Katika blogu hii, tutachunguza njia mbalimbali za kuimarisha ufahamu wetu wa Biblia. Tutajadili mbinu za kusoma Biblia kwa ufanisi, vidokezo vya kukariri maandiko matakatifu, na mikakati ya kutumia somo la Biblia katika maisha yetu ya kila siku. Iwe wewe ni mtaalam wa Biblia mzoefu au unaanza tu safari yako ya imani, "Jifunze Biblia Zaidi" ni rasilimali kamili ya kukusaidia kuongeza ufahamu wako wa Maandiko Matakatifu na kumkaribia Mungu zaidi.

JE WALE MUNGU ALIYEWACHAGUA,ANAWEZA KUWAACHA?

JE WALE MUNGU ALIYEWACHAGUA,ANAWEZA KUWAACHA?


UTANGULIZI:
Tunapenda kutoa shukrani kwa mwenyezi Mungu kwa kutuwezesha kupata ufahamu huu ambao nasi tunawajibika kuutoa kwa wanadamu wenzetu. Katika makala hii, tumetumia Biblia na Roho ya unabii vitabu vilivyoandikwa kwa lugha za Kiingerza, Kifaransa na Kiswahili. Ingawa tumeandika kwa lugha ya Kiswahili, tumetafsiri maandiko hayo kutoka Lugha ya Kiingereza na Kifaransa na hivyo, kwa wale wanaotumia vitabu vya Kiswahili wanaweza kukuta nukuu tulizotumia zikiwa na maelezo mengi zaidi ya kwenye vitabu hivyo vya Kiswahili maana vitabu hivyo ama vilifupishwa au havina kabisa nukuu hizo. Ni vizuri basi, ndugu msomaji, ukatumia vitabu vya Kiingereza pia hasa pale unapotaka kupata ushahidi na ufafanuzi zaidi. Tumeweka rejea ya wapi nukuu hizo zinapatikana kutoka vitabu vya Kiingereza, Kifaransa na Kiswahili pia.
Tunamuomba Mungu akusaidie unapoendelea kujifunza neno lake, maana alisema;      
’’..............sasa basi ikiwa mtaitii sauti yangu kweli kweli, na kulishika agano langu, hapa ndipo mtakapokuwa tunu kwangu kuliko makabila yote ya watu; maana dunia yote pia ni mali
yangu, nanyi mtakuwa kwangu ufalme wa makuhani, na taifa takatifu......        
Kutoka 19:4 - 6 
1.TUJIFUNZE KWA ISRAELI WA ZAMANI.                                                                                 


1.          KUCHAGULIWA KWAO:     Mungu aliwachagua akawapa heshima kubwa sana.
Aliwafanya kuwa  “............mboni ya jicho lake...“  Zekaria 2: 8   “ Tazama nimekuchora
katika viganja vya mikono yangu; kuta zako ziko mbele yangu daima“   ISAYA  49:16.
N.B. Kuwa mboni ya jicho la Mungu, kuchorwa katika viganja vya mikono yake, ni heshima kubwa sana, maana yake wangeendelea kuwa taifa la Bwana milele, kwa sababu Mungu hafi ili mboni na michoro kwenye viganja vyake vioze.
2.AHADI WALIZOPEWA:
a). Mungu alitia sheria Yake ndani yao;
 …….Nitatia sheria yangu ndani yao, na katika mioyo yao nitaiandika.”
b.       Aliwaapia kuwa pasipopatikana mtu wa kupima mbingu na dunia, hatawaacha kamwe.
YEREMIA 31:37
c.                                                                                                                                                                       
      Akawaambia kitu ambacho hawakukijali kwamba “Amri hizi zikiondoka zisiwe mbele zangu, asema Bwana, ndipo wazao wa Israeli wataacha kuwa taifa mbele zangu milele” Yeremia 31:36.
3.          KUASI KWAO.
Manabii wengi walipambana na taifa hili baada ya kuwa limeasi Amri za Mungu.
Malaki 1:6, Yeremia 7:1-7, Yeremia 26:1, Ezekieli 2: 1-7
N.B. Walipokuwa wakionywa kuhusu uasi wao, walikuwa wakitoa udhuru wa kujitegemeza ahadi walizopewa wakati wa kuchaguliwa kwao.
Mfano: Sisi ni mboni, tumechorwa katika viganja, maana Mungu alisema haya: “….Kwake
hakuna kubadilika, wala kivuli cha kugeuka geuka.” 
Malaki 3:6., Yakobo 1:1







Hii ndio shida waliyoipata manabii na wajumbe waliotumwa kwao.
 Mungu alikuwa ameapa kuwa daima ataendelea kulishughulikia taifa la Israeli, ahadi hii wayahudi waliitafsiri vibaya” , Yeramia 31:35-37.
Wayahudi walijidai kuwa kwa vile wao ni uzao wa Ibrahimu kimwili, umewapa haki ya kudai ahadi hiyo. Walisahau matakwa yaliyowekwa na Mungu ambayo wangayatimiza kwanza.
Ahadi hii ilitanguliwa na maneno yafuatayo:    “Nitatia sheria yangu ndani ya mioyo yao, na
katika mioyo yao nitaiandika, nami nitakuwa Mungu wao nao watakuwa watu wangu….maana nitasamehe uovu wao wala dhambi yao sitaikumbuka tena” Yeremia 31:33-34
Kwa taifa lililopewa amri za Mungu mioyoni mwao, lazima Mungu hulishughulikia. Taifa hilo huungana na Mungu. Lakini wayahudi walikuwa wamejitenga na Mungu.  Ndio sababu waligandamizwa na taifa. Roho zao zilikuwa zimjazwa giza na kutotii. Kwa sababu Mungu alikuwa amewapenda upendo mwingi wakati uliopita, walifikiri kwamba na dhambi zao za wakati huo Mungu hatazijali. Walijivuna bure kwamba wao ni bora kuliko mataifa mengine, ndio sababu ya mafanikio yao.
Hayo yote yaliandikwa    “ili kutuonya sisi tuliofikiwa na miisho ya zamani”    
1Wakorintho 10:11, Tumaini la vizazi vyote uk. 51, Jesus Christ pg.86.
Hatimye taifa hilo likaachwa kama vile ilivyokuwa imetabiriwa na manabii.     “Enyi wa
nyumba ya Israeli, njoni, twende katika nuru ya Bwana. maana wewe umewaacha watu wako, wa nyumba ya Israeli,kwa sababu wamejaa kawaida ya mashariki, nao ni wapiga ramli kama wafilisti, na wanapana mikono na wana wa wageni.“ ISAYA 2:5-6
N.B. Badala ya kuzingatia unabii unaolenga kuachwa kwao, wakajivunia ahadi nzuri za
kuchaguliwa kwao. Kwa kweli usipotii matakwa ya Mungu, anakuacha,     ’’Kwa sababu hiyo,
Bwana Mungu wa Israeli asema, ni kweli nalisema kuwa nyumba yako na nyumba ya baba yako itakwenda mbele zangu milele, lakini sasa Bwana asema jambo hili na liwe mballi nami, kwa maana wao wanaoniheshimu nitawaheshimu, na wao wanaonidharau watahesabiwa
kuwa si kitu.“ 2Samweli 2:30
I.                     ISRAELI WA LEO ( WAADVENTISTA )
“Historia ya waisraeli wa kale ni picha halisi ya waadventista...“  
Pambano kuu uk.263, Tragedie des siecles p. 496
“Katika siku hizi za mwisho watu wa Mungu watakabiliwa na hatari zilezile zilizowapata Israeli wa zamani. Wale ambao hawatapokea maonyo yatokayo kwa Mungu wataanguka katika hatari zilezile kama ilivyokuwa kwa Israeli wa zamani, na kukosa kuingia katika raha kwa kutokuamini. Israeli wa zamani walipatwa na msiba kwa sababu ya mioyo yao isiyotakaswa na nia zao kutojiweka chini ya Mungu. Kukataliwa kwao kama taifa kulikuwa ni matokeo ya kutokuamini kwao, kujiamini, kutotubu, upofu wa akili na ugumu wa mioyo. Katika historia yao tunayo ishara ya hatari inayotuonya mbele yetu.“  
Letter 30, 1895, Matukio ya siku za mwisho uk. 55.,
1T 283, 2T 106 – 109, 5T 76







1.          KUCHAGULIWA KWAO NA MSINGI WA IMANI YAO ( JUKWAA )


Tangu kuchaguliwa kwao walipewa Biblia na Roho ya unabii kama chimbuko la mafundisho ya imani yao. Kwa kweli walikuwa taifa la pekee.
 Nimeagizwa kuwaambia wa Adventist wa Sabato ulimwenguni kote kwamba, Mungu ametuita sisi tuwe watu ambao ni hazina ya pekee kwake. Ameagiza kuwa kanisa lake duniani litasimama likiwa limeungana kikamilifu katika roho na  shauri la Bwana wa majeshi mpaka mwisho wa wakati. “ 
2SM p. 392, messages choisis  vol 2. p 458, matukio ya siku za mwisho uk. 50.
“Wadventista wa Sabato wamechaguliwa na Mungu kama watu wa pekee waliotengwa na ulimwengu. Kwa kutumia upanga mkali wa ukweli ukatao kuwili amewakata na kuwatenga kutoka kwenye mfungamano na ulimwengu na kuwaunganisha naye mwenyewe. Amewafanya kuwa wawakilishi wake naye amewaita kuwa mabalozi wake katika kazi ya mwisho ya wokovu. Utajiri mkubwa kabisa wa ukweli uliowahi kukabidhiwa kwa wenye mwili wa kufa, maonyo matukufu na ya kuogofya yaliyowahi kutolewa na Mungu kwa mwanadamu, vimekabidhiwa kwao ili vitolewe kwa ulimwengu.” 
Matukio ya siku za mwisho uk. 41, Testimonies vol 7 p. 136.
II. MSINGI (JUKWAA) WA IMANI.
Biblia na Roho ya unabii  ndivyo vimekuwa msingi wa imani  yao. 
“Tangu mwaka 1844 ndipo paliwekwa msingi unaowaongoza waadventista kwa kutumia kujifunza neno la Mungu (Biblia), na kuomba kwamba, vilivyoshindikana Ellen G. White akapewa maono ndilo chimbuko la vitabu vya Roho ya unabii.” 
EW p. 23, PE p. 22


Mnamo mwaka 1855 walidhoofika, Roho akawatoka,
“Tarehe 20 mwezi wa Novemba 1855 wakati nilikuwa nikiomba, Roho wa Mungu aliniijia akiwa na nguvu, nikapewa maono. Nilionyeswa kwamba Roho wa Mungu alikuwa ameishatoka ndani ya kanisa” 
Testimonies Vol 1. p.113 Temoignages Vol. 1. p.28
Baada ya Roho kuondoka wakatamani kuongozwa na kanuni za wanadamu. Mwaka 1861 Roho wa Mungu akawakemea kwa kuwaambia maneno yafuatayo:
“Biblia ndiyo kanuni yetu. Tunatupilia mbali chochote kinachofanana na kanuni iliyoundwa na wanadamu. Tunaishika Biblia na vipawa vya Roho ya unabii kama msingi wa imani na msingi wa yale yote Mungu anayotaka kutufundisha. Sisi sasa, ni wapinzani wa mtu yeyote anayeweza kuunda kanuni nyingine.“
Review and Herald 8 October 1861.
Ellen White et ledon deprophetie 112.
“Waadventista wa kwanza walikuwa maaadui wa kanuni hizo. Katika mkutano uliofanyika Battle careek mnamo mwaka 1861, ndugu White alilalamika akisema kwamba kanuni hizo zitadhoofisha vipawa vya Roho vilivyoahidiwa ndani ya maandiko.
Vipawa ambavyo vingeendelea kuwa ndani ya kanisa mpaka mwisho wa nyakati. Kwa upande wake kutupa vipawa hivyo ni sawa na kutupa Biblia.”
Ellen G. White and gifts of prophecy p. 112-113
Ellen G. White et le don de prophetie 112-113.
N.B (Zingatia sana kwamba waadventista wa kwanza ni wale wa kabla ya mnamo mwaka
1855.) 
“Kanuni hizo zinapambana na Biblia ana kwa ana. Tuchukue mfano, tunapokifuata kipengele kinachonenwa ndani ya kanuni kwa uaminifu, tena tukataka kuyafuata yanayonenwa ndani ya neno la Mungu kuhusu vipawa, tukiona kwamba yaliyonenwa Na MUNGU Ni kinyume Na Yale yaliyonenwa Na kanuni, hivyo kanuni itakuwa imegeuka machafuko. Mungu alitoa vipawa ndani ya kanisa ili kazi yake isonge mbele, lakini watu walizuia, walimukosoa muweza wa yote wakimuonyesha kile ambacho amesahau kukitenda. Hawataki Mungu afanye kitu kingine tofauti na vile walichokiandika ndani ya kanuni zao. Ndiyo sababu kanuni inapingana bayana na vipawa vya Roho.”
Review & Herald 8 October 1861
Ellen White et le don de prophetie 113.
Baadhi ya makosa mengi waliyoendelea kuyafanya, na mpango wa kuandika kanuni waliendelea kuwa nao. Mwaka 1874 Ellen White alisisitiza akisema:
“Kwa kuweka misingi ya imani yetu mbele ya watu, tunatamani kwamba, watu waelewe vizuri ya kuwa sisi hatuna hatua (maada) yoyote ya imani, kanuni au mwongozo nje ya Biblia”
Signs of the Times Vol. 1 no. 1 p.3, 1874. Ellen White et le don de prophetie p.113.
Mwaka 1885 na mwaka 1904 – 1905, Ellen White alipokuwa anakaribia mwisho wa maisha yake, alisisitiza tena akisema:
“……Biblia, Biblia peke yake ndiyo kanuni yetu, ndicho kiunganishi kinachotuunga, watu wote wanaoliinamia neno Takatifu wataishi katika umoja. Nguvu zetu haziwezi kuongozwa na maoni na mawazo yetu. Kila mtu hujidanganya, neno la Mungu peke yake ndilo lisiloweza kujidanganya…. Tumpinge adui yetu kama alivyofanya Bwana wetu kwa kutumia Imeandikwa, tuinue bendera yenye maandishi: Biblia kanuni ya imani yetu na mwongozo wetu.”
1  SM 416, R&H 15 Dec.1885
Messages choisis  vol.1 p. 487.
“Kama kanisa tunapaswa kusimama imara kwenye jukwaa la ukweli wa milele ulioshinda majaribu yote. Lazima tukumbtie nguzo imara za imani yetu. Kanuni za ukweli tulizofunuliwa na Mungu ndizo msingi wa pekee wa kweli. Misingi hiyo ndiyo iliyotufanya jinsi tulivyo. Pamoja na kuwa imemaliza miaka mingi, thamani yake haipunguki kamwe. Bila kupumzika, adui anajitahidi kuondoa ukweli huo kwenye nafasi yake, ili badala yake aweke nadharia za uongo. Atatumia mbinu zote ili afike kwenye mipango yake ya udanganyifu. Lakini Mungu atainua watu ambao wanaona mbali an kuchunguza kwa kina, ndio watakaorudisha ukweli kwenye nafasi yake ya awali kama Mungu alivyokuwa amekusudia.”
1  SM 202, 1904; Messages choisis vol 1. p 235.





“Pasiwepo mtu yeyote anayeweza kupindua msingi wa imani yetu. Msingi uliowekwa tangu mwanzo wa kazi yetu kwa kutumia kujifunza neno la Mungu pamoja na maono na maombi. Tulijengwa kwenye msingi huo miaka 50 iliyopita. Watu wanweza kudhani kwamba wamegundua njia nyingine mpya na kuweka misingi mingine  iliyo imara sana kuliko ile iliyowekwa na Mungu, hilo ni kosa kubwa sana. Hakuna msingi mwingine unaoweza kuwekwa badala ya ule wa zamani.”
Testimonies vol.3  p. 296 (1904)
Temoignages pour l, eglise vol. 3 p. 328
“Bwana aliniambia kwamba, mwishoni mwa kazi yake, historia ya zamani itajirudia. Kila ukweli alioutoa unaohusiana na siku za mwisho unapaswa kutangazwa ulimwenguni kote. Kila nguzo iliyowekwa lazima iimarishwe. Sasa hatuwezi kwenda kando ya msingi ambao Mungu ameusimamisha. Hatuwezi sasa kuingia katika mfumo mwingine wa utawala maana, kwa kufanya hivyo ingemaanisha uasi kutoka kwenye ukweli.”
2  SM P. 390 (1905)
Messages choisis vol 2 p.449.
II. NABII ALIONYESHWA WATU WAKIKOSOA MSINGI (JUKWAA )
N.B. Kumbukeni kwamba neno la Mungu, maono na maombi ndilo msingi walioupata kwa
shida. (E.W. xxiii)
“…….. Ujumbe wa malaika wa kwanza, wa pili na wa tatu. Nalionyeshwa tena mambo ya habari hizi nikaona mambo yaliyowatokea watu wa Mungu katika maisha yao, jinsi yalivyo ya thamani sana. Waliyapata kwa shida nyingi na mateso makali. Mungu aliwaongoza hatua kwa hatua mpaka mwishowe akawaweka juu ya jukwaa lisilotikisika. Naliwaona watu wengine wakija mmoja mmoja na kulikaribia lile jukwaa kusudi wautazame msingi wake. Wengine kwa furaha wakapanda mara juu ya jukwaa lile. Wengine walianza kutafuta kasoro fulani katika msingi ule. Walitaka ili itengenezwe sehemu nyingine, ndipo jukwaa lingekuwa kamili, na watu wangefurahi zaidi. Wengine walishuka chini ya jukwaa kusudi walitazame, na wakasema ya kwamba lilijengwa vibaya. Lakini naliona ya kwamba karibu wote walisimama imara juu ya jukwaa lile wakiwasihi wale walioshuka ili wayaache manunguniko yao, kwa kuwa Mungu ndiye aliyekuwa mjenzi mkuu tena walikuwa wakishindana naye. Wakisimulia kazi ya ajabu ya Mungu iliyowaongoza hata jukwaa lile lililo imara, na wote wakainua macho mbinguni, wakaanza kumtukuza Mungu kwa sauti kuu. Jambo hili liligeuza nia za wale waliokuwa wamenungunika na kushuka chini, na kwa unyenyekevu wakapanda tena juu ya jukwaa”
E.W p. 259
Permiers Ecrits 260,261
Vita kuu uk. 88,89
III. KUANDIKWA KWA KANUNI NYINGINE.
(  KUKOSOA JUKWAA )


Baada ya kifo cha Ellen White aliyekuwa kizuizi cha kuandikwa kwa kanuni, kama  la tunavyoisoma katika kanuni toleo la 15 la mwaka 1995 uk. xx – xxi, viongozi walipata fursa ya kuiandika kwa uhuru. Alikufa tarehe 16 July 1915, na baada ya miaka 17 kanuni ikaandikwa mwaka 1932. ( Kanuni toleo la kwanza uk. 19 ). Tunataka kuwaelezea ubaya wa





kanuni na jinsi inavyopingana na Biblia na Roho ya unabii. Kwa sababu kila baada ya miaka
5  hutolewa kanuni mpya na kanuni hiyo haiondoi kanuni zilizoitangulia bali huziletea maendeleo mapya ndio maana baadhi ya maneno hatutajali ukurasa kwa sababu yanapatikana katika matoleo tofauti ya kanuni hizo.
BAADHI YA MACHAFUKO YA KANUNI.
1.          KUOMBA: Kanuni inawaruhusu watu kumuomba Mungu wakiwa wamesimama (kanisa lote limefuata utaratibu huo) 
Biblia na Roho ya unabii vinasemaje?
“…… kwa nafsi yangu nimeapa, neno hili limetoka kinywani mwangu katika haki, wala
halitarudi, ya kwamba mbele zangu kila goti litapigwa   ISAYA 45:23
-  Yesu mwenyewe aliomba kwa kupiga magoti……………Luka 22:41
-  Mitume wake pia waliomba kwa kupiga magoti…………       Mt. 28:17, Mdo 7:60
-  Stefano japo alikuwa akipigwa mawe alikumbuka kupiga magoti …..       Mdo 9: 40
Mdo 20:36, Mdo 21:5 ( walipiga magoti pwani ),    Waefeso 3:14
-  Waliokuwa wakitaka msaada kwa Yesu walimpigia magoti,        Mt 2:11; 6:5; 9:18; 
Mt 15:25; 17:14; 20:20; 8:2; Marko 10:17; Yh 9:38
-  Na wanyama walimpigia magoti,       Mzo 24:11
-  Hata waliokuwa ndani ya chombo cha majini walimpigia magoti        Mt 14:33
-  Cha kushangaza waliomsulubisha wametushinda kumpigia magoti        Mt 27:29; 
Mko 15:19
-  Manabii na wafalme wa zamani walimuheshimu Mungu kwa kumpigia magoti 
Zab 95:6; Dan 6:10; Ezr 9:5
-  Wengine hutoa udhuru kwamba Hezekia aliomba akiwa amelala, Ni kweli, kwa 
Sababu alikuwa anaumwa. Lakini baada ya kupona alipiga magoti, 
2  Nyak. 29:27-29
N.B. Elewa vizuri mafungu haya;   MARKO 11:25; MATHAYO 5:23
Wengi hutoa udhuru kwa neno linalosema;     “Kila msimamapo na kusali“ au “ukileta sadaka
yako madhabhuni“
Watu wa zamani kabla ya kuomba walikuwa na mahali pa kusimama kwanza, baada ya hapo
wakapiga magoti. M.F. Kuhusu sala ya Suleman “Suleman akasimama mbele ya madhabahu
ya Bwana.........akasema, Ee Bwana Mungu wa Israeli.....“ 1 Waf 8:22-23
Ukishia hapa waweza kudhani kwamba Suleman aliomba akiwa amesimama. Lakini hebu
soma fungu la 54 panaposema “Hata ikawa, Suleman alipokwisha kumuomba Bwana maombi
hayo, na dua hiyo yote, akasimama na kuondoka  hapo mbele ya madhabahu ya Bwana, hapo
alipokuwa amepiga magoti........“


Hapa ieleweke kwamba hakudhubutu kuomba akiwa amesimama, ilikuwa ni desturi kusimama mbele ya madhabahu kabla ya kupiga magoti.
Lengo la Yesu si kusema kwamba ukatize ombi na bali ni kwenda kujiunga na ndugu kabla ya kuomba. Ukisha simama mbele ya mimbari ukapige magoti.





Mfano: “akasimama mbele ya madhabahu ya Bwana machoni pa mkutano wote wa Israeli.....
maana Suleman alikuwa amefanya mimbari ya shaba, urefu wake mikono mitano, na kwenda
juu kwake mikono mitatu, na kuisimamisha katikati ya ua; akasimama juu yake,     akapiga
magoti mbele ya mkutano wote wa Israeli,........., akasema, Ee Bwana Mungu wa Israeli........“
2Nyak. 6:12-14.
Ellen White amesema:
“Watu walinitumia barua wakiniuliza msimamo unaostahili wakati wa kumuomba muumba wambingu na  dunia. Ni wapi ndugu zangu walipotoa wazo la kuomba wakiwa wamesimama? Mtu mmoja aliyejifunza miaka mitano kwenye chuo kikuu cha Battle Creek alichaguliwa kuomba kabla ya mimi kuanza mkutano (Ellen white). Nilipomuona akiendelea kusimama na ombi karibu litolewe mdomoni mwake, moyo wangu uliniuma , ilinibidi nimukemee
hadharani.  Nilimuita kwa jina lake, kisha nikamwambia, ’piga magoti’ ndio msimamo
unaofaa kwa wakati wote“ 
2SM p. 311; Messages choisis vol. 2 p.359
“Katika ibada ya watu wote au mtu mwenyewe peke yake, imetupasa kupiga magoti yetu mbele za Mungu tunapoomba mahitaji yetu kwake. Yesu aliye mfano wetu alipiga magoti akiomba. Paulo anasema, ‘ kwa hiyo, nampigia Baba magoti’ Daniel alipiga magoti mara tatu kila siku, akisali, akishukuru mbele za Mungu wake”
PK 48; Prophete et Rosi p. 31.
“Siku ya hukumu wapagani watatuhukumu kwa sababu wao walipigia miungu yao, magoti miungu yao na wakati sisi hatukumuheshimu Mungu wetu”
2  SM 314; Messages choisis Vol. 2. p 362
“Tuwe na desturi ya maombi ya kimoyomoyo, tutembeapo, tufanyapo kazi, n.k hapo si lazima kupiga magoti” 
2SM 316; Messages choisis vol. 2p.365
2.          UBATIZO: Kanuni inasema ‘ aliye na  mamlaka ya kufanya huduma ya ubatizo ni
mchungaji tu. Kwa dharura ifanywe na mzee wa kanisa aliyepewa mamlaka na fiela’ BIBLIA INASEMAJE?
-  Shemasi anaruhusiwa kubatiza ......... Mdo. 8:38; Mdo. 21:8      ; Mdo. 6:5
-  Mwanafunzi wa kawaida anaruhusiwa kubatiza.....Mdo. 9:10
-  Mtume au mwinjilisti anaruhusiwa kubatiza            1Wakor. 1:14-16
N.B Biblia inasema kwamba, Aaminiye abatizwe” palepale (Mdo.8:38)
Lakini kwa sasa vigezo vya wenye kubatizwa ni pesa, kupewa vibarua na viongozi na mitihani usipofaulu unarudishwa nyuma. Padri (Rumi) peke yake anaruhusiwa kubatiza, na wachungaji wameiga mfano huo. Msishangae kuona mfano huu ukiigwa ndani ya kanisa la Waadventista pia wakiutoa Rumi.
3.          HUDUMA YA NDOA: Kanuni inasema: ‘Miongoni mwa Waadventista wasabato,
wachungaji tu waruhusiwe kufunga ndoa. Hakuna njia nyingine.’ 
Uk. 253 toleo la 1; uk 230 toleo 15 (1995)







‘Mzee wa kanisa hana ruhusa ya kuifanya huduma ya ndoa. Huduma hiyo itafanywa na mchungaji tu’ 
Uk 80 toleo la 1.
Kujipatia mamlaka ya kubariki ndoa kulianzishwa na papa wa 12 jina lake SOTERI      (Orodha
ya mapap uk 5)
Kanisa, kama makanisa mengine, limeiga mfumo huo.
BIBLIA: Biblia haitaji popote kwamba mtu anaweza kubariki ndoa. Mungu tu ndiye anayeibariki ndoa.
-  Alibariki ndoa ya Adam na HawaMzo. 2:18
-  Kwa kumuomba Mungu ndoa ya Isaka na Rebeka ilibarikiwa.   Mzo. 24:11,26,52,63


Kipindi hicho palikuwepo kuhani anayeweza kulinganishwa na mchungaji wa leo
(  Mzo. 14:18) lakini hakuibariki ndoa hiyo.
-   Mchungaji aliyewaumba wachungaji wengine badala ya bwana na bibi arusi naye alialikwa
kuhudhuria arusi (Yh.2:2)    Sio yeye aliyepanga tarehe ya ndoa hiyo kama wafanyavyo
wachungaji wa leo, bali alitoa mchango wake kama watu wengine.
’Mzo 2:24’Kwa maneno haya alitangaza sheria ya ndoa kwa wanadamu wote mpaka
mwisho wa dunia” 
MB p.64
MLIMA WA BARAKA uk.81 


Aliye na jukumu la kubariki ndoa ni Mungu mwenyewe mpaka mwisho wa dunia, bado hajakombolewa na mtu yeyote.
Hakuna mtu anayeweza kuunganisha watu bali wao hupatana (Amosi 3:3 )    . Siku ya harusi
watu huenda kushangilia utimizo wa ahadi ya maharusi. Kujipatia mamlaka hayo ni mbinu ya kutafuta ulaji na heshima kwa mfano, 
-  mahali pengi maharusi huchunguzwa kama wanatoa zaka na sadaka, ikiwa hawatoi
basi hudaiwa.
-  Chakula kizuri cha wachungaji na zawadi zao ( rushwa )
-  Ikiwa mchungaji hayupo, arusi inaahirishwa
-  Desturi za kirumi zimeingia kanisani, mishumaa inawashwa.
-  Sehemu zingine wanawabariki waliokwisha kuoana eti kwa madai ya kukamilisha
ndoa kama wafanyavyo Rumi.
-   
4.KAZI ZA MASHEMASI: Kanuni inasema, ’Ni juu ya mashemasi kuangalia nyumba ya
kanisa na vitu vyake ni wajibu wao kuona ya kwamba nyumba ya kanisa ni safi na kutengenzwa kwa kadri inavyotakiwa. Pia kiwanja cha kanisa kiangaliwe kiwe safi na kizuri
namna ya kupendeza macho.’
Uk. 85-86  toleo la 1.







Pengine walipojaribu kusema kwamba anaweza kuwashughulikia maskini, lakini hajui mali ya kanisa inaenda wapi.
BIBLIA: Biblia inasema kwamba kazi ya mashemasi ni kuhifadhi mali na kuitumia kwa
kugawia wajane na yatima.       Mdo. 6:1-7; Yakobo 1:27; 1Timo. 5:16
“Kuchaguliwa kwa mashemasi saba ili washike majukumu waliyopewa na Mungu, imekuwa baraka kubwa kwa kanisa. Mashemasi hao kwa makini walichunguza kwa makini mahitaji ya kimwili ya kila mtu tena ndio waliokuwa na jukumu la kuitunza mali ya kanisa kwa ujumla. Kwa sababu walikuwa wakiongoza kwa busara na kuwa kielelezo kitakatifu, waligeuka msaada wa thamani kwa ndugu zao kwa kuunganisha kazi tofauti za kanisa.
..........Ijapokuwa mashemasi hao walichaguliwa kuwashughulikia maskini, haikuwazuia moja kwa moja kutangaza injili.“
AA p.;  Conguerants pacifiques p. 79 – 80
5.          VYAMA VYA KANISA: Kwa kuiga mfano wa Rumi iliyoanzisha vyama vya vijana na wanawake (SKAUTI, SAVERI N.K) kanisa lilianzisha vyama ambavyo havipatikani ndani ya Bibli; kwa mfano;
A.                    Chama cha vijana waadventista ( MV, AYO nk) 
Chama hiki, kama vyama vingine, kilianzishwa kwa makusudi ya kutafuta fedha. Ndio maana wakati wa sabato ya AYO washiriki hulazimishwa kutoa sadaka ya chama hicho isiyo na ushuhuda ndani ya Biblia.
Chama hiki kiliwachafua vijana kiasi kwamba wanadhubutu kuingia kanisana wakiwa
wamevaa kofia vichwani (1 WAKOR. 11:4)
Ellen White anasema: “Baadhi ya ndugu hudhubutu kuingia mahali pa kuombea wakivaa
vibaya, pia na vichwa vyao vukifunikwa (kofia). Hawafikiri kwamba wanaenda kukutana na Mungu na malaika zake watakatifu.” 
5T. p. 499; Temoignages pour l’eglise vol 2. 238


Wanafundishwa mazoezi ya kijeshi (high king) wakivaa nguo mfano wa wanajeshi. Wakiwa na gongo au fimbo na kamba kila baada ya makambi yao wanawasha moto, na wengi hawaelewi kuwa ni namna ya kutambikia.


Vijana wanafundishwa michezo ( dansi ) na hivyo wanawavuta watu kutoa pesa nyingi. Hayo yote ni kinyume na neno la Mungu.
“Je, Kama Yesu angeliingia katika makanisa ya Leo Na kuona mambo ya kianasa yaliyomo, sherehe, biashara, ambayo yanatajwa kwa jina la dini asingaliwafukuza kama alivyowafukuza wale wabadili fedha hekaluni zamani? Wakati kanisa limeandaa sherehe za michezo n abahati nasibu kwa kutafuta fedha, linaifanya kazi ya shetani,”
G.C. p. 474; 387; Tragedie des siecles 515, 418



Washiriki wanapofika kwenye mikutano ya namna hiyo wanakumbwa na hadithi na
vichekesho vilivyopo (1Timo. 4:7)   kisha hujitoa kama watu waliovutwa na Roho wa Mungu.
Roho wa Mungu anasema:    “Kwa namna ya kutafuta fedha pasitumiwe mambo ya anasa
yanayoweza kuwasisimua watu. Katika siku zetu hiz, makanisa ndiyo chanzo cha sherhe mbaya, ulafi, kutapanya mali. Mara nyingi makanisa yanaandaa minada, dansi nk kwa mpango wa kukusanya fedha kwenye hazina zao. Huo ni mfumo ulioundwa na akili ya mwanadam, ili ipatikane fedha iliyotolewa bila moyo wa kujitoa.
Tunapaswa kusimama imara bila kuchelewa tukayapinge hayo machafuko ya kanisa..... sadaka zinazopatikana kwa njia hizo zimelaaniwa na Mungu, zinaangamiza roho.“
R&H 21 Nov. 1878; Ministre de la bienfaisance p. 218
Gwaride ( paredi,kwata) za kujionyesha, zimewaharibu sana vijana   , “Lakini kanisa la Kristo
si la kujionyesha“
DA 261; Jesus – Christ p 245
Badala ya kuhubiri injili, vijana wanafundishwa mashindano ya mpira, nk.  Ellen White anasema:  
“Wanaocheza mpira wa miguu, hawatapata Roho mtakatifu“
1SM 131;  Messages choisis vol. 1 p 152.
Kadri siku zilivyoendelea , na mazingira tofauti, ndivyo machafuko yalivyo tofauti.
B.                     Chama cha Dorikas
Hakuna fungu la Biblia wala Roho ya unabii linaloturuhusu kuunda chama hicho.
“Bali, yeyote aaminiye, awe mume au mke, anapaswa kuwa na moyo wa ukarimu kwake kama
Dorikas” Mdo. 9:36 – 40, Waebrania 13:16.


Kanisa limewainua wanawake kiasi kwamba wanaruhusiwa kuwa wachungaji na kubatiza
kinyume na Biblia. Mchungaji lazima awe mwanamume. ( 1 Timo. 3:2 ), mwanamke si
kichwa. ( 1 Wakor.11:3,), Mume ni mfano wa Kristo, mke ni mfano wa kanisa 
(2Wakor. 11:2, Waef. 5:25)  . Chama hicho cha Dorikas pamoja na vyama vingine, mf. Cha
wanaume, havikubaliwi na maandiko.
NB. Tukumbuke kwamba kila chama kina Sabato yake, mf. Sabato ya Dorikas, Sabato ya vijana, nk. Je, Sabato ya Mungu iko wapi? Hizo ni mbinu za kutafuta ulaji, Sabato zote ni za Bwana Mungu wetu, pasiwepo Sabato ya mtu au ya chama chochote, hiyo ni Sabato bandia na si ya Mungu.
6.          AINA ZA SADAKA: Kanuni inaruhusu kuwa na aina nyingi ya sadaka kinyume na    Biblia, mf. Sadaka ya Dorikas, sadaka ya AYO, sad, sadaka ya union, ya field, sadaka ya shukrani, sadaka ya kuzaliwa, sadaka ya ss, sadaka ya makambi, n.k.
Biblia: Biblia haisemi kitu kingine isipokuwa  zaka na sadaka tu. Zaka ni sehemu ya kumi ya
pato lako, (Mzo. 14:20, Walawi 27:30 – 32, Malaki 3:10).
SADAKA ni nini? Baada ya kutoa zaka, unaweza kutoa kwa kushukuru, kwa kusaidia n.k
kulingana na jinsi unavyovuviwa na Roho wa  Mungu. (2Wakor.9:7 )    . Sadaka zote ni kitu
kimoja na si aina nyingi.





7.          VYETI / VITAMBULISHO VYA WATENDAKAZI: Kanuni inakataza watu kutangaza injili bila kuwa na vitambulisho.
(  1Wathes. 2:16 ).Kanuni inasema: ‘Watendakazi wote wa kanisa la waadventista wa sabato
wastahili kupewa cheti cha kawaida. Vyeti hutolewa na baraza zenye mamlaka na hufaa kwa mda ule ulioandikwa juu yake…….ijapokuwa anacho cheti kilichokoma, hana mamlaka ya kutenda kazi ya mhudumu’
Kanuni uk. 169 toleo 1; Kanuni uk. 149 toleo 15 (1995)
Biblia inasema: “Basi enendeni ulimwenguni kote, mkawafanye mataifa kuwa wanafunzi
wangu, mkiwabatiza kwa jina la Baba, na Mwana na Roho Mtakatifu, na kuwafundisha
kuyashika yote niliyowaamuru ninyi…” Mt. 28:19
Ellen White anasema: “Agizo la mwokozi huwahusu waumini wote mpaka mwisho wa wakati.
Ni kosa kubwa kudhani kuwa kuokoa roho inawategemea wachungaji wenyewe. Wote waliompokea Roho wa Mungu hujiunga na kazi ya injili. Wanaokubali kupokea uzima wa Kristo mioyoni mwao, hapo hapo wamechaguliwa kufanya kazi ya kuwaokoa wenzao. Kanisa lilianzishwa kwa ajili ya kufanya kazi hii, tena wanaojiunga na kanisa wote wameahidi kuwa tangu hapo ni watenda kazi pamoja na Kristo.”
DA p. 822; Tumaini la vizazi vyote uk.464; Jesus Christ p822 – 823.. 
“Bwana anataka tena anaweza kuwatumia watu ambao si wenye elimu kutoka vyuo vya dunia. Kuwa na mashaka kwa jambo hilo, ni ishara ya kutokuamini; na kuweka mpaka dhidi ya nguvu za muweza yote. Jinsi gani kazi iliyotendwa na watumishi hao huwa inadharauliwa! Jinsi gani watumishi hao wanadharauliwa sana! Kuwa na mashaka juu ya watumishi kama hao, ilileta hasara kubwa kwa sababu nguvu nyingi za kanisa zilikufa bure; ilifumga milango na kumzuia Roho Mtakatifu asiwatumie watu. Iliwaletea wivu wale ambao walikuwa wanataka kutumika kulingana na agizo la Kristo; iliwadhoofisha wengi waliokuwa wanataka kuingia katika kazi ya Bwana, tena wangelipewa nafasi wangekuwa watumishi wazuri wa Bwana” 
G.W. Ministre evangelique;  476 SC. 31 – 32; ChS pg. 24 – 25
Ellen White anaendelea kusema:
“Baadhi ya ndugu zetu viongozi huwa wanaonyesha roho ile ya Yohana aliposema: ‘Mwalimu, tulimuona mtu akitoa pepo kwa jina lako ambaye hafuatani nasi; tukamkataza kwa sababu hafuatani nasi’ utaratibu na adabu ni muhimu, lakini kuna hatari kubwa ya kujitenga mbali na unyenyekevu wa ujumbe wa Kristo. Tunachohitaji ni kufungamana na nguvu za utakaso wa kweli, kuliko kuongozwa na kanuni na desturi za kidini. Acheni wenye vielelezo vizuri kwa tabia na maisha waingie kazini, watumie vipawa vyao vyote. Wajapotenda kazi tofauti na taratibu zenu, msiseme neno hata moja la kuwahukumu au la kuwadhoofisha. Wakati mafarisayo walipomwambia Yesu kuwanyamazisha watoto waliokuwa
wakiimba sifa za Mungu, Bwana aliwaambia, ‘Wakinyamaza hawa mawe yatapiga kelele’
Luka 19:40, lazima unabii utimie………………..Mungu alimpa kazi mtu kulingana na uwezo
wake. Watu waliopewa vipawa vya muhimu na Mungu hawawezi kunyamazisha kimya, wale walio na vipawa vidogo vidogo ambao hawajaelimika. Wenye talanta moja, mbili au tano hawezi kulifikia. Watu mashuhuri na watu wa kawaida nao ni vyombo vilivyochaguliwa ili vifikishe maji ya uzima kwa wenye kiu. Wahubiri wa neno la Mungu wasije wakamwambia mtumishi mwenye talanta moja eti, ‘kama hautaki kufanya kazi kulingana na utaratibu wetu,





acha.’ Kila mtu atende kazi kulingana na ujuzi na uwezo wake, akivaa silaha zote, akiwa na unyenyekevu, ndipo vipawa vyake vitaongezeka. Wakati wetu huu si wa kuinua ufarisayo, acheni Bwana amtumie anayempenda. Kinachotakiwa ni kutangazwa kwa ujumbe.”
5  T. pg. 461 – 462; Temoignages pour l’ eglise vol. 2 p. 193 – 194
Ellen White anaendelea kusema:
“Wale wanaohusika na uongozi wa taifa la Mungu,…….wasidhani kwamba kila kazi itatendeka kwa kibali cha mihuri yao…..”
9  T.259; Temoignages pour l’ eglise p. 484 – 485
Vibali vya wana wa Mungu sio vikaratasi. Neno la Mungu linasema kwamba, vibali vyetu ni kuwa na ukweli na tabia nzuri. 
Ellen White anasema:
“Mungu anaweza kumtumia mtu yeyote wakati anapomkubalia kumimina Roho wake moyoni mwake. Kazi inayokubaliwa na Mungu ni ile ionyeshayo sura yake. Wanafunzi wa Kristo wanapaswa kuwa na tabia za kudumu zifananazo na kanuni za ukweli zisizokuwa na kikomo. Hicho ndicho kibali chao duniani.“
7  T. Pg. 144; Temoignages pour l’ eglise vol.3 p.169; SC pg. 297, ChS. 244
“Ninyi ndinyi barua yetu iliyoandikwa mioyoni mwetu inajulikana na kusomwa na watu wote; mnadhihirishwa kwamba mmekuwa barua ya Kristo tuliyoiratibu, iliyoandikwa si kwa wino, baki kwa Roho wa Mungu aliye hai; si katika vibao vya mawe, ila katika vibao ambavyo ni mioyo ya nyama.” 
2  Wakori. 3: 2 – 3
8.          KUJIUNGA NA ULIMWENGU. ( Serikali na Madhehebu mengine )
Kanuni inasema: ’Ili adui wa kazi yetu wasipate nafasi ya kutumia mimbari zetu, tunasihi
sana washiriki wasimuruhusu mtu yeyote kuhubiri katika mkutano asipoonyesha cheti cha kanisa letu kinachofaa kwa tarehe za siku hizi. Inafahamika ya kwamba pengine hufaa kwa watu wa serikali au utawala, ama wakuu wa mji, au nchi, kutoa hotuba kwa washiriki wetu, bali wote wengine wakatazwe wasitumie mimbari zetu.“
Kanuni uk. 168, 104 Toleo la 1.
Kanuni uk. 149 Toleo la 15 ( 1995 )


Hapo panaonyesha umoja wa kanisa na serikali.
Katika kitabu cha kanuni ya mzee wa kanisa kilichoandikwa na halmashauri kuu ya waadventista wa sabato 12501 Old Columbia, Pike, Silver spring, Maryland 20904 U.S.A.  cha mwaka 1994 katika somo linalosema “SHEREHE YA KUTENGENZA KIWANJA“ Panaonyesha kwamba tuna umoja na madhebu mengine.
BIBLIA   inasemaje?
“.........Usifanye agano nao, wala kuwahurumia; wala usioane nao...“ Kumb.   Torati 7:2






“Msifungiwe nira pamoja na wasioamini, kwa jinsi isivyo sawa; kwa maana pana urafiki
gani kati ya haki na uasi? ……..au yeye aaminiye ana sehemu gani pamoja na asiyeamini?” 2
Wakor. 6:14
Roho ya unabii   inasemaje?
“Siasa ya dunia na kanuni imara za ukweli wa Mnugu, ni vitu viwili tofauti visivyoweza kuambatana hata kidogo kama rangi ya upinde wa mvua. Mungu wa milele aliweka mstari dhahiri kati ya kanuni hizo. Sura ya Kristo hutofautiana na ya shetani kama mchana na
usiku.“ DA 313; Jesus Christ p 302; Tumaini la Vizazi uk. 168.
“Wakristo wa kwanza walikuwa taifa la pekee. Mwenendo wao usio na waa na imani yao imara vilikuwa ni kemeo la kuvuruga amani kutoka kwa wenye dhambi. Ijapokuwa walikuwa wachache, bila mali, bila usajili serikalini na bila majina ya heshima, walikuwa tishio kwa wavunja amri za Mungu popote ambapo tabia na imani yao vilikuwa vimejulikana.” 
G.C. 46; Tragedie des siecles 46
“Umoja wa kanisa na serikali kwa kiwango chochote ikiwa umoja huo ni wa kukaribisha ulimwengu kwa kanisa, matokeo yake ni kugeuza kanisa kuwa kama walimwengu.“
GC 297; Tragedie des siecles 319 – 320



“Sasa, kama ilivyokuwa siku za Kristo, wanaofanya kazi ya kujenga ufalme wa Mungu ni watu ambao hawatamani kujulikana serikalini au kupewa msaada na tawala za kidunia au kutegemea sheria zilizotungwa na wanadamu.“
DA 510; Jesus - Christ 507; Tumaini la vizazi vyote uk. 287.
N.B. Maneno haya hayamkatazi mtu binafsi kutii sheria za serikali ikiwa hazipingani na
sheria za Mungu. ( Warumi 13:1 – 7; Mdo. 5:29; Mdo 4: 19 )
Kanisa ni mtumishi wa Mungu, na serikali pia. Lakini tangu zamani, kabla mfalme kufanya chochote, alikuwa anafuata ushauri na sheria kutoka kanisani 
(  Kumb. 17:18; Malaki 2:7; 1Wafalm 22:7 – 8)
Aliyepewa “........mamlaka yote mbinguni na duniani, Mat.28:18“ NDIYE ALIYETUMA
AKISEMA: “Basi, enendeni mkawafanye mataifa yote kuwa wanafunzi....“      Mat. 28:19.
Hatuna haja ya ruhusa kutoka kwa mwanadamu.
MUUNGANO WA KANISA NA MADHEHEBU MENGINE.


Ellen White alionyeshwa harakati za kuunganisha makanisa yaliyokuwa yakipinga 
(  protestant ) imani ya kirumi. Tunasoma kuwa:
“Watu wengi huamini kuwa kwa kuwa kuna tofauti nyingi katika makanisa  ya kiprotestant, haitawezekana kuwaunganisha wote katika imani moja. Lakini miaka kadhaa kumekuwa na msukumo mkubwa katika makanisa hayo wa kutaka waungane kwa baadhi ya mafundisho ya imani. Ili wafikie umoja huo, wanajilinda kujadili mafundisho ambayo hawakubaliani, japo Biblia inayaunga mkono.“ 
GC 444; Tragedie de siecles p. 481; Pambano kuu uk. 255





Ellen White anasema:
“Kamwe hatupaswi kuwa na mapatano na watu waabuduo sabato ya miungu. Hatupaswi kupoteza mda kujadili  na watu waliojua ukweli na nuru ya Mungu ikawaangazia, lakini wakaamua kuacha ukweli na kugeukia  hadithi za kubuni. Nimeambiwa kwamba baadhi ya watu watafanya iwezekanavyo ili waondoe tofauti inayowatenganisha waadventista wa Sabato  na waabuduo siku ya kwanza ya juma, jumapili. Walimwengu wote watapigana vita
hiyo, tena mda ni mfupi. Huu sio wakati wa kushusha bendera yetu.....
Nilionyeshwa kundi la watu waliojiita waadventista wa Sabato wakiwaamuru washiriki wasiendelee kuinua ishara ya bendera inayotutenganisha , wakisema, ’inaweza kuhatarisha taasisi zetu’. Lakini bendera hiyo lazima ipepee ulimwenguni  kote mpaka kufungwa kwa mlango wa rehema. Yohana alizungumzia masalio wa Mungu akisema: ‚’Hapa ndipo penye
subira ya watakatifu, hao wazishikao amri za Mungu na imani ya Yesu’     ufun. 14:12. Hii
ndiyo sheria na injli. Makanisa na ulimwengu yanaungana   pamoja kuvunja sheria ya Mungu,
kuondoa kumbukumbu ya Mungu na kuinua sabato bandia yenye mhuri wa mtu wa kuasi.
Lakini Sabato ya Bwana Mungu lazima iwe ishara ya kutofautisha wanaomtii Mungu na
wasiomtii Mungu. Nilionyeshwa watu walioinua mikono yao ili kuondoa bendera na kuweka
giza juu ya tafsiri zake.“
2  SM 385; Messages choisis vol 2. p. 433
Tumbuke kwamba bendera hiyo ni Amri za Mungu na nembo yake au ishara ni Sabato.
Ellen White anasema: 
“Msitari wa kutenganisha kati ya wanafunzi wa Yesu na wa shetani kamwe usifutwe. Mungu mwenyewe aliweka msitari wa kutenganisha kanisa na dunia, aliweka kati ya washikao Amri zake na wavunjao A mri zake, hawawezi kupatana. Wanatofautiana kama mchana na usiku, wana utofauti wa ladha na utamu, malengo yao ni tofauti, shughuli na tabia zao ni  tofauti. Ikiwa tunashikamana na upendo na utiifu kwa Mungu, tutachukia uhusiano wowote unaoweza kututia uchafu.“ 
5  T 602; Teimoignages pour l’ eglise vol. 2 p. 288
Kwa sasa kanisa limeshajiunga na dunia na madhehebu mengine. Ellen White anasema:
“Mkanisa mengi ya kiprotestant yamefuata mfano wa Rumi kwa kuungana na wafalme wa dunia; makanisa yanapokubalika serikalini, yanapojiunga na serikali hizo, pia na kujiunga na madhehebu mengine kwa kufuata kupendwa na dunia, neno’ BABELI’ au machafuko lazima liitwe kwa makanisa hayo, yanapodai kupata mafundisho yao kutoka katika Biblia, na wakati bado yanagawanyika katika vidhehebu vingi mno ambavyo vinapingana kwa mafundisho.“ 
GC 383; Tragedie des siecles p. 414; Pambano kuu uk. 221.
Sanamu ya mnyama haiwezi kutimia kabla ya kanisa kuasi. Ellen White anasema:
“Uasi uliongoza kanisa la kwanza kuomba msaada wa serikali, na hii ilitayarishia upapa njia, yaani,’mnyama’. Paulo alisema: ‚’’utakuja ukengeufu. Akafunuliwa yule mtu wa kuasi’’
2  Wathes. 2:3,vivyo hivyo, uasi wa kanisa utatayarisha sanamu ya mnyama“
GC 443; Tragedie des siecles p. 480 – 481; Pambano kuu uk. 255


 ___________     _____________________________________




Kwa uhakika wa kanisa la waadventista wa Sabato kujiunga na umoja wa makanisa, tembelea
tovuti ya umoja wa makanisa yaani www.wcc-coe.org  nenda hadi ecumenical links, church
graphics scroll hadi christian communion utalikuta kanisa la waadventisata likiwa la saba
kwenye orodha hiyo ya makanisa likiwa limeandikwa Genaral conference of Seventh Day
Adventists  Chini ya ``Christian Communion`` ambacho ni kitengo cha umoja wa makanisa.


NB. Katika ujumbe utakaofuata, tutawaeleza mengi kuhusu muungano wa madhehebu likiwemo la waadventista wasabato.
9.          MUONGOZO WA KANISA – Kanuni ( Papa anakubaliwa kama kiongozi na kanisa la waadventista.).
Kanuni inakubali aina nne za kutawala kanisa. Cha kushangaza, PAPA kiongozi mkuu wa Babeli , na yeye anakubaliwa kama kiongozi wa kanisa.
Kanuni inasema: ‚’Ziko namna nne za utawala wa kanisa, nazo ni hizi:
1.                      utawala wa maaskofu
2.                      Utawala wa papa
3.                      Utawala wa kanisa moja kwa moja ( independent )
4.                      Utawala wa wajumbe ( representative – federatif )
Kanuni uk. 43 Toleo la 1; Kanuni uk. 25 Toleo la 15 ( 1995 )
BIBLIA: Kanisa la Mungu halina kiongozi wa dunia yote isipokuwa YESU tu. 
(  Waef. 1:22; 4:15)
Wakati mitume walihubiri injili na kuunda makanisa, na kila kanisa lilichagua mzee wa kanisa, yaani askofu, mchungaji ( pasta ) espicope, haya majina yote ni cheo kimoja na ofisi
moja na kazi moja. ( 1 Timo. 3:1- 5; Tito 1: 5 – 9; Mdo. 14: 23 ). Karibu na mzee wa kanisa
kuna mashemasi wanaohusika na kupokea mali, kuzitunza na kuzigawa kwa wahitaji n.k.     (
Mdo. 6:1 – 7; 1Timo. 5:16; Yakob. 1: 27 ). Mfumo wa uongozi wa makanisa ya leo
unaofanana na ngazi za kiserikali za kidunia, haupatikani ndani ya Biblia. Sisi tunaitwa kurudi
kwenye msingi wa mitume. “Mmejengwa juu ya msingi wa mitume na manabii, naye Kristo
Yesu mwenyewe ndiye jiwe kuu la pembeni“ Waef. 2:20


Ellen White anasema: 
“......vivyo hivyo hatuwezi kushuhudia ndani ya maandiko kuwa vipawa vya Roho vimeondolewa. Na kwa kuwa milango ya kuzimu haikufaulu kulitikisa kanisa, na mpaka sasa bado Mungu angali na taifa lake duniani. Tuwe tayari tutaona vipawa vikiinuka ndani ya kanisa vikitokana na uhusiano wa ujumbe wa malaika wa tatu, ujumbe utakaorejesha kanisa kwenye msingi wa mitume, utaupatia ulimwengu nuru na wala sio giza.“
EW 137 – 138; Premier ecrits p. 138.
“Hebu kanisa lirejee kwenye imani na nguvu iliyokuwemo wakati wa kanisa la mitume ndipo roho ya mateso itainuka na moto wa mateso utawashwa“
GC 48; Tragedie des siecles p. 48; Pambano kuu uk. 29.
10.      IBADA YA WAFU.
Vikitoka Roma, vifo na mazishi vimegeuka kuwa sherehe kuu zenye desturi ambazo hazipatikani ndani ya maandiko matakatifu. Kanisa nalo limechukua desturi hizo kutoka Roma.





Kanuni inasema: ‚’....Ikiwa ni lazima kufanya mazishi siku ya Sabato, basi watu waangalie ili
mazishi yasizuie huduma za kawaida katika nyumba ya Mungu.....“
Maiti inapelekwa kanisani, kanuni inasema: ‚’Watu wakiisha kuketi kanisani, omba sala fupi
ya kwamba Mungu afariji kila moyo kwa ahadi yake ya ufufuo na hivyo kuliangaza giza la kaburi. Kisha mafungu ya maandiko matakatifu yatasomwa mengi au machache kwa kadri ya
umri na maisha ya marehemu.....“
“..............kisha sala fupi ifuate yenye shukrani kwa wema wote wa Mungu kwake yule
marehemu.......“
Kanuni uk. 245 – 246 Toleo la 15 ( 1995 )
Ukweli ni kwamba, kufanya mazishi siku ya Sabato ni kuvunja Sabato, ni kazi inayoweza kuahirishwa kwa sababu si kuponya.
Mat. 12:12 ; PP 307; PP (Fr.) 280.
Baada ya kuingia kwenye muungano wa makanisa, na kukubali Biblia ya muungano wa makanisa, ndipo kanisa lilianza kupeleka wafu kanisani na kuwaombea wakijitegemeza katika
fungu la Biblia bandia la  2 MAKABAYO 12:45. Biblia Takatifu inaeleza kwamba,      “Wafu
hawajui neno lolote“   Mhubiri 9:5,10. kuwaombea haifai kitu. Kuhusu desturi za mazishi,
Ellen White anasema:
“Wakati wa Kristo, kwenye makaburi ya wafu, palifanyikia desturi za mila potofu, tena walikuwa wanatumia fedha nyingi kwa kuyapamba. Machoni pa Bwana hivyo ilikuwa  sawa na kuabudu miungu. Wakati watu wanapowapatia wafu heshima kuu, ni kuonyesha Kwamba hawampendi Mungu kuliko vyote, wala hawawapendi ndugu zao kama wanavyojipenda. Kuomba  miungu kwa namna hiyo, na leo kumeenea pote. Huwa wengi wanasahau wajane, yatima, wagonjwa na maskini wakati wanajengea makaburi ya waliokufa ya ukumbusho kwa gharama kubwa, wakapoteza mda mwingi, fedha na nguvu nyingi, kisha wakapuuzia majukumu waliyopewa na Kristo ya kuwashughulikia walio hai.“
DA 618; Jesus – Christ  616
“Wengi, zawadi zao za thamani wanawapelekea wafu. Maneno mengi ya upendo yanatajwa juu ya maiti, wakatumia maneno ya huruma na sifa kwa mtu ambaye hasikii tena, maneno hayo yangelikuwa harufu nzuri kama angaliambiwa mwenye masikio ya kusikia na roho ya kutafakari“
DA 560; Jesus – Christ 555
“Kuna tofauti kubwa kati ya mazishi yanayokubaliwa na desturi za mila potofu za wakati wetu. Siku zetu, mazishi ya watu mashuhuri yaligeuka na kuwa ya  kujionyesha na kupoteza mali. Heshima ya Mungu haiwezi kuambatana na wingi wa mila potofu, zinazosindikiza wafuwanaorudi mavumbini.“ 
PP. pg.406.
11.      MAANA YA KUKARIPIA
Kanuni inasema: ‚’ Neno la kukaripia ni kwa mda fulani unaotajwa, kwa mfano mwezi
mmoja, miezi mitatu, miezi sita ama miezi tisa....’
KANUNI uk. 224 Toleo la ;. KANUNI uk. 198 Toleo la 15 (1995)





Pengine kuna viwango vya dhambi kwa mwenye kukaripiwa ili arudishiwe ushirika  wake, lazima abatizwe.
BIBLIA:  „“Na ndugu yako akikukosea, enenda ukamuonye wewe na yeye peke yenu,
akikusikia, umempata nduguyo, la! Kama hasikii, chukua pamoja nawe tena mtu mmoja au wawili ili kwa vinywa vya mashahidi wawili au watatu kila neno lithibitike. Na asipowasikiliza wao, liambie kanisa; na asipolisikiliza kanisa pia, na awe kwako kama mtu wa mataifa na mtoza ushuru. Amini nawaambieni, yoyote mtakayoyafunga duniani yatakuwa
yamefungwa mbinguni.......“ Math. 18:15 – 18
Wakati mwenye dhambi amekiri dhambi zake, hapohapo anakubaliwa, iwe duniani au
mbinguni. (Yeremia 3:13 – 14 ; Mat. 18:15).    Hatuoni miezi ya karipio ndani ya Biblia.


Kama mwenye dhambi hatatubu ( ungamo ), ataendelea kuwa mwenye dhambi milele. Shida tuliyonayo ni kwamba, wakosaji wanapopewa miezi ya karipio, badala ya kuungama ili wasamehewe na Mungu, wanasubiria mwisho wa miezi ya karipio, pasipo kuungama, miezi si
kafara ya dhambi. Yakobo 5:16; Mithali 28:13


Kwa Mungu dhambi zote ni dhambi, hakuna dhambi inayomfanya mtu abatizwe mara ya pili na dhambi nyingine asibatizwe.


Kama ametenda kinyume na utaratibu wa kanisa ( uwe wa maandiko au usiwe wa maandiko ),
mara nyingi wanatenga mtu kwa kutumia fungu hili la Mathayo 18:18. maneno haya
hayamruhusu mtu yeyote kuhukumu. Ellen White anasema:
“........Mathayo 18:15 – 18------ wakati mkosaji amewakatalia watu wawili au watatu, ndipo sasa shauri hili litaletwa mbele ya kundi lote la washiriki. Hebu washiriki wote waungane
katika maombi kama wawaklishi wa Kristo,wakimsihi ndugu huyo apate kurudi........mtu anayekataa maneno haya ya upatanisho huwa amejiondoa mwenyewe kutoka kwa Kristo. Kwa hiyo, Kristo aliseama’ awe kwako kama mtu wa mataifa na mtoza ushuru’. Wasimuhesabu kama mtu aliyeishiwa na neema za mbingu. Lakini asidharauliwe na kutojaliwa na ndugu zake wa kwanza, mtendee kwa fadhili wala si kwa uhasama kama kondoo wa Kristo anayemhitaji kumrudisha zizini.“
DA 441; Jesus – Christ 438 – 439; Tumaini la vizazi vyote uk. 251.
“Wowote mtakaowaondolea dhambi, wameondolewa; na wowote mtakaowafungia dhambi,
wamefungiwa. Yoh. 20:23 Hapa Kristo hakumpa yeyote ruhusa ya kuwahukumu wengine.
Katika hubiri lake mlimani Yesu alikataza mambo hayo. Hii ni haki ya Mungu tu. Lakini kanisa kama shirika, lina majukumu na uwezo kwa kila mshiriki. Kwa wale wenye kuanguka katika makosa, kanisa lina haki ya kuwaonya, kuwafundisha na ikiwezekana kuwarudisha tena kwa waaminifu……..kama wakidumu dhambini; hukumu unayowakatia kufuatana na neno la Mungu, hupitishwa mbinguni.”
DA 805; Jesus – Christ  p. 806; Tumaini la vizazi vyote uk. 454 – 455
N.B. Utofauti wa kanuni na Maandiko Matakatifu, tutaendelea kuwaeleza katika makala zitakazofuata.





Ijapokuwa Mungu alikataa kanuni nyingine isipokuwa Biblia na Roho ya unabii
(  Review & Herald 8 Oct 1861 )lakini kanisa limeagiza washiriki kuinua kanuni zaidi ya vitabu vyote.
“Kanuni ya kanisa, na kanuni ya mzee wa kanisa, vitabu hivi vizingatiwe sana, tena kila mzee wa kanisa awe navyo. Kitabu cha kanuni za kanisa, kitabu kilichochaguliwa na halmashauri kuu ya kanisa duniani kote, lazima kipewe nafasi ya kwanza kabla ya kitabu kingine chochote……”
(  DIBAJI ) KANUNI YA MZEE WA KANISA
12501 Old Columbia pike, Silver spring, Maryland 20904 U.S.A, 1994.
“Lakini Mungu atakuwa na watu wenye kushika Biblia na mafundisho yake peke yake, kuwa ndizo kanuni za maisha na msingi wa mafundisho na matengenezo yote. Mawazo ya wataalamu, na tafsiri potofu za Biblia wanazoaeleza watu wa sayansi, kanuni na mashauri ya kidini yanayofanywa na kuamuliwa na mabaraza kwa kura ya wengi, hata moja wapo lisingefikiriwa kuwa ushahidi wa mafundisho ya imani. Kabla ya kukubali mafundisho na
maagizo yoyote, sisi tungeshikilia neno kuwa, ‘Ndivyo asemavyo Bwana’”
GC 595; Tragedie des siecles 645
III. UDHURU WA LAODIKIA.
“Kwa kanisa lisilo na uhai, lisilo na Kristo, shahidi mwaminifu asema: ‘ Nayajua matendo yako ya kuwa hu baridi wala hu moto; ingekuwa heri kama ungekewa baridi au moto. Basi kwa sababu una uvuguvugu, wala hu baridi wala moto, nitakutapika utoke katika kinywa
changu’ Ufunuo 3:15 – 16. tahadhari sana kwa maneno yafuatayo: “kwa kuwa wasema,
mimi ni tajiri, nimejitajirisha, wala sina haja ya kitu; nawe hujui ya kuwa wewe u mnyonge na mwenye mashaka, na maskini, na kipofu na uchi. Ufun.3: 17. tazama hili ni taifa linalojivunia ujuzi wake wa mambo ya kiroho na mali zake. Lakini halikujali mibaraka lililopewa na Mungu ambayo halikustahili. Limeshajaa uasi na halina shukrani kwa Mungu wake, limemsahau Mungu wake aliyelisimamia kama mzazi mwenye huruma kwa mtoto aliyemkosea. Lilipinga neema yake, likaharibu fursa liliyopewa, muda wa heri likauacha bila kuutumia, limelala katika usingizi wa kujitumaini desturi zisizo na maana na unafiki, tena halina shukrani kiasi cha kutisha. Kwa kujitwika kiburi cha mafarisayo, limejisifu kiasi
kwamba Mungu alisema kwake hivi:   Ufunuo 3:17”
1  SM 357 – 358; Messages choisis vol. 1 p. 418 – 419
Ellen White anaendelea kusema:
“Mungu hakubadilisha lolote kuhusu watumishi wake waaminifu waliolinda mioyo yao bila mawaa. Lakini wengi hupaza sauti na kusema: ‘Ni amani, amni na usalama’ bila kujua kwamba wanakaribiwa na uharibifu wa haraka wasipotubu kikamilifu, wasiponyenyekeza mioyo yao kwa ungamo na kupokea ukweli kama ulivyo katika Yesu, hawawezi kamwe kuingia mbinguni. Wakati tohara itatendea kazi miongoni mwetu, hatutaendelea kufurahishwa na majivuno ya utajiri wetu na kusema kwamba hatuna haja ya kitu. Nani, kwa kweli, anayeweza kusema: ‘dhahabu yote imejaribiwa kwa moto, mavazi yetu hayakuchafuliwa na ulimwengu?’ nilionyeshwa mwalimu wetu akichana nguo zao wanaojifanya wenye haki na kuweka wazi uchafu wao na machafuko chini ya tanda jeupe,




jinsi gani mji wa Baba umegeuka KAHABA! Nyumba ya Baba imegeuka mahali pa biashara, ambapo, kuwepo kwa Mungu na utukufu wake vimeondolewa! Ndiyo sababu kuna udhaifu na nguvu zinakosekana”
Endapo kanisa lililojawa na uasi lisipotubu na kujirudi, litakula matunda ya matendo yake mpaka litakapojigeuza binafsi kuwa chukizo…”
8  T 250; Temoignages pour l’ eglise vol. 3 p. 302 – 303


Kulingana na maneno haya, ni dhahiri kwamba kanisa limeasi, limekuwa KAHABA, NI NYUMBA YA BIASHARA. Ukilionya kanisa, ulimwenguni kote udhuru ni:
“USILIITE KANISA BABEL”
1.          FAHAMU VIZURI MANENO HAYA:. (Usiliite kanisa babeli)


Kumbukeni kwamba, kuna tofauti kati ya vitabu vya Roho ya unabii  kama;( GC, PP, PK, AA, COL, DA, nk. ), na shuhuda, yaani TESTIMONIES.
4  T. 390; 5 T. 681; Colparteur Ministry 124 – 130; Temoignages pour l’ eglise vol. 2. p341.


Vitabu vya Roho ya unabii vinawalenga watu wote na nyakati zote.
Vitabu vya shuhuda vilitolewa kama kuwakemea watu wasiojali neno la Mungu. 
5  T 666 – 667; Temoignages vol. 2 p. 331 -332
NB. Ellen White anasema kwamba, kwa kutumia shuhuda, ni kuzingatia muda, mahali na
walengwa.
“Katika yote yanayopatikana ndani ya shuhuda, hakuna cha kudharauliwa, hakuna cha kutupwa; lakini, ni lazima kuzingatia muda na mahali. Tusiliweke jambo katika nafasi isiyo yake. “
1  SM 58; Messages choisis vol 1. p 65
Wakati Ellen White aliposema, ‘Usiliite kanisa la waadventista kuwa ni babeli’ mnamo
mwaka 1893, alikuwa anawalenga watu wafuatao:
“Kwa kawaida, ujumbe wa kulihukumu kanisa na viongozi ulikuwa umepelekwa na kikundi kilichojidai kwamba wamepewa nuru mpya; mara nyingi na tarehe ya kurudi kwa Yesu iliwekwa. Mchakato (movement) wa namna hiyo unaojulikana kwa jina la ‘kilio kikuu cha malaika wa tatu’ kiongozi alikuwa ni Mr. Stanton, tulipingana naye katika shuhuda zilizotolewa mnamo mwaka1893 katika Review and Herald kichwa cha maneno kinasema. ‘Kanisa la masalio si babeli’ (Maneno hayo yaliingizwa katika kitabu cha Testimonies to ministers 32 – 36, kadhalika katika kitabu cha The Remnant Church p. 23 – 53). Vipengele vyote vya somo hilo vinasonda kikundi hicho tena vinaorodhesha vikundi vingine vilivyoinuka na msimamo kama huo…..) 
2  SM 62; Messages choisis  vol.2 p. 71.


Wakati M. Stanton alipoona makosa ya watu kanisani, aliamua kuacha shule na kutangaza kuwa kanisa limegeuka kuwa babel, Ellen White alimuandikia kuwa:





“Ninakushauri, endelea kukaa shuleni ……..Bwana hakukupa wewe ujumbe wa kuwaita waadventista Babeli, na kuwaita watu wa Mungu watoke kwake, sababu zote uwezazo kuzitoa haziwezi kuwa na uzito kwangu juu ya somo hili…..” 
2  SM 63; Messgaes choisis vol 2. p 72 ( 1893 )
Palikuwa pameinuka mchungaji K. na uongo mwingine tofauti ikiwemo na maneno ya kuliita kanisa babel.
2SM 64; Messages choisis vol. 2 p. 73, messages choisis Vol 1. p 207      
Pia na N. wa Red Bluff, Kalfonia alitusumbua sana, akili yake ilikuwa imechanganyikiwa  ilitulazimu kumpeleka hospitali” 
2  SM 64; Messages choisis vol 2. p 73
“…..mwingine alikuwa anaitwa Garmire……alikuwa na mabinti waliojidai kwamba wamepewa maono” 
2  SM 64, 72, 79; Messages choisis vol. 2 p 73, 82 – 90


Hao waliinuka wakati kanisa lilikuwa na udhaifu, lakini lilikuwa bado halijatimiza sharti (condition) za kuligeuza kuwa babeli. Kwa kanisa dhaifu, Ellen Whit anasema:
“Tungepewa kukumbuka kuwa, kanisa, ijapokuwa liwe    dhaifu na pungufu kiasi gani, ni
chombo peke yake duniani ambacho Kristo huweka juu yake heshima kuu. Anaendelea kulishughulikia na kuliangalia sana, na analiimarisha kwa Roho wake Mtakatifu.” 
2  SM 396 (1902); Messages choisis vol. 2 p. 457 (1902)
Kwa sasa, kanisa limeasi neno la Mungu kwa kujiunga na dunia na madhehebu mengine, kwa kanisa la namna hiyo, Ellen White anasema:
“Wakati kanisa linapodhihirika kutokuwa na uaminifu kwa neno la Bwana, ijapokuwa msimamo wao uweje, ijapokwa wito wao uwe wa juu na mtakatifu kiasi gani, Bwana hawezi kuendea kutenda kazi pamoja nao. Wengine huchaguliwa  kushika majukumu haya muhimu…..” 
14 MR (1903); Matukio ya siku za mwisho 54
Kanisa lolote linalopinga mafundisho ya Roma, wakati linapojiunga na serikali na madhehebu mengine, linastahili kuitwa BABEL.”
GC  383; Tragedie des siecles p. 414


Hizo ndiyo sharti ( condition ) za kuligeuza kanisa BABELI.
“Ikiwa tunaasi ushuhuda wa neno la Mungu, na kufuata mafundisho ya uongo, kwa udhuru kuwa na waliotutangulia walifuata, tunaanguka chini ya hukumu ya BABEL pia tunakunywa mvinyo ya machafuko yake.“
GC 536.3; Tragedie des siecles p. 585






“Kamwe ulimwengu usiingizwe kanisani na kuoana na kanisa, ili vifanye umoja. Vikifanya hivyo, hakika muelekeo wa kanisa ni machafuko, kama vinavyoelezwa vizuri katika ufunuo‚’ngome ya kila ndege mchafu mwenye kuchukiza’“
TM 265
Waadventista wameanguka, wameasi, kama ilivyotabiriwa, wanaongozwa na shetani
“Kanisa liko katika hali ya ulaodikia, kuwepo kwa Mungu hakumo katikati yao“
3S 84 (1903); 1NL 99 ( 1898 ); Matukio ya siku za mwisho 164
“Ndio maana imepita miaka mingi, sioni General Conference kama sauti ya Mungu“
17MR 216 (1898); Evenements des desnies pour 54
“Kwamba watu hawa wangepaswa kusimama katika mahali patakatifu, kuwa kama sauti ya Mungu kwa watu, kama hapo mwanzo tulivyoamini General Conference kuwa – hilo sasa limepitwa na wakati” 
GC Bulletin April 3, 1901, p. 25
N.B. Waliochaguliwa, wanapoasi, Mungu huwaacha (1Samuel 2:30)
Kwa Waisraeli wa zamani, mafungu yaliyoandikwa juu yao wakati wa kuchaguliwa kwao, yaliendelea kuwepo hata baada ya kuagwa, wakayafanya kuwa udhuru na tumaini kuwa Mungu hawezi kuwaacha.
Isaya 49:16; Zekaria 2:8; Yeremia 7:3 – 5; Isaya 2:5 – 6.
Hata Leo, maneno yaliyotajwa juu ya kanisa la waadventista kabla ya kuanguka, yamefanywa kuwa udhuru Na kinga baada ya kuanguka kwao, Kwa sababu mpaka sasa bado yanapatikana ndani ya magombo.
Historia inajirudia  (MUHUBIRI 1:9)
Kwa nini baada ya Waisraeli kuanguka na Mungu kuwaacha, bado Mungu aliacha ahadi
Ndani ya Biblia bila kuzifuta, alizokuwa amewapa ya kuwa hatawaacha  ?
“…... yakaandikwa ili kutuonya sisi, tuliofikiwa na miisho ya dunia”            1Wakor.10:11, 
“Kila andiko lenye pumzi ya Mungu, lafaa kwa mafundisho, na kuwaonya watu makosa yao
na kwa kuwaongoza, na kwa kuwabidisha katika haki” 2Timo. 3:16.
KUMBE!  
“WALIOCHAGULIWA, MUNGU HUWAACHA NA KUCHAGUA WENGINE PALE WANAPOMUASI.”

                                                                 

KWA MAWASILIANO ZAIDI WASILIANA NASI
0756959525,0752164685
Share:

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni

Popular Posts

Lebo

Recent Posts

Pages