Mungu amekusudia kuwaamsha watu wake, ili
waone hali yao ya kiroho, Ujumbe huu unamhusu kila mtu ndani ya kanisa. Mtu au watu watakao ukubali ushuhuda huu wa
shahidi Mwaminifu watatakaswa kwa ile kweli na watakuwa tayari kusimama peke
yao na kuutangaza ukweli bila kuupindisha. “Niliuliza maana ya mpepeto
niliokuwa nimeuona na nikaonyweshwa kuwa umesababishwa na ushuhuda yakinifu
(wazi usiopinda) wa shahidi Mwaminifu kwa walaodiakia.Huu utakuwa na mvutano
kwa yule aupokeae, na utamuongoza kuinua kiwango chake cha kusambaza ukweli bila kuupindisha .
Wengine hawatakuwa tayari kuusambaza ushuhuda huu watainuka kinyume chake na
jambo hili litasabisha mpepeto. MATUKIO
SURA 12 UK 162”
Wengine hawatakuwa tayari kuupokea ushuhuda huu
wa shahidi Mwaminifu watachukua Msimamo wao kinyume na
ushuhuda huu kwa kuukataa na kuupinga, huku wakiendelea kushikilia nadharia na
mapokeo ya watu, Migawawanyiko itatokea kanisani. Makundi mawili yatatokea.
Wakati wa hatari kuu upo mbele yetu. Kila mmoja anayejua kweli angeamka, na
kuweka mwili wake, Mawazo, Moyo na roho chini ya uongozi wa MUNGU. Adui yukatika
njia yetu, Yatupasa tukeshe tukimpinga. Yatupasa tuvae silaha zote za Mungu.
Yatupasa tufuate maagizo tuliopewa kwa njia ya Roho ya unabii. Yatupasa tumtii
na kuupenda ukweli wa wakati huu. Kwa njia hii tutaokolewa katika kuupokea
udanganyifu ambao MUNGU amezungungumza nasi kwa njia ya Maonyo kwa kanisa, na
kwanjia ya vitabu ambavyo vilisaidia kuufanya wazi wajibu wetu wa sasa na hali
ambayo tungekuwa nayo. Onyo ambalo limetolewa Mstari kwa Mstari, amri kwa amri
lingefuatwa, tusipojali, tutatoa udhuru gani? 8T UK 298, 2K/NJIA SURA 8 UK 51.
“Nilionyeshwa kuwa ushuhuda kwa walaodikia unafaa kwa watu wa MUNGU
katika wakati huu… umeazimiwa kuamusha watu wa MUNGU, kuwafunulia kuasi kwao,
na kuwaongoza katika bidii ya toba ili wapate kibali kwa kuwamo kwa Yesu, na
kufaa kuutangaza ujumbe wa Malaika watatu” 1T UK 186 UFUNUO 3:17-19.
Kwa namna ya pekee Waadventista Wasabato
wamewekwa ulimwenguni kama walinzi na wachukua nuru kwao limekabidhiwa onyo la
mwisho kwa ulimwengu unao potea. Juu yao inag’aa nuru ya ajabu kutoka katika
Neno la MUNGU. Wamepewa kazi muhimu na nzito sana utangazaji wa jumbe za
malaika wa kwanza, wapili, na watatu. Hakuna kazi nyingine yenye umuhimu mkubwa
kama hiyo. Hawapaswi kuruhusu jambo lingine lolote kuingilia kati kuwatenga na
jukumu hili. 9T UK 19(1909) MATUKIO YA
SIKU ZA MWISHO SURA YA 4 UK 41 P.3
Shetani anajitahidi kwa nguvu zake zote,
kuwatenga watu wa Mungu na wajibu wao wa kutangaza ujumbe wa Malaika watatu.
Kwa kutumia viongozi wa kanisa wasiojitakasa kwa kutii ile kweli wanaingiza nadharia
na mafundisho ya uongo ndani ya kanisa, kwa njia hiyo kanisa litachafuliwa na
kunajisiwa.
“Wakati
upepetaji utakapoanza kwa uingizwaji wa nadharia za uongo, hawa wasomaji wa juu
juu, ambao hawakuweka nanga mahali popote (Maandiko Matakatifu) wako kama
mchanga upeperushwao huko na huko. Wanateleza kuingia katika nafasi yeyote ili
kuupendeza mwenendo wa hisia zao. MATUKIO UK 162 p.2 SURA YA 12,” “Adui
ataingiza nadharia za uongo kama vile kuwa huduma za Yesu. Katika patakatifu
hili ni moja wapo ya mafundisho ambayo yatasababisha wengi kujitenga na Imani.
MATUKIO SURA 12 UK 63 p.4, EV 224(1905)”
“Wakiwa hawakuupokea upendo wa ukweli,
watachukuliwa katika madanganyifu ya adui, watasikiliza roho zidanganyazo na
mafundisho ya mashetani na watajitenga na Imani MATUKIO SURA 12 UK 163 p.3, 6T 401(1900)” YEREMIA 17:12-13.
“Wengi watasimama katika Mimbari zetu
wakiwa wamenyanyua Mienge ya unabii wa uongo mikononi mwao, iliyowashwa kutoka
kwenye Mwenge wa shetani ambao ni Mwenge wa jehanamu MATUKIO SURA YA 12 UK 165 p.4, TM UK 409,411(1898)”.
“Adui amedhamilia kuingiza dhana za
uongo ndani ya kanisa la Waadventista Wasabato. Mabadiliko makubwa yatafanyika
itakuwa ni pamoja na kuachana na misingi ya Imani yetu, iliyosimama kama nguzo
ya kanisa, uasi huu utapelekea kanisa kupangwa upya. Matengenezo haya ya bandia
yatakapoanza yataleta matokeo gani? Kanuni za ukweli ambazo MUNGU kwa hekima
yake alizitoa kwa kanisa la masalio zitatupwa chini, dini yetu itabadilika. 1SM UK 204 p.2. ”
Mambo mbalimbali ambayo yamepelekea kanisa
la Waadventista Wasabato kupangwa upya ni kuingizwa kwa mafundisho ya
kikatoliki na sera za ulimwengu ambazo ni;
IDARA YA WANA WA KIKE NA HUDUMA
MIMBARINI
Haki sawa ni sera ya kiulimwengu
iliyojajadiliwa mnamo Mwaka 1995 Beijing China na Getruda Mongela aliyekuwa
katibu wa mkutano huo Mkuu wa nne (4) ulimwenguni juu ya habari za Wanawake.
Fouth World Conference on Women Beijing China 1995-UNITED NATIONS (4-15
September 1995 Beijing China)
Baada ya hapo harakati za kuwainua
wanawake kuwa na nafasi za madaraka sawa na wanaume zilianza katika mataifa na
makanisa. Na shetani kwa sasa amefaulu katika jambo hili maana ulimwengu
umekwisha piga hatua na kuiweka siku maalumu katika juma la kwanza la Mwezi watatu
kwa kila Mwaka, katika juma hilo Serikali zote na makinisa yote husheerekea
likiwemo na kanisa la SDA-GC, wao wamejificha wakiita huduma za wana wa kike,
na sabato ya juma hilo huitwa Sabato ya Wanawake Ulimwenguni na wanawake huhubiri
Mimbarini.
Idara hii imetoka ulimwenguni na huenzi
Miungu ya kike ya kipagani ambayo wao walikuwa wakiifukizia uvumba Miungu hiyo
ya kike. Haki za wana wa kike kanisani zimekuja na sera ya kuhubiri kwenye
Mimbari mbele ya wanaume kinyume kabisa na neno la MUNGU. Kama ilivyokuwa siku
za Makuhani leo wanaume wanaagizwa na neno la MUNGU”Nataka wanaume wasalishe kila mahali… Wanawake na wajifunze kwa utulivu
wakitii kwa kila namna, simpi ruhusa Mwanamke kufundisha wala kumtawala
Mwanaume” 1T:2:8:11, 12. Tunapoona wanahubiri na kushika nafasi za utawala ni
uasi sawa ni ule uliofanywa na Wanawake wa yuda waliofukizia uvumba Miungu ya
kike. “YEREMIA 44:15-30”
Shetani kupitia wanawake aliingiza
ibada ya kufukiza uvumba kwa Miungu Mingine yaani Malkia wa Mbinguni (Mungu
Mke). Katika historia ya Biblia huduma za hekaluni ziliendeshwa na Makuhani
waliochaguliwa na MUNGU nao walikuwa ni wanaume M/Walawi 7:35, 8:12, 21:10, Kutoka 40:13-15. siku zetu leo tunaona
wanawake wakifanya yaleyale yaliofanywa na wale wanawake wa zamani katika yuda.
Kitendo tu cha kufukiza uvumba kilikuwa ni kinyume na maagizo ya MUNGU, na
hakuna sehemu yeyote katika Biblia iliyomruhusu Mwanamke kufundisha au kutoa
huduma Mimbarini.
“Nilionyeshwa kwamba roho ya
ulimwengu kwa kasi inatia chachu kanisa. Mnafuata njia ile ile waliyoifuata
Israeli ya kale. Kuna kuanguka kule kule kwa Mwito wenu Mtakatifu kama watu wa
pekee wa MUNGU. Mwashikamana na Matunda ya kazi zisizofaa za giza. Makubaliano
yenu ya kuungana kidini na wasio amini yameleta hasira ya Bwana. Huyajui mambo
ya Amani yako na kwa haraka yamefichwa usiyaone. Maneno yale yale yalitumiwa
kuwaonya Israel iliyoanguka, kukataa kwako kuifuata nuru kutakuweka katika
nafasi mbaya Zaidi kuliko Wayahudi “5T PAGE 75-76 (75 p.3)”.
“Kama Israeli ya kale kanisa
limemdharau MUNGU wake kwa kuondoka kwenye nuru likiacha wajibu wake likitumia
vibaya upendeleo wake Mkuu kwa kuwa wapekee na safi kwa tabia. Washiriki wake
wamevunja Agano la kuishi kwa ajili ya mungu na kwa yeye tu. Wameungana na
wabinafsi wanaopenda dunia, kiburi, wanaopenda anasa na vimendelezwa, na KRISTO
AMEONDOKA. Roho wake amezimwa katika kanisa.Shetani anafanya kazi bega kwa bega
na wakristo wanaokiri Imani lakini ni Maskini wa utambuzi wa kiroho kiasi
kwamba hawamgundui” 2T UK 441-442. (441
p.3)
A.
MWANAMKE KUFUNDISHA KANISA
1TIMOTHEO
2:11, 12, 1KORITHO 11:31-35. “Watu wengi hujiona kuwa hawafai eti kwasababu
hawana kazi Maalumu kanisani, kwamba hawana kazi inayoonekana wazi ya kuendesha
Injili… Mama anaye walea watoto wake na kuwafundisha ukweli, MUNGU humuhesabu
kuwa Muhubiri Mkuu kama vile Mchungaji anaye hubiri Mimbarini. MANABII NA WAFALME UK 124 P.2 SURA YA 17, PROPHET AND KING (PK) UK 119 P.1
Yampasa Mwanamke kushika Madaraka
ambayo MUNGU alimwekea tangu zamani sawa na yale ya Mumewe. Ulimwengu unahitaji
hakina Mama ambao ni Mama siyo kwa jina tu, bali kwa kweli kama ilivyo maana ya
neno lenyewe. Twaweza kusema kuwa kazi zimuhusuzo Mwanamke ni Takatifu Zaidi ya
zile za Mwanaume. Basi Mwanamke na afahamu uwakifu wa kazi yake na kwa nguvu na
Kicho cha Mungu ashike kazi yake ya Maisha. Hebu awafundishe watoto kwa ajili
ya manufaa katika ulimwengu huu na kwaajili ya makao katika ule ulimwengu bora
Zaidi… Yampasa kuona kuwa anahaki sawa na Mumewe kusimama karibu naye, akiwa
Mwaminifu kwa kazi na wajibu umpasao. Kazi yake katika mafundisho ya watoto wake
ni yenye kukuza hali kwa kila jambo na yenye kuadilisha sawa na kazi iwayo
yeyote awezayo kufanyia Mumewe… Malaika asingeweza kuomba kazi ya cheo kikubwa
Zaidi ya hiyo maana kwa kufanya kazi hii (Mama) humtumikia MUNGU. 1k/NJIA UK 163 p.2, 3, 4.
