washiriki wake wamevunja agano lao la kuishi kwa ajili ya Mungu,
naamu yeye tu…naye Kristo ameondoka. Roho wake amenyamazishwa ndani ya
kanisa. Shetani hufanya kazi bega kwa bega na wakristo kwa jina; lakini
wanakosa utambuzi wa kiroho kiasi kwamba hawamgundui. Kweli kuu wanazodai
kuziamini haziwasaidii…Nilishangaa nilipotazama giza la kutisha la washiriki
wengi wa makanisa yetu. Kukosekana kwa uchaji wa kweli kulikuwa ni kwa
kiwango kikubwa kiasi kwamba
waligeuka chanzo cha uovu na mauti, bila ya kuwa nuru kwa ulimwengu. Wengi walidai kumpenda Mungu,
lakini kwa matendo walimkana…Uchafu wao utawatisha katika siku ile ambayo
inatujia upesi sana”. 2T 439-446 Kwa kusema kitovu cha kazi ingemaanisha
nini kama si General Conference? Hakika uongozi na walinzi wa kanisa la SDA
wamelala wakamruhusu shetani aingie kanisani. Shetani kwa ustadi amepanda
bendera yake ya kuzimu akapanda magugu maovu katikati ya ngano na sasa mbegu ya
thamani na mbaya zimechanganyika pamoja ndani ya kanisa. Sasa gugu ni nini? Kwa
kweli gugu ni mbegu chungu inayosababisha kichefuchefu na kutapika. Pia ni
mbegu yenye sumu kali yenye kulewesha inayosababisha usingizi na ikiwa nyingi imetumiwa,
husababisha kifo. Kwa hiyo kwa maneno mengine inasababisha usingizi wa kifo. Ni
hali gani ambayo punde nimeifafanua? Hali ya Laudikia hali ya usingizi ya
Laudikia.na ikibaki kama ilivyo kwa muda mrefu zaidi itasababisha usingizi wa
kifo. Sasa je, hali ya walaudikia
inawakilisha magugu? “Tunao
ushahidi tele kwamba magugu yanaota pamoja na ngano katika kanisa la Mungu. Kuna
wakristo waaminifu katika kanisa la Mungu na kuna wakristo wa uvuguvugu pia.Waadventista
wa uvuguvugu.” Ellen G white Upward look, p. 35 Je, hawa
walaudikia wanamsababishia nani kichefuchefu na kutapika? KRISTO.. “Basi
kwa sababu una uvuguvugu, wala hu baridi wala moto, nitakutapika utoke
katika kinywa changu.” Ufunuo3:16
Kwa hiyo Kanisa la laodikia la
SDA ndilo linalomsababisha Kristo kulitapika kwa sababu ya uvuguvugu wake na
bado wanafikiria wanamtumikia Kristo kwa hali hiyo na wanaamini wataokolewa. Ina
maana gani kwa Kristo kuwatapika watoke kinywani mwake? “Kitendo cha kutapikwa
na Kristo ina maana kwamba Hawezi kuwakilisha maombi yao na maelezo yake kwa
Mungu. Hawezi kukubaliana na mafundisho yenu ya neno Lake au kazi yenu ya
kiroho kwa namna yoyote. Hawezi kuwakilisha mazoea yenu ya kidini na maombi
ambayo angewapa neema” 6T 408.
Je, Ni lini ambapo kwa ishara
Kristo anawatapika kutoka katika kinywa chake walaodikia? Je Ni wakati
wanapodidimia kikamilifu katika hali hii ya uvuguvugu? Au ni wakati wa badae wa
kukaribia kufungwa kwa mlango wa rehema?
“Kwa wale ambao hawaweki kivitendo
neno la Mungu, ni barua iliyokufa. Kristo anasema kwa hao; ‘Heri ungekuwa
baridi au moto. Kwa hiyo, kwa kuwa u vuguvugu, hu baridi wala moto,nitakutapika
utoke kinywani mwangu’. Hawezi kupeleka mahitaji yao kwa Baba. Kama watatambua
kuwa ni wadhambi, angeweza kuwaombea, na Bwana angewanyanyua kwa Roho mtakatifu
wake. Lakini ni wabaya kuliko wafu kwa makosa na dhambi. Wanasikia neno, lakini
hawalifanyii kazi; badala yake wanalifanyia kazi neno kwa majirani zao.” 7BC
96 col 2& 964 col 1.
