USIWE NA MIUNGU MINGINE ILA MIMI
:KUTOKA 20:3
Katika kitabu cha Kutoka 20:1-17 ndipo pana Amri zote
kumi, hapo zimeandikwa kama mhutasari Je umewahi kufahamu kuwa Biblia yote ina
zifafanua amri hizi? Hebu twende pamoja
kwa moyo wa unyenyekevu, tuone angalau kwa ufupi, jinsi Biblia yenewe
inavyofafanua Amri ya kwanza. Pia zingatia ya kwamba ni vizuri tujifunze amri
hizi, tuzifahamu na kuzishika, maana kwakufanya hivyo, tutakuwa tumeanza
kuifahamu Biblia, na kubwa kabisa, tutakuwa tumefahamu kanuni ya kumpenda
Mungu; kama tunavyosoma:-
Kwa
maana huku ndio kumpenda Mungu, kwamba tuzishike amri zake.Wala Amri zake si
nzito. 1 Yohana 5:2-3.
Yeye aliye na Amri zangu, na kuzishika, yeye ndie
anipendae, naye anipendae atapendwa na baba yangu; name nitampenda
nakujidhirisha kwake” Yohana 14:21.
SWALI
Je kama mtu anaenda kanisani kila siku,
lakini hazishiki amri za Mungu je, Biblia inasema huyo niwa namna gani?
Yeye asemaye nimekujuwa wala hazishiki Amri
zake, ni mwongo, wala kweli haimo
ndazni yake. 1 Yohana 2:3 - 4
Hivi
kipimo cha kumtambua mtumishi wa Mungu mwaminifu ni nini?
Sikiliza Biblia yenyewe inavyosema.
“Nakatika hili twajua yakuwa tumemjua yeye,
ikiwa tunashika amri zake.1 Yohana 2:3
Umesikia ndugu
yangu, yakwamba kumpenda Mungu nikuzishika amri zake.Je unazishika? Zingatia
yakwamba mtu anadai kuwa anamjua Mungu lakini huyo anayesema hivyo ikiwa hazishki
wala kuzitii Amri (1) Nimwongo (2) Hata kweli ya neno la Mungu haimo ndani
yake. Kweli ni nini Yohana 17:17 ina sema kweli ni neno la Mungu. Tazama hata
na kipimo cha kumtatambua mtu wa Mungu mwaminifu ni njinsi huyo mtu anavyo
zishika amri za Mungu .
Huu ndio ukweli
ukiupenda ama usiupende utabaki kuwa ukweli wa milele.
Sasa
hebu tuanze amri ya kwanza.
“Mungu akanena
maneno haya yote akasema, Mimi ni Bwana, Mungu wako, niliyekutoa katika nchi ya
Misri katika nyumba ya utumwa, usiwe na Miungu mingine ila mimi Kutoka
20:1-3.
Unaweza kuwa na
swali, mbona sijawahi kuwa mtumwa mbona hatutawaliwi na Misri, na ukadhani amri
hii haikuhusu.Utumwa unaozungumzwa hapa niuitumwa wa dhamnbi.Ingawa hatukuwa
watumwa wa Misri lakini dhambi zile za misiri tumeshiliki kuzitenda, huo ndio utumwa
unaotajwa hapa.
“Lakini Mungu
ashukuriwe, kwa maana mlikuwa watumwa wadhambi, lakini mlitii kwa mioyo yenu
ile namna ya elimu ambayo mliwekwa chini yake; namlipokwisha kuwekwa huru mbali na dhambi,mkawa watumwa wa
haki”. Warumi 6:17-18
Sasa jambo lakujifunza katika amri hii, tunapaswa
tuchunguze tufahamu kwanini Mungu amekataza mwanadamu asiwe na Miungu mingine;.
SABABU
YA 1.
Umestahili wewe Bwana wetu na Mungu wetu,
hupokea utukufu na heshima na uweza; kwakuwa wewe ndiwe uliyeumba vitu vyote,
nakwasababu ya mapenzi yako vilikuwako, navyo vikaumbwa”. Ufunuo
4:11.
“Eee Bwana wa Majeshi, Mungu wa Israeli,
ukaaye juu ya Makerubi, wewe naam, wewe peke yako, ndiwe Mungu wa Falme zote za
dunia.Wewe ndie ulieziumba mbingu na nchi.
Isaya 37:16.
“Bwana Mungu akamfanya mtu kwa mavumbi ya
ardhi, akampulizia puani pumzi ya uhai; mtu akawa nafsi hai”. Mwanzo 2:7.
