MIUJIZA
Katika somo hili
tutajifunza mambo yafuatayo:
1.
Manabii
wa uongo
2.
Njia
ya kumfahamu nabii wa kweli na nabii wa uongo
3.
Kiapo
cha shetani
4.
Je
shetani, ama watumishi wa shetani, wanaouwezo wa kufufua?
5.
Uchawi
wa zamani na uchawi wa kisasa
6.
Je,
uko nyuma shetani aliwahi kufanya miujiza?
7.
Ni
jinsi manabii wa uongo wanavyotafuta hela
8.
Tutajifunza
ibada za manabiii wauongo jinsi wananvyoomba
9.
Je,
wacha MUNGU wanaombaje?
10. Miujiza ya uongo ni ubunifu kutoka
taifa gani na toka makanisa gani?
11. Ni roho za mashetani
12. Jambo la mwisho tutakalo jifunza. Je,
waatumishi wa MUNGU waaminifu leo wanaweza kufanya kazi kwa njia ya miujiza?
Katika ulimwengu wa Kikristo wa siku hizi za
mwisho tunashuhudia matangazo makubwaya miujiza, tunasikia na kuona kwenye
vyombo vya habari mahubiri ya uponyaji, mahubiri ya utajirisho; mara utasikia matangazo
kwenye redio au kwenye television au gari mtaani au vipeperushi;
1.
Viwete
watatembea
2.
Matumbo
yaliyofungwa yatafunguliwa
3.
Utapandishwa
cheo kazini
4.
Njoo
uponywe
5.
Njoo
utajirike
Je, haya yote yanayofanyika sasa ni kweli?
Hebu fungua moyo wako Roho wa MUNGU azungumze na wewe na sasa ukweli halisi
unaomkononi. Somo hili hakikisha usilipoteze maana ni ufunguo wa kukutoa gizani
bali zalisha uwagawie na wengine.
Mpenzi wangu msomaji miujiza ya uongo
ni miongoni mwa dalili za kurudi kwa Yesu. Hebu sikiliza Yesu mwenyewe
alivyosema;
1.
MANABII
WA UONGO
“Kwa maana watatokea makristo wa uongo na
manabii wa uongo nao watatoa ishara kubwa na maajabu (miujiza) wapate kuwapoteza kama yamkini hata walio wateule”MATHAYO 24:24.
Umesikia ndugu msomaji
kutokea kwa makristo wa uongo, manabii wa uongo, wanaofanya miujiza na maajabu;
ni lengo la shetani kuwatumia hawa ili kuwapoteza hata walio wateule. Je,
watapoteaje? Wataamini uongo sababu ya
ishara, sababu ya miujiza.Jambo hili limeshatimia katika siku zetu. Leo
tunashuhudia watu wanaojiita wenyewe kuwa ni manabii na mitume, wenye majina
ambayo hatuyasomi katika maandiko.
Hayamo, mfano:
1.
Mungu
wa bendera
2.
Mungu
wa upako
3.
Mungu
wa epafa
4.
Mungu
wa ngurumo
5.
Mungu
wa yawe
6.
Baba
Godi – yaani yeye ni baba yake na Mungu.Maajabu kabisa. Ni kwambie ndugu
msomaji haya ni majina yanayotukuza miungu siyo MUNGUmuumbaji.
MUNGU
anao manabii na mitume. Na manabii na mitume wa MUNGU hatuko nao kimwili maana
walikwisha toweka.Ila tunao kupitia maandishi yao, lakini shetani anamanabii na
mitume ambao wanaonekana na wanaofanya ishara.
JE, MANABII WA UONGO NI
NINI?
“Jiadharini
na manabii wa uongo watu wanaowajia wamevaa mavazi ya kondoo walakini kwa ndani
ni umbwa mwitu wakali.Mtawatambua kwa matunda yao” MATHAYO 7:15
AH
– manabii wa uongo ni watu.Je, kuja wamevaa mavazi ya kondoo maana yake ni nini?
Wanakuja wakijifanya kuamini ukristo; kuamini Biblia,ila kwa ndani ni mbwa mwitu
na si mbwa mwitu tu, bali mbwa mwitu wakali. Andiko hilo mwishoni linamaliza
kwa kusema kuwa mtawatambua kwa matunda yao.
Mpendwa msomaji endelea kufuatilia makala hii na Mungu akubariki AMINAAA!!!!!!
ITAENDELEA.
KWA MAWASILIANO ZAIDI WASILIANA NASI
0756959525,0752164685