Katika blogu hii, tutachunguza njia mbalimbali za kuimarisha ufahamu wetu wa Biblia. Tutajadili mbinu za kusoma Biblia kwa ufanisi, vidokezo vya kukariri maandiko matakatifu, na mikakati ya kutumia somo la Biblia katika maisha yetu ya kila siku. Iwe wewe ni mtaalam wa Biblia mzoefu au unaanza tu safari yako ya imani, "Jifunze Biblia Zaidi" ni rasilimali kamili ya kukusaidia kuongeza ufahamu wako wa Maandiko Matakatifu na kumkaribia Mungu zaidi.

SERIKALI MOJA NA DINI MOJA





Alama ya mnyama inatajwa mara nyingi sana katika Biblia. Ni dhahiri kwamba wale wote watakaokuwa na alama hii hawataingia mbinguni Ufunuo 19:19-21 inaeleza hivyo. Ujumbe mkali kabisa unaosimama kinyume na alama hii unapatikana katika kitabu cha Ufunuo. Ni ujumbe unaotoka kwa Mungu na amb

ao watakaoukataa watakabiliwa na ghadhabu kali ya Mungu ambayo ndani yake hakutakuwa na rehema.

        Ujumbe huu unapaswa kutangazwa kwa mataifa yote, kabila, lugha na Jamaa na makutano. Kwani ni ujumbe utakao amua hatima ya kila mtu na kuigawa dunia katika makundi mawili. Kundi la kwanza ni wale wamwabuduo Mungu na kuzishika amri zake. Ufunuo 14:12, 19:10. Kundi la pili ni wale mwabuduo mnyama na sanamu yake na kuipokea chapa yake. (Alama). Ufunuo 13:8’

Mungu hawezi kufanya Jambo lolote bila kuwafunulia watumishi wake manabii siri yake, Mungu ametoa ujumbe wa onyo kwa wakazi wa dunia hii, Amosi 3:7. Jumbe hizi ni; ujumbe wa malaika wa kwanza ambao unawaalika watu kumwabudu MUNGU aliyeziumba mbingu na nchi, Ufunuo 14:6-7. Na ujumbe wa malaika wa pili hutoa Tangazo la kuanguka kwa makanisa na watu kama matokeo ya kukataa neno la Mungu na kushika mapokeo na desturi za wanadamu, ufunuo 14:8; Marko 7:7-8; Isaya 29:13, na ujumbe wa malaika watatu ni ujumbe unaotoa onyo kwa watu watakao mwabudu mnyama na sanamu yake, na kuipokea chapa yake (Alama). huu ndio ujumbe ambao Yesu alisema. “ Tena habari njema ya Ufalme itahubiriwa katika ulimwengu wote kuwa ushuhuda kwa mataifa yote; Hapo ndipo ule mwisho utakapo kuja:, Mathayo 24:14.    

“Na mwingine Malaika wa tatu, akafuata akisema kwa sauti kuu mtu awaye yote akimsujudia huyo mnyama  na sanamu yake na kuipokea chapa katika kipaji cha uso wake au katika mkono wake yeye naye atakunywa katika mvinyo ya ghadhabu ya Mungu iliyotengenezwa pasipo kuchanganywa na maji, katika kikombe cha hasira yake; naye atateswa kwa moto na kiberiti mbele ya malaika watakatifu na mbele ya mwanakondoo. Na moshi wa maumivu yao hupanda juu hata milele na milele wala hawana raha mchana wala usiku, hao wamsujudio huyo mnyama na sanamu yake na kila aipokeaye chapa ya jina lake”. ufunuo 14:9-11.

 

 

 

“Kisha nikaona mnyama akitoka katika bahari mwenye pembe kumi, na vichwa saba, na juu ya pembe zake ana vilemba kumi, na juu ya vichwa vyake majina ya makufuru.

 

Na Yule mnyama niliyemwona alikuwa mfano wa Chui, na miguu yake ilikuwa kama miguu ya dubu na kinywa chake kama kinywa  cha Simba, na Yule Joka akampa nguvu zake na kiti chake cha enzi na uwezo mwingi”. Ufunuo 13:1-2

 

 

73E27353                          

Ili kumuelewa mnyama huyu wa Ufunuo 13:1-10 ni lazima kwanza tujifunze historia na tabia za wanyama walio tangulia kuitawala dunia sifa zao na utendaji wao. Daniel 7:1-25 Falme zilizotawala kwa mfuatano, Nabii Yohana anamuona mnyama anatoka baharini.

1.   Mnyama alikuwa mfano wa Chui.

2.   Alikuwa na pembe kumi na juu ya pembe zake  ana vilemba kumi.

3.   Alikuwa na vichwa saba na majina ya makufuru.

4.   Alikuwa na kinywa  kama cha Simba

5.   Alikuwa na miguu kama ya Dubu.

6.   Joka akampa kiti chake cha enzi na uwezo mwingi .

Ni dhahiri kuwa mnyama huyu anakalia kiti cha shetani na ameundwa  na tabia za wanyama wa Danieli 7:1-17, 19-23.

Yapo mambo ya kuzingatia katika kujifunza unabii wa Biblia kitabu cha Danieli na Ufunuo

Mungu alitumia mifano na mafumbo kuwakilisha Historia na Unabi wa mambo yatakayotokea. Isaya 44: 7-8

“Ee Bwana, jinsi yalivyo makuu matendo yako! Mawazo yako ni mafumbo  makubwa. Mtu mjinga hayatambui hayo, wala mpumbavu hayafahamu. Zaburi 92:5-6

 

Tena nimenena na hao manabii, nami nimeongeza maono, na kwa Utumishi wa manabii nimetumia mifano” Hosea 12:10.

 

Unaposema kitabu cha Daniel na Ufunuo lazima uzingatie vidokezo ambavyo Mungu alivitumia kuwakilisha  masomo haya ya Unabii, wa mambo yaliyo kwishakutokea, yaliyopo na yatakayo tokea siku za mwisho mfano Danieli 7:8, Ufunuo 13-17 na Danieli 2:, Ufunuo 12: Mungu ametumia alama au vidokezo ili usikosee. Wanyama, vichwa, pembe , Bahari, Upepo haya ni mafumbo ambayo msomaji lazima azingatie ili kuuelewa maana yake. “Danieli akanena, akasema, Naliona katika maono yangu wakati wa usiku; na tazama, hizo pepo nne za mbinguni zilivuma kwa nguvu juu ya bahari kubwa. Ndipo wanyama wakubwa wanne wakatokea baharini, wote wanamna mbalimbali”  Danieli 7: 2-3

 

*    Upepo ni –Alama ya vita, mapinduzi. Yeremia 4:11, Danieli 11:40

*    Bahari  ni – Alama ya watu wengi mataifa mengi kabila lugha na jamaa. Isaya 17:12-13, Ufunuo 17:15.

*    Wanyama ni –Alama ya Ufalme, Dola. Danieli 7:16-17, 19,23

*    Pembe ni –Alama ya Mfalme .Ufunuo 17:12, Danieli 8:20-21

*    Vichwa  ni –Alama ya mfalme .Ufunuo 17:9-10

 

Utakuwa umeelewa kila ambacho Mungu anahitaji kutufundisha  kuhusu chapa ya mnyama na alama yake.  Mungu alitumia vielelezo na mifano ya wanyama kuwakilisha  tabia za wafalme watakao tawala dunia –hadi wakati atakapozikomesha  falme hizi za dunia na kuusimamisha ufalme wake utakao dumu milele na milele na watakatifu watarithi pamoja naye.Danieli 2:44-45, 7:27-28.

 

Kutumia wanyama wakali wa mwituni ni kuonyesha uhodari wa ufalme husika na mfalme  mtawala na aina ya mamlaka .Simba, Dubu, Chui, Mnyama wa kutisha na aina mbalimbali za wanyama. Kupitia tabia za wanyama hawa Mungu alikusudia kutuonyesha hasa tabia ya Mfalme husika na mamlaka yake. Katika kitabu cha Danieli 2 alitumia madini mbalimbali kuonyesha utajiri wa taifa husika na nguvu za kutawala .  Yeremia 5:6, Amosi 5:19, Mithali 30:30 , 20:2.

“Lakini mimi ni Bwana, Mungu wako tangu nchi ya Misiri; wala hautamjua mungu mwingine ila mimi;wala zaidi hakuna mwokozi mimi nalikujua katika jangwa, katika nchi yenye kiu nyingi . Kwa kadri ya malisho yao, kwa kadri  iyo hiyo walishiba; ndio sababu wamenisahau mimi.Basi nimekuwa kama simba kwao;  kama chui nitavizia njiani njiani; nitakutana nao kama dubu aliyenyang’anywa watoto wake ; nami nitararua nyama ya mioyo yao; na huko nitalalua  kama simba; huyo mnyama mkali atawararua.  Hosea 13:4-8. 

“Wangepaswa kujua mambo ambayo yatatokea kabla ya kufungwa kwa historia  ya ulimwengu”……

 

“Twapaswa kuona katika historia utimilizo wa unabii tujifunze utendaji wa Mungu katika mmavuguvugu makubwa ya matengenezo, na kufahamu maendeleo ya matukio katika upangaji wa safu  za  mataifa kwa ajili ya pambano la mwisho la vita kuu” – MATUKIO YA SIKU ZA MWISHO  UK 14

 

“Hebu sasa walinzi  (Wachungaji) wapaze sauti zao na kutoa ujumbe ambao ni ukweli wa leo kwa wakati huu. Hebu na tuwaonyshe watu mahali tulipo katika historia ya unabii”. MATUKIO YA SIKU ZA MWISHO UK 15.

 

Ujumbe wa Malaika wote watatu yapasa tuutawanye katika ulimwengu kwa njia ya uchapishaji (Vitabu na magazeti) na kwa njia ya mahubiri mbalimbali, tukionyesha kwa vielelezo, vyenye michoro ionyeshayo historia ya kiunabii mambo ambayo yalikwisha kutokea na yale yatakayotokea”.MATUKIO YA SIKU ZA MWISHO UK 82. 