“Shahidi mwaminifu asema kuhusu ubaridi,
maisha hafifu, kanisa lisilo na Kristo, ‘nayajua matendo yako, kwamba hu
baridi wala hu moto… Kwa hiyo kwa kuwa u vuguvugu, hu baridi wala hu moto,
nitawatapika watoke kinywani mwangu,’ (Ufun.3:15-16). Kwa kuwa
wasema, mimi ni tajiri, na mwenye kila kitu, na sihitaji chochote….Kristo
hawezi kuchukua majina ya wale ambao wameridhika kwa namna
walivyojitosheleza. Hawezi kuwaombea watu wasiohisi hitaji la msaada
wake, wanaodai kujiona kuwa na kila kitu.” 1SM p. 357- 358
Je, neno importune lina
maana gani? Lina maana ya kujibu maombi na matakwa. Hivyo mara kanisa au mtu
anapoangukia kabisa katika hali ya uvuguvugu ya kujitosheleza, ya
ulaudikia,Kristo hawezi kujibu sala au maombi ya baraka .Hawezi kupeleka maombi
yao kwa Baba, ambayo humaanisha kwamba wameshatapikwa! kabla hawajapata nafasi
ya kuokolewa, lazima watubu na kutoka kwenye hali hii. Mama White alisema
kwamba kanisa la SDA lilikuwa katika hali hii ya kuhuzunisha.
Lakini je, Mungu aliliacha kanisa
katika hali hii ya kutapikwa lipotee? Hapana! Mungu
alituma jumbe za kweli za
kujaribu ambazo zingewaamsha watu wake na kanisa, akiwasababisha kudhihirisha
Roho wa kweli katika mioyo yao ama kwa maneno mengine kuzaa matunda. Kweli
hizi za kujaribu zingeonyesha nani alikuwa ngano na nani alikuwa gugu ama
kwa kukubali na kuzifanyia kazi AU kwa kukataa kuzipokea na kuzikana kweli hizi
au kuzipinga hivyo kutapikwa! Unaweza kuniambia kwamba jumbe hizi za moja kwa
moja na zakujaribu ambazo ndizo zimebeba
majaliwa ya watu wa Mungu ni
nini? Ni ujumbe kwa Laudikia au kweli za karipio kali. Ellen White anasema
katika Early writings EW p. 270, Kwamba kwa kweli hatua ya kanisa
inategemea ushuhuda wa moja kwa moja wa shahidi mwaminifu (Kristo) kwa
walaudikia. “…Huu utaubadilisha moyo wa mpokeaji, nao utamfanya ainue bendera
na kumwaga ukweli usiopinda...Ushuhuda huu lazima umbadilishe kwa ungamo la
dhati; kwa kweli wote watakaoupokea watautii na kutakaswa. Baadhi
hawatauvumilia ushuhuda huu usiopinda, wataupinga, na hili ndilo
litakalosababisha pepeto miongoni mwa watu wa Mungu.” EW 270;
Kwa hiyo wanaoukubali na kuutii ukweli huu usiopinda wenye kujaribu watazaa
tunda au kujidhihirisha wazi kwamba ni ngano halisi, na wale wanaoukataa
na kuupinga watazaa tunda au kujidhihirisha kuwa magugu halisi.
Je, ni lini
ushuhuda huu usiopinda kwa laodikia na washiriki wake ulianza?
“Watu wa Mungu lazima wayaone
makosa yao na kuamka kufanya toba ya dhati, na kuachana na dhambi zile ambazo
zimewaweka kwenye hali ile yakusikitisha ya umasikini, upofu, unyonge, na udanganyifu
wa kutisha. Nilionyeshwa kwamba ushuhuda mkali lazima udumu kanisani. Hili peke
yake litajibu ushuhuda unaofaa kwa walaodikia. Makosa lazima yakemewe, dhambi
lazima iitwe dhambi, na uovu lazima ushughulikiwe mara moja na kwa dhati na
kuondolewa mbali na sisi kama watu.”
“Wale wenye roho ya upinzani kwa
kazi ambayo kwa miaka ishirini na sita sisi (yeye na mume wake ) tumesukumwa
na Roho wa Mungu kuifanya, ambao wangeuvunja ushuhuda wetu, niliona hawapigani
na sisi, bali na Mungu…” 3T 260
Hivyo kwa miaka 26 yeye na James
walikuwa wakitoa ushuhuda usiopinda wenye karipio kali kwa kanisa na washiriki
wake. Ushuhuda huu uliandikwa lini basi? Mwaka 1873.Hivyo 1873 ukitoa
miaka 26 unaweza kupata mwaka 1846-47 ambapo ujumbe wa kweli kwa Walaodikia
ulipoanza kuhubiriwa kwa watu wake. Hakika walinzi wa kanisa waliwahi kulala, wakiruhusu
magugu ya shetani yaingie, yote haya yalitokea miaka miwili tu baada ya1844.
JE, PEPETO
LILIANZA LINI BASI?
“ Pepeto kali limeanza na
litaendelea, na wote watapeperushiwa nje wasiotaka kuchukua msimamo wa ujasiri
na usio tetereka kwa ajili ya kweli, na kujitoa mhanga kwaajili ya Mungu nakazi
yake.” EW 50
Nini maana ya ‘msimamo wa ujasiri
usio tetereka’? ni wazi kwamba huo si kitu kingine bali ujasiri wa kufanya
maamuzi magumu ya kujitenga na mfumo unaopendelea magugu au mafundisho ya
Uongo.
