Katika blogu hii, tutachunguza njia mbalimbali za kuimarisha ufahamu wetu wa Biblia. Tutajadili mbinu za kusoma Biblia kwa ufanisi, vidokezo vya kukariri maandiko matakatifu, na mikakati ya kutumia somo la Biblia katika maisha yetu ya kila siku. Iwe wewe ni mtaalam wa Biblia mzoefu au unaanza tu safari yako ya imani, "Jifunze Biblia Zaidi" ni rasilimali kamili ya kukusaidia kuongeza ufahamu wako wa Maandiko Matakatifu na kumkaribia Mungu zaidi.

MIUJIZA, MANABII WA UONGO



 MIUJIZA
Katika somo hili tutajifunza mambo yafuatayo:
1.   Manabii wa uongo
2.   Njia ya kumfahamu nabii wa kweli na nabii wa uongo
3.   Kiapo cha shetani
4.   Je shetani, ama watumishi wa shetani, wanaouwezo wa kufufua?
5.   Uchawi wa zamani na uchawi wa kisasa
6.   Je, uko nyuma shetani aliwahi kufanya miujiza?
7.   Ni jinsi manabii wa uongo wanavyotafuta hela
8.   Tutajifunza ibada za manabiii wauongo jinsi wananvyoomba
9.   Je, wacha MUNGU wanaombaje?
10.  Miujiza ya uongo ni ubunifu kutoka taifa gani na toka makanisa gani?
11.  Ni roho za mashetani
12.  Jambo la mwisho tutakalo jifunza. Je, waatumishi wa MUNGU waaminifu leo wanaweza kufanya kazi kwa njia ya miujiza?
Katika ulimwengu wa Kikristo wa siku hizi za mwisho tunashuhudia matangazo makubwaya miujiza, tunasikia na kuona kwenye vyombo vya habari mahubiri ya uponyaji, mahubiri ya utajirisho; mara utasikia matangazo kwenye redio au kwenye television au gari mtaani au vipeperushi;
1.   Viwete watatembea
2.   Matumbo yaliyofungwa yatafunguliwa
3.   Utapandishwa cheo kazini
4.   Njoo uponywe
5.   Njoo utajirike
Je, haya yote yanayofanyika sasa ni kweli? Hebu fungua moyo wako Roho wa MUNGU azungumze na wewe na sasa ukweli halisi unaomkononi. Somo hili hakikisha usilipoteze maana ni ufunguo wa kukutoa gizani bali zalisha uwagawie na wengine.
          Mpenzi wangu msomaji miujiza ya uongo ni miongoni mwa dalili za kurudi kwa Yesu. Hebu sikiliza Yesu mwenyewe alivyosema;

1.   MANABII WA UONGO
“Kwa maana watatokea makristo wa uongo na manabii wa uongo nao watatoa ishara kubwa na maajabu (miujiza) wapate kuwapoteza kama yamkini hata walio wateule”MATHAYO 24:24.
Umesikia ndugu msomaji kutokea kwa makristo wa uongo, manabii wa uongo, wanaofanya miujiza na maajabu; ni lengo la shetani kuwatumia hawa ili kuwapoteza hata walio wateule. Je, watapoteaje?  Wataamini uongo sababu ya ishara, sababu ya miujiza.Jambo hili limeshatimia katika siku zetu. Leo tunashuhudia watu wanaojiita wenyewe kuwa ni manabii na mitume, wenye majina ambayo hatuyasomi katika maandiko.  Hayamo, mfano:
1.   Mungu wa bendera
2.   Mungu wa upako
3.   Mungu wa epafa
4.   Mungu wa ngurumo
5.   Mungu wa yawe
6.   Baba Godi – yaani yeye ni baba yake na Mungu.Maajabu kabisa. Ni kwambie ndugu msomaji haya ni majina yanayotukuza miungu siyo MUNGUmuumbaji.
MUNGU anao manabii na mitume. Na manabii na mitume wa MUNGU hatuko nao kimwili maana walikwisha toweka.Ila tunao kupitia maandishi yao, lakini shetani anamanabii na mitume ambao wanaonekana na wanaofanya ishara.
JE, MANABII WA UONGO NI NINI?
“Jiadharini na manabii wa uongo watu wanaowajia wamevaa mavazi ya kondoo walakini kwa ndani ni umbwa mwitu wakali.Mtawatambua kwa matunda yao” MATHAYO 7:15
          AH – manabii wa uongo ni watu.Je, kuja wamevaa mavazi ya kondoo maana yake ni nini? Wanakuja wakijifanya kuamini ukristo; kuamini Biblia,ila kwa ndani ni mbwa mwitu na si mbwa mwitu tu, bali mbwa mwitu wakali. Andiko hilo mwishoni linamaliza kwa kusema kuwa mtawatambua kwa matunda yao.
 

                                 Mpendwa msomaji endelea kufuatilia makala hii na Mungu akubariki AMINAAA!!!!!!
                               ITAENDELEA.

 KWA MAWASILIANO ZAIDI WASILIANA NASI

0756959525,0752164685 
Share:

Popular Posts

Lebo

Recent Posts

Pages