73E27353
 

 

 

 

 

 

 

 

 


                                                                                   

 

 

Daniel 7:4, Hababuki 1:6-11. SIMBA

 

Wakati wa utawala wa Babeli ulifananishwa kitabia na mnyama Simba  uliotawala mwaka 605 KK-539KK. Utawala huu wa Babeli ulitawala dunia yote na ulikuwa na nguvu na ukatili kama wa simba, ulikuwa chini ya Mfalme Nebukadreza Yeremia 27:5-8, 4:6-7, 50:44 na  uliwakosesha watu na kuwafanya waabudu sanamu ya mfalme Nebukadreza  aliyo simamisha katika uwanda wa dura katika  Wilaya ya Babeli, na amri ilitolewa na Mfalme, watu waiabudu sanamu yake,  atakaye kataa, ataazibiwa vikali kwa kutupwa katika tanuri la moto uwakao.  Hii ndiyo njia iliyotumika kuwa ogopesha watu wasimtii Mungu wa Mbinguni na kuvunja amri zake, na wakati huo watu walivunja amri ya pili kwa kuabudu sanamu. Yeremia 51:7-8, Kutoka 20:4-6, M.Walawi 26:1, Danieli 3:1-7”.

Licha ya amri kuwa kali kwa mtu asiyeanguka na kuisujudia sanamu, vijana watatu walikataa kuisujudia sanamu ya Mfalme Nebukadreza na wakabaki kuwa watiifu kwa amri za Mungu, hao ndio waliokuwa washindi na masalio waaminifu wanao wakilisha washindi wa kipindi  cha  mwisho.Ufunuo 12:17, Ufunuo 14:12, 3:10. 73E27353

Vijana watatu washitakiwa mbele ya Mfalme kwa kutotii sauti ya Mfalme na kutojali au kuheshimu miungu yake hivyo walikabiliwa na shitaka. “Danieli 3:7-23.

 Mfalme alishangaa kuona watu wanne na wakati wao waliwatupa watu watatu na mmoja alikuwa mfano wa mwana wa Mungu huyo si mwingine ni Yesu Kristo, Mikaeli Kamanda wa vita alishuka kuja kuwaokoa watumishi wake waaminifu .Na ndivyo atakavyosimama kuwapigania watu wake waaminifu katika zamu hii ya mwisho Dan 12:1, Ufunuo 17:12-14.

Mwisho Mfalme alikili na kumheshimu Mungu wa Mbinguni, na akawaita wale vijana  watoke nje na wakatoka hali wakiwa wazima bila madhara yoyote .Hivyo ndivyo watakavyoitwa washindi  wa pambano la mwisho .Dan 3:24, Ufanuo 15:2. Ni heri kumtii Mungu kuliko mwanadamu Matendo ya mitume 5:29 .Pambano kuu liko mbele yetu ibada ya mnyama na sanamu yake na chapa yake je wewe utakuwa upande gani katika Pambano hili la mwisho?. Utawala wa Babeli ulifuatiwa na Wamedi na Waajemi.

Babeli ilikufa kwa sababu ya utajiri wake  ilimsahau Mungu, na ikasema utukufu wa mafanikio yake ni mafanikio ya mwanadamu4BC 1168;5

Daniel 2:37-42.”Uwakilishwaji wa Duara” “Picha iliyofunuliwa kwa Nebukadreza, wakati ikiwakilisha kuzorota (kudhoofika) kwa falme za dunia kwa nguvu na utukufu, pia inawakilisha vyema kuzorota (kudhoofika) kwa dini na maadili kati ya watu wa Falme hizi, kama mataifa yanamsahau Mungu kwa idadi sawa wanakuwa dhaifu kimaadili” 4BC 1168.4. Babeli iliangushwa na wamedi na waajemi

 

 

 

 

 

 

 

 






73E27353



 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 


Danieli 7:5   DUBU                            Danieli 8:1-4,20 KONDOO MUME

 

Wakati  utawala wa Umedi-Uajemi ulio fananishwa na mnyama katiri Dubu uliotawala mwaka 539 KK -331 KK. Mji wa babeli ulikuwa umejegwa juu ya mto frati na ilikuwa kazi kuuteka na ndipo wamedi chini ya Jemedari Dario na Waajemi chini ya Jemedari Koreshi, waliamua kuungana ili kuipiga babeli na kuiteka. Mbavu tatu katika kinywa cha dubu huwakilisha mataifa matatu ambayo ilikuwa ni lazima wayashinde ili watawale dunia.

Mataifa yaliyo wakilishwa na mbavu ni:-

1.   Makedonia  Filipi-Ugiriki 2. Babeli 3. Misri

 

Ili tuweze kuelewa Mungu alimfunulia Danieli kielelezo cha mfano mwingine. Kondoo dume mwenye pembe mbili, moja fupi na nyingine ndefu aliona ikisukuma upande wa Magharibi yaani Ugiriki na upande wa Kaskazini, Babeli yenyewe na upande wa Kusini Misri Danieli 8:4-20. kielelezo cha kondoo na Dubu vyote huwakilisha ufalme wa Umedi na Uajemi “Yule kondoo mume uliyemuona, mwenye pembe mbili,hizo ndizo wafalme wa Umedi na Uajemi” Danieli 8:20 .Mbavu tatu ni sawa na majimbo matatu au pande tatu za Dunia, Magharibi, Kaskazini na  Kusini.

Baada ya kuushinda utawala wa Babeli Isaya 13:15-22, 45:1-3, 44-27:28 Yeremia 51:11-14, 51:20-39, 50:33-44, Danieli 5:25-31, 7:5.Wamedi na Waajemi walipenda kuabudiwa na waliweka sheria ya kumwabudu Mfalme Dario kwa muda wa mwezi mzima siku 30.Dani 6:1-9. Hili lilikuwa jaribu kwa Danieli maana yeye alikuwa anatii amri za Mungu. Amri ya kumwabudu Mfalme ilikuwa kinyume kabisa na Imani yake Danieli 6:10  alikuwa na uelewa mzuri kuhusu amri ya kwanza. “Usiwe na miungu mingine ila mimi” Kutoka 20:3, Isaya 42:8, 48:11.  

Sheria ilipitishwa ya kuwaazibu wote watakao kataa kumwabudu Mfalme Dario   na kuabudu kwa Mungu mwingine isipokuwa Dario Mfalme wa umedi –Uajemi. Danieli 6:4-9.Katika kipindi hicho Danieli naye alisimama Imara na akawa mshindi kama wale walioshinda enzi za utawala wa Babeli wakati huo shetani alibadili mbinu badala ya kutumia tanuru la moto, alitumia Simba wenye njaa kali ili yule atakaye kataa kumwabudu Mfamle Dario atupwe katika tundu la Simba. Danieli  6:11-28 lakini Mtumishi wa Mungu Danieli hakuogopa vitisho, na Mungu alimuokoa na makanwa ya Simba wakali. Danieli 6:21 -22, Esta 3:1-6 Pia Danieli ni mfano wa watu watakao shinda  katika  siku za mwisho. Nabii Danieli alimsimulia Mfalme Dario wa Umedi mambo yatakayotokea siku za mwishoni mwa Historia ya Dunia, Mataifa yatakavyo pigana na kupinduwana hadi mwisho wa wakati.Danieli 11:1-45. Babeli kwa leo ni nchi ya Iraki, Umedi kwa leo ni nchi ya Siria, Uajemi kwa leo ni nchi ya Irani.

“Ufalme wa umedi na uajemi ulipatwa na ghadhabu ya Mbinguni kwa sababu katika ufalme huu sheria ya Mungu ilikanyangwa chini ya miguu, hofu ya Bwana haikupata nafasi mioyoni mwa watu, ushawishi uliotawala katika umedi na uajemi ulikuwa ni uovu, kufuru na ufisadi. 4BC 1168:6

“Falme zilizofuata zilikuwa na misingi mibaya zaidi, walidhoofika kwa sababu walitupa uaminifu wao kwa Mungu, walipomsahau walizama chini na chini katika kiwango cha maadili. 4BC 1168:7 Mkufunzi wa vijana (September 22, 1903) YOUTH’S INSTRUCTOR Septermber 22,1903

 

2D29044FDaniel 7:2-7 Ni alama ya Masihi mwana Kondoo. Daniel alipewa maono ya wanyama wakali, wanao wakilisha nguvu za dunia. Lakini ishara ya ufalme wa Masihi ni kondoo. Wakati falme za Kidunia zinatawala kwa Nguvu ya mwili, Kristo anapiga marufuku kila silaha ya mwili, kila kitendo cha kulazimisha. Ufalme wake ulitakiwa kuinuliwa ili kuinua na kukuza ubinadamu ulioanguka” LETTER 32, 1899.4BC 1171.5

 



91315BD9
 

91315BD9

                   

   KONDOO MUME NA BEBERU                                               CHUI

Danieli 7:6, Habakuki 1:5-11                              Daniel 8:1- 8, 11: 20-23

 

Utawala wa Umedi-Uajemi ingawa ulijitukuza sana na kupenda kuabudiwa nao haukudumu muda mrefu  mwaka 331 KK uliangushwa na taifa dogo lililofananishwa na mnyama Chui mnyama mwenye akili sana, na anayetumia mbinu katika mawindo yake .Danieli 7:6, “Nami nilipokuwa nikifikiri, natazama beberu kutoka upande wa Magharibi, juu ya uso wa dunia nzima bila kuigusa nchi; na beberu yule alikuwa na pembe mashuhuri kati ya macho yake. Naye akamuendea huyo kondoo mwenye pembe mbili niliyemuona akisimama karibu na mto, akamshambulia kwa ghadhabu za nguvu zake. Nikamuona akimkaribia kondoo mume, akamuonea hasira kali, akampiga kondoo mume akazivunja pembe zake mbili; na huyo kondoo mume alikuwa hana nguvu kusimama mbele yake; bali akamuangusha chini akamkanyaga kanyaga; wala hapakuwapo awezaye kumuokoa kondoo mume katika mkono wake” Danieli  8:5-8, 11:1-3 .Wagiliki chini ya Jemedari Alexanda mkuu waliuteka ulimwengu kwa haraka na kwa muda mfupi waliyashinda majeshi ya wamedi na Waajemi. Hawa waliamini elimu sana na masomo ya nadharia, Sayansi Nk. Mpaka leo ulimwengu unaharibiwa na falsafa zao. Hata katika vyuo vikuu na vyuo vya thiologia za dini vinaharibiwa   1Wakorintho 1:22. Wagiliki waliiharibu Dunia kwa kuwafanya watu wategemee elimu hata kama ni ya uongo. Historia za uibukaji wa mwanadamu kuwa alitokana na Sokwe kinyume kabisa na neno la Mungu. Mwanzo 1:25-27 ,2:7, 1:1 .Angalia  nadharia waliyo isababisha kwenye Taifa la Israeli kundi la mafalisayo na Masadukayo hawaamini ufufuo  .Walishindwa kuelewa ukweli kwa sababu ya nadharia. Mathayo 22:15-40

 

 

 

Daniel 8:8 “Na Yule beberu akajitukuza sana , na alipo kua na guvu, pembe ile kubwa ilivunjika  na badala yake zikazuka pembe nne mashuhuri zilizo elekea pepo nne za binguni”.

 

 

 

 

Daniel 8:21 “Na Yule beberu mwenye manyoya mengi  ni mfalme wa uyunani, na ile pembe kubwa iliyo kati ya macho yake ni mfalme wa kwanza”. Daniel 11:3 Na mfalme hodari atasimama atakaye watawala kwa mamlaka kubwa na kutenda apendavyo.

 

“Naye atakapo simama, ufalme wake utavunjika, na kugawanyika katika pepo nne za mbinguni; lakini hautakuwa wa uzao wake, wala hautakuwa kama mamlaka yake ambayo alitawala kwayo; kwa maana ufalme wake utang’olewa, hata kwa ajili ya wengine zaidi ya hao” Daniel 11:4.

 

Baada ya kifo cha Alexander mkuu aliyefananishwa na pembe ndogo iliyo katikati ya macho ya beberu. Ufalme wa uyunani uligawanyika katika pembe nne zilizo elekea pepo nne za mbinguni. Pepo nne huwakilisha vita vilivyo piganwa na majemedari wa uyunani wakigombania ufalme, mwisho waliamua kupatana na kuigawa dunia katika majimbo nne, na huo ulikua mwanzo wa kudhoofika kwa uyunani.

1.  Magharibi, ambayo ni Uyunani (Greece) alitawala jemedari cassander.

2.  Kaskazini, ambayo ni Uturuki, (Asia ndogo) alitawala jemedari Lysimachus.

3.  Mashariki, ambayo ni Ashuru, Shamu, Babeli, India alitawala jemedari Seleucus.

4.  Kusini, ambayo ni, Misri, Libya, Kushi na shamu ya kusini alitawala jemedari Ptolemy.

 

Katika mgawanyiko huo wa uyunani, polepole Rumi ilikuwa ikiinuka kwa nguvu kubwa kuitawala dunia, kutokea magharibi, Rumi, (Italia) na kuzishinda falme za Wayunani. Wayunani walishindwa  kupambana na Warumi. Matukio yote yaliyotabiliwa katika Daniel 8,11, yanawakilisha pia vita vinavyoendelea katika ulimwengu wetu leo.

Nuru ambayo Danieli aliipokea kutoka kwa Mungu, ilitolewa hasa kwa ajili ya siku za mwisho. Maono aliyoyaona katika ukingo wa ulai na Hedekeli, Mito mikubwa ya shinari, sasa yanaendelea kutimizwa, na matukio yote yaliyotabiliwa hivi karubuni yatatokea” LETTER 57, 1896,4 BC 1166.5.Danieli 8:1-

 

 

Danieli 7:7, 19-24, 8:9-12  MNYAMA WA KUTISHA

 

Ufamle huu wa nne  unaofuata ni wenye mamlaka makubwa zaidi, ambao katika sura ya pili ya Danieli 2 :40 ulifananishwa  na nguvu za chuma,  wenye ukatili, hauna mfano miongoni mwa wanyama walio fananishwa na ukatili wa Rumi  na mwenye hamu ya kumwaga damu. Ulitawala  tu baada ya kuwashinda Wayunani vitani, Mwaka 168 KK-476 BK. Rumi ya kipagani ndio Ufalme uliotawala sehemu kubwa ya Dunia kuliko mataifa

yaliyotangulia kutawala dunia.Danieli 7:7,  19-23,Luka 2:1-2, 3 :1, Matendo ya Mitume 27: 1-8

 

Yesu Kristo alisulubiwa na kuuwawa chini ya Utawala wa Rumi ya kipagani Yohana 19:14-15, 11:47-54,Mitume nao waliteswa na kuchinjwa na Rumi ya kipagani watakatifu walitupiwa kwa wanyama wakali,walitupwa gerezani, walipigwa kwa mawe,walikatwa kwa misumeno nk. Waebrania 11:33-39, Mathayo 27:11-18. Taifa la Wayahudi lilikuwa limeasi sheria za Mungu liliungana na serikali ya Rumi na kumuua Yesu nakuendelea kuwatesa Wanafunzi wake. Mathayo 10:17-28, Matendo ya mitume 12:1-2, Marko 3:6 ,Mathayo 22:16, 27:1-8, 28:11-14,  16:22.

 

Mambo ya kuzingatia kwa watu wanaoishi katika siku hizi za mwisho mambo yaliyotendeka yatajirudia tena. ”Yaliyokuwako ndiyo yatakayekuwako; na yaliyotendeka ndio yatakayotendeka; wala jambo jipya hakuna chini ya jua.

Je! Kuna jambo lolote ambalo watu husema juu yake, Tazama, ni jambo jipya? Limekwisha kuwako tangu zamani za kale zilizokuwa kabla yetu sisi” Mhubiri 1:9-10, “yale yaliyoko yamekuwako; na hayo yatakayokuwako yamekwisha kuwako naye Mungu huyatafuta mambo yale yaliyopita”. Mhubiri 3:15. Hali ya kuwatesa watu wa Mungu itarudiwa tena na mamlaka za Dunia kama ilivyokuwa kwa nyakati zilizopita .Ufunuo 6:9-11.      

 

Kwa kuwa shetani alilkuwa akitumia Serikali ya RUMI kuwaua watu wa Mungu, je ataiongoza serikali hiyo ikaketi  katika Kanisa la Mungu? HAPANA! Shetani akaona kuwa aingie katika Kanisa la Mungu, (Kupitia mawakala wake) ajifanye Mkristo, akaketi humo, aachane na Serikali, aanzishe DINI, ili apotoshe Kanisa la Mungu. Na hapo ndipo atakuwa ametimiza kiapo chake. Shetani aliongoza mawakala wake, waabudu sanamu, waabudu mizimu, wote wakaingia Kanisani. Hata mfalme aliyekuwa akitawala wakati huo (Katika utawala wa Rumi) aliyekuwa akiitwa COSTANTINE, aliingia Kanisani. 2Wathesalonike 2:2-4

 

“Kwa hiyo shetani alipanga vita kwa njia nyingine ya kufauru zaidi.Alisimamisha bendera yake katika Kanisa la Kikristo, ili kupata wakristo wadanganyifu, wenye hila, hivyo alifauru kuliko alivyotumia mateso. Badala ya mateso, akatumia vishawishi na heshima. Ibada ya sanamu ilikubaliwa kuwa  ni sehemu ya ukristo, na ukweli halisi ukakataliwa… katika vazi hili jipya la ukristo wa kujifanya, shetani alijipenyeza kanisani na kuchafua imani yao” (Pambano kuu sura 2. Uk 26:2-3).

 

“Uongofu bandia wa Mfalme Costantine ulileta burudiko kubwa Kanisani.Kwa hiyo sasa uharibifu ulizidi mno Kanisani”. (Pambano kuu sura 3, uk 30:2)

Kwa hiyo shetani aliichafua imani yao, lakini kumbuka kuwa mwanzoni walikuwa na imani ya kweli, walishika amri za Mungu na imani ya Yesu, lakini sasa amri za Mungu wamezikanyaga mavumbini na wakaruhusu ibada ya sanamu. Kwa hiyo sasa si Kanisa la Mungu tena, bali sinagogi la shetani. Ufunuo 2:13-14.

“Wakristo wengi baadaye walipotoka kabisa na kushusha hadhi yao.Mwisho muungano wa ukristo na umizimu ulifanyika. Ingawa waabudu sanamu walijidai kuungana na Kanisa, lakini walishikilia sanamu zao tu, ila walibadili sanamu zao ziwe mfano wa Yesu, na mfano  wa Maria, na watakatifu wengine. Wakaingiza mafundisho ya uongo”  (Pambano kuu sura 2, uk .26:4).

 

“Mfalme Costantine aliamuru kuwa, Jumapili iwe siku ya kupumzika katika Dola yake yote” . (Pambano sura 3, uk. 32:2)

Kwa hiyo Kanisa hili lililoanzishwa na Yesu mwenyewe pamoja na Mitume, likapotoka kabisa. Likaacha kutii amri za Mungu.Wakaanza kuabudu sanamu, nakujichongea sanamu za Bikra Maria, na za Yesu. Hata Sabato ya Mungu wakaacha kuitunza, wakatii agizo la Mfalme Costantine kutunza Jummapili. Wakasahau njia ya Mitume na manabii, maana wakati wa Yesu na Mitume, hawakuchonga wala kuabudu sanamu, hata Sabato ya Mungu ilitunzwa vizuri (Soma LUKA 4:16, 31, MATENDO 16:13). Lakini sasa wamepotoka.

 

“Wanafunzi wa kwanza walipomalizika na kulala makaburini, watoto wao pamoja na waongofu wapya wakafuata njia nyingine “ {Pambano kuu  sura 21; uk 222:3} .

Baada ya Kanisa kuasi watu wa kila aina waliingia Kanisani na kuendeleza mambo yao ya kipagani ndani ya kanisa bila kuacha. Waabudu sanamu, waabudu mizimu, wanywa pombe (walevi), kila aina sasa kanisa likawa la watu wote na mahali pote kwa wote. Hawakuitwa tena wakristo walichagua jina lingine ambalo ni  “KANISA LA KIRUMI KWA    WATU WOTE; =ROMANI CATHOLIC.

v ROMANI={RUMI} Ni serikali ya awamu ya nne iliyokuwa ikitawala.{Rome- Italy} DAN  7:7       

v CATHOLIC = Maana yake, ‘kwa wote, mahali pote.

Kwa hiyo wakapewa JINA LA ROMAN CATHOLIC

{FAHAMU :- ROMA, RUMI = NI KITU KIMOJA}

 

Kwa hiyo Kanisa la Romani Catholic  {au Rumi} lilianzia hapo mwaka wa 538 AD. Hivyo, utawala wa RUMI ukabadilika, toka Serikali ya RUMI, kuwa RUMI YA KIDINI. Soma kitabu Cha Historia ya kanisa vipindi vyake saba kilichoandikwa na F. PORTMANN UK 112:3                 

 

Katika karne ya sita upapa ulikuwa umeimarika kabisa. Kiti cha mamlaka yake kilikuwa kimewekwa katika mji wa Kifalme na askofu wa Roma alikuwa ametangazwa kuwa kichwa cha Kanisa lote. Upagani ulipewa nafasi katika Kanisa. Joka alikuwa amempa mnyama uwezo wake na kiti chake na mamlaka yake kuu, Ufunuo 13:2. Na sasa ikaanza miaka 1260 ya mateso ya upapa yaliyotabiriwa katika unabii wa Danieli na Ufunuo. Daniel 7:25; Ufunuo 13:5-7 Wakristo walilazimishwa kuchagua ama kuacha uaminifu na msimamo wao na kukubali taratibu na ibada ya upapa au maisha yao kupotelea katika magereza au kuuawa kwa kutumia kitanda cha kutesea, kuchomwa moto au kwa Shoka la Muuaji mkuu. Ndipo sasa maneno ya Yesu yakatimia kwamba! “Nanyi mtasalitiwa na wazazi na ndugu, na jamaa na marafiki, na baadhi yenu watawafanya muuawe nanyi mtachukiwa na watu wote kwa ajili ya jina langu” Luka 21:16; 17 Mateso yalianzishwa kwa watakatifu kwa ghadhabu kubwa mno kuliko wakati wowote hapo kabla, na ulimwengu  ukawa uwanja mkubwa wa vita. PAMBANO KUU .uk 50-51.

 

Hatuwezi kujizuia tusione uhusiano uliopo kati ya ile pembe ndogo ya Danieli ambayo habari zake zimetajwa katika sura ya 7 na ya 8 ya kitabu  hiki. Ile pembe ndogo ilikuwa na kinywa kilichonena maneno ya makufuru. Pia iliwatesa watakatifu wake aliye juu. Pembe hiyo ilisimama badala ya mamlaka ya upapa. Mnyama huyu pia anasimama badala ya ule uwezo wa papa, amekufuru na kunena maneno makuu kinyume na Mungu na isitoshe anaabudiwa kama Mungu na “Duniani anatambulika kama Mungu mwingine. Naye amefanya vita na watakatifu na historia inadhihirisha kwamba maelfu walikufa kwa ajili ya imani yao. Kanisa la Roma halitakataa kwamba liliwatesa watu ambao walikataa kuwatii. “Mnyama”. Ufalme wa kirumi ulipodhoofika kwa ajili ya kushambuliwa na wapagani katika siku za Costantine, kile kiti cha enzi cha utawala wa kirumi kilihamishwa toka mji wa Roma mpaka Costantinopole. Kwa njia hii ufalme wa Kirumi ulikitoa kiti chake cha enzi kwa mamlaka ya Kanisa la Roma. Mwaka baada ya mwaka, Wafalme walimpa papa uwezo mwingi zaidi na nguvu, na lile jumba la utawala wa kirumi lilichukuliwa na Kanisa. Ndiye “Mnyama” ambaye alipokea uwezo toka kwa yule Joka.Ufunuo 13:2.

 

 

 

 

 

 



2D29044F
 

 

 

 

 

 

 

 


Danieli 7:8   PEMBE NDOGO

 

 “Nikaziangalia sana pembe zake na tazama, Pembe nyingine ikazuka kati yao, nayo ilikuwa ndogo, ambayo mbele yake pembe tatu katika zile za kwanza zikang’olewa kabisa, na tazama, katika pembe hiyo mlikuwa na macho kama macho ya mwanadamu na kinywa kilichokuwa kikinena maneno makuu.  Na habari za zile pembe kumi zilizokuwa kichwani mwake, na ile pembe nyingine iliyozuka, ambayo mbele yake zilianguka pembe tatu, yaani pembe ile yanye macho na kanwa lilinena makuu ambayo kuonekana kwake kulikuwa hodari kuliko wenzake”. Danieli 7:8, 20

 

Kwanza kabisa, pembe ndogo ilijitokeza miongoni mwa pembe kumi ambazo ni   1. Uingereza,   2. Ujerumani   3. Ufaransa   4. Ureno     5. Hispania,  6. Italia,     7. Uswisi   8. Heruli,   9. Vandalis,  10. Ostrogoths.  Pembe  hii kijiografia ipo katika utawala wa ulaya magharibi. Pili, ilijitokeza baada ya kutokea  kwa zile pembe kumi, “Ilizuka kati ya hizo pembe” kwa kuwa zile Pembe kumi  ziliibuka mnamo mwaka 476 B.K. baada ya kusambaratika kwa rumi ya kipagani na kutokea mataifa kumi ya ulaya. Tatu, Pembe ndogo ingeanza utawala wake muda Fulani baada ya  kuzing’oa himaya tatu miongoni mwa zile kumi, wakati pembe hii ikiinuka kutawala. Aya ya nane inasema kuwa kabla ya pembe hiyo ndogo kutawala  Pembe tatu katika zile za kwanza zikang’olewa kabisa”. Nne, pembe ndogo ingekuwa na “Macho kama macho ya mwanadamu, na kinywa kilichokuwa kikinena maneno makuu “.  Hii huonesha kuwa mwanadamu ndiye angekuwa kiongozi wa utawala huu uliowakilishwa na pembe ndogo.  Tano, “atakuwa mbali na hao wa kwanza” (Aya ya 24). Hii inamaanisha kuwa pembe ndogo ingekuwa tofauti kabisa na falme zingine zilizotangulia ambazo zilikuwa za kisiasa. Sifa ya sita imeonyeshwa katika sehemu ya kwanza ya aya ya ishirini na tano .

Naye atanena maneno kinyume chake aliye juu Danieli 7:25 “atanena “Maneno ya makufuru”  (Ufunuo 13:5)

Alama ya mnyama inatajwa kwa mara ya kwanza katika kitabu cha Ufunuo 13:16 na   hiyo inaeleza sifa za mnyama huyo .

 

1.   Naye akapewa kinywa cha kunena maneno makuu ya makufuru. Ufunuo 13:5,6 2. Akapewa nguvu za kufanya vita na watakatifu na kuwashinda. Ufunuo 13:7 .3. Mnyama huyo ataabudiwa . Ufunuo  13:8 4. Ana chapa . Ufunuo 13:16 5. Anapokea kiti chake na uwezo mkuu toka kwa Joka .Ufunuo 13:2







2D29044F

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 


                                                                                                      

                                                                                                                               

    Pembe ndogo ni sawa na mnyama wa Ufunuo 13.    Ni mamlaka moja.

 

“Na habari za zile pembe kumi, katika Ufalme huo wataondoka Wafalme kumi, Danieli 7:24.

 

NINI MAANA YA KUKUFURU?

Maana ya kukufuru ni mwanadamu mwenye mwili wa kufa kusema yeye ni Mungu, na anasamehe dhambi za wanadamu wenzake na kujiita baba mtakatifu. Kuna mamlaka moja tu duniani imejitwalia majina ya Mungu na heshima yake

1.   Upapa umejiita Baba Mtakatifu duniani. PAPA NI NANI UK 22:2 na UK 26 soma kitabu cha Papa ni nani UK 9 – 10 CHEO CHA BABA MTAKATIFU. Biblia imesemaje kuhusu madai ya Upapa kujiita baba mtakatifu “Wala msimwite mtu baba duniani; maana Baba yenu ni mmoja aliye wa mbinguni” Mathayo 23:9, Yohana 17:11, Isaya 48:11 na Isaya 42 : 8, Mambo ya Walawi 24:16 na 1Wafalme 21:9-10, Zaburi 74:10, 18. Hii ndiyo maana ya kulitukana jina la Mungu. Ufunuo 13:6, PAMBANO KUU UK 50-51,52:2,535

2.    Upapa unasema unasamehe dhambi za watu pale ambapo watu hawawezi kufika kwa papa, ameweka wawakilishi wake yaani mapadri, watu kwenda kutubu kwa Papa na kwa mapadri. Marko 2:5-10, Luka 5:21-24. Biblia inasemaje kuhusu madai haya Papa kusamehe dhambi? 1Yohana 2:1-2, Wakolosai 1:14-20, Waebrania 9:25-28, Danieli 7:25, Ufunuo 13:5, PAMBANO KUU 51:1.

3.   Upapa unadai haukosei

Papa ni nani Uk 30, PAMBANO KUU UK. 47(51)

Biblia inasemaje kuhusu madai haya ya upapa? Mhubiri 7:20, 1Wafalme 8:46 na 2Nyakati 6:36, Warumi 3:23, 1Yohana 1:8, Ufunuo 13:5, Danieli 7:25

4.   Upapa ulibadili majira na sheria (Amri) za Mungu

Uliweka siku ya kwanza ya juma (Jumapili) kama alama (chapa) yake Ufunuo 13:14-18, kitabu cha Papa ni nani Uk 46, Kitabu cha historia ya kanisa vipindi vyake saba Uk 24.

Biblia inasemaje kuhusu madai haya ya Upapa kubadili Sabato ya Bwana?

KUTOKA 20:8-11, 31:16 – 17, ISAYA 24:4 – 6, WAEBRANIA 4:9, ISAYA 66:22-23, EZEKIELI 20:12,20, DANIELI 7:25, ZABURI 119:126, PAMBANO KUU 49, 545, 546, 549.   

“Ni ndani ya mji wa Roma uitwao mji wa vilima saba, hivyo eneo lote la Serikali ya Vatican limekuwa mpaka kikamilifu” THE CATHOLIC  ENCYLOPIDIA Page 529. Pambano uk 74:4, uk 188, Ufunuo 17:9

“Vigillius alikalia kiti cha upapa AD 538 Chini ya ulinzi wa jeshi la Belisanius” HISTORY  OF CRISTIAN CHURCH, VOL 3 P 327.

{Kanisa na Serikali} Papa ni nani 50-51 AD 538 juu ya amri ya Mfalme Jastian na chini ya ulinzi wa Jeshi Belisarius. 