HII ILIANDIKWA
LINI? January
26,1850. Kwa hiyo pepeto tayari limeanza kabla ya mwaka 1850, na pepeto hili
lilikuwa linasababishwa na ushuhuda usiopinda wa ukweli wa kuwajaribu uliokuwa
unamwagwa kwa watu wa Mungu na watu wake. Kwa hiyo watu walikuwa tayari wakijidhihirisha
kuwa magugu na ngano halisi kufikia mwaka 1850, ama kwa kupokea
onyo kali wakijitakasa na kutangaza ujumbe huo huo au kwa kuukataa na kuupinga
ujumbe na wale walio uhubiri.
Basi ni muhimu kukumbuka kwamba
Kristo alianza kanisa lake la Masalio kwa usafi, lakini kwa vile uongozi
uliruhusu magugu kuingia kanisani na kwenye mfumo, na kuzaa matunda ya uovu, kanisa
na mfumo wote, unakoma kuitwa kanisa la “Masalio” kwa sababu ya magugu yaliyo
ndani yake. Sasa nini kinafuata? Mungu anawaita watu wake waaminifu na
kuwafanya kuwa ‘masalio’ wake. Watu wanaoendelea kuzaa matunda ya haki na
kutimiza maelezo na masharti ya ufunuo12:17 wangali wanachukuliwa
kama Masalio (Watu watiifu ndio wanaitwa Masalio na si mfumo unaoitwa
Masalio). Ni kwa vile tu kanisa la Masalio haliwezi kutumiwa kutaja
kanisa lote na
mfumo, kama ilivyokuwa mwanzoni,
kwa sababu uongozi ulilala na kuruhusu mawakala wa shetani kuingia kanisani.
Ndiyo maana katika Mathayo
13:26-28, watumishi waaminifu wanahamu ya kujaribu kuliepusha kanisa na
magugu haya, au mawakala na watoto wa shetani, ili waweze kulirudisha kanisa na
mfumo wake katika usafi wake halisi.
Lakini Kristo anasema katika Mathayo
13:29-30 kwamba hawapaswi kulifanya hili, wasijaribu kuyatenga magugu
na ngano, kwa sababu anayo njia bora zaidi; “Acha vyote vikue pamoja
mpaka wakati wa mavuno, na katika wakati wa mavuno nitawaambia wavunaji,
yakusanyeni kwanza magugu myafunge matita matita mkayachome, bali
leteni ngano safi ghalani.” Katika Mathayo 3:12 anaongeza
zaidi na kusema “ambaye pepeto lake li mkononi mwake, naye
atausafisha sana uwanda wake; na kuikusanya ngano yake ghalani, bali makapi
atayateketeza kwa moto usiozimika”.
Tunazo alama nyingine chache
tunazohitaji kuzifafanua na tutaanza na MAVUNO. Naamini hii nimoja ya
alama zinazofafanuliwa vibaya katika mfano huu wote, nao wanaoutafsiri vibaya
namna kwamba hawataweza kuona na kutambua kile ambacho Bwana anawataka
wakifanye. Kabla yayote hebu tupitie mchakato mzima wa uvunaji na hatua
mbalimbali zinazohusika, ndipo tutaona ni lini kipindi cha mavuno kitaanza.
Mara matunda
yanapozaliwa na kukomaa, uvunaji unaweza kuanza, tena kuna hatua mbili za
mavuno.
HATUA YA KWANZA
YA MAVUNO INAHUSISHA MAMBO HAYA.
-Wavunaji wanaajiriwa kuvuna
ama kukata vichala vya ngano au vichala vya magugu ambavyo vimezaa matunda.
-Wavunaji wanaanza kutenganisha
vichala vya ngano na vichala vya magugu
-Vichala vya ngano vinakusanywa
katika matita matita na kufungwa pamoja kwa kamba.
-Hayo yanafanyika hata kwa
vichala vya magugu.
HATUA YA PILI YA
MAVUNO INAHUSISHA MAMBO YAFUATAYO.
-Wavunaji wanaovuna
shambani au kukusanya matita ya ngano zilizofungwa huiondoa Shambani kupeleka
mahali pa kupepetea, ambayo kwa kawaida ilikuwa juu ya shamba.
-Matita matita ya magugu
yaliyofungwa hurundikwa katika rundo kubwa yachomwe.
-Uputaji wa ngano zilizovunwa
shambani unafanyika ili kutenga ngano na makapi.
-Upepetaji unafanyika pale
makapi yanapokuwa yametengwa na mbegu za ngano.
