Katika blogu hii, tutachunguza njia mbalimbali za kuimarisha ufahamu wetu wa Biblia. Tutajadili mbinu za kusoma Biblia kwa ufanisi, vidokezo vya kukariri maandiko matakatifu, na mikakati ya kutumia somo la Biblia katika maisha yetu ya kila siku. Iwe wewe ni mtaalam wa Biblia mzoefu au unaanza tu safari yako ya imani, "Jifunze Biblia Zaidi" ni rasilimali kamili ya kukusaidia kuongeza ufahamu wako wa Maandiko Matakatifu na kumkaribia Mungu zaidi.

KUSIMAMA AU KUKAA WAKATI WA KUOMBA NI KINYUME NA MPANGO WA MUNGU.

KUSIMAMA AU KUKAA WAKATI WA KUOMBA NI KINYUME NA MPANGO WA MUNGU.
UTANGULIZI:
Namshikuru mungu kunipatia nafasi hii ya kuandaa nakala hii.ndugu msomaji unayetoa au kutenga muda kwa kusoma nakala hii Mungu akujalie na akupe hekima na maarifa ya kumjua yeye na kuenenda  kwa kufuata neno lake kama lisemavyo  nawe utapata uzima wa milele usikubali kudanganywa na walimu wa uwongo na kufuata mapokeo ya wanadamu. Makanisa mengi ulimwenguni yamekwenda kinyume na mpango wa Mungu. Hekima na kicho kimetoweka makanisani. Makanisamengi wanaomba wakiwa wamesimama au wamekaa.Hata na kanisa la sabato,soma Biblia na Roho ya unabii uone kile Mungu  anachosema kuhusu maombi ,pia katika nakala hii tutaona na baadhi ya mapokeo yaliyoingia ndani ya kanisa la wasabato yaliyo kinyume na  la Mungu,Bima ya maisha,Idara ya wanawake na kuomba wakiwa wamesimama au wamekukaa.
KUOMBA
“Njooni tuabudu,tusujudu,tupige magoti mbele za BWANA aliyetuumba”  ZABURI 95:6
“Kwa nafasi yangu nimeapa neno hili limetoka kinywani mwangu katika haki, wala halitarudi ya kwamba mbele zangu kila goti litapigwa,kila ulimi utaapa”ISAYA 45:23
Katika jambo hili Mungu ametoa msimamo kwa kila mwanadamu anavyopaswa kuja mbele zake.Mfalme Daudi anatumia neno “Njooni tuabudu,tupige magoti mbele za BWANA” alielewa kuwa Mungu anapaswa kuabudiwa kwa unyenyekevu.Maana ndio msimamo wa wacha Mungu.Isaya naya anasema kilekile sawa na daudi. Neno kupiga magoti ni agizo la Mungu , maana amesema kila goti litapigwa mbele zangu na kwenda kinyume na mpango huo ni makosa  au uasi.
Kielelezo hiki cha kupiga magoti, kiliendelezwa na watakatifu  kizazi hadi kizazi  Mtume Paulo anasema “kumbukeni wale waliowaongoza kwa neno la Mungu tena kwa kuchunguza sana  mwisho wa  mwenendo wao waigeni imani yao”.WAEBRANIA 13:7.
Tuone mifano  michache ya watakatifu namna walivyo mwomba Mungu.Mtume Paulo anasema
            “Kwa hiyo  tena  Mungu alimwadhimisha mno,akamkilimia jina lipitalo kila jina,ili kwa jina la yesu kila goti lipigwe na vitu vya mbinguni , na vya  duniani na chini ya nchi;na kila ulimi ukiri ya kuwa YESU KRISTO NI BWANA, kwa utukufu wa Mungu Baba”WAFILIPI 2:9-11.
            “YESU ambaye ni jiwe kuu la pembeni  Efeso 2;20 akapiga magoti akaomba”LUKA 22:41
NABII DANIEL “Alipiga magoti mara tatu kila siku akisali,akimshukuru mbele za Mungu wake”
                           DANIEL 6:10    
EZRA KUHANI “Na wakati wa sadaka ya jioni,nikainuka baada ya kunyenyekea kwangu nguo yangu na joho yangu imeraruliwa,nikaanguka magoti nikiinia juu mikono yangu mbele za BWANA  Mungu Wangu”
MTUME PAULO “Alipokwisha kunena haya akipiga magoti, akaomba pamoja nao wote. MATENDO 20:36, 21:5.
MTUME PETRO: “Petro akawatoa nje wote,akipiga magoti akiomba “
STEFANO:”Akapiga magoti ,akalia kwa sauti kuu” MATENDO 7:60
“Tukisali katika chumba chetu au kanisani inatulazimu kupiga magoti mbele za mungu  popote tuombapo ni haki kupiga magoti”MANABII NA WAFALME UK 21
Ndugu msomaji , linganisha  jinsi watu wa mungu walivyofanya na ujiulize kile kinacho fanywa na makanisa ya leo na hata  wewe mwenyewe.swali , wanao omba hali wamesimama au kukaa, agizo hilo walilitoa wapi? Jibu ni kwamba kuomba watu wakiwa wamesimama waliridhi desturi ya mafalisayo wapinzani wa yesu .MATHAYO 6:5-23:1-30, LUKA 18:9-12. Nanyi mwaicha amri ya Mungu na kuyashika maagizo ya wanadamu.MATHAYO 15:6-12, MARKO 7:6-9.
Mpendwa msomaji Mungu akusaidie,kufanya mabadiliko katika jambo hili usiendelee kufanya kinyume na mpango wa mungu.Na kama utaendelea kuomba umesimama au umekaa ,utambue kuwa huna sehemu yoyote miongoni mwa wacha Mungu.

KWA MAWASILIANO ZAIDI WASILIANA NASI
0756959525,0752164685
Share:

Popular Posts

Lebo

Recent Posts

Pages