 “Wakati ufalme wa Rumi ulipo upokea Ukristo, Kanisa  likahakikishiwa amani, na Mfalme aliiacha Rumi kwa Papa, ili iwe kiti cha enzi cha mamlaka ya mwakilishi wa Kristo, ambaye angetawala hapo ikiwa huru bila kuingiliwa na mamlaka zote za binadamu hadi ukamilisho wa vizazi vyote, hadi mwisho wa wakati . RIGHT AND PRIVILEGES UK 13,14.

Haya ni mataifa yaliyotokea baada ya Rumi kusambaratika 1. Uingereza,   2. Ujerumani   3. Ufaransa   4. Ureno     5. Hispania,  6. Italia,     7. Uswisi   8. Heruli,   9. Vandalis,  10. Ostrogoths.

 

lakini unabii ulikuwa umetabiri kuwa ndani ya mgawanyiko huo kutokuwemo  nguvu za chuma.Daniel 2:41. Baadaye Nabii aliona pembe ndogo yenye macho na kinywa na ilikuwa hodari na kuzing’oa pembe –falme tatu katika zile za kwanza. Daniel 7:20, 24, Daniel 2:41 -45 ,Ufunuo 13:1-3

  Pembe ndogo iliangusha pembe tatu Heruly, Vandals na Ostrogoths.

 

Falme hizi tatu ziling’olewa kabisa na hazipo hata kwenye ramani ya dunia  kwa sababu zilipinga sera za pembe ndogo ambayo ilikuwa ikiinuka kisiasa na kidini, jambo ambalo falme zilizong’olea zilipinga kabisa mfumo huo wa pembe ndogo kutawala mambo ya siasa na dini mataifa saba yalikubali na ndiyo yaliyoisaidia pembe hiyo kuyang’oa mataifa hayo.

1.   Atanena maneno  kinyume chake aliye juu. Danieli  7:25

2.   Nikatazama na pembe hiyo ilifanya vita na watakatifu na kuwashinda.Danieli 7:21

3.   Ataazimu kubadili majira na sheria . Daniel 7:25

4.   Nao watatiwa mikononi mwake kwa wakati, na nyakati mbili, na nusu wakati. Danieli 7:25.

 Upapa kudai kuwa makamu wa mwana wa Mungu kwa ukweli huonyesha ufanisi kwa nguvu nyingine. Anaelekeza kwa uwekaji wa Jumapili kama alama ya Mamlaka yake lakini kwa badiliko la sheria na majira ya Mungu, anajaribu tu kufanya kile shetani alichojaribu mbinguni, kuonyesha ubaya wa amri na mtoa amri. Kwa kujidai kuwa juu ya Amri za Mungu anahisi tu tabia ya mdanganyifu mkuu, Mungu aliweka Sabato kama alama ya mamlaka yake na nguvu zake. Na upapa ukifanya kazi ya Mfalme wa uovu unaelekeza Jumapili kama alama ya uwezo wake.

 

SHERIA YA JUMAPILI YA CONSTANTINE

 

 Sheria ilipitishwa na Mfalme mkuu costantine tarehe 7, March 321 BK kuhusu siku ya kupumzika na kazi inasomeka hivi.

“ Mahakimu wote na watu wa mijini na mafundi stadi watapumzika katika siku ya heshima ya jua.Hata hivyo, watu wa mashambani wanaweza kuwa huru kwenda kulima mashambani, kwa sababu mara kwa mara inaonekana kwamba hakuna siku nyingine iliyo bora zaidi iliyotolewa kwa ajili ya kupanda nafaka (Kwenye mashamba makondeni au mizabibu kwenye mifereji. Ili kwamba mibaraka inayotolewa kwa ukarimu kutoka mbinguni kwa muda mfupi isipotee bure” Joseph Cullen Ayer, A sourse Book for Ancient Church History (New York: Charles Seribner’s sons, 1913), div 2, per 1, ch.1, sec.59 uk 284-285.

Unabii ulikuwa umetabiri majira na sheria  vitabadilishwa  unabii huu ulitimia tarehe 7, March 321 AD. Kaisari Konstantine alipotangaza tarehe hiyo kwa mara ya kwanza watu wakaanza kupumzika siku ya kwanza ya juma na mwaka 364 AD Maaskofu wa Kanisa la Rumi waliiwekea mkazo kuhakikisha kila mtu anapumzika siku hiyo.Danieli 7:25, Isaya 24: 5.

 

“Mara ya kwanza kuishika Jumapili  kukakazwa kuwa wajibu wa kisheria ilikuwa amri ya Konstantine AD 321  aliamuru ya kwamba baraza zote za hukumu, na wenyeji wa mjini na viwanda vyote vya kazi havina budi kupumzika Jumapili siku ya jua yenye heshima”.Encylopidia Britarnica, Art Sandary.

 

 

Baada ya miaka kadha wa kadha “Baraza la laodikia (AD 364) ilikazwa mara ya kwanza kuishika siku ya Bwana. Prynne’s Dissertation on the Lords Day Sabbath, P.153.

 

“Mambo yote yaliyopaswa kutendeka siku ya Sabato sisi tumeyageuza kuwa siku ya Bwana” Eusebius mwandishi wa Historia aliyeishi wakati wa baraza ya Laodikia.

 

Unabii ulikuwa umetabiri mamlaka ya upapa ungetawala dunia kwa muda wa siku elfu moja mia mbili na sitini AD 538 –AD 1798 ambapo utawala huu ungepata jeraha ya mauti na unabii wa ufunuo 13:3 ungetimia kwa sehemu.Upapa ulikomeshwa na taifa la Ufaransa .

“Katika mwaka 1798 AD Jenerali Bethier aliingia Roma akauondoka kabisa utawala wa Papa na kuanzisha utawala mwingine”. ENCYCLOPIDIA  BRITANNICA EDITION 1914.

 

“Mapinduzi ya Ufaransa” yalienea katika bara la Ulaya. Wakati ule Wafaransa walipigana vita na nchi za jirani. Hivyo walieneza mawazo ya mapinduzi katika bara la Ulaya. Mwaka 1799 Jemadari Napoleoni, Mfaransa, alijichukulia uwezo wa kutawala, akashinda vita katika Italia na Ujerumani. Napoleoni aliamuru, Papa Pius VI mzee asafirishwe  kwa nguvu, aletwe Ufaransa. HISTORIA YA KANISA VIPINDI VYAKE SABA UK 84 :3

 

Upapa ulipoteza mamlaka yake kwa muda katika Februari 20, 1798 Berthier Jemadari wa Jeshi la Ufaransa chini ya Napoleon alimkamata Papa Pius wa VI na kumfunga hadi Valensia Ufaransa akafia huko mwisho wa upapa. Ufunuo 13:9-10

 

  Baada ya jeraha la mauti kwa utawala wa upapa ulimwengu ulikuwa huru bila upapa kwa muda. Uhuru wa dini ulienea katika nchi mbalimbali lakini unabii ulikuwa umetabiri kuwa jeraha la mauti litapona na Upapa kurudia mamlaka yake tena. Ufunuo 13:3-8, 17:10-11. 1922-1929 harakati za kuponywa kwa jeraha la mauti ziliwekwa katika mazungumzo kati ya serikali ya Italia na Vatikani ili kuirudishia mamlaka kufikia mwaka 1929 makubaliano yalisainiwa kati ya Serikali hizo mbili.

 

“MUSSOLINI AND GASPARRI, SIGN HISTORIC ROMAN PACT”

Suala la Romani usiku huu lilikuwa ni jambo lililopita, na Vatican ilikuwa katika amani na Italia …..katika kuweka sahihi kwenye mkataba wa kumbukumbu kwa kuponywa jeraha la miaka mingi, uchangamfu kupindukia ulionyeshwa na pande zote” The San Francisco Chronicle.Feb.11, 1929.

 

“Roma Jun 7-kutoka saa 5 kamili asubuhi hii kulikuwa na mtawala mwingine wa Serikali ya kujitegemea duniani. Katika muda huo waziri mkuu Mussolini, kama waziri wa mambo ya nje Italia akimuwakilisha mfalme Victor Emmanuel-Waziri mkuu wa kwanza Italia kuvuka kizingiti cha chini cha mlango wa Vitican –akibadilishana na Kadinari GASSPARI, WAKALA WA Serikali ya Upapa, akimuwakilisha papa Pius VI, makubaliano ya mikataba yalisainiwa katika Ikulu ya Letaran Feb. 11. Kwa kitendo hicho rahisi mtawala wa Serikali ya kujitegemea ya mji wa Vatican umekuwepo”. NEW YORK TIME JULY 7, 1929.

 

Kwa kuwa Unabii ulikuwa umetabiri kuwa jeraha la mauti litapona na Dunia itamwabudu mnyama, ni lazima jambo hili litatokea Upapa na serikali vyote vitaungana tena, tangu mwaka 1929 Italia ilipo urudishia Upapa eneo lake la Vatican , na maeneo mbalimbali yaliyo kuwa yamechukuliwa wakati wa jeraha la Upapa. Sasa Upapa unaendelea  kukusanya nguvu kimyakimya, mvuto wake unazidi kuenea katika Mabunge, vyombo vya kutunga sheria katika mioyo ya watu.Upapa unaendelea kuyaunganisha mataifa yote,na makanisa,dini zote kuwa chini ya himaya yake. Muda si mrefu jeraha lake la mauti litapona. UFUNUO 13:3.  



435B3FB0
 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 


  Ufunuo 13:11-18

Kisha nikona mnyama mwingine, akipanda juu kutoka katika nchi; naye alikua na pembe mbili mfano wa mwana kondoo, akanena kama Joka” Ufunuo 13:11.

Nchi kiunabii huwakilisha watu wachache. Hivyo mnyama huyo anainuka kutoka eneo ambalo hapo awali halikukaliwa na watu. Yeremia 2:16.

“Katika mwaka 1798 ni Taifa gani liliinuka na kustawi likawa na nguvu, ambalo lilivuta macho ya ulimwengu kulielekea.? Ni taifa moja tu peke yake ndilo linalo patana na unabii huu – yaani Marekani (United States of America) maneno ya maandiko matakatifu ndio yamelieleza Taifa hili karibu kila kitu bila kasoro; jinsi kuinuka kwake kutakavyokuwa … “Marekani “imezuka” “kimyakimya” “kila siku huongezeka kuwa maarufu” kwa uwezo na kiburi

pambano kuu 427.

 

Marekani inafananishwa na mnyama kama mwanakondoo Ufunuo 13:11 – 18. Hapo kwanza Marekani ilikuwa nchi ya uhuru wa dini na nchi ya makimbilio, kwa watu waliokuwa wakinyanyaswa kutoka sehemu zote za dunia. Mwanakondoo huwakilisha uungwana wa taifa hili lililopanda kwenye utawala bila kumwaga damu, kama yale mataifa yanayowakilishwa na wanyama wakali. Soma Danieli 7:1-8, 16-17. Nchi huwakilisha watu wachache Yeremia 2:6. Kwa hakika hakuna mahali pengine duniani ambako uhuru wa dini ulipofurahiwa kwa ukamilifu kama nchi ya Marekani. Kunena kama joka ni kitendo cha Marekani kunena kinyume cha uhuru wa dini, na kuwalazimisha watu kutenda kinyume cha dhamiri zao, hapo Marekani itakuwa imeunga mkono upapa, na hapo Marekani itatumia uwezo wa mnyama wa kwanza ambaye ni chui. Ufunuo 13:1-10.  

 

MAREKANI,  UNITED STATES OF AMERICA

Marekani itaikana katiba yake ya Uhuru wa dini na kuwalazimisha watu kutii kanuni za dini na mapokeo yaliyo kinyume na dhamiri zao, kwa kitendo hicho marekani itakuwa imeutukuza Upapa yaani mamlaka ya Rumi.

wakati Uprotestanti utakaponyosha mikono yake kulivuka lile shimo kubwa la tofauti yao wataziondoa tofauti zinazowatenga kiimani na kuukumbatia mkono wa mamlaka za kirumi, wakati utakaponyosha mkono wake juu ya shimo refu sana ili kukumbatiana mikono na umizimu, wakati wakiwa chini ya uwezo wa muungano huu wa washirika watatu nchi yetu itaikana kila kanuni katika katiba yake kama serikali ya Kiprotestanti na ya Jamhuri na kufanya maandalizi kwa ajili ya uenezaji wa uongo mwingi na madanganyo ya kipapa hapo ndipo tutakapojua kuwa wakati umekuja kwa ajili ya utendaji wa ajabu wa miujiza  ya shetani na kuwa mwisho uko karibu” MATUKIO YA SIKU ZA MWISHO 122: “Naye atumia uwezo wa mnyama Yule wa kwanza mbele yake. Aifanya dunia na wote wakao ndani yake wamsujudie mnyama wa kwanza ambaye jeraha lake la mauti lilipona Ufunuo 13:12. Ufunuo 13:13-15

1. Mnyama ni utawala (Dola) mnyama chui huwakilisha utawala wa Upapa (Danieli 7:8, 23

2. Sanamu ya mnyama ni –Alama ya umoja wa Makanisa, Muungano wa Makanisa:

      Ufunuo 13:13-15 . Pambano kuu uk 426 -427, Pambano kuu uk 422.

3. Chapa ya Mnyama au Alama ya ibada ya Jumapili. Ufunuo 13:16-18, Pambano kuu uk 427 ambayo walianzisha wao kama ishara ya uwezo mamlaka yao.

 

BARAZA LA UMOJA WA MAKANISA ULIMWENGUNI

Baraza la umoja wa makanisa ulimwenguni (Word council of churches – WCC) liliundwa kikatiba kule Amsterdam, uholanzi Augusti 23/1948 limejengwa na matawi ya jumuiya mbalimbali kama ilivyo kwa umoja wa mataifa ndivyo pia ilivyo kwa umoja wa makanisa (WCC) ni kuuwa dini, na kuvurga au kuharibu imani mbalimbali za vikundi vya dini Makanisa kupitia umoja huu wa makanisa ulimwenguni hata kama inatokana ma maandiko matakatifu. Kanisa la kirumi lilianzisha chombo hicho kwa kusudi la kuunganisha makanisa yote na dini zote ili iwe rahisi kuyatawala. Warumi wao huita muungano huo Ekumeni.

 

EKUMENI NI NINI?

“Hatuna neno la Kiswahili linalotoa kwa kifupi maana kamili ya Ekumeni ambalo ni neno la kigiriki. Neno “Polepole” linaeleza kwa karibu zaidi maana ya Ekumeni. Katika kanuni ya mitume tunasali: Nasadiki kwa kanisa moja takatifu, katoliki la mitume; tukiyaunga pamoja maneno “moja” na “katoliki” tunakaribia kuipata ile maana ya Ekumeni, yaani, jitihada za kuufikia umoja kati ya wakristu. Tangu miaka mingi iliyopita wakatoliki walifanya maombi ya siku nane katika mwezi wa Januari kwa ajili ya umoja huo. tarehe 25 Januari 1959. Yaani siku ya mwisho ya maombi hayo, Baba mtakatifu Yohane alitangaza kusudi lake la kufanya mtaguso. Alinuia kuwaalika wakristu wote, wanaotengana nasi, ili yafanywe majaribio ya kuupata umoja kati ya wakristu, umoja unaotamaniwa popote duniani. Wazo hili la umoja linatokeza katika hali nyingi za Mtaguso, kwa mfano katika hati ya liturjia imeandikwa:

 

“……… kusaidia kufikia umoja kati ya wale wanaosadiki mafundisho ya kristu.”

Watu wa madhehebu mbalimbali ya kikristu walikuwepo Roma wakati wa mtaguso wakihudhuria vikao mbalimbali; wengi kati yao walishtuka kuona kuwa wakatoliki wanaangalia maandiko matakatifu kama msingi wa imani yao. Mtaguso mkuu wa pili wa vatican uk 67

 

Viongozi wa dini mbalimbali wamekuwa wakinukuliwa na kurekodiwa kupigwa picha na vyombo mbalimbali vya habari wakihimiza kwa haraka umoja huo wa makanisa, na viongozi wa makanisa, na wa dini mbalimbali duniani wamekuwa wakienda Vatican kuomba umoja na Papa, wa kanisa la kirumi na mikataba ya umoja imesha sainiwa ya kuhakikisha dini zote zinaungana na kuwa dini moja chini ya kiongozi mmoja ambaye ni Papa mwenyewe manabii wa Mungu walionyeshwa namna dunia ya sasa itakavyo rahisisha upashaji wa habari na matukio muhimu kupitia aina zote za vyombo vya habari, hata Yesu mwenyewe alisema katika kitabu cha Mathayo 24:6 “Nanyi mtasikia habari za vita na matetesi ya vita;….

 “Madhara yatakuja juu ya madhara, na habari ya shari juu ya habari ya shari; ….. Ezekieli 7:26 Unabii huu upashaji umeshatumia ndiyo maana taarifa zote tunazisikia kutoka kwenye vyombo vingi vya habari na teknolojia itakayotumika kutangaza dini moja duniani na serikali moja ya dunia na siku moja ya ibada.

 

Wale wamwabuduo mnyama na sanamu yake na chapa yake (Alama). Ulimwengu mzima utakuwa upande wa mnyama mataifa yote yatauunga mkono upapa, na hapo mateso yataanza tena kwa watu wa Mungu wazishikao amri za Mungu na sabato ya amri ya nne katika amri kumi .K .Torati 10:4, Kutoka 34:28, 31:18 K. Torati 9:9-11 kutoka 32:15-16.

 

Kwa kitendo cha mataifa kuungana pamoja na upapa na kutangua amri za Mungu hasa sabato kutaiingiza dunia katika vita kubwa ya kupambana na Mungu mtoa sheria. Ufunuo 16:12-16, Isaya 41:1-2, Zaburi  119:26,  Isaya  24:3-6, Danieli 7:25, Isaya 2:17-21.

Amri inayolazimisha ibada ya siku hii itatangazwa ulimwenguni kote - - - maonjo na mateso yatawajia wale wote ambao kwa kulitii neno la Mungu, watakataa kuisujudu sabato hiyo ya uongo”. (7 BC 976)

 

“Ulimwengu wote utachochewa kuwa na uadui dhidi ya Waadventista wa Sabato, kwa sababu hawatatoa utii wao kwa upapa, kwa njia ya kuiheshimu Jumapili, Siku iliyowekwa na Mamlaka hiyo ya mpinga Kristo.Ni kusudi la shetani kusababisha wafutiliwe mbali duniani, ili kwamba mamlaka yake hapa duniani yasipate kupingwa”. (TM 37:  RH 22/8/1893)

“Mamlaka za dunia, zikiungana pamoja kufanya vita dhidi ya wakubwa kwa wadogo, na matajiri kwa masikini, na walio huru kwa watumwa (Ufunuo 13:16) wanatakiwa kufuata desturi za Kanisa kwa kuitunza sabato ya uongo. Wale wote watakaokataa kukubaliana na sheria hiyo watakabiliwa na adhabu kutokana na sheria za serikali zao, na hatimaye itatangazwa kwamba wanastahili kifo. (GC 604)

“Wakati utunzaji wa Sabato ya uongo kwa kuitii amri ya Serikali, Kinyume na amri ya nne, utakuwa ni kiapo cha utii kwa mamlaka  inayopingana na Mungu, utunzaji wa Sabato ya kweli, kwa kutii sheria ya Mungu, ni ushahidi wa utii kwa Mwumbaji. Wakati kundi moja, kwa kuikubali alama ya utii kwa  mamlaka za dunia, linapokea alama ya mnyama, kundi jingine kwa kuichagua ishara ya utii kwa mamlaka ya Mungu, linapokea muhuri wa Mungu”.  (GC605).

 

“Ni suala la kuogofya ambalo litaukabili ulimwengu. Mamlaka za ulimwengu zikiungana pamoja kufanya vita dhidi ya amri za Mungu, zitatangaza amri kwamba wote, wadogo kwa wakubwa na matajiri kwa maskini na walio huru kwa watumwa, (Ufunuo 13:16), wanatakiwa kufuata desturi za Kanisa kwa kuitunza Sabato ya uongo. Wale wote watakaokataa kukubaliana na sheria hiyo watakabiliwa na adhabu kutokana na sheria za Serikali zao, na hatimaye itatangazwa kwamba wanastahili kifo. Kwa upande mwingine, sheria ya Mungu inayoamuru siku ya mapumziko iliyowekwa na mwumbaji inadai utii na kutishia ghadhabu dhidi ya wote wanaovunja maagizo yake.