-Mbegu za thamani za ngano
zinaondolewa toka kwenye uwanja wa kupepetea na
kuwekwa ghalani ambapo zinalindwa
dhidi ya dhoruba.
Hivyo tunaona kwamba hatua mbili
za mavuno zinafanyika katika maeneo mawili tofauti naya pekee!
1. -Hatua ya kwanza ni shambani
2. -Hatua ya pili ni nje ya
shamba
Pia tuliona kwamba mwanzo wa kila
moja ya hatua hizi mbili huitwa “mavuno”. Mwanzo wa hatua ya kwanza, au wa
ukataji wa nafaka ngano isiyozaa matunda unaitwa “mavuno” na ya pili inapoanza,
au yakukusanya ngano iliyofungwa, kuiondoa shambani inaitwa pia “mavuno”.Tazama
katika dictionary yako kama huamini.
Websters inaliorodhesha
neno mavuno kama lenye sehemu au mfuatano wa sehemu mbili. Harvest:
1. The time when
farmers gather in the corn, fruit, or vegetables they have grown.
2 The crop that
is gathered in Mavuno:
1. Wakati
wakulima wanapokusanya nafaka, matunda au mboga walizolima.
2. mazao
yaliyokwisha kusanywa toka shambani na kuwekwa ghalani.
Matukio haya mawili tofauti kila
moja linaitwa mavuno nayo lazima yote yafanyike ili mwenye shamba aweze kupata
nafaka bora za ngano na kuzitunza katika ghala lake.
Sasa ingekuwaje kama mavuno ya
kwanza yangefanyika na hatua zake, na ngano iliyofungwa isingeondolewa
shambani; Je, ungekuwepo uwezekano wa matita haya ya ngano kutoka shambani?
Hapana! Zingepotea kwa sababu zingebaki shambani, nao msimu wa mavuno ungepita
na kukoma. Ndipo dhoruba na pepo zingevuma ghafla nazo zingeoza na kuharibiwa
na mvua nyingi. Au zingeharibiwa na moto uleule unaochoma magugu. Aidha matita
hayo ya ngano yangepotea kwa sababu yalibaki shambani kwa muda mrefu sana bila
kuvunwa.
Hatua ya pili ya mavuno, ya
kuondoa ngano shambani, ni ya lazima sana ili kwamba michakato ya kuputa na
kupepeta ianze kutenga makapi na mbegu safi za ngano. Katika hatua hii ngano
yote huzungukwa na maganda yaitwayo makapi, nayo hujulikana kama machipukizi ya
ngano. Sasa tazama ngano hii iliyodumaa, kila moja ina uwezekano wa kuwa na
mbegu za ngano ndani.
Lakini usingeweza kujua kama zote
zilikuwa na ngano ndani, au kama baadhi zilikuwa tu zinaonesha lakini hazikuwa
nazo, kwa sababu zote zilikuwa zinafanana kwa nje. Mdudu anaweza kuwa aliingia
ndani ya baadhi yake na kuharibu mbegu au labda mbegu haikuweza kuumbika hata kidogo.
Hivyo hizi zingekuwa makapi ambayo mwenye shamba hazihitaji hata
kidogo.Machipukizi yote yanayokuja kwenye viwanja vya kupepetea yanauwezekano
wa kuwa na mbegubora ya ngano ndani na kuokolewa. Lakini haitafahamika ni kiasi
gani cha mavuno kingepatikana mpaka makapi yasiyofaa yanapotengwa yasiwe pamoja
na ngano ndipo ngano inatolewa kwenye
viwanja vya kupepetea na kuwekwa
ghalani ambapo inalindwa dhidi ya dhoruba na upepovinavyotarajiwa punde. Lakini
ngano hiyo iliyofungwa matita isipoondolewa shambani, ngano hiyo haina nafasi
ya kuokolewa katika ghala la mwenye shamba.
Tumeona tayari mchakato wa mavuno
hatua zote za ndani na nje ya shamba, na sasa tutautazama muda wa mavuno.
Uvunaji unafanyika lini na ngano kutengwa na magugu? Watu wengi leo wanaamini
tena wamefundishwa kwamba mavuno yanavunwa Kristo anaporudi mara ya pili katika
mawingu ya mbinguni, ndipo wakati huu kutenganishwa ngano na magugu kutafanyika.
Hivyo wanajenga hoja kwamba hakuna wanaopaswa kujitenga mpaka Kristo aje. Je, hii
ni kweli? Hapana!
Hebu tuangalie Kristo anachosema
kuhusu muda wa mavuno tuone kama tunaweza kuondoa kiasi fulani cha machafuko na
ujinga wa uelewa katika mfano wa mpanzi ambao ni muhimu kuufahamu kama
ilivyokusudiwa na Yesu Mwenyewe.
Kristo anasema katika Mathayo
13:39 kwamba “yule adui aliyepanda magugu ni Ibilisi; mavuno ni
mwisho wa dunia; na wale wavunao ni malaika”.Neno la kiyunani linalo
maanisha dunia lililotumika hapa ni “Aion” linalomaanisha “zama”.
Lakini hasa linamaanisha “kipindi cha masihi kiwe cha wakati huu au ujao”.
Hivyo tunaona kwamba mwisho wa
dunia unamaanisha mambo mawili.
1. katika wakati uliopo
inamaanisha kukoma au kufungwa kipindi cha Masihi
2. katika wakati ujao inamaanisha
kikomo kamili cha wakati unaomuhusisha Masihi.
Neno “Masihi” linamaanisha
mwokozi na mfunguaji wa watu wake kutoka kwenye utumwa na kifungo. Je, ni nani
Masihi na Mwokozi hasa? Kristo Yesu. Hivyo tukiweka maana zote hizi pamoja tunaona
kwamba uvunaji wenyewe unafanyika katika kikomo au kufungwa kwa kipindi cha
wakati ambacho Kristo anawahudumia watu wake. Pia tunaona kwamba mavuno kamili yanafanyika
baada ya kipindi cha wakati ambapo Kristo amemaliza kabisa kuwahudumia watu wake
milele. Mavuno katika vipindi vyote yanahusisha Kristo kuwaokoa na kuwafungua
toka kwenye utumwa na kifungo.
Je, tunaishi katika kipindi gani
cha wakati sasa? Tunaishi katika siku zilizotabiriwa za upatanisho.
Katika huduma ya patakatifu, siku
ya upatanisho ilikuwa huduma ya mwisho iliyoendeshwa na kuhani mkuu kwa ajili
ya watu wake. Hivyo leo tunaishi katika kipindi cha huduma ya Yesu kwa watu
wake au wakati wa Mavuno.
Je, kipindi hiki kilianza lini?
1844. Hivyo tangu 1844 tumekuwa katika wakati na mchakato wa mavuno. Hatua ya
kwanza ya mchakato wa mavuno ni kukata au kuvuna nafaka yenye matunda, kutenga
ngano na magugu, kuzikusanya katika matita na kuzifunga kwa kamba. Je, Ellen
White analiunga mkono hili? Ndiyo!
“Kisha nikaona malaika. Alisema
malaika anayeniongoza, ‘Kazi yake ni ya kutisha. Utume wake ni wa ajabu. Ni
malaika atakaye tenga ngano na magugu, na kutia muhuri, au kufunga ngano kwa ajili
ya ghala ya mbinguni. Mambo haya yanapaswa kutawala akili yote, fikra zote.” EW
p. 118
Hapa tunaona kuwa Malaika ndiye
anayetenga ngano na magugu, na kama tulivyoona hapo awali,hatutarajii kuwa
kitendo hiki ni cha kimwili, bali ni cha kiroho maana tuliona kuwa “….mbegu ni neno
la Mungu” Luka 8:11 na kwa hiyo mbegu chafu ni neno au mafundisho
ya shetani. Vyote vinapandwa katika shamba la Mungu, au katika Kanisa la Mungu.
Lakini pia tumeona kuwa mwenye shamba au Kristo anaporudi mara ya pili haji
kuvuna bali anakuja kuchukua ngano safi iliyovunwa tayari na malaika na kuipeleka
Mbinguni. Na kwa hiyo wale wanaoelewa kuwa mwisho wa dunia aliosema Yesu kwamba
mavuno yatafanyika inamaanisha siku atakayokuja Yesu mara ya pili wanaelewa
kimakosa fundisho hili kwa sababu mwisho wa dunia yanapofanyika
mavuno ni tofauti na siku ya
Bwana anayokuja Yesu kuchukua mavuno yaliyokwisha kuvunwa tayari ili ayapeleke
ghalani – yaani mbinguni.
Ni lini malaika wa tatu alianza
kufanya kazi hii kwa kutoa jumbe hizi zenye kweli za kujaribu? Mwaka 1844.
Hivyo tangu mwaka 1844 tumekuwa katika muda wa mchakato wa mavuno. Tangu octoba
22,1844 hadi mnamo 1846-47 Kweli hizi zenye kujaribu zilitolewa kwa watu wetu.
Mwaka 1844 unatokana na unabii wa Daniel 8:14 kuhusu siku 2300 za kiunabii sawa
na miaka 2300 halisi iliyoanza mwaka 456 KK na kuishia mwaka 1844 BK. Alama au
neno lingine ni MWISHO WA DUNIA.
Watu wengi wameelewa visivyo
maana ya ‘mwisho wa dunia’ wakidhani kuwa ni siku Yesu anaporudi mara ya pili.
“ …mavuno ni mwisho wa dunia;
na wale wavunao ni malaika” Math. 13:39
“Basi kama vile magugu
yakusanywavyo na kuchomwa motoni; ndivyo itakavyokuwa katika mwisho wa dunia...”
“Ndivyo itakavyokuwa katika mwisho wa dunia; malaika watatokea, watawatenga
waovu mbali na wenye haki na kuwatupa katika tanuru ya moto; ndiko kutakuwepo
kilio na kusaga meno” Math 13:40, 49,50
Je, mwisho wa dunia uliosemwa
hapa unamaanisha kurudi kwa Yesu mara ya pili? Hapana! Wengi wamekuwa
wakifikiri kuwa Yesu alimaanisha mwisho wa dunia kuwa ni siku ile atakaporudi,
ndio maanaYesu akifahamu kuwa watu watatafsiri tofauti mfano huu kama hawatasoma
kwa uangalifu na kwa uongozi wa Roho wake, alisisitiza mara baada ya kufafanua mfano
huu, akisema: “…mwenye masikio na asikie” Math. 13:43. Kama
tulivyoona hapo juu kuwa mavuno yanafanyika kwa hatua kadhaa kabla ya kupelekwa
ghalani na si mara moja kama itakavyokuwa ile siku ya Bwana atakapokuja Yesu
mara ya pili ambayo ni siku moja. Mwisho wa dunia unapotajwa
kwenye Biblia una maana ya tangu siku za mwisho wa dunia zianze, yaani
tangu mwaka 1844 hadi waovu
watakapoangamizwa pamoja na shetani na kuwa mwisho wa dhambi. Kwa hiyo, hivi
sasa tunaishi katika mwisho wa dunia au siku za mwisho wa dunia.
Tunasema hivyo kwa sababu
tunatambua kuwa waovu au magugu hayatachomwa siku Yesu atakaporudi duniani mara
ya pili. Siku Yesu atakaporudi anakuja kuchukua watu wake au ngano safi
na waovu watakufa na kukaa makaburini hata baada ya miaka elfu moja wakati
watakatifu na mji mtakatifu watakaposhuka, ndipo waovu watafufuliwa na kuchomwa
moto pamoja na shetani.Je, ungeulizwa uelezee kuhusu siku ya Sabato ungesemaje?
Ungesema “Sabato inaanza tangu kuzama kwa jua siku ya sita hadi kuzama kwa jua
siku ya saba”; kadhalika ndivyo mwisho wa dunia unavyoanza mwaka
1844 hadi shetani, malaika zake na waovu (magugu) watakapotupwa katika
tanuru iwakayo moto.
Je, Biblia inaiitaje siku ya kuja
Yesu mara ya pili? Siku Yesu anapokuja imetambulika katika Maandiko kama Siku
ya Bwana. na si mwisho wa dunia, [japo pia siku ya Bwana ni siku
ya Sabato: “Nalikuwa katika Roho, siku ya Bwana…” Ufun.1:10; kumbuka
kuwa neno moja kwenye Biblia laweza kuwa na maana mbili]; “Jua
litageuzwa kuwa giza, na mwezi kuwa damu,kabla haijaja hiyo siku ya Bwana iliyo
kuu na itishayo.” Yoeli 2:31. Hii ndiyo siku ya kuja kwa Yesu
mara ya pili anayoisema Yoeli ambayo ni tofauti na siku za mwisho wa dunia.
“Walakini habari ya siku ile
na saa ile hakuna aijuaye, hata malaika walio mbinguni, ila Baba”.Marko
13:32. Yesu akiwa hapa duniani anaitaja siku ya kuja kwake mara ya pili
kama “Siku” na wala hasemi “walakini habari ya ‘mwisho wa dunia’…”
maana siku za mwisho wa dunia zimefunuliwa kwetu ila siku ya kuja Yesu ndio
hatuijui.
Huoni faida ya kusoma mwenyewe
kwa uongozi wa Roho wa Mungu badala ya kutegemea wanadamu wakufundishe? Umeona
namna ambayo Yesu alimaanisha katika mfano huu?
JE, MWISHO WA
MAVUNO NI LINI KAMA YALIANZA TANGU MWAKA 1844?
“Ngano na magugu vinakuwa pamoja
hadi wakati wa mavuno; na mwisho wa mavuno ni kufungwa kipindi cha rehema” (au
mwisho wa mavuno ni kufungwa kwa mlango wa rehema) Christ Object
Lesson p. 72
Yohana yeye anaelezea mwisho wa
mavuno kwa kusema, “Mwenye kudhulumu na azidi kudhulumu; na mwenye uchafu na
azidi kuwa mchafu; na mwenye haki na azidi kufanya haki; na mtakatifu na azidi
kutakaswa”. Ufun. 22:11. likimaanisha kuwa malaika wameshamaliza
kazi ya kuvuna na mavuno yako tayri. Tangazo hilo litatolewa mara Kristo
atakapomaliza kazi ya upatanisho kule mbinguni. Mara baada ya maelezo hayo,
tangazo la kuja kwa Yesu linafuatia,
“Tazama, naja upesi, na ujira
wangu u pamoja nami, kumlipa kila mtu kama kazi ilivyo”.
Ufun 22:12. hapa Krsito
anakuja kuchukua mavuno na kuyapeleka kwa Baba mbinguni.
Ukweli ni kwamba, tangu mwaka
1844 mavuno yanaendelea, na mlango wa rehema
utakapofungwa ndio itakuwa mwisho
wa mavuno.
Kwa hiyo ndugu, kama ulifikiri
kuwa mwisho wa dunia ni siku Yesu anaporudi na ndio wakati wa kufanyika mavuno,
hivyo sivyo maana Mama White anatuambia kuwa mwisho wa mavuno ni wakati wa
kufungwa mlango wa rehema na tunatambua kuwa mlango wa rehema utafungwa kabla hata
ya kuja kwa Yesu mara ya pili; hivyo ina maana pia kuwa mavuno yanafanyika
kabla ya kurudi Yesu mara ya pili. Kwa hakika malaika wanaendelea kuvuna ngano
katika shamba la Bwana.
Kuna wanosema kuwa wafuasi wa
kweli wa Kristo wasitengwe na mifumo iliyoasi kwa kusema kuwa ngano na magugu
vinakuwa pamoja hadi wakati wa mavuno, hawajui kuwa kazi inayofanyika ni
mchakato wa mavuno, wanafikiri kuwa wokovu unapatikana kwa kujiita wakristoau
kujiita kwa jina fulani la kanisa; roho ya unabii inatuambia nini juu ya
wokovu?Mungu analitaka kanisa hili lifanye mabadiliko. Walikuwa na jina la
kudumishwa, lakini kazi zao hazikuwa na upendo wa Yesu. Ah, ni wangapi
wameanguka kwa kutegemea sifa zao kwa wokovu! Ni wangapi wamepotea kwa
kufanya juhudi za kuenzi jina. Kama kuna mtumwenye sifa ya kuwa
muinjilisti, mwenye mafanikio, Mhubiri mwenye karama, mwenye imani, mtu mwenye
kicho cha pekee, Kuna hatari ya wazi kwamba ataharibu imani atakapojaribiwa na majaribu
madogomadogo ambayo Mungu angependa yaje’’ – Ellen white – 7 BC, 958.
“Si kwa jina lake,
bali
kwa tunda lake thamani ya mti hutambulika. Kama tunda halifai, jina haliwezi
kuuokoa mti kwa uangamivu” DA, pg. 107
“Hatuokolewi kwa kundi:, Hakuna
jina la dhehebu lenye uwezo wa kutupatia upendeleo kwa Mungu. Tunaokolewa
mmoja mmoja kama waumini wa YESU Kristo.” – E.G.W. RH 02/ 1891 Ukweli
ni kwamba, Maandiko yanaelezea tatizo hili kama hivi: Kama unajisikia kujiita
mu SDA,fikiria ni nini unachokifanya. Jiulize swali hili: Ni nini
kinachomfanya mtu awe mu SDA wa kweli? Tazama jibu hapa chini.
Paulo asema: “Bali ni Myahudi
aliye myahudi kwa ndani; na tohara ni ya moyo, katika roho, si katika
andiko; ambaye sifa yake haitoki kwa mwanadamu, bali kwa Mungu”.
Warumi 2: 29, Nami nasema: “Bali ni Muadventista
msabato aliye muadventista msabato kwa ndani; na tohara ni ya
moyo, katika roho, si katika andiko; ambaye sifa yake haitoki kwa
mwanadamu, bali kwa Mungu”.
Ufafanuzi wa hatua mbili
zinazoitwa ‘mavuno’ katika mfano wa ngano na magugu ni huu: Kama tulivyoona
kwamba hatua ya kwanza inafanyikia ndani ya shamba, hii inamaanisha kwamba watu
wa Mungu wamekuwa wakivunwa ndani ya kanisa tangu mwaka 1844. Tuliona pia
kwamba hatua ya pili ya mavuno ilifanyika nje ya shamba ambapo ngano safi
huandaliwa kwa ajili ya kupepetwa na kuondoa makapi. Wakati huo huo magugu
hufungwa katika matita matita tayari kwa kuchomwa moto. Hii inamaanisha kwamba
wale waliojitenga kutoka kwenye kanisa potofu (shamba) wamechangamana na magugu
na huko ndipo panapofanyika hatua ya mwisho ya
kupepeta ngano na kuwekwa ghalani
wakati magugu yanafungwa pamoja ili kusubiri moto. Je, wale waliobaki ndani ya
kanisa (shamba) potofu ni akina nani? Hao ni miiba na sio ngano safi wala
magugu tena. Kumbuka mfano wa Yesu kuhusu mpanzi aliyepanda mbegu zingine zikaanguka
penye miiba na hazikuweza kuzaa matunda. Kwa ufupi, ngano na magugu (Wakristo safi
na Wakristo kwa jina) wamejitenga na kanisa potofu ikimaanisha hatua ya pili ya
mavuno wakati miiba (Wakristo wanaofanya dhambi za wazi na kumkufuru Roho
Mtakatifu) wanaendelea kubaki ndani ya kanisa asi na kamwe hawatazaa matunda
safi.
JE; UNATAKA
KUZAA MATUNDA YA SDA?, Yesu anasema “Kaeni ndani yangu, namindani
yenu.Kama vile tawi lisivyoweza kuzaa peke yake, lisipokaa ndani ya mzabibu;
kadhalika nanyi msipokaa ndani yangu”. Yohana 15:4.
Yesu hasemi tutafute kwanza
kanisa au dhehebu, ila anasema tukae ndani yake, naye
Atatuwezesha kuzaa matunda safi
ya SDA maana Yeye ndiye kanisa na kanisa sio mfumo wawatu. Ellen White
Acts of Apostles p. 11
“Hakuna kanisa jingine la Mungu
zaidi ya mkusanyiko wa wale walio na neno la Mungu, na ambao
wamesafishwa nalo” Sprit of Prophecy Vol. 4, p237.
“Wale wanaotunza Amri za Mungu,
wale wanaoishi si kwa mkate pekee, lakini kwa kila neon kutoka kwenye kinywa
cha Mungu, wanaunda kanisa la Mungu anayeishi”.
7BC 949 “Mungu analo
kanisa.Sio majengo makubwa, wala sio lililoundwa kitaifa, (au sio
mfumo ulioundwa kidunia) wala si madhehebu mbalimbali; ni watu
wanaompenda Mungu na kushika Amri zake, ‘wakutanapo wawili au watatu
kwa ajili ya jina Langu, nipo kati yao’ (Mat 18:20). Pale Kristo
anapokuwepo kati ya wachache wenye unyenyekevu, Hilo ni kanisa la Kristo, Kwa
maana uwepo wa Mtakatifu aliye Juu ambaye ana umilele ndio tu unaounda
kanisa lake” Ellen White: The Upward Look p 315. Je, ninahusikaje
na dhambi wanazozifanya viongozi wa kanisa langu wakiwa wanatekeleza majukumu
ya kanisa wakati mimi sizifanyi? Ninahusikaje na mafundisho ya uongo
yanayotolewa na viongozi wa kanisa langu kama mimi siyaamini
ingawa nimo ndani ya kanisa hilo au mfumo wa kanisa? Upo
uwajibikaji wa pamoja (collective responsibility) kutokana na dhambi
zinazofanywa na viongozi wa kanisa wakiwa wanatekeleza majukumu
ya kanisa. Kisa cha Akani ni kielelezo kizuri. Akani alifanya
dhambi yeye mwenyewe kama anavyosema ‘Kweli nimefanya dhambi juu ya
Bwana, Mungu wa Israeli’ Yosh. 7:20. Lakini Bwna alisema nini juu ya dhambi ya
Akani?
‘Israeli WAMEFANYA dhambi,
wamelivunja agano langu…. Kitu kilichowekwa wakfu kiko katikati yako Ee
Israeli; huwezi kusimama mbele ya adui zako hata mtakapokiondoa kitu
mlichonacho’.Yosh. 7:11-13. Kwa vile Akani alikuwa ni kiongozi wa kanisa na
alifanya dhambi akiwa katika kazi za kanisa, Mungu aliwahesabia hatia
washiriki wote wa kanisa na hata kusababisha vifo vya watu waliodhaniwa
kuwa hawakuwa na hatia!
Hivyo basi unapokuwa ndani ya
mfumo wa kanisa unaoliongoza kanisa katika makosa, wewe pia unashiriki makosa
hayo. Yesu alisema ‘Kipofu akimuongoza kipofu, wote wataangukia shimoni.’Tena
imeandikwa ‘Wawaongozao ndip wawapotoshao’ hivyo ‘watu wangu wanaangamizwa kwa kukosa
maarifa.’ Sasa nifanye nini Kama viongozi wangu wanafundisha uongo na kuufanya
kuwa msingi wa imani?
‘Tokeni kwake enyi watu
wangu, msishiriki dhambi zake (dhambi za kanisa), wala msipokee mapigo yake’.
Ufu. 18:4. Dawa ni kujitenga na mfumo mzima wa kanisa kwa lengo la kuokoa roho
yako!
Sambaza ujumbe huu kwa watu wengi
kadri uwezavyo!
Mungu akubariki unapoendelea
kutafakari neno lake!.
KWA MAWASILIANO ZAIDI WASILIANA NASI
0756959525,0752164685
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni