1. IFUATAYO
NDIYO NJIA YA KUMTAMBUA NABII WA KWELI NA NABII WA UONGO.
SOMO:MIUJIZA INAENDELEA................................
Na katika hili twajua ya kuwa tumemjua yeye
ikiwa tunashika amri zake. Yeye asemaye, nimemjua, wala hazishiki amri zake, ni
muongo, wala kweli haimo ndani yake” 1YOHANA
2:3-4
“kwa
maana watu hawa ni watu waasi, watoto wasemao uongo, watoto wasiotaka kuisikia
sheria ya BWANA”ISAYA 30: 9
Kipimo
cha kumtambua nabii wa kweli na nabii wa uongo kiko katika Biblia yenyewe,
usiulize mchungaji wako, usiulize wazazi wako, wala mke au mume wako,usiulize
mwanao.Na kipimo hicho ni ikiwa anazishika amri. Na kama anadai kumjua MUNGU na
huku hazishiki amri ndiye nabii wa uongo;wala kweli (neno la Mungu) halimo
ndani yake (Yohana17:17) Kwa maana wasio taka kuitii sheria ya MUNGU ni waasi,
na wanamafundisho ya uongo. Hata maombi yao ni udanganyifu tu maana MUNGU
ameangiza ifuatavyo juu ya maombi;
“Na
lolote tuombalo tutalipokea kwake, kwakuwa twazishika amri zake; na kuyatenda yapendezayo
machoni pake”1YOHANA 3:22
Mpenzi msomaji ili kumjua nabii wa
uongo Biblia hapa inachofundisha ni kuwa wanakataa amri kumi za MUNGU.Na mojawapo
ya amri kumi ni amri ya nne, yaani amri ya sabato, na huo ndio mpango wa
shetani leo kuwafanya watu wawe wanasali lakini wanavunja amri angalau moja tu,
basi huwa makusudi yake yametimia.Maana katika hesabu ya mbinguni amri kumi ukitoa
amri moja jawabu ni sifuri.Divyo neno la MUNGU linavyotufundisha katika kitabu
cha Yakobo;Neno linasema;
“Maana
mtu awaye yote atakayeshika sheria yote, ila akajikwaa katika neno moja (amri
moja) amekosa juu ya yote. Kwa maana yeye aliyesema, usizini, pia alisema,
usiue. Basi ijapokuwa hukuzini, lakini umeua, umekuwa mvunja sheria”YAKOBO 2;10-11
Hiki ndicho kipimo
1. Nabiiwa kweli
anashika amri kumi
2. Nabii wa uongo
anakataa amri kumi
Uchaguzi ni wako utaenda wapi? MUNGU anawatumishi
wanashika amri.
Shetani
naye anawatumishi hawataki amri, ila wanafanya miujiza, na wakiwa na majina
makubwa makubwa.Mara utasikia matangazo huyu anayekuja ni nabii na mtume. Lakini
wao wenyewe hawakubaliani, kila mtu anakanisa lake.Kwanini hawapatani, kwanini
hawakubaliani, wakati mitume na manabii wa MUNGU hawakupingana?Kupitia manabii
hawa injili makanisani imebadilika;
·
Kila kanisa njoo
uponywe
·
Kilakanisa njoo
utajirike
·
Kila kanisa njoo
upandishwe cheo
·
Kila
kanisa njoo upate mchumba
Manabii
wa uongo wanaibada,wanasali, wanamakanisa na wangeitumia biblia, na wengetumia
jina la Yesu.Lakini wakiwa na lengo la kupoteza hata wateule.
“Umizimu
sasa unababdilisha mfumo wake, ukiwa umeficha baadhi ya sehemu zake muhimu
zinazochukiza, sasa umejivika vazi la Kikristo …. Wakati zamani ulimkana Kristo
na Biblia, sasa unakiri kukubali vyote viwili” (Biblia na Ukristo) E.G White – Dhiki kuu uk,61:1
3.
KIAPO
CHA SHETANI
“Nawe
ulisema moyoni mwako, nitapanda mpaka mbinguni, nitakiinua kiti changu juu
kuliko nyota za MUNGU; nami nitaketi juu ya mlima wa mkutano, katika pande za
mwisho za kaskazini.Nitapaa kupita vimo vya mawingu, nitafanana na yeye aliye
juu. Lakini utashushwa mpaka kuzimu; mpaka pande za mwisho za shimo. Wao
wakuonao watakukazia macho, watakuangalia sana, wakisema je! huyu ndiye
aliyeitetemesha dunia, huyu ndiye aliyetikisa falme; aliyeufanya ulimwengu
ukiwa akaipindua miji yake; asiyewafungua wafungwa wake waende kwao?”ISAYA 14;13
Hiki ndicho kiapo cha
shetani; ingawa na angamizo lake linatajwa hapo hapo. Aliapa kuwa angefanana na
yeye aliye juu.
1.
Aliye
juu anakanisa – shetani naye ana makanisa
2.
Aliye
juu anaabudiwa – shetani naye anaabudiwa
3.
Aliye
juu anamanabii – shetani naye ana manabii
4.
Aliye
juu ana mitume – shetani naye ana mitume
Ila cha ajabu watumishi wa
shetani wangefanyaibada, miujiza, siyo kwa jina la shetani, bali kwa jina Yesu;
ndipo ulimwengu ungewapokea na kuwaamini. Ndugu msomaji katika jambo hili
umepona?
“Watu wangu wamekuwa kondoo waliopotea,
wachungaji wao wamewapoteza; wamewapotosha milimani;(makanisani) wamekwenda
toka mlima hata mlima (kanisa hadi kanisa)wamesahau mahali pao pa kupumzika”. YEREMIA 50: 6
Mpaka leo ni watu wengi
wanaohama kanisa hadi kanisa wakitafuta miujiza, wengine wakitafuta ukweli;
sababu ya kukoseshwa na wachungaji. Na watu wamesahau mahali pao pa kuabudu
yaani kwa wanao shika amri.
“Na ishara hizi zitafuatana na hao waaminio;
kwa jina langu watatoa pepo; watasema kwa lugha mpya;watashika nyoka; hata
wakinywa kitu cha kufisha, hakitawadhuru kabisa; wataweka mikono yao juu wagonjwa,
nao watapata afya”MARKO 16:17
Shetani akalidaka hilo maana aliazimu
kufanana na yeye aliye juu. Swali,je, watumishi wa shetani wanao uwezo wa
kufanya miujiza? Ndio; mtumishi wa Mungu Paulo anajibu swali hili;
“Maana watu kama hao ni mitume wa uongo,
watendao kazi kwa hila, wanaojigeuza wawe mfano wa mitume wa Kristo.Wala si
ajabu.Maana shetani mwenyewe hujigeuza awe mfano wa malaika wa nuru.Basi si
neno kubwa watumishi wake nao wakijigeuza wawe mfano wa watumushi wa haki ambao
mwisho wao utakuwa sawasawana kazi zao’’2
KORINTHO 11;13-15.