Kama watu walio-oa wanakwenda kazini,
wakawaacha wake zao kuwatunza watoto nyumbani, Mke na Mama anafanya kazi kamili
na kubwa anayoifanya Mume na Baba. Ingawa mmoja yupo katika shamba la
umishonari, mwingine ni mishonari wa nyumbani ambaye kujali kwake, shauku na
mizigo yake mara kwa mara huzidi ile ya Mume na baba. kazi yake ni kubwa na
muhimu, kutengeneza tabia za watoto wake kuwafundisha wawe watumishi hapa, na
kuwafanya wafae wakati ujao kuwa na maisha milele. Mume akiwa katika shamba la
umishonari linaloonekana anaweza kupata heshima ya watu wakati anayeangaika
akiwa nyumbani anaweza asipate sifa yeyote ya kidunia katika kazi. Lakini kama
atafanya kazi yake kwa ajili ya mafanikio ya Familia yake, akitafuta
kutengeneza tabia zao kwa mfano wa mbinguni Malaika anayetunza kumbukumbu
huandika jina lake kama mmoja wa wamishonari wa kuu katika ulimwengu. Mungu
atazami vitu kama Mwanadamu mwenye kikomo cha kuona vitu. HUDUMA YA KIKRISTO UK 175 p.1 SURA 21, 5T UK 594, 1K/NJIA UK 165 p.5
B.MWANAMKE KUWA SHEMASI, MZEE WA
KANISA (MCHUNGAJI)
1TIMOTHEO 3:12-13, 3:1-7, TITO 1:5. “Uangalifu
katika kuchagua viongozi wa kanisa hebu Bwana awaangazie nia na mioyo ya wale,
waliojiungamanisha na kazi takatifu ya Mungu, waone Umuhimu wa wale wanaopaswa
kutumika kama Mashemasi na Wazee kuwa wanapaswa
kuwa Wanaume safi walioaminiwa na kundi la MUNGU. Yesu anajiita mwenyewe
kuwa mchungaji mwema. EG WHITE COMMENTS
ON 1TIMOTHEO 3:1-13, SPIRIT OF PROPHET VOL. 3 PAGE 2123, 7BC UK 914 P.11 SURA
17. ”MWANZO 3:16, 1TIMOTHEO 2:12- 1
“…..Lakini baada ya Hawa kutenda
dhambi, kama alivyokuwa wa kwanza katika kukosa, Bwana alimwambia kuwa Adamu
atakutawala. Aliwekwa chini ya mamlaka ya mume wake, na hii ilikuwa ni sehemu
ya Laana. Katika matatizo mengi; Laana imefanya uzao wa mwanamke kuwa na
machungu na maisha yake kuwa mzigo….” 3T, 484.1
“Hawa
alikuwa mwenye furaha kamili kuwa kando ya Mme wake katika nyumba yake ya
Edeni, lakini, kama akina Hawa wa Kisasa alijisifu kwa kuwa na matumaini ya
kuwa juu Zaidi ya nafasi aliyowekewa na MUNGU katika kujaribu kupanda Zaidi ya
nafasi yake ya Asili alishushwa chini Zaidi ya nafasi yake ya Asili. Matokeo
kama hayo yatafikiwa na wale wasiopenda kwa hiari yao na kwa furaha kushika
Majukumu yao katika mpango wa Mungu katika juhudi za kutaka kuwa katika nafasi
ambazo Mungu hakuwapangia, wengi wanaacha nafasi wazi ambapo wangekuwa Mbaraka
katika kutamani nafasi za juu. Wengi wametoa kafara heshima na hadhi ya kweli
kama Mwanamke, na wameacha kile mbingu ilicho wapangia.” WAZEE NA MANABII UK 31p.1 SURA 3, PP (PATRIACHES AND PROPHET) UK 59
p.1
WAJIBU AMBAO MUNGU ALIMPANGIA MWANAMKE: CHS: UK 25
i). Kuwalea watoto na kuwafundisha Maadili Mema ya kumcha MUNGU.
“Mwalimu wa kwanza wa watoto ni mama,
katika kipindi ambacho ni rahisi sana kuathiriwa na ushawishi na ambacho ni cha
kukuwa haraka elimu yake kwa sehemu kubwa Imo Mikononi Mwa Mama yake. Mama
amepewa fursa ya kwanza ya kufinyanga tabia kwa wema ama kwa ubaya anapaswa
kuelewa thamani ya fursa hiyo na Zaidi ya Mwalimu Mwingine yeyote yule yafaa
awe amestahili kutumia kwa ubora Zaidi. Na bado hakuna mwingine ambaye Mafunzo
yake hufikiriwa kwa kiwango kidogo sana huyu ambaye Mvuto wake katika elimu ni
Muhimu sana na wenye kwenda mbali sana, ndiye ambaye Msaada wake umepewa
jitihada ndogo kabisa.” HELIMU YA KWELI
SURA 12 UK 222 p.1, 201 p.1, EDUCATION 275 p.1
“Yokobedi
alikuwa mwanamke mtumwa. sehemu ya maisha yake ilikuwa duni, na mzigo mzito
lakini hajapatikana Mwanamke Mwingine yeyote ukimuondoa Mariamu wa Nazareti
aliyeupatia ulimwengu baraka kubwa Zaidi akijua kuwa lazima mototo wake
angekuwa mbali na malezi yake, kwenye malezi ya wale wasiyo mjua MUNGU kwa moyo
wake wote alijitahidi kuunganisha nafsi ya Musa na mbingu alitafuta kujenga
Moyoni Mwake upendo na utii kwa MUNGU. Na kwa uaminifu kazi ilimalizika, zile
kanuni za ukweli ambazo zilikuwa Mzigo wa mafundisho ya mamaye, somo la maisha
yake, hakuna mvuto wa baadaye ambao ungemfanya Musa azikane.” HELIMU YA KWELI UK 46 p.3, 42 p.5,
EDUCATION 61 p.3, WAZEE NA MANABII UK 228 p.4, PP 243 p.4
II). KUSHUHUDIA NENO LA MUNGU NYUMBA KWA NYUMBA
“Wengi
wanaitwa kuingia shambani na kufanya kazi ya nyumba kwa nyumba, wakitoa Masomo
ya Biblia, na kuomba pamoja na walio na shauku. 9T 172”. “Wanawake walio jitoa kweli kweli wanapaswa kufanya kazi
ya Biblia nyumba kwa nyumba. 9T 120”
III). KUSAMBAZA UKWELI KWA NJIA YA VITABU,
MAJARIDA, VITINI NA VIJIZUU VILIVYOBEBA UKWELI WA LEO.
“Akina
dada wanaweza kufanya kazi kwa ufasaha kwa kutafuta wale watakaoweza kusambaza
vijuzuu na majarida, nuru itasambazwa kwenye akili za wengi kwa njia hii. Wapo
Wanawake ambao wanajua siri kwa kutaka ukweli uenee kutokana na uzito wa
ushuhuda wao. Wamekubali ukweli kwa dhati. Wanazo mbinu, muono na uwezo mzuri,
na Watakuwa watenda kazi wenye Mafanikio kwa Bwana wao. Wanawake wakristo
wanaitwa kwa ajili hiyo. RH DEC 19,
1878”
“Dada
zetu wanaweza kuwa watenda kazi wakubwa katika kuandikia na kuwavuta Rafiki
wote wenye hisia za ukweli ambao wamepokea karatasi na vijizuu vyetu… Wanawake
walio imara katika utendaji na tabia nzuri wanahitajika, wanawake wanao amini
kwamba hakika tunaishi katika siku za Mwisho na kwamba tuna ujumbe Muhimu wa
onyo la Mwisho unaotakiwa kutolewa ulimwenguni… hawa ndio wale wanaoweza
kutumiwa na Mungu. Kufanya kazi ya vijizuu na umishionari hawa wanaweza kufanya
kazi ya thamani kwa namna mbalimbali kwa kusambaza vijizuu na jarida la Sign of
times (Alama za nyakati). RH DEC 19 1878”
IV). KUWAHESHIMU WAUME ZAO NA KUVAA KWA HESHIMA NA ADABU: IK/NJIA UK
205.
Mke
anapaswa kumheshimu mumewe. Mme anapaswa kumpenda na kumtunza mkewe; na
kadri viapo vya ndoa
vinavyowaunganisha kuwa kitu kimoja, kwa hivyo Imani yao kwa Kristo inapaswa
kuwafanya wawe mmoja ndani yake: ADVENTIST
HOME 114:2, 1PETRO 3:1-6, EFESO
5:22,1KORINTHO 11:3, AH UK 114 P.2, 115 P.3, MATUKIO SURA 6 UK 81 P.2 (3SM
242(1856)), ELIMU YA KWELI SURA 27 UK 202 P.4, IK/NJIA UK 210 SURA 34.
V). KUFUNDISHA ELIMU YA UPISHI, UKARIMU NA KARAMA YA UNABII.
Tangu
zamani wanawake wamekuwa wakimtumikia MUNGU kwa namna mbalimbali, walikuwa
watumishi kwenye hekalu kutoka 38:8,
Wakati wa yesu walimuhudumia kwa mali zao Luka 8:3, Wakati wa Mitume
waliendeleza karama ya kumtumikia MUNGU. Matendo
9:35-40, Warumi 16:1-2, Kwa karama ya unabii walitumika. Waamuzi 4:4 Debora aliwaamuru watu
chini ya mtende kutoka 15:20, Miriam
aliongoza wanawake kuimba, na Musa aliongoza taifa zima kuimba kutoka 15:1-19, Ana alitoa Unabii Luka 2:36, wakati wa Mfalme Yosia,
Hulda alitoa Unabii 2falme 22:14-19,
Mabinti wa Filipo walikuwa Manabii Matendo
21:9-14. Hata wakati za Wa-adventista Wasabato MUNGU alimtumia E.G.W kwa karama
ya unabii kwa ajili ya kulielekeza kanisa, kulionya na alitabiri mambo mengi
yatakayo tokea kanisani na ulmwenguni. Mengi yamekwisha timia na yataendelaekutimia.
Kati ya Wanawake wote hao hakuna hata mmoja aliyefanya kazi ya Ukuhani, uongozi,
Kuwa mzee wa kanisa, Shemasi au wadhifa wowote wa utawala kanisani.
WANAWAKE KUWEKEWA MIKONO YA KUWA
MASHEMASI NA WACHUNGAJI
Hakuna jambo la hatar kama hili la
kuwawekea Mikono Wanawake Kushika nyadhifa hizi kanisani, Ni UASI wa kupindua
Mpango wa MUNGU. NI kuwakosesha watu na kuharibu njia ya mapito ya zamani ya
watu wa MUNGU “MWANZO 3:16, 18:19,
YEREMIA 6:16, WAEBRANIA 13:7”
Katika historia ya kanisa la MUNGU hakuna
sehemu yeyote katika Maandiko Matakatifu ambayo wanawake waliwekewa Mikono
yakuwa Viongozi. UASI huu wa kuwawekea Wanawake Mikono ulijadiliwa na
kupitishwa na viongozi wa General Conference (GC) Mwaka 2010 nakuingizwa ndani
ya kanisa, Soma kanuni ya kanisa TOLEO
LA 18 SAHIHISHO LA 2010.
“Huduma ya kuwawekea Mikono Mashemasi Wakike. Huduma hiyo haina budi
kufanywa na Mchungaji aliyewekewa Mikono Mwenye cheti hai kutoka Conference.
Huduma ya kuweka Mikono haina budi kuwa sahihi na ifanywe mbele ya kanisa.
Kanuni ya Kanisa UK 86.” Maelekezo
haya ya GC ya kuwawekea Wanawake mikono
yanapingana na ushuhuda wa roho ya unabii na Biblia
“Sipendekezi kwamba Mwanamke atafute kuwa mpiga kura wala kushika
wadhifa wa Ofisi; lakini akiwa kama Mmishonari, akifundisha ukweli kwa njia ya
Majarida, kwa kusambaza Vijuzuu na Majarida yaliyobeba ukweli wa leo anaweza
kufanya kazi kubwa Zaidi. HUDUMA YA KIKRISTO UK 19 P.4, CHS 28 P.4 SURA 1”
MATENDO 6:5-6, 14:23.
“Wale wanaofikiria kwamba wameitwa kutetea
harakati za kutafuta haki za wanawake na kile kinachoitwa Matengenezo ya Mavazi
hawataweza kuunganika katika utangazwaji wa ujumbe wa Malaika watatu. 1T UK 421 p.4”
“Kuna umuhimu wa kutosha na ulazima wa kazi
katika ulimwengu huu wenye uhitaji na kuteseka pasipo kupungukiwa na thamani
kwa Uzuri na kujionyesha… Wakati MUNGU alipomuumba Eva hakupanga Eva awe chini
au juu ya Adam kimamlaka bali katika mambo yote atakuwa sawa naye. Wazazi wetu
wa kwanza wasingekuwa na Mipango inayojitegemea kila mmoja wala kila mmoja
asingekuwa na mawazo binafsi na kutenda kwa Ubinafsi; lakini baada ya Eva
kutenda dhambi, kama alivyokuwa wakwanza kukosa Bwana alimwambia kuwa Adam
atakutawala. Aliwekwa chini ya mamlaka ya mume wake na hii ilikuwa ni sehemu ya
laana. 3T 484 P.1”
“Mstari unaotofautisha kati ya wanaodai
kuwa wakristo na Makafiri sasa haiwezekani kutofautisha. Washiriki wa kanisa
wanapenda yale ambayo ulimwengu unayapenda na wako tayari kujiunga nao, na
shetani anadhamiria kuwaunganisha katika kundi moja na kwa kufanyia hivyo
anaimarisha kazi yake kwa kuwaswaga wote katika safu za UMIZIMU. Wakatholiki
ambao wanajivuna Miujiza kama Ishara Maalumu ya kanisa la kweli watadanganyika
kwa urahisi na uwezo wa utendaji huu wa ajabu; na Waprotestant wakiwa wameshatupa
tayari ngao ya ukweli nao pia watadanganyika. Wakatholiki, Waprotestant na
Wapagani wote kwa pamoja watakubali kuwa na mfano wa utauwa tu bila nguvu na
wataona katika Muungano Maendeleo
Makubwa ya kubadilika kwa ulimwengu na kuanzisha milenia iliyo tarajiwa kwa
muda mrefu. PAMBANO KUU UK
588(KINGEREZA) UK 481(KISWAHILI P.2)”
Bima
ya maisha ni sera ya ulimwengu
inayoondoa utegemezi wa Mwanadamu kwa MUNGU wake juu ya ulinzi wa maisha yake,
utendaji wa kazi yake ya Injili, Na kuweka kikwazo kikubwa, kinacho kwamisha
kazi ya MUNGU kwa kujiungamanisha pamoja
katika biashara na ulimwengu.SPIRIT OF
PROPHECY VOL 2550
Nilionyeshwa kwamba Wa-adventista Wasabato
hawapaswi kujiunga na bima ya maisha. Hii ni biashara ya ulimwengu ambao Mungu
hakuithibitisha. Wale wote wanaojiingiza katika biashara hii wamejiunga na
ulimwengu wakati Mungu anawaita watu wake watoke na kujitenga nao, Malaika
alisema “Kristo amewanunua ninyi kwa kafara ya maisha yake, vipi? Hamjui yakuwa
miili yenu ni hekalu la Roho Mtakatifu aliye ndani yenu ambaye ni Wa mungu, na
sio wenu! Kwa maana mlinunuliwa kwa thamani kwa hiyo mpeni utukufu Mungu katika
miili yenu, na ndani ya roho zenu ambavyo ni vya Mungu. Kwa maana mmekufa na
maisha yamefichwa katika kristo ndani ya Mungu. Wakati kristo ambaye ni uhai
wenu atatokea, ndipo mtatokea pia pamoja naye katika utukufu. Hii ndiyo bima
pekee ya maisha ambayo mbingu inakusudia.
1T 176-177, LIFE INSURANCE, 1T 550 SURA 96, Warumi 14:7-8, 1PETRO 1:17-19,
1KORITHO 6:19-20, 1KORITHO 7:23” warumi 14:7-8
1 petro 1:17-19 1 korintho
6:19-20, 7:23, 1T 549.2, 1T 176-177 p.1-3, 1T 550 p.1-3 SURA 96. “Wanafunzi walipaswa kuendele kazi yao
mbele kwa jina la Kristo. Kila neno na tendo lao lilikuwa kuzingatia jina Lake,
kama kuwa na nguvu hiyo muhimu ambayo wenye dhambi wanaweza kuokolewa. Imani
yao ilikuwa kwa kuzingatia yeye ambaye ndiye chanzo cha rehema na nguvu. Kwa
jina lake walipaswa kuwasilisha maombi yao kwa Baba na wangepokea
jibu.walipaswa kubatiza kwa jina la Baba,Mwana na Roho Mtakatifu.Jina la kristo
lilikuwa liwe neno lao la kutazama alama yao ya kutofautisha, kifungo chao cha
umoja, mamlaka ya mwenendo wao, na chanzo cha mafanikio yao.hakuna kitu ambacho
kilitambulika katika ufalme wake ambacho hakikuchukua jina lake na chapa yake.”ACTS
OF THE APOSTLES 28p.2
Bima
ya maisha ni sera ya ulimwengu ambayo imeingizwa kanisani na ni sera inayo
haribu utaratibu wa Injili. Mtu hawezi kufanyia kazi ya kupeleka injili kutoka
sehemu moja kwenda nyingine bila kulipia bima, hakuna sehemu yeyote katika
historia ya maandiko Matakatifu ambapo watu wa MUNGU walipeleka injili kwa
kulipa Bima, kulipa Bima ni kinyume na mpango wa MUNGU. 1T 550 P.1, 1PETRO 2:9-10, YAKOBO 4:4
Bima
ya Maisha ni Mpango wa shetani wa kuondoa unyenyekevu na upekee wa
Wa-adventista Wasabato na kuungana na Ulimwengu 1T550 p.2
Ni
mpango wa shetani kuleta udanganyifu na kuweka watu katika hali ya mzubao ili
washindwe kufahamu nini kinacho ukumba ulimwengu, na wao wenyewe kushindwa
kujiandaa kwa ajili ya marejeo ya Kristo 1T
550 p.3
MFUMO WA KANISA LA MUNGU.
Kanisa la Mungu duniani ni chombo kiteule kwa
ajili ya Maisha Matakatifu. MUNGU amelipa Kanisa Mamlaka ya kutenda na kuamua
kwa ajili ya utukufu wake. Tangu kupaa kwa Kristo kwenda mbinguni Kanisa
limekuwa likitenda kwa niaba yake hapa duniani.kanisa ni jumuiya ya watu wawili
au watatu wanapopatana katika neno la
MUNGU na kukusanyika pamoja na kumwamini yesu na kushika amri zake, hao ndio
Kanisa la MUNGU Duniani hata kama ni wachache ndilo kanisa la MUNGU.
“Mitume
walikuwa waangalifu sana kuwazunguka waumini wapya na ulizi wa utaratibu wa
Injili. Makanisa yalipangwa na kufunguliwa mahali pote waumini walipotokea.
Maofisa wa kanisa walichaguliwa, na mpango kamili wa Kanisa uliimarishwa kwa
ajili ya Mambo ya Kiroho ya waumini….PAULO alikuwa mwangalifu sana kuendesha
mpango bora wa utaratibu wa kanisa mahali popote makanisa yalipofunguliwa, na
yote yaliambatanishwa katika Kristo aliye kichwa cha wote. Hata pale palipo
kuwa na waumini wachache tu palifunguliwa kanisa pia na walifundishwa
kusaidiana wao kwa wao wakikumbuka ahadi kwamba “Wakusanyika watu wawili au watatu kwa jina langu mimi nipo kati yao”
Mathayo 18:20, MAONJO HADI USHINDI UK 79 p.3-4 sura 18”
“MUNGU aliweka juu kanisa lake uwezo
na hali ya juu kabisa chini ya mbingu. Ni sauti ya MUNGU kupitia watu wake
walio na Umoja katika mamlaka ya kanisa ambayo yapaswa kuheshimiwa.” 3T 451 p.1
sura 36.
MFUMO WA KANISA LA AWALI (MITUME)
Baada ya kifo cha Sitefano wanafunzi
walisambaa na kukimbia mateso wakaanza kuubiri Injili kwa nguvu na kutii agizo
la Yesu, “Enendeni ulimwenguni kote mkahubiri injili”. MATHAYO 28:19-20, MARKO
16:15-16. Makanisa yalianza kufunguliwa na kila mahali na kuongezeka katika
idadi ya waumini, na makanisa. Na wote walikuwa na umoja wa Imani, na
Mafundisho. WAEFESO 4:1-6. Na mfumo uliendelea kuimarishwa sambamba na
utaratibu wa Injili. “EW sura 23”
“Mfumo
wa Kanisa kule Yerusalemu ulitakiwa uwe mfano wa mfumo wa kanisa kila mahali
ambapo wajumbe wa kweli watakapo ongoa roho katika Injili baadaye katika historia
ya Kanisa la awali wakati katika maeneo mbalimbali ya ulimwengu ambapo makundi
ya waumini yalipopatikana na kutengeneza makanisa, Mfumo wa kanisa ulizidi kufanywa
kuwa kamili kiasi kwamba utaratibu na matendo yenye ulinganifu yaweza
kudumishwa. Kila mshiriki alifundishwa kufanya sehemu yake. Kila mmoja alitakiwa
kutumia talanta zake kwa hekima.”AA (Act
of Apostles) sura 9 UK 91 p.2,Maonjo ushindi UK 29 P.sura9.
Baraza la makanisa yote ulimwengunii lilikaa Yerusalemu
kujadili mada zote za mafundisho na hasa juu ya swala la tohara. Wajumbe
walitoka Makanisa mbalimbali yaliyokwishwa funguliwa na Mitume ili kuwakilisha
Makanisa yote.
“Sehemu mbalimbali zilisemwa ili
kuleta matatizo Barazani, baada ya majadiliano mengi sana, Petro alisimama
akasema “ndugu zangu mnajua kwamba mwanzo MUNGU alinichagua kwamba watu wa
mataifa wasikie neno la Injili kwa kinywa changu na kuamini.”” MAONJO HADI
USHINDI UK 82 P.6 SURA 19, MATENDO15:7
“Roho
matakatifu hakuona kuwa inafaa kuwalazimisha waumini wa kimataifa kushika
sharia ya Musa kwa hiyo mawazo ya mitume juu ya jambo hili alikuwa
tusiwataabishe waumini wakimataifa …… uamuzi huu ulikomesha majadiliano juu ya
jambo hili katika jambo hili tunakanusha wazo la kusema kuwa Petro alikuwa
ndiye wanayemfuata katika uongozi wa kanisa, Hawana uthibitisho wowote wa
maandiko matakatifu kupatana na madai wao. Petro hakuwa mkuu kuliko ndugu zake.
Kama wale wanaodai wanamfuata petro, kila mara wengekuwa na ndugu zake,
wakibaki kayika hali ya ulinganifu na engine.” MAONJO HADI USHINDI UK 83 P.5, 6 SURA 19
Yakobo
alikuwa Mwenyekiti wa kikao hiko cha mjadala huo na hakuna Mwenyekiti wa
makanisa kama walivyo wengi leo. Mwenyekiti wa kikao hawezi kuwa Mwenyekiti
wamakanisa. Makanisa yalikuwa na viongozi wake ambao n wazee wa Makanisa na
Mashemasi. Walipokuwa wakikutana kwenye vikao walikuwa wanamchagua Mwenyekiti
wa Barazaa na baada ya kikao kuisha wenyekiti wake. Ulishia hapo hapo
utekelezaji wa mipango yote ulibaki kwa mitume na wazee na Mashemasi.
“Utaratibu uliofuatwa katika kanisa la
kwanza, uliwawezesha kuwa jeshi Imara lisiloshindwa. Waumini ingawa
walitawanyika katika sehemu mbalimbali walikuwa na Umoja. Matatizo yalipoteikea
mahali pa kanisa Fulani hakuachiwa yaligawe kanisa zima mitume na wazee
waliliongoza kanisa kwa ukamilifu.”Maonjo hadi Ushindi UK 42 p.2 Sura 19, Act
of Apostles (AA) 95 P.3
“Baraza
lililoamua kesi hii lilikuwa la mitume na waalimu waliokuwa nguzo za taifa la
wayahudi, na wakristo kutoka makanisa yote kama walivyochaguliwa, kutoka mahali
mbalimbali. Makanisa makubwa yote yalikilishwa. Baraza liliendeshwaa kwa
utulivu kutoka katika makanisa yaliyofunguliwa kwa Utukufu wa MUNGU. Wote
waliona kuwa MUNGU amejibu hoja hiyo kwa njia ya kumwaga roho mtakatifu kwa
watu wa mataifa. Sasa ilikuwa sehemu yao kufuata maongozi ya roho.” MAONJO HADI USHINDI UK 84 P.4
Kanisa
la Yerusalemu lilikuwa ndio kanisa pekee lililopokea utume wa injili, na kufungua makanisa kila mahali ulimwenguni Matendo 1:6-26, Mathayo 28:16-21 katika
historia ya kanisa tunaona Umoja wa hali ya juu utaratibu wa kanisa kuwa na
amaamuzi ya pamoja. Mfumo huo ndio uliotumiwa na Wa-adventista Wasabato kabla
ya kuiga Mfumo wa Ulimwengu yaani utawala wa Msonge. Utawala wa kanisa la MUNGU
mamlaka ya maamuzi imo mkononi mwa washiriki wa kanisa huu ndio muundo wa la
kanisa la siku za mitume, na Wa-adventista Wasabato wa mwnzo “Wakati Mmlaka ambayo
MUNGU amelikabidhi kanisa, yanapotelewa kwa jumla. Kwa mtu mmoja na atakuwa mamlaka
ya kuwa mwamuzi kwa niaba ya watu wengine basi utaratibu wa kweli wa Biblia
umekiukwa. Juhudi za shetani mawazoni mwa mtu kama huyo zitakuwa za hila nyingi
na wakati mwingine karibu zenye kutisha kwa sababu adui atatumaini kwamba
kupitia kwa mawazo ya mtu huyo ataweza kuwageuza wengine wengi. Hebu tuto kwa
mamlaka ya juu kabisa katika kanisa. Kile ambacho tunataka kumpa my mmoja au
kikundi ha watu.” 9T UK 261 P.1
Ni kwa jinsi gani kanisa la Wa-adventista
Wasabato leo limegeukia mbali na kuacha mfumo aliounzaisha MUNGU kupitia kanisa
la Mitume utakao dumisha kazi yake hata mwisho? Kanisa kwa sasa limekuwa
taasisi mpya, Shirika jipya la dini ambalo utaratibu wa zamani (Mfumo)
ulioliwezesha kanisa kusimama imara na kulifanya kuwa la pekee ulimwenguni umeachwa.
“Adui amedhamiria kuingiza dhana za
uongo ndani ya kanisa la Wa-adventista Wasabato. Mabadiliko makubwa yalifanyika
itakuwa ni pamoja na kuachana na misingi ya Imani yetu, iliyosimama kama nguzo
ya kanisa.uasi huu utapelekea kanisa kupagwa upya. Matengenezo haya bandia yatakapoanza
yataleta maokeo gani? Kanuni za ukweli ambazo MUNGU kwa hekima yake alizitoa
kwa kanisa la masalio zitatupwa chini. Dini yetu itabadilika kanuni kuu ambazo
zimeendimisha kazi ya MUNGU kwa Zaidi ya miaka 50 zitaonekana kama zilikosewa.
Shirika jipya la dini litaanzishwa.vitabu vyenye mabadiliko mapya vitaandikwa
na mfumo wenye falsafa ya kisomi utaanzishwa. Waanzilishi wa mfumo mpya
watakwenda kwenye mji na kufanyia kazi ya kutisha. Sabato haitachukuliwa katika
uzito wake na hata yule aliyeitoa. Hakuna mambo ya zamani yatakayo simama
katika mfumo huu mpya. Viongozi hawa watawatazimisha waumini kwa watu badala ya
MUNGU, watajenga mfumo wao katika mchanga na tufani na dhoruba itafagilia mbali
nyumba zao.” 1SM 204 P.2 SURA 29
Moja ya mambo yaliyopelekea kanisa kupangwa
upya ni pamoja na kuweka mfumo wa msonge na kuweka makao makuu ya kanisa
ulimwenguni. “Imani ambayo kwa muda
karne nyingi ilishikiliwa na kufundishwa na wakristo wakialdensis ulitofautiana
kabisa na mafundisho ya uongo yaliyotoka rumi. Imani ya dini yao ilipatikana
katika neon la MUNGU lililoandikwa, ambao ni mfumo wa kweli wa kikisto. Lakini
hawo wakulima wanyenyekevu, katika
makimbilio yao ya faragha, wakiwa wamejitenga mbali na ulimwengu na kulazimaka
kila siku kufanyia kazi za taabu katika makundi ya mifugo yao na katika mashamba
yao wao hakuweza kufikiwa na upinzani uliotokana na Dogma na uzushi wa kanisa liloasi. Imani yao
haikuwa Imani mpya iliyopokelewa.imani ya dini yao ilikuwa urithi kutoka kwa
baba zao. Walipambana kwa ajili ya Imani ya kanisa la mitume, Imani waliyo
kabidhiwa watakatifu mara moja tu. “Yuda
1:3” kanisa lililoko jangwani lilikuwa ndio kanisa la kweli la kristo, Mlinzi
wa hazina za ukweli ambao MUNGU amewakabidhi watu wake kwa ajili ya kuzitoa kwa
ulimwengu, wala sio lile lenye mfumo msonge wa utawala wakiburi na majivunio
lililoweka makao yake makuu ulimwenguni.” PAMBANO KUU UK 51 P.3 SURA 4 GC UK 64
P.2
“Roho
ya kuyaunganisha na ulimwengu inavamia makanisa mahali pote katika ulimwengu wa
kikristo. Robert Atkins, katika hotuba yake iliyohubiriwa London, Kuhusu picha
ya giza la kiroho linaloenea uingereza: “Haki ya kweli imetoweka duniani, na
hakuna mtu anayelitia moyoni. Maprofesa wa leo wa dini katika kila kanisa, ni
wapenda ulimwengu, wanafuata ulimwengu, wanapenda faraja za watu, na watafutaji
wa heshima. Wanaitwa kuteseka pamoja na kristo, lakini wananywea kwa kushutumiwa
tu…. UASI, UASI, UASI unachongwa kwenye
makao makuu kabisa ya kila kanisa, Na kama wangelijua hilo, na kama wangeliona
hilo, kungekuwepo na tumaini, lakini loh!
Wanapiga kilele, tumetajiri, tuna mali nyingi na hatuna haja ya
chochote. ” PAMBANO KUU UK 370 P.3 SURA 21 GC 388 P.1
“Kadri moyo wa mwanadamu unavyo sukuma
damu katika kila sehemu ya mwili ndivyo uongozi wa mahali hapa, Makao Makuu ya
kanisa letu unavyo athiri jamii nzima ya washiriki, ikiwa Moyo una afya njema
basi na damu inayozunguka mwili wote ni safi, lakni iwapo chemichemi ni; chafu
viungo vyote vitaugua kwa ajili ya sumu iliyo katika damu, ndivyo ilivyo kwetu
pia kama chanzo cha Makao Makuu ya kazi yetu kitachafuka; kanisa zima katika
matawi yake mbalimbali na mipango iliyo enea katika uso wa dunia itaathirika
hatimaye.” 4T 210 P.4 SURA18, “4T 210 P.5””. “Kazi kubwa ya shetani ipo katika
makao makuu ya Imaniyetu.”
Kitendo
cha kuanzisha makao makuu Duniani, kanisa lilifungua mlango kwa shetani kuingia
na kuanza kufanyia mabadiliko makubwa kupitia sauti ya kiongozi aliyepewa
mamlaka ya kuwa msemaji Mkuu na kwa njia hiyo tunayaona mambo mengi yeingizwa
kanisani yakiwemo hayo ambayo tumeyaorodhesha.
“Watawala,
Wanasiasa, Madaktari, Wanasheria, Wafanyabiashara, wote walijiunga na kanisa
kama washirika, ili iwe njia ya kuendeleza mambo yao ya kiulimwengu.
Halmashauri za kanisa zilikuwa zikiongozwa na makafiri hao ambao walifanya kana
kwamba ni waongofu wa kweli hukuwakitafuta anasa za ulimwengu. Makanisa
makubwa, maridadi sana yaliyojengwa Wachungaji hodari ambao amabo kazi yao hasa
ilikuwa kuwaburudisha watu, walikuwa wakilipwa mishahara mikubwa sana. Mahubiri
yao yalikuwa ya kuwaburudisha tu wasikilizaji. Hivyo dhambia zilifichika chini
ya uonngofu wa mfumo tu.”PAMBANO KUU UK
223 P.1 SURA 21, PAMBANO KUU UK 322 P.2, GC 88 P.1 SURA 21
“Kama misingi ikiharibika, Mwenye haki atafanya nini?” Zaburi 11:3
Wakati kanisa linapoacha kutii Neno la
MUNGU na kushikilia mapokeo na desturi; Waaminifu huitwa kujitenga na mfumo wa
kanisa Asi.Kama vile ambavyo tumeona kanisa la Wa adventista wasabato wa chini
ya taasisi ya General Conference (GC) wameshikilia mafundisho potofu yaliyo
kinyume na neno la MUNGU “YUDA 1:3-4,
17-19”
“Bwana yesu daima atakuwa na watu wake wateule kumtumikia yeye, wakati
wayahudi walipomkataa kristo Mfalme wa uzima, aliuondoa ufalme wa MUNGU kutoka
kwao na kuwapa watu wa Mataifa. MUNGU ataendelea kutenda kazi kwa kutumia
kanuni hii kwa kila tawi la kazi kwa yake, wakati kanisa linapodhihirika
kutokuwa na uaminifu. Kwa neno la Bwana; Ijapokuwa msimamo wao uweje, ijapokuwa
wito wao uwe wajuu na mtakatifu Kiasi gani, Bwana hawezi kuendelea kutenda kazi
pamoja nao. Wengine huchaguliwa kushika majukumu haya muhimu Lakini na Kama hao
nao hawajasafisha maisha yao kuondokana na kila tendo baya. Kama hawakuzi
kanuni safi na takatifu katika mipaka yao yote ndipo Bwana kwa masikitiko
atawapa mateso na kuwanyekeza na wasipotubu atawaondoa kutoka katika mahali pao
na kuwafanya kuwa karipio na aibu.” MATUKIO
SURA 4 UK 54 P.2, 3MR.VOL 14 UK 102 P.1, MR (MANUSCRIPT RELEASE), WARUMI
11:17-21,1SAMWELI 2:30
“Baada
ya mda mrefu na Mapambano makali waaminifu wachache waliamua kuvunja umoja wote
na kanisa Asi kama linaendelea kukataa kujiondoa lenyewe kutoka kwenye uongo,
na Ibada ya Sanamu.Waliona kwamba hutengano ulikuwa lazima ufanyike kama
wangetaka kulitii neon la MUNGU. Hawakuthubutu na kuweka Mfano ambao
ungehatarisha Imani ya watoto wao na wajukuu wao. Ili kupata amani na umoja
walikuwa tayari kukubali kufanya Mapatano yeyote kwa unyoofu na MUNGU; Lakini
waliona kwamba hata amani ni ya thamani ndogo mno kununuliwa kwa kutoa mhanga
kanuni. Kama umoja ungeweza kupatikana tu Kwa kuhasatarisha ukweli na haki,
Hebu kuwepo utengano na hata kwa Vita. PAMBANO
KUU SURA 2 UK 36P.3, PAMBANO KUU SURA 2 UK28 P.1 GREAT- CONTROVERSY UK 45 P.3”
“Miongoni
mwa wale waliopinga ujitwaliaji usio halali wa utawala wa upapa, waldense
walikuwa mstari wa mbele…. Hata hivyo walikuwepo baadhi waliokataa kusalimu
amri Kwa mamlaka ya upapa, au ya Maaskofu. Walidhamiria kudumisha uaminifu wao Kwa
MUNGU na kulinda usafi na unyofu wa Imani yao. Ndipo utengano ukatokea. Wale
walioshikilia Imani ya awali sasa walijitenga; baadhi walihamia kwao katika
milima ALPS, wakainua bendera ya ukweli katika nchi za kigeni; wengine
wakakimbilia sehemu za faragha za mabonde membamba na katika majabali imara
kabisa ya milima, na huko walitunza uhuru wao wa kumwabudu MUNGU. PAMBANO KUU, UK 51 P.2, UK 39 P. GREAT
CONTROVERSY UK 64 P.1
Mwenyewe
kwamba inapaswa kuthubutu kusimama peke yangu kupingana na upapa na kumhubiri
kuwa ni Mpinga KRISTO…. Pambano kuu UK
118 P.1, UK 84 P.6, Great Contro versy
UK 143 P.1 Sura 7.” “Luther alifanya Uamuzi wake wa mwisho wakutengana na
kanisa kwa mashindano ya kutisha. Ulikuwa wakati huu alipoandika kwamba: ”Kila
siku ninaona jinsi ilivyo vigumu kabisa kuacha aibu ambazo mtu amezihifadhi
akilini katika utoto.Lo! ni Mamivu kiasi gani niliyopata ingawa nilikuwa na Maandiko
yakiniunga Mkono, kuutetea uamuzi huo na kujithibitishia
“Wakati wapritan kwa mara ya kwanza taifa
lalazimika kujitenga kutoka kwenye kanisa la kingereza (Angilikana),
walijiunganisha pamoja wao wenyewe kwa Agano Kuu la “kutembea pamoja katika
njia zote za Bwana zilizo funuliwa au zitakazofunuliwa kwao kama watu wa Bwana
walio huru.Pambano Kuu UK 247 P.1, UK 171 P.3 Sura16, Great Controversy uk 291 p.3”
“Ee
Yerusalem, Yerusalem, Uwauae Manabii na kuwapiga kwa mawe wale waliotumwa kwako!
ni mara ngapi nimetaka kuwakusanya pamoja watoto wako kama vile kuku
avikusanyavyo pamoja vifaranga vyake chini ya mbawa zake, lakini
hamkutaka.”katika maombolezo ya kristo moyo wa MUNGU uliguswa. hivyo ulikuwa Kwa heri ya
kisirisiri ya uvimilivu wa upendo wa MUNGU.Mafarisayo na masadukayo
walinyamazishwa kimya.Yesu aliwakusanya wanafunzi wake wakatoka hekaluni, akiwa
sio kama mtu aliyeshindwa, bali kama ambaye ametimiza kazi yake. Aliondoka
akiwa Mshindi toka katika mapambano .Katika siku hiyo ya ajabu katika mioyo mingi
mawazo mapya yalichipuka, na historia mpya ikaanza baada ya kusurubishwa na
kufufuka. Watu hawa walijokeza mbele wakiwa na hekima na bidii ….. Lakini
Israeli Kama taifa lilikuwa limejitenga toka Kwa MUNGU akiangalia ndani ya
hekalu Kwa mara ya mwisho, yesu alisema Kwa huruma na kuomboleza angalieni
nyumba yenu mmeachiwa hali ya ukiwa.Kama vile mwana wa Mungu alivyo zitoka zile
kuta utukufu wa kuwepo MUNGU Utaondolewa milele kutoka katika hekalu lililojengwa
kwa ajili ya utukufu wake”. TUMAINI LA
VIZAZI VYOTE UK 348 P.1-4 UK 310 P.1-4 DA 620 P.1-4 SURA 67. ”
“Wakati
kazi yake ilipolenga kujenga Makanisa kwa mda kitambo ilipendwa. Lakini wakati
wachungaji na viongozi wa dini walipokataa fundisho la Marejeo na kunuia
kukomesha na kuzima hamasa na majadiliano yote ya mada hii, hawakuipinga kwenye
Mimbari tu, bali waliwanyima washiriki wao furusa ya kuudhuria Mahubiri juu ya
kuja mara ya pili au hata kuzungumzia tumaini lao katika Mikutano ya Jumuiya za
kanisa hivyo ndivyo wahumini walivyojikuta katika jaribu la mfadhaiko,
mkanganyiko na upinzani mkali. Waliyapenda makanisa yao na hawakutaka kutengana
nayo; Lakini walipoona ushuhuda wa neno la MUNGU ukinyamazishwa na haki yao
yakuchunguza unabii ikizuiwa waliona kwamba uaminifu wao kwa MUNGU unawazuia
kutii, wale waliotafuta kufungia nje ushuhuda wa neno la MUNGU hawawezi kuhesabiwa
kuwa Miongoni Mwa wanao lifanya kanisa la kristo kuwa nguzo na umoja wa ukweli.Hivyo
walijiona kuwa na sababu ya kujitenga kutoka kwenye Mathehebu yao ya Zamani.
Katika Majira ya joto ya Mwaka 1844 karibu waumini 50 elfu waliondoka kutoka
Makanisani.” PAMBANO KUU UK 314 P.3, UK
217 P. 3, GREAT CONTROVERSY UK 376 P.1 SURA 21
“Kwa
kila kizazi historia ya kristo kujitenga na yuda zilitangazwa. Wakati
watengenezaji wa dini walipohubiri neno la MUNGU, hawakuwa na wazo la
kujitengana na yuda lakini viongozi wa kanisa hawakukubaliana na nuru hiyo
mpya; na hao waliokuwa na nuru hiyo walipaswa kutafuta. Watu wanao kubaliana na
ukweli huo. Siku zetu hizi ni watu wachache tu baina ya wafuasi watenganezaji
wa kanisa yaani reformers, husikia sauti ya MUNGU, na kuwatayari kukubaliana na
neno linalo hubiriwa.kila mara wale wanaofuata hatua za watengenezaji hulazimishwa
la MUNGU; Wengi hutoka na kutengana na Makanisa ya Baba zao, hili wapate kumtii
MUNGU: TUMAINI LA VIZAZI VYOTE UK 123
P.3, UK 108 P.5 DA UK 232 P.2 SURA 23.”
“Kulikwepo na kutoka nje, utengano wa
kujitenga na waovu uliotolewa Maamuzi, kukimbia ilikuokoa Maisha.Ndivyo
ilivyokuwa katika siku za Nuhu; ndivyo ilivyokuwa kwa Luthu; ndivyo ilivyokuwa
kwa wanafunzi muda mfupi kabla ya angamizo la Yerusalemu; Na ndivyo
itakavyokuwa katika siku za Mwisho. Sauti ya MUNGU inasikika tena ikiwa na
ujumbe wa onyo ikiwataka watu wake wajitenge kutoka katika Wimbi la uovu”. WAZEE
NA MANABII UK 145 P.1. PATRIACHS AND PROPHET (PP) UK 166 P.4. RH JULY 24 1894
P.2-3
“Nilionyeshwa
Masalio wa MUNGU wakilichukua jina Makundi Mawili yalipitishwa mbele yangu. Kundi moja ilikumbatia jamii kubwa ya
kikristo. Waliokuwa wakikanyaga sharia ya MUNGU na kutukuza taasisi ya
kipapa.Waliokuwa wakitunza siku ya kwanza ya juma kama sabato ya Bwana. Kundi lingine ambao walikuwa wachache kwa
idadi, walikuwa wakimsujudia mtoa Sheria Mkuu. Wao walikuwa wakitunza amri
ya nne. Upekee na Muonekano wa tabia ya Imani yao ulikuwa utunzaji wa siku ya
saba, na kutazamia muonekano wa Bwana wetu kutoka Mbinguni”1 T 223 P.1 SURA 42.
Kundi la kwanza seveth day
Adventista of General Conference GC
|
Kundi la pili seventh day Adventista
church masalio.
|
i)Makao Makuu yao yako duniani
“ MUNGU amewakabidhi watu wake
kwaajili ya kuzitoa kwa ulimwengu wala sio lile lenye mfumo msonge wa utawala
wakiburi na majivuno lililoweka makao yake Makuu ulimwenguni” PAMBANO KUU UK 51 P.1 GC 64 P.2
ii)” Roho ya kufungamanisha na
ulimwengu inavamia makanisa mahali pote katika ulimwengu wa kristo…….. Uasi,
uasi, uasi unachongwa kwenye makuu kabisa ya kila kanisa” PAMBANO KUU UK 388 P.1 SURA 21.
Kanuni ya kanisa inayobadilika kila
baada ya miaka mitano
“Kuna wajenzi wa mnara katika wakati
wetu….. Katika ulimwengu wa kikristo wengi ugeuka na kuwa mbali na mafundisho
ya Biblia yaliyo wazi na kutegemea kanuni kutokana na hadithi zinazo
wapendekeza” WAZEE NA MANABII UK 98
P.2, 3 PATRIACHS AND PROPHET UK 124 P.1, 2 SURA 10.
|
i) Makao Makuu yao yako Mbinguni: 2NYAKATI 30:27 EFESO 2:18-20
“Hebu wote wanaoteswa ama kutendewa
hiana wamlilie MUNGU…. Tunamwaga yale maitaji yetu ya moyo katika chumba
chetu cha ndani, twayatoa Maombi ya kimya tunapotyembea, na maneno yetu
yanafikia kiti, cha Kifalme cha mtawala wa malimwengu. Sala zetu zinaweza
kuwa azisikilizani kwa masikio ya wanadamu. Yanapanda juu ya makelele mpaka
kufikia makao makuu Mbinguni VIELELEZO
VYA MAFUNDISHO YA KIKRISTO UK 124 P.2 SURA 14”.
ii) Kanuni yao ni Biblia na Roho ya
unabii
ISAYA 8:20 UF, 19:9-10, ZABURI
119:129-130, 2
NYAKATI 20:20
“ Lakini MUNGU atakuwa na watu wenye kush
Ika Biblia na mafundisho yake peke kuwa ndio”
Kanuni ya maisha na msingi wa Matengenezo
Yote…. PAMBANO KUU UK 339 P.1
SURA 37.
|
iii)Muongozo wa kujifunza Biblia (
Lesson)
“Kama ingewezekana sehsmu kubwa ya
vitabu vilivyokwisha kuchapishwa kutumiwa, baalinaloogofya sana. Watu akilini
na Moyoni lingezuiwa hadithi za mahaba, hadithi zisizo na mahana zenye
kusisimua pia hadi vitabu vya jamii ile iitwayo hadithi za riwaya za kidini
vitabu ambavyo ndani yake. Mwandishi hutia kwenye hadithi yake fundisho la
wema na ubaya maneno ya dini yaweza kuchanganywa katika kitabu cha riwaya
lakini Mara nyingi shetani hujivika, Mavazi ya Malaika Wema apate kudanganya
Zaidi. Hakuna walioimarika katika Mafundisho mazuri wala hakuna wanaosalimika
Majaribuni hata wasiweze kuwa hatarini kwa uovu unao haribu hali ya kiroho
wenye kuitagiza uzuri wa Biblia huanzisha fadhaa, hitiwa wasiwasi Akilini,
hudhofisha Akilini za moyoni zisiweze kuwa na manufaa, huiachisha roho ya mtu
Maombi, na kuiharamisha roho kwa ibada yeyote ya kiroho. 1 1 k 191 p.4, uk 192 p.4 CCH UK 168 P.4.”
*kwa mfano angalia Lesson ya Robo ya
tatu ya Mwaka 2007: ambayo inanjia: kwa wema au kwa ubaya; Ni laana kwa
msomaji.
|
iii) Muongozo wa kujifunza ni Biblia
ni Roho ya Unabii: YOHANA 14:25,
YOHANA 16:13, ZABURI 119:167-168, ZABURI 119:129
“Shuhuda hizi zingeingizwa kwa kila
watu wa nyumbani washikao sabato, na yapaswa ndugu kujua thamani yao na
kuombwa kuzisoma. Haukuwa mpango wa busara sana kuviweka vitabu hivi hesabu
ya chini na kuwa na seti moja tu. Kanisa yapasa pawepo katika jamii vitabu
(maktaba) ya kila watu nyumbani na kusomwa mara kwa mara. Hebu viweke mahali
viwezapo kusomwa na wengi ”1K/NJIA UK
109 P.3, CCH ( COUNCIL TO THE CHURCH) UK 94P.5,5T 681P.2
“Naliitwaa Biblia na kuizinga na
hizi shuhuda kwa kanisa, ambazo zilitolewa kwaajili ya watu wa Mungu hapa
nikasema habari za watu karibu wote zaguswa. Mashauri mema ambayo hayatamani
huweza kupatikana hapa, yametolewa kwa ajili ya mambo ya wengine yakiwa na
hali ya kuwafaa wao wenyewe pia. Mungu amependezwa kuwapa amri juu ya amri
kanuni juu ya kanuni. 1K/NJIA UK
1164P.4,
|
UKATAAJI NA SHUHUDA
“Jambo moja ni hakika: Wale Wa-adventista
wasabato wanaochukua msimamo wa chini ya shetani wataanza kwanza kuikataa Imani
inayohusu maonyo na shutuma zilizomo katika shuhuda za roho wa Mungu”MATUKIO YA SIKU ZA MWISHO UK 164 P.1 SURA
12.
“Eleni white alifanya madai kuhusu huduma yake
ambayo hayatuachi njia panda, alidaikuona mambo ambayo yangalitokea tu katika
muujiza wa uvuvio. Iwe madai yake ni kweli ama alikuwa amechanganyikiwa au
muongo mkuu aliweza kudumisha mafundisho yake tangu katikati ya karne ya 19
hadi muongo wa wa pili wa karne 20 (yaani 1844-1915). Nimaelezo gani ya kiakili
mtu awezayo kutoa Iwapo atadai kuona Mama White aliyoyaona, akiwa njozini?
Alidai kuona watu waishio katika sayari nyingine; na pia wakiwaona malaika
wakiwalinda watu wa MUNGU alidai kuona, njozini akiwa yesu katika Patakatifu pa
Mbinguni, na uzuri aliokuwa nao shetani kaua ajaanguka alidai kuwaona Malaika
wakimtembelea Adam na Hawa bustanini edeni, alidai kuuona uso wa yesu, njozini
mara baada ya uzoefu wa kufunga nyikani siku 40 alidai kuona ufufuo wa yesu
akitoka kaburini na pia kumuona malaika akiwafungulia Paulo na Sila kutoka
gerezani. Mtu hufanyeje na madai hayo? Vipi Kwa wale wanao linganisha huduma
yake na ile ya Martin Luther, hakika wanaishi katika ulimwengu wa ndoto yapasa
tuwe tunamchukulia kutokana na vile alivyojielekeza (ambapo Hakuzuki Maswali)
au tumkatae kama Muongo, aliyechanganyikiwa, au kuvuviwa na yule Muovu. Hizo ndizo
baadhi ya hoja za kiakili” LESSON YA
ROBO 1 UK 2000, KWA WATU WAZIMA UK 67 P.1-3.
“Wa-adventista
Wasabato wamechaguliwa na MUNGU kama watu wapekee, waliotengwa na ulimwengu.
Kwa kutumia upanga Mkali wa kweli ukatao kuwili amewakata na kuwatenga kutoka
kwenye Mafungamano na ulimwengu na kuwaunganisha na yeye mwenyewe.” MATUKIO YA
SIKU ZA MWISHO UK 41 P.2 SURA 4, 7T UK 138 (1902), IK/NJIA SURA 7 UK 67 P.4,
KUMB 7:6-7
Lesson
inataka kuwa sio wa pekee soma “LESSON
YA INJILI NA HUKUMU YA 1844 JULY ROBO 3 MWAK 2006 UK 3 P.1. “Kama
Wa-adventista, mengi ya mafundisho yetu ya pekee, sio ya pekee, tuliipata hata
hivyo, sabato ya siku ya Saba kutoka Kwa Baptist watunza sabato, na isitoshe
wapo wakristo wengine, japo siyo wengi wenye kutunza sabato ya siku ya saba ya
juma Kutoka 20:20.”
“Sabato
ya siku ya Saba ulitolewa na MUNGU Mwenyewe na siyo wabaptist kama wanavyo sema
kwenye lesson.”
KANISA KUUNGANA NA MATHEHEBU MENGI
“Kamwe
atupaswi kuwa na mapatano na watu.Waabuduo sabato ya Miungu (Jumapili) 2SM 35 P.1. Mstari wa kutenganisha kati
ya wanafunzi wa yesu na wa shetani usifutwe’’.5T UK 502P.
Lessoni ya dini ya mahusiano Robo 3 Mwaka
2oo4 UK 54p.2 Lesson inasema kuwa “Hatatuwe tunawajbika kiasi gani kwa utume
wetu, hatupaswi kuelewe ujumbe wetu Zaidi kile unavyoelezea kama kukumbatia
Imani kuwa sisi wa-adventista ndio pekee ambao tutaokolewa.Mtazamo huu kamwe
haujawahi kuwepo, na wala sasa haupo katika misingi ya Imani kanisa la
wa-adventista wasabato:
“Tunayatambua
mashirika yenye kumuinua kristo machoni mwa wanadamu Kama sehemu ya mpango wa
kimbinguni wa kupeleka habari njema ya injili kwa ulimwengu, natunawaheshimu
sana wanaume kwa wanawake katika mathehebu mengine ambao wanashiriki katika
kazi njema yakuleta roho kwa kristo” GC
WORKING POLICY 1999-2000 UK494 POLICY 0.100 AKTICLE1.
IBADA YA SANAMU NDANI YA KANISA LA
WASABATO WA GC
Kanisa
kuchora picha za Watakatifu ni kuenzi Ibada za sanamu na machukizo machoni pa
Mungu, angalia vitabu vilivyo na upagani wa mapicha ya Watakatifu, Kanisa
limefikia hali mbaya na kuharibu mafundisho ya Imani kwa kuingiza Ibada ya
Sanamu Kanisani na sasa ni sehemu ya mafundisho ya Kanisa.
Mikutano
mbalimbali utaona wanaonyesha picha ya Yesu ya uongo, picha za Watakatifu hata
akina Musa, Nuhu, Adam, Eva, Maria, Petro, na Senema za Mitume, Mnabii na watu
hawashtuki au kuuliza swali wakati maandiko matakatifu yanakataza kuchonga
sanamu na kuchora.
“Sanamu
ya kuchora yafaa nini, hata yeye aliyeifanya ameichora? Sanamu ya kuyeyuka,
nayo ni mwalimu wa uongo, yafaa nini hata yeye aliyeifanya aiwekee tumaini
lake, na kufanyia sanamu zisizoweza kusema? HABAKUKI 2:18-19, KUTOKA 20:4-6, ZABURI 115:2-9. Kwa kitendo hiki
Kanisa la Wasabato chini ya GC na Viongozi, Wachungaji, Wainjilisti, Wazee wa
Makanisa na Washiriki wote wameungana kuvunja Amri ya pili “KUTOKA 20:4-6” na kushuhudia uongo kwa
kusema picha hiyo ni Yesu na mapicha mbalimbali na kuvunja Amri ya tisa
“Usimshuhudie jirani yako uongo” KUTOKA
20:16.”
“Wakristo wengi sana hatimaye
walikubali kushusha kiwango cha Ukristo wao na Muungano ukafanyika kati ya
Ukristo na Upagani. Ingawa waabudu sanamu walijifanya kushilia na kugandama
kwenye Sanamu zao, walibadilisha tu vielelezo vyao vya Ibada zao kwa Sanamu za
Yesu na hata za Maria, na Watakatifu wengine, chachu mbaya sana ya Sanamu
iliingizwa Kanisani kwa njia hiyo, iliendeleza kazi yake ya uovu. Mafundisho ya
uongo, desturi za kishirikina na taratibu za vitendo maalumu vinavyoambatana na
Ibada ya Sanamu ziliunganishwa katika Ibada za Kanisani”. PAMBANO KUU 34(42-43)
Kanisa
la Wasabato chini ya GC limejiunga
na Romani Katoliki kwa kuendeleza Ibada za Sanamu, Sanamu za Kisasa za kupiga
picha, kuchora na kunakshi. Ni nani alimpiga picha Yesu, picha Adamu, Ibrahimu,
Musa, Isaka na kutunza picha zao huo ni uongo. Yesu mwenyewe alisema “waheri
wale watakaoamini bila kuona” YOHANA
20:29, 1PETRO 1:8, 2WAKORINTHO 5:7. Kuchora, kutengeneza senema za mkanda
wa maigizo ya Yesu n.k, ni uongo na kumzarau Mungu na kumvunjia heshima. Nani
ataondoa uovu na takataka hizi za uchafu? Nabii wa Mungu Ellen G. White
anasemaje kuhusu mapicha yanayochorwa kwenye vitabu, picha za Ukatili wa Kirumi
na mateso. Ondoa picha za Kikatoliki kwenye vitabu vyetu “CW 172:1”
Picha
ya Yesu-CW 171:2-3, 175:4 “Hakuna maonyesho ya kutisha, weka nje
vitabu vyenye vielezo vya picha za Kikatoliki za Mateso na kuchomwa moto.
Inatosha kusoma juu ya matendo haya maovu bila kujaribu kuyaleta katika maelezo
yao yote mabaya mbele ya macho”. Barua 28, 1897 CW UK. 172 aya 1.
“Usahihishaji
ni muhimu, je hatupaswi kufanyia uchunguzi kuhusu suala la kuonyesha vitabu
vyetu kwa kaisi kikubwa? Je, akili haingekuwa na maono wazi kikamilifu Zaidi ya
Malaika, Kristo au kitu chochote cha Kiroho, ikiwa hakuna picha
zilizotengenezwa kuwakilisha vitu vya mbinguni? Picha nyingi zilizotengenezwa
ni za uongo kabisa. Je, picha ambao zipo mbali na ukweli hazitoi sauti ya
uongo? Tunatakiwa kuwa wa kweli katika uwakilishi wetu wote wa Yesu Kristo
lakini maandishi mengi ya kusikitisha yaliyowekwa kwenye vitabu vyetu na
majarida ni mashtaka kwa umma”. BARUA YA
145, 1899-CW 171.2.
“Mifano inayofaa, mawazo ya wengi
katika kurejea mambo yanayohusu kazi ya Mungu ni ya bei rahisi sana. Katika
uteuzi wa picha kuonyesha mambo matakatifu ni upungufu wa hekima umeonyeshwa
kuwa Mungu hawezi kuubali”. Barua ya 39, 1899 CW 171 aya 3.
“Ndugu
zangu, je hamtalipa kundi la Mungu mkate, na sio jiwe? Kamwe usichapishe katika
majarida yetu neni ambalo litashusha kiwango ambacho Mungu anatarajia watu wake
wakutane. Msimwite mtu yeyote mwenye kipaji ambaye hana hekima ya kumchagua
Bwana Yesu Kristo, mwanga na uzima wa ulimwengu, ubora wa mtu huamuliwa na
umiliki wake na fadila za Kristo kwa wanadamuwenye dhambi. Ukweli lazima uwekwe
mbele ya watu. Kiwango cha usafi, kiasi cha utakatifu lazima kiinuliwe CW, UK 175 aya 4.”
Ondoeni
mapicha ya sanamu za kikatoliki kwenye vitabu “2WAFALME 21:1-6, 11-15”, matengenezo yanahitajika kwenye kila
msimamo wetu wa Imani “2WAFALME 23:1-14”.
Kwani hasira ya Bwana imewaka juu ya watu wake waabuduo sanamu. MATENDO 17:16 “Paulo alipokuwa
akiwangojea huko Athene na kuona jinsi mji ule ulivyo jaa sanamu roho yake
ilichukizwa sana ndani yake.” “KUTOKA
32:19 Hata alipo yakaribia yale malango akaiona ile ndama na ile michezo.
Hasira ya Musa ikawaka, akazitupa zile mbao mikononi mwake akazivunja chini ya
mlima. Akaitwaa ile ndama waliyoifanya akaichoma moto, akaisaga hata ikawa
mavumbi, akinyunyuzia juu ya maji akawanywesha wana wa Israeli.”
MJADARA KUHUSU KANUNI YA KANISA
Loughborough
alipendekeza kwamba kama ndivyo ilikuwa, walikuwa wakifuatisha makanisa mengine
kwa kujenga nyumba za mikutano. Alisema, “Tunayaita makanisa Babelii sio kwa
sababu wamefanya agano ili kumtii Mungu.” Alirejea nakala ambayo alikuwa
ameandika kwa tathmini ambayo aliitangaza: 1BIO
453.1
Hatua ya kwanza ya uasi ni kuwa na kanuni ya Imani, ikituambia tuamini
nini. Hatua ya pili ni kuifanya kanuni hiyo kuwa kipimo cha ushirika. Hatua ya
tatu nikuwajaribu washirika kwa kanuni hiyo. Hatua ya nne kuwashutumu kama
wazushi wale ambao hawa amini kanuni hiyo. Na hatua ya tano, kuanza mateso
dhidi yao. 1BIO 453.2
Ninahisi
kwamba hatufanyi kulingana na makanisa kwa maana yoyote isiyo na sababu katika
hatua iliyopendekezwa.-Ibid.1BIO 453.3
Cornell
hakuona kwamba kukubali agano kama hilo ilikuwa nikufanana makanisa Kisha James
White alitoa taarifa ya kina na muhimu:
Nathibitisha,
si kwa yale ambayo ndugu wasema, kwa maana nilikuwa nimeshawishika hapo awali.
Ningependa kusema nao sasa kuunga mkono azimio hilo. Napendelea kwamba ndugu
wanapaswa kuwa kitu kimoja katika jambo hili. Hii ingeleta umoja katika kanisa.
Hebu tuweke mfano sahihi hapa, na tuache uende nje ya mkutano huu. Hii ndio
sababu moja kwanini nitapigia kura azimio hili 1BIO 453.3
Kuhusu
mada ya kanuni za Imani, nakubaliana na ndugu loughborough. Sikupima vidokezo
ambavyo amewasilisha, kama vile nilivyoanza kuchunguza mada hiyo mwenyewe.
Katika WAEFESO 4:11-13, tunasoma,
“Naye alitoa wengine kuwa mitume, na wengine kuwa manabii, nakadhalika.” Hapa
tunakarama za kanisa zilizotolewa. 1BIO
453.6
Sasa
ninachukua msingi kwamba kanuni za Imani zinasimama kinyume kabisa na karama.
Hebu tufikirie: Tunapata kanuni, ikisema tutakavyoamini juu ya jambo hili na
lile, na tutafanya nini kwa kuzingatia jambo hili na lile, na tuseme tutaamini
karama hizo pia. 1BIO 454.1
Chukulia Bwana, kupitia karama ametupatia nuru mpya haikuendana na
kanuni yetu, basi, ikiwa tunabaki thabiti katika karama, inapinga kanuni yetu
mara moja. Kufanya kanuni ni kuweka vigingi na kuzuia njia ya maendeleo yote ya
baadaye. Mungu aliweka karama kanisani kwa lengo kubwa na zuri, lakini watu
ambao wamemiliki makanisa yao, wamefunga njia au wamejiweka nje ya njia
za… Mwenyezi. Sawa nakuwa wanasema
kwamba Bwana asifanye chochote Zaidi ya kile ambacho kimewekwa kwenye kanuni.
1BIO 454.2
Kanuni na karama zinapingana moja kwa moja.
Sasa msimamo wetu kama watu ni upi? Biblia ndio kanuni yetu. Tunakataa kila
kitu chenye kanuni za kibinadamu. Tunachukua Biblia na karama za Roho;
tukishilia Imani kwamba Bwana atatufundisha mara kwa mara. Na katika hili tunachukua msimamo dhidi ya utengenezaji wa kanuni.
Hatuchukui hatua moja, katika kile tunacho kifanya, kulekea kuwa Babeli.-1BIO
554.3
Hakuna kosa kama hili la Kanisa la
Wasabato chini ya General Conference kuunda kanunu ya Imani kinyume kabisa na
Biblia na Roho ya Unabii. Kanuni au muongozo ni mawazo ya nadharia ya viongozi
wa juu na huwa zinasahihishwa au kuboreshwa kila baada ya miaka mitano. Neno la
Mungu limejitosheleza na hakuna mwanadamu mwenye ruhusa kuliboresha au
kulirekebisha, kanuni za Kanisa au makanisa huwa zinaborehswa kulingana na
mitazamo ya viongozi wa kanisa kulingana na matakwa yao. “Kila neno la Mungu
limehakikishwa; yeye ni ngao yao wamwaminio. Usiliongeze neno katika maneno
yake; asije akakulaumu, ukaonekana u mwongo. METHALI 30:5-6, UFUNUO 22:18,
K/TORATI 4:2”
“Katika ulimwengu unaodaiwa kuwa wa
kikristo wengi hukataa mafundisho ya wazi ya Biblia na kujenga Imani kutoka
katika kanuni za mawazo ya kibinadamu na hadithi za kupendeza, na wanaelekeza
kwenye mnara wao kama njia ya kupanda juu mbinguni… IKIWA WALE WANAODAIWA KUWA
WAFUASI WA KRISTO wengekubali kiwango cha Mungu, ingewaleta katika umoja;
lakini maadamu hekima ya mwanadamu imeinuliwa juu ya neno lake takatifu,
kutakuwa na mafarakano. Machafuko yalipo ya Imani na madhebu yanayopingana
yanawakilishwa vyema na neno Babeli, Ambayo ni unabii (Ufunuo 14:8; 18:2)
inatumika kwa makanisa yanayopenda ulimwengu wa mwisho.” Patriarchs and
Prophets UK 124 aya 1
WACHUNGAJI WA MISHAHARA.
“Mtu
wa mshahara wala si mchungaji ambaye kondoo si mali yake humwoma mbwa mwitu
anakuja akawaacha kondoo na kukimbia, na mbwa mwitu huwakamata na kuwatawanya.
Yule hukimbia kwa kuwa ni mtu wa mshahara; wala mambo ya kondoo si kitu kwake”.
YOHANA 10:12-13, EZEKIELI 34:1-10,
YEREMIA 23:1-4, ZEKARIA 11:15-17, MALAKI 2:1-3.
“Kristo
mchungaji mkuu amewaachia watumishi wake waangalizi wa kundi lake kama wachungaji
wasaidizi; na anawataka kuwa na majukumu matakatifu kwa kazi aliyowaachia
amewaamuru wawe waaminifu, kulinda kundi, kuwatia nguvu wanyonge, kuwaamsha
waliozimia na kuwakinga wasiliwe na mbwa mwitu. Ili kuwaokoa kondoo hawa Kristo
aliutoa uhai wake na anawaelekeza wachungaji wake katika upendo aliowaonyesha
kama mfano kwao. Lakini “aliye wa mshahara; ambaye kondoo siyo mali yake,” hana
nia ya kweli kwa kondoo. Anatumika kwa ajili yakupata faida na anajijali yeye
mwenyewe, anaangalia matwakwa yake tu. Badala ya kuangalia matwaka ya kundi na
wakati wa hatari, atakimbia na kuliacha kundi.” WAZEE NA MANABII UK 172-173 (191P.1-4):1 PETRO 5:2-3. TIMOTHEO 3:3 TITO
1:7, KUTOKA 18-21. Kwa wale wote
walioitwa na kristo kumtumikia yeye katika kazi yake ya wokovu. Hakuwa ahidi
mshahara wa aina yeyote kama malipo.
“Kristo alipowaita wanafunzi wake wamfuate,
hakuwatumainisha kwamba watapata cheo na sifa katika maisha haya. Hakuwahidi
mapato wala heshima, wala wao hawakuweka masharti juu ya mambo ambayo walitaka
kuyapata. Mathayo alipoketi forodhani, mwokozi alimwambia;
“Nifuate. Akaacha vyote, akaondoka,
akamfuata.” (MATHAYO 9:9, LUKA 5:27-28) Mathayo
hakungoja na kudai mshahara kadri ya ule alioupata katika kazi yake kama mtoza
ushuru, ndipo amfuate yesu, mara moja pasipo kuuliza neno lolote wala
kusitasita. Kuwa pamoja na mwokozi apate kuyasikia maneno yake na kushirikiana
naye katika kazi yake, ndiyo mambo yaliyomtosha. Vivyo hivyo na wale wanafunzi
walioitwa mwanzoni. Yesu alipomwambia petro na wenzake ili wamfuate wakaviacha
vyombo na nyavu zao mara. Wengine
walikuwa na jamaa waliowatazamia kwa riziki zao; lakini waliposikia mwito wa
mwokozi, hawakusitasita na kuuliza nipateje riziki na nitawezaje kuwasaidia
jamaa zangu? Waliitikia mwito huo na baadaye Yesu alipowauliza, “Je?
Nalipowatuma hamna mfuko wala mkoba, wala viatu, mlipungukiwa na kitu?”
Waliweza kusema “LA?” LUKA 22:35,
WAJUMBE WA KRISTO UK 31P.1-2, HUDUMA YA UPONYAJI UK 479 P.3-4: SURA 40, TUMAINI
LA VIZAZI VYOTE UK 147P.4-5 SURA 28 DA (DESIRE OF AGES) UK 273P. 2-6 SURA 28
Wachungaji wote wanaofanya kazi na
huku wanalipwa mishahara, Hawamtumikii MUNGU. Bali MUNGU wao ni tumbo: WAFILIPI 3:18-19 “Maana wengi huenenda,
ambao nimewaambieni mara nyingi habari zao, na sasa nawaambia hata wa machozi, kuwa
ni adui za msalaba wa kristo; mwisho wao ni uharibifu mungu wao ni tumbo,
utukufu wao u katika fedheha yao waniao mambo ya duniani. ”, WARUMI 16:17-18,
MIKA 3:5 “Bwama asema hivi katika
habari za manabii wanaowakosesha watu wangu; hawa waumao kwa meno yao, na
kulia, Amani; na mtu awaye yeyote asiyetia kitu kinywani mwao, wao humwandalia
vita.”
“Tofauti kubwa kati ya roho ya watu
waliotengeneza maskani jangwani na wale waliojenga hekalu la sulemani,
inatufundisha fundisho muhimu watu waliojenga hekalu ambao walikuwa wakitufuta
faida yao wenyewe walikuwa na tabia iliyo ya watu wengi leo, ambao hujipenda
nafsi zao tu, wenye kutafuta vyeo na mishahara mikubwa. Roho yakujitolea kwa
hiari kufanya kazi kama ile iliyoonekana wakati wakutengeneza maskani imeadimika
mno hasa. Lakini roho ya namna hiyo ndiyo inayotakiwa wafuasi… wa wakristo kuwa
nayo. Bwana wetu ametuonyesha mfano wa jinsi ipasavyo wanafunzi wake kufanya
kazi. Kwa wale wanaowaita na kusema kwamba: “nifuateni, naminitawafanya kuwa
wavuvi wa watu,” Hakuwa ahidi mshahara wa aina yeyote kwa ajili ya kazi yao.
Yawapasa kushiriki kijikana kwake na kujinyima.” MANABII NA WAFALME UK 32P.3, SURA 4, UK 29P.3, PROPHETS AND KING UK
64P.3 SURA
Hiramu
alikuwa mfalme wa Tiro na alikuwa mjuzi wa kazi ya ufundi stadi za kuchora.
Hiramu alizaliwa na wazazi mchanganyiko (mama yake alikuwa mwisraeli wa kabila
la dani, Baba yake alikuwa mtu wa Tiro) Hakuwa na sifa njema ndiyo sababu ya
yeye kufanya kazi kwa kudai mshahara. Kitendo cha kuchanganya mafundi wa
Israeli na mafundi wa kutoka Tiro kulileta chachu mbaya kwa wajenzi kutaka
mshahara, walidai mishahara mikubwa. 1FALME
5:1-2, 6
“Hivyo,
aliyekuwa msimamizi wa wafanyakazi wa Sulemani, alikuwa mtu aliyekuwa akifanya
kazi kwa kujitumikia mwenyewe. Hakumtumikia Mungu. Kwa moyo ya kujinyima.Yeye
alimtumikia mungu wa dunia hii, yaani mali. Makusudi ya maisha yake yote
yaliongozwa na kujipenda nafsi. Kwa ajili ya ufundi wake mkubwa, Hiramu alidai
mshahara mkubwa sana mwishowe hali yake ya uroho wa fedha iliwaambukiza wenzake
pia. Kwa vile walivyokuwa wakifanya kazi pamoja kila siku na kulinganisha
mshahara wake na mishahara wao, mwisho hata wao wakapotoka, wala hawakuhesabu
kazi yao kuwa ni kazi takatifu. Roho ya kujinyima ikawatoka na badala yake
wakawa na roho ya uroho wa fedha. Matokeo yakawa kudai mishahara mikubwa,
ambayo walipewa. Hivyo basi mvuto mbaya huo ulienea katika sehemu zote za kazi
ya Bwana, hata kuenea popote katika ufalme wake. Mishahara mikubwa uliyodaiwa
na kupeana iliwafanya watu wengi waishi maisha ya anasa sana na starehe. Watu
maskini walionewa na matajiri; na roho ya kujinyima ilitoweka kabisa haki hii
ya upotevu, iliyoenea pengi sana; mtu ambaye apo mwanzo alikuwa miongoni mwa
wenye hekima yakutisha, aliyewapita wote, na sasa amekuwa Mwaasi”. MANABII NA
WAFALME UK 31P.4-3 2P.1-2 UK 28P.3-5, ISAYA 56:10-12, PROPHETS AND KINGS UK
63P.3-64P.2 SURA 4
Wale
wanaolipwa leo na kudai mishahara wanafuata roho ile ile ya Hiramu. Badala ya
kufuata tabia ya Yesu na mitume wake na ile ya wale waliojenga hema Kule
jangwani. Mungu anaitaji watumishi waliojitoa wakfu na kujikana nafsi. MATHAYO 16:24-29, 10-38, LUKA 9:23. “Akawaambia wote, mtu yeyote akitaka
kunifuata, na ajikane mwenyewe, ajitwike msalaba wake kila siku, anifuate”
“leo
mwokozi anatuita sisi pia, kama vile alivyomuita Mathayo, Yohana, na Petro.
Naikiwa tumeguswa moyoni na upendo wake, hatutafikiri sana jambo la malipo na
ridhaa. Tutafurahi kuwa watendakazi
pamoja na kristo, na tutatumaini ulinzi wake bila hofu. Tukimfanya Mungu kuwa
nguvu zetu, tukifahamu dhairi wajibu wetu utupasao tutakuwa na moyo wa
kuwapendelea wengine kuliko mwenyewe tutaongozwa na nia iliyo bora ambayo
itatuinua hali ya moyoni tusiwe na nia yakutaka mambo afifu ya dunia hii.” WAJUMBE WA KRISTO UK 31P.3 SURA 8
“Wachungaji wa leo wanalipwa mishahara
kwa zaka wakisema wao ni makuhani. Makuhani na wachungaji ni huduma mbili
tofauti. HESABU 18:21-24 makuhani
walikaa hekaluni siku zote na hawakuwa na urithi wala mashamba wao walihudumu
hekaluni, wakati wachungaji wanamiliki nyumba na wengine ni wafanya biashara na
wanamiliki mashamba na magari n.k. Wakati wa huduma ya kikuhani makuhani
walikula zaka na matoleo yaliyotoka kwa waisraeli. Pia wale waliohudumu kwenye
madhabahu walikula vya madhabahuni. 1NYAKATI
9:32, KUTOKA 40:23 MARKO 2:25-6, LUKA 6:3-4, WALAWI 24:8-9.
Mtume Paulo aliposema watu wa madhabahuni
hula vya madhabahuni na watu wa hekaluni hula vya hekaluni 1Korintho 9:13 alimaanisha hivi wale wahubirio injili watakula
kutokana na hiyo injili yaani mtu yeyote anayeacha shughuli zake na kwenda
kuhubiri injili ni haki yake kupewa fedha ya nauli pamoja na ya mahitaji yake
mbalimbali. Na sivyo kama wengi wafanyavyo leo kwa kulipwa mishahara kila
mwezi. “Mchungaji wa mshahahara si mchungaji” YOHANA 10:12,1KORINTHO 9:14-17, LUKA 10:14-7
“Bwana anatamani watoto wake kutenda
kwa njia hiyo ya kujikana, ya kujitolea ambayo itakuletea kuridhika. Kwa kuwa
tumetimiza wajibu wetu vizuri kwa sababu ulikuwa ni wajibu. Mwana pekee wa
MUNGU alijitoa mwenyewe kwa kifo cha aibu pale msalabani, na je tunapaswa
kulalamika kwa dhabihu ambazo tumeitwa kuzitoa? 2SM UK206P.1 SURA 25. “Maana
japokuwa naihubiri injili, sina la kujisifia; maana nimewekewa sharti; tena ole
wangu nisipoihubiri injili! Maana nikitenda kazi hii kwa hiari yangu
ninathawabu; ila ikiwa si kwa hiari yangu, nimeaminiwa uwakili basi thawabu
yangu ni nini? Ni hii, yakuwa nihubiripo, nitaitoa injili bila gharama bila
kutumia kwa utimilifu uwezo wangu nilio nao katika injili 1WAKORITHO 16:19”.
Zaka
ni ya Bwana kwaajili ya wale wahubirio injili, na siyo yakuwalipa mishahara
wachungaji. Wote wanaopeleka injili kwa ulimwengu. MATHAYO 28:19-21 wanapaswa kuhudumiwa kwa zaka na michango mbalimbali.
“Ni askari gani aendaye vitani wakati wowote kwa gharama zake
mwenyewe?”1WAKORITHO 9:7. Ukuhani wa leo ni upelekaji wa injili. “Lakini
nawaandikia kwa ujasiri Zaidi katika sehemu za waraka huu, kana kwamba
kuwakumbusha, kwa neema ile niliyo pewa na mungu, ili niwe muhudumu wa kristo
Yesu, katik ya watu wa mataifa, niifanyie injili ya Mungu kazi ya ukuhani
kusudi mataifa wawe sadaka yenye kibali ikiisha kutakaswa na Roho mtakatifu.”
WARUMI 15:15-16, 1PETRO 2:9-10
“Zaka ni ya Bwana, na wale wanaoiingilia
kati wataadhibiwa kwa kupoteza hazina yao ya mbinguni kazi isizuiwe kwa sababu
zaka… Mungu hajabadilika; zaka bado
inapaswa kutumika kwa wahubiri wa injili. TESTIMONIES FOR THE CHURCH
VOL.9:247-250, CS 102aya 4. Sura 21”
“Katika siku zijazo kazi yetu inapaswa
kupelekwa mbele kwa njia ya kujikana na kujitolea hata zaidi ya ile ambayo
tumeiona katika miaka iliyopita. Mungu anatutaka tukabidhi roho zetu kwake ili
afanye kazi kupitia sisi kwa njia nyingi. Najisikia sana juu ya mambo haya.
Ndugu zangu, natuenende kwa upole na unyenyekevu wa akili, nakuweka mbele ya
washiriki wetu mfano wa kujitolea ikiwatutafanya sehemu yetu kwa Imani Mungu
atafungua njia mbele zetu ambazo hazijatarajiwa.” 2SM 206P.3 SURA26
MWONEKANO UNAOFAA KATIKA KUOMBA
“Njoni,
tuabudu, tusujudu,Tupige magoti mbele za BWANA aliyetuumba” ZABURI 95:6 “Kwa nafsi yangu nimeapa
neno hili limetoka kinywani mwangu katika haki, wala halitarudi, ya kwamba
mbele zangu kila goti litapigwa, kila ulimi utaapa” ISAYA 45:23.
Katika
jambo hili Mungu ametoa msimamo kwa kila mwanadamu anavyopaswa kuja mbele zake.
Mfalme Daudi anatumia neno “Njoni tuabudu, tupige magoti mbele za BWANA”
alielewa kuwa Mungu anapaswa kuabudiwa kwa unyenyekevu. Maana ndio msimamo wa
wacha Mungu. Isaya naye amesema kile kile sawa na Daudi. Neno kupiga magoti ni
agizo la Mungu, maana amesema kila goti litapigwa mbele zangu, na kwenda
kinyume na utaratibu huo ni uasi.
Kielelezo
hiki cha kupiga magoti, kiliendelezwa na watakatifu, kizazi hadi kizazi Mtume
Paulo anasema. “Kumbukeni wale waliokuwa wakiwaongoza, waliowaambia neno la
Mungu, tena kwa kuuchunguza sana mwisho wa mwenendo wao iigeni Imani yao.” WAEBRANIA 13:7. Tuone mifano michache
ya watakatifu namna walivyo mwomba Mungu. Mtume Paulo anasema,
“Kwa
hiyo tena Mungu alimwadhimisha mno, akamkilimia jina lile lipitalo kila jina;
Ili kwa jina la Yesu kila goti lipigwe na vitu vya mbinguni, na vya duniani, na
chini ya nchi; na kila ulimi ukiri ya kuwa YESU KRISTO NI BWANA, kwa utukufu wa
Mungu Baba” WAFILIPI 2:9-11. “YESU ambaye ni jiwe kuu la pembeni EFESO 2:20 alipiga magoti akaomba” LUKA 22:41. Nabii DANIELI “Alipiga
magoti mara tatu kila siku akisali, akshukuru mbele za Mungu wake” DANIELI 6:10. EZRA kuhani “Na wakati wa
sadaka ya joini, nikainuka baada ya kunyenyekea kwangu Nguo yangu na joho yangu
zimeraruliwa, nikaanguka magotini nikainua juu Mikono yangu mbele za BWANA
Mungu Wangu”. SULEMANI Kiongozi, “Akasemama mbele ya madhabahu ya BWANA,
machoni pamkutano wote wa Israeli, akanyosha Mikono… akasimama juu yake,
akapiga magoti mbele ya mkutano…. 2NYAKATI
6:12-13, 1WAFALME 8:54.” MTUME PETRO: “Petro akawatoa nje wote. Akapiga
magoti akaomba” MATENDO 9:40.
STEFANO: “Akapiga magoti, akalia kwa sauti kuu” MATENDO 7:60. MTUME PAULO. “Alipokwisha kunena haya akapiga magoti,
akaomba pamoja nao wote.” MATENDO 20:36,
21:5
Linganisha
jinsi watu wa Mungu walivyofanya na ujiulize kile kinacho fanywa na makanisa ya
leo, na hata wewe mwenyewe. Swali wanaoomba hali wamesimama au kukaa agizo hilo
wamelitoa wapi? Jibu kuomba watu wamesimama, walirithi desturi ya mafalisayo
wapinzani wa Yesu. (Injili) MATHAYO 6:5-23:1-30. LUKA 18:9-12.
Nanyi mwaicha amri ya Mungu na kuyashika maagizo ya wanadamu. MATHAYO 15:6-12, MARKO 7:6-9, ISAYA 29:13
Hata
viumbe vya mbiguni husujudu “Na hao wenye uhai wanapompa yeye aketiye juu ya
kiti cha enzi utukufu… Ndipo hao wazee ishirini na nne… huanguka… nao
humsujudia yeye aliye hai huta... Milele na milele”… UFUNUO 4:8-11, ISAYA 6:3 “Na malaika wote walikuwa wamesimama pande
zote za kile kiti cha enzi, na za hao wazee na zale wenye uhai wane, nao
wakaanguka kifulifuli mbele ya kile kiti cha enzi, wakamsujudu MUNGU” UFUNUO
7:11
“Na
wale wazee ishirini na nne na wale wenye uhai wanne, wakusujudu wakamwabudu
Mungu”... UFUNUO 19:4, 5:6-8, 5:11-14
ROHO
YA UNABII
“Tukisali
katika chumba chetu, au kanisani, inatulazimu kupiga magoti. Mbele za Mungu.
Popote tuombapo ni haki kupiga magoti” MANABII
NAWAFALME UK 21
“Nimaepokea Barua nyingi zikiniuliza kuhusiana
na namna sahihi ya kuwa wakati wakutuo maombi kwa mkuu wa ulimwengu. Ni wapi
ndugu zetu wamepata wazo yakuwa wanaweza kusimama kwa miguu yao wakimuomba
Mungu? Mmoja amabaye alisoma kwa miaka takribani mitano katika Battle Greck
aliomba kuongoza katika maombi kabla dada White hajaanza kuongea na watu.
Lakini nilipo muona akisimama wima kwa miguu yake huku midomo yake ikiwa tayari
kupanuliwa ili amuombe Mungu, moyo wangu uliwaka ndani yangu ili nimkemee kwa
wazi. Nikimwita kwa jina lake nikisema” “Nenda chini katika mgoti yako.” Hii
ndyo inayotakiwa daima. Kama moyo upo tayari Kupokea somo hili ni la thamani
kujifunza.
Kupiga
magoti tunapo muomba Mungu, ndivyo tunavyopaswa kuwa wakati wote. Namna hii ya
Ibada ilihitajika kwa mateka watatu Wakiebrania waliokuwa Babeli... Lakini namna
hii ilikuwa heshima iliyopaswa kutolewa kwa mungu peke yake ambaye ni mkuu na
mtawala wa dunia na hawa vijana watatu Wakiebrania waliokataa kutoa heshima
kama hiyo kwa sanamu yoyote hata kama ilitengenezwa kwa dhahabu. Katika
kufanyia hivi katika haki na makusudi wangempigia magoti mfalme wa Babeli kwa
kukataa kutekeleza amri ya mfalme waliadhibiwa kwa kutupwa katika tanuru la
moto. Lakini kristo alikuja mwenyewe na kutembea nao katika moto nao hawakupata
madhara. Iwe katika hadhara au katika
Ibada za faragha nijukumu letu kupiga magoti mbele za mungu tunapopeleka
maombia yetu kwake. Hii huonyesha utegemezi wetu kwake… 2SM 310-315
Mpendwa
msomaji Mungu akusaidie, kufanya mabadiliko katika jambo hili usiendelee
kufanya kinyume na utaratibu wa Mungu na kama utaendelea kuomba umesimama au
kukaa, utambue kuwa hauna nafasi yoyote miongoni mwa wacha Mungu.
NEMBO MSALABA
Ishara
au alama ya msalaba (mti) ulitumiwa na mataifa ya kipagani kwa ibada za Miungu.
Historia inaonyosha jinsi makuhani wa Kimisri n.k walivyokuwa wakutoa heshima.
Wakati wa utawala wa Waajemi mti (msalaba) uliutumia kwa kuwanyonga watu mfano
ni ule wa Hamani kutaka kumnyonga Mordekai na kuwaangamiza Wayahudi wote
waliokuwa kule utumwani. Soma ESTER
5:13-14, 7:7-10. An Expository Dictionary of New Testament Words (London 1962
W.E.Vine Uk 265). “Kuabudu msalaba ilikuwa ni sehemu ya ibada ya Mungu
Tamuzi ukiwa katika umbo la T, au ya kifimbo ikiwakilisha herufi ya kwanza ya
jina lake”
The worship of dead (LONDON 1904)
Kanali J.Garnier UK 226
“Msalaba
katika umbile la Crux Ansta... ulichukuliwa katika Mikono ya makuhani wa
kimisri na walafme na maaskofu kuwa ufananisho wa mamlaka yao, wakiwa makuhani
wa Mungu jua waliitwa ishara ya uhai.”
Kwa
hiyo kuchora au kutumia ishara ya msalaba kwenye vitabu vyetu kwenye makanisa
na kwenye nembo. Ni kuendeleza ibada za kipagani.
“Sasa yesu aliwaambia wanafunzi wake kuwa maisha yake ya kujinyima” na
kimasikini ni kielelezo cha maisha ambayo lazima
waishi. Alisema: “Mtu yeyote atakaye kunifuata lazima
ajikane nafsi yake, ajitwike msalaba wake kila siku anifuate.” Msalaba ulikuwa
ikitumika katika utawala wa kirumi. Ulikuwa kitu cha uchungu sana, na kifo
chake ki1ikuwa cha ukatili kuliko vyote. Wahalifu walio husika kwa kifo cha msalaba iliwapasa
kujichukulia msalaba mpaka mahali pa kusulubiwa. Kila mara walipobebeshwa misalaba walifurukuta sana
na kutaka kuj iokoa. Maneno ya kristo kwa wanafunzi wake
ingawa waliyafahamu kigizagiza yaliwaonyesha mauti ya kritso"
“E.G. WHITE Tumaini uk. 236
“Msalaba
uliokuwa umetayarishwa kwa ajili
ya Baraba. ulitwishwa katika mabega ya yesu yaliyokuwa yakichuruzika damu. Wezi
wa Baraba waliopaswa kusulubiwa
pamoja naye nao walibebeshwa misalaba yao. Tangu alipokula pasaka pamoja
na wanafunzi wake, yesu alikuwa hajala wala kunywa chochote. Alikuwa amevumilia
uchungu wa kusalitiwa, na alishuhudia wanafunzi wake wakimwacha na kutawanyika. Alikuwa amepelekwa kwa Anasi.
Kwa Kayafa,
Kwa pilato, Kwa Herode na kurudishwa kwa
Pilato tena. Usiku ule wote palikuwapo tukio baada ya tukio kiasi cha kuweza kudhoofisha
roho ya mtu hadi kuzimia. Lakini Kristo hakushindwa. Alikabili fadhaa zote kishujaa. Lakini badaa kupigwa
mara ya pili na kutishwa msalaba hali ya kibinadamu haikuweza kustahimili
zaidi. Alianguka na kuzimia chini ya mzigo huo” “E.G. WHITE TUMAINI UK. 420.
Desturi ya kuweka
misalaba kama Nembo ilirithiwa
na kanisa la Roma. Wao huvaa msalaba shingoni, madhabahuni, makaburini kila
mahali wanautukuza msalaba (mti) pia na makanisa ya Kiprotestanti yamefuata
mfano wa Roma
kwa kuweka ishara ya msalaba
kwenye makanisa yao n.k. “Kama mama ya mtu alivyo ndivyo alivyo na binti
yake EZEKIELI 16: 44 wanatumia msalaba
kama Nembo ya ukristo huo ni uongo ishara au alama ya ukristo ni tabia MATHAYO 5:14-16, 2WAKORITHO 3:1-3 MATENDO
11: 24 -26
Wayahudi wakati wa kristo ... hali kadhalika warumi
hujidai kuwa wanautukuza msalaba. Huweka msalaba kila mahali:makanisani,
madhabauni, kwenye mavazi n.k. klla mahali wanautukuza msalaba kijuju. Lakini mafundisho ya kikristo wakiyazika
chini na kuyainua mapokeo ya bure ya kibinadamu “E.G.WHITE PAMBANO KUU UK. 323 – 324”
Shetani hunasa watu wengi kwa njia ya
kuwaunganisha pamoja na maadui za Mungu, au msalaba wa krisio. Muungano huu unaweza kuwa
wa kuzaliwa, kuoana, au urafiki.
watu wa namna hii hawatamani kutimiza wajibu wao. E.G. WHITE PAMBANO KUU UK. 340”
Viongozi wa majeshi
ya kirumi walikusudia kutoa kipimo kizito kwa wayahudi ambacho
kingewafanya wasalimu amri mara moja. Mateka
walipigwa, wakateswa sana na kutundikwa mtini,
mbele ya kuta za mji. Kufuata bonde la Yehoshafati na kuendelea mapaka
mlima wa Golgota, misalaba mingi sana, ambako watu walikuwa wametundikwa
ilijazana tena. Hapakuwa na nafasi ya kupita kati yake. “E.G. WHITE PAMBANO KUU UK. 21 SURA 1.
Nabii “Ellen G. White Alionyeshwa msalaba ukiingizwa ndani ya kanisa la Wasabato.
“Usiku ule niliota kwamba nipo Battle Greek nikiwa nachungulia nje ya
vioo mlangoni nikaona kundi linatembea kuja kwenye nyumba wawili wawili
walionekana wakakamavu na vanaojielewa. Nilikuwa na wafahamu vizuri nikawa
tayari kwa kuwapokea kwa kuwafungulia mlango.
Lakini wazo likanijia
nitazaine tena. Safari hii nikaona
kitu kingine. Sasa nikaona kanisa katoliki katika maandamano, mmoja ameshikilia
msalaba mkononi mwake na mwingine maagizo la kanisa lao. Nao walipo ikaribia wale
waliobeba maagizo ya kanisa wakafanya duara kuizunguka nyumba yetu
wakisema mara tatu nyumba hii haipaswi kuwepo mali zake zote lazima
zichukuliwe wameongea na kupingana na Kanuni yetu ya imani. Nilia machozi na
kufanya maombi nilipoona mali zetu zikichukuliwa.” 1T 578.
“Ulikumbuke kusanyiko lako,
ulilolinunua zamani ulilolikomboa liwe kabila ya urithi wako, Mlimani Sayuni ulioufanya
maskani yako. Adui ameufanya kila ubaya katika
patakatifu. Watesi wako wamenguruma
kati ya kusanyiko lako;wameweka bendera zao ziwe alama”. ZABURI 74:2-9
“Kwahiyo tokeni kati yao, mkatengwe nao, asema
Bwana, msiguse kitu kilicho kichafu, nami nitawakaribisha.” 2KORINTHO 6:17, ISAYA 52:11-12, EZEKIEL
12:1-5, YEREMIA 51:6 “Natoa mwito kwa wote ambao wameungana katika mwenendo wa
kanuni hizi mbaya, hufanya maamuzi ya matengenezo na kutembea kwa unyenyekevu
mbele za Mungu. Huu si upuuzi wala hadithi bali ni ukweli. Ninauliza tena ni
upande gani unaosimama? 1WAFALME 18:21 ikiwa BWANA ndiye MUNGU mfuateni, bali
ikiwa baali basi mfuate” 8T UK 68
KANISA
LA WA-ADVENTISTA WA SABATO (WANA MATENGENEZO)
KISASA, DODOMA, TANZANIA
0756959525, 0768315787, 0624141001,
0682,773384