 

 “Suala hili likiwa limewekwa wazi hivyo mbele ya kila mtu ndipo yeyote atakayeikanyaga sheria ya Mungu ili kuitii amri ile iliyotungwa na binadamu atapokea alama ya mnyama”.

(GC 604)

“Mungu anayapatia mataifa muda Fulani wa rehema” (4BC 1143)

“Kwa usahihi usioweza kukosea Mungu wa milele angali bado anatunza akaunti ya mataifa yote. Wakati rehema zake zinaendelea kubaki wazi, lakini wakati hesabu itakapofika kiwango Fulani ambacho Mungu amekiweka, utekelezaji wa ghadhabu yake utaanza. Akaunti hiyo itafungwa uvumilivu wa Mungu utakoma. Hakuna tena maombezi ya rehema kwa ajili yao”. (5T 208).

 

“Mungu anatunza kumbukumbu ya mataifa; hesabu inaongezeka dhidi yao katika vitabu vya mbinguni, na wakati itakapokuwa imepitishwa sheria kwamba uvunjaji wa siku ya kwanza ya juma utakabiliwa na adhabu, hapo ndipo kikombe chao kitakuwa kimejaa” (7 BC 910).

 

Katika pambano la mwisho ulimwengu wote utahusika makundi mawili yatatokea waziwazi. Pambano ni kati ya amri za Mungu na mapokeo ya wanadamu , kundi moja watamwabudu mnyama na sanamu yake  na chapa au (Alama) yake. Ufunuo 13:3-10.

Kundi la pili ni wale washikao Amri za Mungu na Imani ya Yesu na kuwa na muhuri wa Mungu .Ufunuo 14:12, 12:17, Isaya 8:20.

 

Kama tulivyoona mnyama anawakilisha utawala wa mamlaka ya Upapa. Sanamu ya mnyama inawakailisha Muungano wa Makanisa Uprotestanti ulioasi (WCC).

 

UNABII HUU UTATIMIA WAKATI MAREKANI ITAKAPO TANGAZA IBADA YA JUMAPILI ULIMWENGUNI KOTE

 

Waromani wanasema kwamba “Ushikaji wa jumapili unaofanywa na Waprotestanti ni heshima kuu wanayotoa kwa mamlaka ya kanisa katoliki wao wenyewe”. Ushurutishaji wa kushika jumapili kwa upande wa makanisa ya kiprotestanti ni ulazimishaji wa kuabudu upapa- Mnyama. Wale ambao, wanafahamu madai ya amri ya nne huchagua kuishika sabato ya uongo badala ya sabato ya kweli kwahiyo, wanatoa heshima kuu kwa utawala huo ambao umeamriwa kwake tu. Lakini kwa kitendo halisi cha kushurutisha wajibu wa kidini kwa kutumia nguvu ya serikali, makanisa yenyewe yatakuwa yameunda sanamu kwa mnyama, kwahiyo ulazimishaji wa kushika jumapili katika Amerika (United State) utakuwa ni ulazimishaji wa kumwabudu mnyama na sanamu yake. ………………. Anamwabudu mnyama na sanamu yake. Ikiwa watu watakataa sabato ambayo Mungu ameisema kuwa ishara ya mamlaka yake, kwahiyo watakuwa wamepokea na kukubali alama ya uaminifu kwa Roma- “Chapa ya mnyama”. Na ni mpaka jambo hili liwekwe wazi kabisa mbele ya watu ili waweze kuchagua kati ya amri za Mungu na maagizo ya wanadamu, ili wale wanaoendelea kuasi watapokea “Chapa ya mnyama”. PAMBANO KUU U. 427(449).

Unabii wa Ufunuo 13: unaeleza kwamba mamlaka inayowakilishwa na mnyama mwenye pembe kama mwana Kondoo ataifanya “Dunia na hao wakaao ndani yake kuabudu upapa – ambaye anawakilishwa na mnyama chui, kwamba wamfanyie mnyama sanamu” na zaidi ya hayo, atawaamuru wote wadogo kwa wakubwa, matajiri kwa masikini, na walio huru kwa watumwa, kupokea chapa ya mnyama. UFUNUO 13:11-16. Imeonyeshwa kwamba Marekani (United States)  ndio utawala unaowakilishwa na myama mwenye pembe kama mwana kondoo na kwamba unabii huu utatimia wakati marekani (United State) itakapo lazimisha utunzaji wa jumapili, ambayo Rumi, inadai kuwa ndio ukubali wa mamlaka yake ya juu Kabisa. Lakini marekani (United State) haitakuwa pekeyake katika heshima hii kwa upapa. Mvuto wa ushawishi wa Rumi katika nchi ambazo hapo awali zilikiri na kuukubali utawala wake bado nchi hizo hazijaangamizwa. PAMBANO KUU UK. 549.   

“ Ushindi wetu uliopatikana kwa machozi haukuja kupitia tu kile tulichokidhamiria wenyewe. Tuliwezeshwa na kuhamasishwa kwa msaada –wa mali, hali na kiroho –ulitolewa kwetu na Baraza la umoja wa makanisa ulimwenguni, na makanisa yake wanachama”. American Opinion, January 1982-ukr 44.”Mtawanyiko mkubwa wa imani katika Makanisa ya Kiprotestanti” Pambano kuu 423:1  444:3

 

EKUMENI

-      Siku hizi neema za Roho Mtakatifu zinawasukuma watu popote duniani, wasali na wafanye juhudi za kufikia umoja ule unaotakiwa na Bwana wetu. Mtaguso unawataka wakristo wote washiriki katika juhudi hizi za kuleta umoja wa wakristo.

Katika shughuli za EKUMENI inatakiwa kuangalia mambo kama haya:-

1.   Kuepukana na maneno na matendo maovu kwa ndugu zetu walio jitenga nasi.

2.   Kutoa nafasi ya mazungumzo kwa wataalamu wa dini wa madhehebu zote mbili.

3.   Kujaribu kufahamu maoni ya wengine na kuepukana na matumizi ya maneno yanayoweza kuwaumiza wengine

4.   Kumpatia kila mmoja nafasi ya kueleza mafundisho yote yanayohusiana na imani, ibada yake ili baadae ipatikane njia ya kufahamiana. Soma 2MTAGUSO MKUU WA VATIKAN uk. 71,

Kwa sababu sera za muungano wa makanisa, kila kanisa litalazimika kuacha msimamo au misingi ya imani yao hata kama ni ya kimaandiko na kanisa lolote litakalofundisha ukweli kama ulivyo ndani ya Biblia litachukuliwa hatua za kisheria hii ndiyo sera ya muungano wa makanisa (WCC). Wachungaji, wainjilisti na viongozi, maaskofu, watazuiliwa wasiuseme ukweli na “wahubiri maneno laini” Isaya 30:8-13, Isaya 56: 10-12.

“Wakati makanisa makubwa ya Marekani (UNITED STATE) yanapoungana katika vipengele hivyo vya mafundisho wanavyovishikiria kwa pamoja, ndipo yatakapo ishawishi serikali kulazimisha amri zao na kukubaliana na Taasisi zao ndipo Amerika ya kiprotestanti itakapokuwa imeunda sanamu ya utawala wa kiromani na adhabu za serikali kuwatesa wazushi hazita epukika.”

PAMBANO KUU UK. 423 (445).

Hivyo, polepole, itakuwa rahisi kufikia hatua ya kuamua ni lini tunaweza kusali ama kufanya ibada pamoja au kuona ni mambo gani yanayoweza kurekebishwa au kuachwa kando ili EKUMENI ifanikiwe. Matendo ya namna hiyo yakitendwa kwa uadirifu na chini ya uongozi wa Maaskofu yanaweza kutuletea mapatano, umoja na mapendo ya kindugu. Baada ya kuondoa vikwazo vya muungano polepole wakristu wote watafikia hali ya kushirikiana katika ibada ya ekaristi Takatifu, katika umoja ulio takiwa na Bwana wetu. Sisi tunaamini, kuwa umoja huo umo katika kanisa Katoliki. MTAGUSO MKUU WA VATIKANI WA PILI UK. 71-72.

Mtawanyiko mkubwa wa Imani katika makanisa ya KIPROTESTANTI unatazamwa na wengi kama ushahidi ulio wazi wa kutofanikiwa kwa juhudi za kupata umoja unaotafutwa daima. Lakini kwa miaka mingi katika makanisa ya imani ya kiprotestanti kumekuwepo kauli nzito inayopendelea umoja uliojengwa katika vipengele vya mafundisho ya pamoja. Ili kupata umoja wa aina hiyo, majadiliano ya mafundisho ambayo makanisa yote hayakubaliani nayo hata kama ni muhimu kiasi gani kutokana na msimamo wa Biblia ni lazima yaachwe kabisa PAMBANO KUU UK 423:1

“Leo mwelekeo wa kuwapelekea injili wa zamani usio na amani –kusisitiza hasa mambo ambayo tunatofautiana kutoka makundi ya dini zingiine zote- ni kipindi cha nyuma, kabisa .Na hilo ndiyo lilivyotakiwa kuwa”.Ministry Magazine, March 1966 uk 10.

 

Kanisa katoliki lasema “Kuwa geuzi la (Sabato hadi Jumapili) ilikuwa tendo lake - - - na tendo hilo ndilo alama ya uwezo wake wa kidini” Cardinal Gibbons Nov 11 1895

 

KAMPENI YA MWISHO YA SHETANI NI KUHAKIKISHA ANAUTEKA ULIMWENGU WOTE

Kampeni ya Shetani ni kukusanya ulimwengu wote kuwa chini ya mipango yake ya kushindana na Mungu na kuvunja amri zake. Katika pambano hili la mwisho ataunganisha shughuli zote na mipango yote ya wanadamu kuigeuza na kuwa kinyume na Mungu. Kupitia mashirikisho mbalimbali na miungano ya kikanda vyama mbalimbali na vikundi na vyama vya makabila  

 

Kutakuwa na miunganiko ya kitaifa na kikanda. Mfano Afrika mashariki, Afrika Magharibi, kusini mwa Afrika, kaskazini mwa Afrika, Afrika ya kati, Ukanda wa maziwa makuu, Umoja wa nchi huru za Afrika, Umoja wa ulaya, Umoja wa nchi za kiarabu, Umoja wa nchi zinazounda Amerika na Canada, Asia, Amerika ya kusini, na n.k. mwisho umoja wa mataifa utaunganisha zote kuwa chini ya serikali moja ya dunia chini ya mwamvuli wa umoja wa mataifa. Mataifa yote yataunganishwa pamoja ili kupingana na serikali ya Mungu. Ufunuo 16:13-16

 

“Fanyeni haraka mje enyi mataifa yote, wapande zote jikusanyeni pamoja na huko watelemshe mashujaa wako wote ee Bwana. Mataifa na wajihime wakapande juu katika bonde la Yehoshafau, maana huko ndiko nitakapo keti niwahukumu mataifa yote yaliyo pande zote …” Yoeli 3:11-14

 

Umoja wa mataifa ulianzishwa na kanisa la kirumi chini ya mapapa ili iwe rahisi kuwatawala mataifa yote duniani, baada tu ya vita vya kwanza na vya pili vya dunia, chombo hicho kiliundwa rasmi kushughulikia masuala mbalimbali ya kimataifa. Umoja wa mataifa si chombo kizuri kama wengi wanavyo dhani. Ni chombo ambacho kiliundwa kwa makusudi ya watu wachache ili kuhakikisha dunia inakuwa serikali moja, chini ya kiongozi mmoja ambaye ni Papa wa kanisa la Kirumi na kuwa na dini moja ya dunia chini ya Papa mwenyewe. Unabii wa Biblia katika kitabu cha Ufunuo 17:12-18, Danieli 2:41-43.

   Robert Muller katibu msaidizi mstaafu wa umoja wa mataifa alisema; “Tunapaswa kuenenda kwa haraka sana kama inavyowezekana katika serikali moja ya dunia, Dini moja ya dunia chini ya kiongozi mmoja wa dunia” THE WORLD LAST DICTATOR WOODBUM, OREGON=SOND ROCK BOOKS, INC. 1995, PAGE 81.

  Kazi ya umoja wa mataifa ni kuivuruga dunia na kuifanya isitawalike, ili watu waone umuhimu wa kuungana kwa kigezo cha amani na wakati huohuo wao wenyewe ndio chanzo cha matatizo yote duniani, migogoro yote unayoiona ulimwenguni wao ndio wanaohusika. Biblia inaeleza wazi kuwa amani ya dunia haitapatikana soma Ezekieli 7:25-27. Amani ya kweli ni kutii amri za Mungu Zaburi 119: 165.

 

“Mtaguso unadhani kuwa nilazima kuunda umoja wa mataifa wa kuweza kuleta amani duniani, yani kuungana kuwa jamii moja. Lakini ni kazi ya polepole hutaka wakati azimio na utaratibu mtaguso unatoa azimio lake MTAGUSO MKUU WA VATICAN ni wapili maelezo ya hati ya 16 uk 149 -153

 

SHIRIKISHO LA MATAIFA YENYE NGUVU DUNIANI

 

UMOJA WA ULAYA 1-Australia, 2-Bulgaria, 3-Denmark, 4-Eire, 5-Estonia, 6-Hispania, 7-Hungaria, 8-Italia, 9-Krotia, 10-Kupro, 11-Latvia, 12-Lituanya, 13-Luxembourg, 14-Malta, 15-Poland, 16-Romania, 17-Slovakia, 18-Slovenia, 19-Ubelgiji, 20-Ucheki, 21-Ufaransa, 22-Uholanzi, 23-Ujerumani, 24-Ureno, 25-Uswisi,

 26-Ugiliki. North Atlantic Treaty Organization was signed on 4th April 1949: Headquarter, Brussels Belgium

Wanachama wakujihami wa nchi za magharibi (NATO’s)

1-Albania, 2-Belgium, 3-Canada, 4-Croatia, 5-Czech Republic, 6-Denmark, 7-Estonia, 8-France, 9-Germany, 10-Greece, 11-Hungary, 12-Iceland, 13-Italy, 14-Latvia, 15-Lithuania, 16-Luxembourg, 17-Montenegro, 18-Netherlands, 19-North macedonia, 20-Norway, 21-Poland, 22-Portugal (ureno), 23-Romania, 24-Slovakia, 25-Slovenia, 26-Spain, 27-Turkey, 28-United kingdom, 29-United states, 30-Burgaria

 

*BG5 America, Uingereza, Ufaransa, China, Urusi- hawa ni wanachama wanaounda baraza la usalama la umoja wa mataifa (UN).

*G7 America, Uingereza, Japani, Canada, Ufaransa, Ujerumani, Italia

*G8 America, Uingereza, Japani, Canada, Ufaransa, Urusi , Ujerumani, Italia

*G10 Belgium, Canada, Nitherlands, Uingereza, Japani, Ufaransa, Sweden , Ujerumani, Italia, Marecani

*G20 Argentina, Australia, Brazil, Canada, China, France, German, india, Indonesia, Italia, Japani, Korea, Mexico, Russia, Saudi-Arabia, South-Africa, Turkey, UK, USA na Umoja wa Ulaya

 “hawa wanashauri moja” kutakuwepo na muunganiko wa kiulimwengu, umoja thabiti, shirikisho la majeshi ya shetani. “Nao watampa yule mnyama nguvu zao na mamlaka yao” Ufunuo 17:13-14

hivi mateso holela dhidi ya uhuru wa dini yatarudiwa tena, uhuru wa kumwabudu Mungu kulingana na maongozi ya dhamiri yatarudiwa tena kama ilivyowahi kufanywa na upapa wakati uliopita ulipowatesa wale waliothubutu kukataa kukubaliana na taratibu za ibada na maadhimisho ya kikatoliki. Matukio ya Siku za Mwisho uk 137.

Kanisa la Rumi hudai kwamba ndio waliogeuza (Sabato hadi Jumapili ) Hawangetoa kufanya kitu chochote cha kiroho au kidini bila wao. Na KITENDO HICHO NI ALAMA ya sheria na uwezo wa kidini”.James Caedinal  Gibbons barua kwa J.F Sinyder wa Bloomigton, Nov 11  1895.

 

“Mataifa ya Marekani ndiyo yatakayoongoza ya kigeni yatafuata mfano wa marekani.  Japokuwa Marekani ndiyo itakayoongoza, lakini hali ileile ya wasiwasi itawapata watu wetu katika sehemu zote za ulimwengu”. Matukio ya Siku za Mwisho uk 126 ufunuo 13:12-16

 

“Kupitia mfumo wa utandawazi dunia itaunganishwa kuwa kama kijiji, mawasiliano yatasambazwa kote duniani hadi kijijini kwako umeme, Elimu, Kilimo, vyombo vya habari, muziki, Sinema na kumbi za maigizo na michezo. Yote hayo nikuwafanya watu wasisome neno la Mungu (Biblia) na huku watu wakisifia na kusema nimaendeleo na huku serikali moja ya dunia na dini moja ya dunia ikiendelea kuandaliwa na huku watu wakiwa hawana habari ya kile kinachokwenda kutokea ulimwenguni. Yeremia 25:32. Soma kitabu kinachoitwa  COEL TANZANIA uk 90 -93

 

Wakati watu wakifurahia na kusifia maendeleo ndipo kwa ghafla watasikia Marekani ikitangaza serikali moja na dini moja na siku moja ya ibada kupitia vyombo mbalimbali vya mawasiliano. Tunapo ona teknolojia ya mawasiliano, umeme, barabara, n.k vinasambazwa kila kona elewa kuwa nimaandalizi soma 1Watesalonike 5:3, Ufunuo 13; 15-17, Danieli 3:1-8

 

“Serikali ya ulimwengu - - - mipaka ya haraka na yenye nguvu kwa mamlaka ya Taifa huru. Utawala kimataifa wa majeshi yote na meli na wanajeshi wa majini. Mfumo wa ulimwengu kifedha, uhuru ulimwenguni katika uhamiaji. Mwendelezo wa kuondoa ushuru kwa bidhaa zinazoagizwa kutoka nje na vizuizi kwa bidhaa hizo katika biashara ulimwenguni, Benki inayotawaliwa kidemokrasia kimataifa- - -.“Mpango mpya wa maisha ya kiuchumi uko njiani na ni wa lazima kwa njia ya ushirikiano wa hiari katika mfumo wa demokrasia au kwa njia ya mlipuko wa mapinduzi ya kisiasa”. Time magazine, March 16, 1942 ukr 44-48.  Danieli 11:39-41

 

Historia itajirudia. Dini ya uongo itatukuzwa sana. Siku ya kwanza ya juma, ambayo ni siku ya kawaida ya kazi isiyokuwa na utakatifu wowote,itainuliwa juu kama ilivyosimamishwa sanamu ile ya babeli, mataifa yote na kabila na watu wataamuliwa kuiabudu

sabato hii ya uongo …… amri ilazimishayo kuiabudu itatolewa iende ulimwenguni pote” Matukio ya Siku za Mwisho uk 125

Siyo mbali Marekani itaondoa uhuru wa dini na kuwalazimisha watu wote waabudu jumapili na hapo jeraha la Upapa litakuwa limepona. Na kuwatesa tena watu watakaokataa kanuni zake na hawatauza wala kununua Ufunuo 13:17.

“Yule mnyama uliyemwona alikuwako, naye hayuko, naye yu tayari kupanda kutoka kuzimu na kwenda kwenye uharibifu. Na hao wakaao juu ya nchi …… watastaajabu wamwonapo……… Ufunuo 17:8, 13:3,8”

                                

 

Na watu washikao amri za Mungu watakabiliwa na wakati mgumu na Mungu ataingilia kati ili kuwaokoa watu wake Daniel 12:1, Ufunuo 17:13-14.

Na watu wa dunia watachagua kutunza Sabato ya Mungu au Jumapili ya kipapa na wote watakao chagua kutunza siku ya jumapili watakuwa wamepokea chapa ya Mnyama na hapo hawataepuka hukumu za Mungu. Ufunuo 14:9-11, ufunuo 19:19-21, Wito unatolewa Ufunuo 18:4-5

 

KANISA LA WAADVENTISTA WASABATO

(MATENGENEZO) MLOLE KIGOMA TANZANIA

 

+255 766-629-091+255 756-959-525+255 755-486-703

Share:

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni

Popular Posts

Lebo

Recent Posts

Pages