Sababu ya kwanza iliyofanya Mungu akataze
mwanadamu asiwe na Miungu mingine; ni kwasababu ndie alietuumba tena ndie aliviumba vitu vyote.
SABABU YA 2.
“Mtanifananisha na nani, nakunisawazisha
naye, na kunilinganisha naye, ili tuwe sawasawa? Isaya 46:5, 44:6.
Kumbukeni mambo yazamnai za kale; maana mimi
ni Mungu wala hapana mwingine; mimi ni Mungu, wala hapana aliye kama
mimi”. Isaya 46:9.
Mimi ni Alfa na Omega,Mwanzo na mwisho asema
Bwana Mungu, aliyeko na aliekuwako, na atakayekuja, mwenyezi . Ufanuo
1:8.
Sababu ya pili
iliyofanya Mungu akataze mwanadamu asiwe na Miungu mingine, nikwa sababu hakuna
Mungu mwingine alie kama yeye, hakuna wakumlinganisha nae, hakuna
wakumfanananisha nae. Zingine maandiko yanasema, aliyekuwako aliyeko na atakae
kuja. Maana yake ni wamilele, na ndio maana amri inasema, Usiwe na Miungu
mingine ila mimi.Je rafiki yangu huyu
ndie Mungu unaemwabudu? Kama ulikuwa haujamfahamu tafadhali anza sasa kumwabudu
mfalme wa uzima.
Amri hizi zote
huonyesha kanuni ya upendo.Amri yakwanza haiwezi kushikwa na yapili
kuvunjwa.Napenda tu tumpendavyo Mungu kadri iwezekanavyo, ndivyo itakavyo
wezekana kumpenda jirani bila upendeleo.Kristo aliwafundisha wasikilizaji
wake kuwa amri za Mungu niza muhimu
zote, wala hazitengani.Hakuna ya muhimu kuliko nyingine kumpenda Mungu
kutadhirika katika kuzishika amri zake zote.
Tumaini la vizazi vyote 340:
3 Elen
G. White
Hebu
tujifunze kidogo ukuu wake na kiti chake
cha enzi ndipo ujue huyu ndie Mungu anaestahli kuabudiwa:
Kiti chake cha enzi
na jinsi alivyo nabii yohana anasema:-
Namara nalikuwa
katika Roho natazama, kiti cha enzi kimewekwa mbinguni na mmoja ameketi juu ya
kile kiti; nay eye aliyeketi alionekana
mithiri ya jiwe la yasipi na akiki, na upinde wa mvua likuzunguka kile
kiti cha enzi, ukonekana mithili ya zumaridi.
Ufunuo 4:2 -3
Tuendelee
kuona kiti chake cha enzi.
“Katika
mwaka ule aliokufa Mfalme Uzia balimwona Bwana ameketi katika kiti cha
enzi, kilicho juu sana nakuinuliwa juu sana napindo za vazi lake zikalijaza
hekalu.” Isaya 6:1
“na katika kila
kiti cha enzi kunatoka umeme na sauti na ngurumo, nataa saba za moto zikiwaka
mbele ya kile kiti cha enzi, ndizo roho saba za Mungu.Nambele ya kiti cha enzi
kulikuwa na mfano wa bahari ya kioo, kama biurauli, nakatikati ya kile
kiti cha enzi, na pande zote za kile kiti, walikuwako wenye uhai wanne, wamejaa
macho mbele na nyuma .Ufunuo 4:5-6
Jinsi
alivyo –ukuu wake.
Kichwa chake kikoje, macho yake, Miguu yake
na sauti yake vikoje, sikiliza:-
“Kichwa chake na nywele
zake zilikuwa nyeupe kama sufu nyeupe,
kama theruji, na macho yake kama mwali wa moto, na miguu yake kama shaba
iliyosunguliwa sana. Kana kwamba imesafishwa katika tanuru; na sauti yake kama
sauti ya maji mengi.” Ufunuo
1:14-15.
Hebu tuendelee
kuchunguza katika neno lake, Mungu aliekataza mwanadamu asiwe na Mungu mingine,
ukuu wake ulivyo: sasa hebu tuangalie mwili wake, uso wake, macho yake, mikono
na miguu vikoje. Sikiliza neno linavyosema:-
Mwili wake pia ulikuwa kama zambarajadi safi,
na uso wake mfano wa umeme, na mamcho yake kama taa za moto, na mikono yake na miguu yake, rangi yake kama
shaba iliyosuguliwa sana, na sauti ya maneno yake kama sauti ya umati wa watu”. Daniel 10:6
Mungu ni mzee, maandiko yanasema ni
mzee wa siku hebu tuthibitishie hayo, tuangalie na mavazi yake nywele zake,
nakiti chake cha enzi jinsi kilivyo:-
“Nikatazama hata
viti vya enzi vikawekwa, na mmoja alie mzee wa siku ameketi; mavazi yake
yalikuwa meupe kama theruji, na nygwele za kichwa chake kama sufu safi; kiti
chake cha enzi kilikuwa miali ya moto, na gurudumu zake kama moto uwakao.” Daniel 7:9
Ni mavazi gani hayo ambayo ni meupe
kama theruji?.
“Umejivika
nuru kama vazi, umezitandika mbingu kama pazia” Zaburi
104:2
Hebu
tuchunguze Umri wake:-
“Tazama, Mungu ni mkuu, nasi hatumjui, hesabu
ya miaka yake haitafutiki” Ayubu 36:26
“Natena, wewe, Bwana hapo mwanzo uliitia
misingi ya nchi, na mbingu nikazi ya mokono yako, hizo zitaharibika, bali wewe
unadumu; nazo zote zitachakaa kama nguo, nakama mavazi utazizinga, nazo
zitabadilika; lakini wewe, u yeye Yule, namiaka yako haitakoma”. Ebrania 1:10-12
“Yehova, wa milele,
mwenye uwezo wakuwepo mwenyewe, ambaye hakuumbwa, yeye mwenyewe akiwa chanzo na
mpaji wa wote, ni yeye peke yake mwenye haki yakuheshimiwa na
kuabudiwa.Mwanadamu amekatazwa kutoa nafasi ya kwanza wa kitu au kiumbe
chochote katika upendo na utumishi wake.
Chochote kinachopelekea kupunguza upendo wetu kwa Mungu au kuingilia utumishi
wetu kwake, hicho tunakifanya kiwe Mungu” (Mwsingine).1 Wazee na manabii Uk 293 -294 E.G White.
Hebu sasa tuchunguze uwezo wake.
“Tazama, mimi ni Bwana, Mungu wa wote wenye
mwili; Je! Kuna neno gumu lolote nisiloliweza?. Yeremia
32:27
“Lakini Mungu wetu yuko mnbingni, alitakalo
lote amelitenda”. Zaburi 115:3
“Yesu akawakazia macho, akasema, kwa wanadamu
haiwezekani bali kwa Mungu sivyo: maana yote yawezekana kwa Mungu” Marko 10:27
Wala
hakuna kiube kisichokuwa wazi mbele zake, lakini vitu vyote vi utupu
nakufunuliwa machoni pake yeye aliye na mambo yetu”. Ebrania
4:14
“Ee Bwana,
umenichunguza nakunijua. Wewe wajua kuketi kwangu nakuondoka kwangu;
umelifahamu wazo langu tokea mbali. Umepepeta kwenda kwangu na kulala kwangu,
umeelewa na njia zangu zote.Maana hamna neno ulimini mwangu usilolijua kabisa,
Bwana. Umenizingira nyuma na mbele, ukaniwekea mkono wako.Maarifa hayo ni yaajabu, yanishinda mimi, hayadirikiki, siwezi kuyafikia. Niende wapi nijiepushe na roho yako? Niende wapi niukimbie
uso wako? Kama ningepanda mbinguni, wewe uko ningefanya kuzimu kitanda changu,
wewe uko. Ningezitwaa mbawa za asubuhi, nakukaa pande zote za mwisho wa bahari;
huko nako mkono wako utaniongoza, na mkono wako wa kuume utanishika. Kama nikisema, hakika giza litanifunika, na nuru inizungukayo ingekuwa
usiku; Giza nalo halikufichi kitu, bali usiku huangza kama mchana, giza na
mwanga kwako nisawasawa” Zaburi 139: 1- 12.
Rafiki yangu umeona
uwezo wa muumbaji wetu, yakwamba hakuna neno asiloliweza, analolitaka huko mbinguni
analitenda, yote yawezekana kwake, wala hakuna kiumbe kisichokuwa wazi mbele
yake.Angalia maandiko yanafafanua kwamba, hata kama mtu angeenda kuzimu, maana
leo kuna watu wanasikika kuwa wanaenda kuzimu, kupata nguvu ya miujiza, uongo,
na kupata utajirisho toka nguvu za giza,
neno linasema huko nako atakuona, huko nako mkono wake upo.Yakwamba niwapi
utaenda ujiepushe na uso wake hakuna.Huyu ndie Mungu anae sitahili
kuabudiwa.Nandio maana amri inasema;
“usiiwe na miungu mingine ila mimi”.
Je ufalme wake na kiti chake cha enzi vina
ukomo?.
Kiti chako cha enzi,Mungu niche milele na
milele, fimbo ya ufalme wako ni fimbo ya adili”. Zaburi
45:6.
Je! Wewe waweza kuuvumbua ukuu wa Mungu?
Waweza kuufikilia upeo wa huyo mwenyezi? Ni juu mno kama mbingu; waweza kufanya
nini wewe? Niwenyekina kuliko kuzimuni; waweza kujua nini wewe? Cheo chake
nikirefu kuliko dunia, nikipana zaidi ya bahari.Yeye akipita, na kufunga
watu, nakuwaita hukumuni, ni nani basi awezaye kumzuai?. Ayubu 11:7-10.
Mungu ni roho;
lakini ni nafsi, maana mtu aliumbwa kwa sura yake. Kazi ya mikono ya Mungu
kwenye viumbe si mungu mwenyewe.Viumbe vya asili ni ufunuo wa tabia ya Mungu; kwanjia
ya viumbe hivyo twaweza kuufahamu upendo wake; uwezo wake, na utukufu wake;
lakini haitupasi kuvihesabu viumbe kama ni Mungu.Akili ya kazi ya sanaa ya
wanadamu hutoa ustadi mzuri ajabu, vitu vinavypendeza macho, navitu hivi hutupa sisi wazo Fulani la fundi huyo
wasanaa. Lakini viumbe vikiwa ufunuo wa mawazo ya Mungu, siyo viumbe bali Mungu
alieviumba ambae hupaswa kutukuzwa”. 1 Kutayarisha njia Uk.86:2 Elen G. White
Huyu ndie Mungu anayestahili kuabudiwa .Na
ndiyo maana amri inasema”usiwe na miungu mingine ila mimi” .Hebu tunapoelekea
kumaliza somo letu tuangalie je leo mwanadamu anayekufa nakuoza anaweza kumuona
Mungu? Mtumishi wa Mungu Musa ambae maandiko yanasema alikuwa mpole kuliko
wanadamu wote dunian,aliwahi kusii aonyeshwe utukufu wa Mungu :Jibu alilopewa
Musa: Ndio jibu letu sote, sikiliza:-
MUSA
Akasema, nakusihi unionyeshe utukufu wako
Kutoka 33:18
Jibu
la Bwana
Kisha akasema, huwezi kuniona uso wangu,
maana mwanadamu hataniona akaishi”. Kutoka 33:20
Rafiki
yangu tunapomaliza somo letu zingatia yafuatayo:-
“Moyo
wangu na uwe mkamilifu katika amri zako nisije mimi nikaaibika” Zaburi 119:80
“Ee
Bwana, unifundishe njia ya amri zako, name nitaishika hata mwisho Zaburi 119:33
“Wokovu
umbali nawasio haki, kwa maana
hawajifunzi Amri”. Zaburi 119:155
“Lakini
mtu mbaya akighairi, nakuacha dhambi zake zote alizozitenda. Nakuzishika amri
zangu zote, nakutenda yaliyo halali na
haki, hakika ataishi, hatakufa”. Ezekieli 18:21
“Mkinipenda mtazishika amri zangu” Yohana 14:15
“Mpaka mbingu na
nchi zitakapopita, yodi moja au nukta moja ya torati haitondoka, hata yote
hatimae”.Jua liwakalo na nchi isimayo imara nimashahidi wa Mungu kwamba sheria
yake n yamilele.Hata kama mbingu na nchi zitapita, lakini sheria ya Mungu
itadumu.Kawaida ya mfano kwamba Yesu nimwanakondoo wa Mungu, itapita wakati
wakifo cha Yesu, lakini Amri za Mungu
zitadumu kama kiti chake enzi
kidumuvyo” Tumaini la vizazi Uk.
166:3
(Elen
G. White).
Mpendwa msomaji endelea kufuatilia makala hii na Mungu akubariki AMINAAA!!!!!!
ITAENDELEA.
Mpendwa msomaji endelea kufuatilia makala hii na Mungu akubariki AMINAAA!!!!!!
ITAENDELEA.
KWA MAWASILIANO ZAIDI WASILIANA NASI
0756959525,0752164685
0756959525,0752164685
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni