DHAMBI NI NINI?
Dhambi ni:
•uasi
•kutotii(disobedience)
•uhuru nje ya Mungu
•Tendo lolote lisilokubaliwa na mbingu ni
dhambi.
’the original translation means«to miss the
mark of God's holy standard of righteousness
»
•Torat9:7 «Kumbuka, usisahau ulivyomtia
Bwana, Mungu wako, kasirani jangwani; tangu
siku uliyotoka nchi ya Misri hata mlipofika
mahali hapa, mmekuwa na uasi juu ya Bwana
8 Tena mlimkasirisha Bwana katika Horebu,
Bwana akakasirika nanyi hata akataka
kuwaangamiza.»
•1Yoh3:4«Kila atendaye dhambi, afanya uasi;
kwa kuwa dhambi ni uasi»
Nabii asema:
“Mungu anakusudia kutufahamisha kuwa
kutotii(disobedience) na dhambi ni machukizo
makubwa machoni pake;na lazima
yasichukuliwe kiurahisi!
Anatuonesha kuwa wakati dhambi ijitokezapo
ktk kanisa lake lazima hatua kali zichukuliwe
ili gadhabu yake isilikumbe kusanyiko zima
kwa ujumla!”TE1 383.1
«Wakati ambapo viongozi wa kuaminika
wanapopuuza kufichua dhambi Bwana
atawaonjesha hasira yake na kanisa zima
litawahibika ktk dhambi hizo.
Bwana alionesha tangia zamani jinsi ilivyo
lazima kwa kanisa kujitakasa.Mdhambi
mmoja aweza kuwa chanzo cha nuru ya
mbinguni kulihama kanisa kwa ujumla.Wakati
kanisa linapogundua kuwa linaatamiwa na
giza na lisijue nini chanzo,linakazimika
kumtafuta Mungu kwa juhudi na kwa
unyenyekevu wa hali ya juu saana mpaka pale
watakapogundua kinachomhuzunisha Roho na
kukitupilia mbali”TE1 383.2
Nizungumzapo nawe ktk walaka
huu,nikijitahidi kufafanua kuhusu dhambi
silengi wizi,uongo,utukanaji nk nalenda
dhambi mbaya kuliko donda la kansa(UZINZI)
•√NI KTK NJIA ZIPI DHAMBI HII HUTENDEKA?
__________________________
N°1—Mahusiano ya watu wenye jinsia tifauti
hata kama ni dada/kaka ktk Kristo,maana
kumbukeni miili yenu haijaongoka,kwa
kuepuka hilo acheni mahusiano hayo!
★Rumi8:7“Kwa kuwa ile nia ya mwili ni uadui
juu ya Mungu, kwa maana haitii sheria ya
Mungu, wala haiwezi kuitii.”
N°2— kwa kusifiwa ati u-mzuri(handsome/
beautiful) itakuamshia hisia mbaya,kuepuka
hili kemea yeyote anayeskusifia na ueuke
kuwasifu watu–mkumbukeni Yusufu!
★Mithal27:21b “....na mtu hujaribiwa kwa
sifa zake”
N°3—wengine hufikia umri na sifa za kuoa/
kuolewa ila wanaamua kubaki bila kuaoa/
kuolewa wanajisababishia kujikuta wakizini
bila kutambua!
★1korinto7: 9 “Lakini ikiwa hawawezi
kujizuia, na waoe; maana ni afadhali kuoa
kuliko kuwaka tamaa”
N°4—Wengine hukaa upweke bila kazi kwa
masaa kadhaa wawapo maofisoni au sehemu
zingine hivyo wanaruhusu mawazo potofu na
kumkosea Mungu kama ilivyomtokea Daudi.
N°5—na wengine wapatapo marafiki ktk
mitandao mara tu baada ya kuishiwa
maongezi wanalazimika kuongelea
yaufurahishao moyo(uzinzi furaha ya kizazi
cha Nyoka-The happiness of the snack
Generation)
ILI KUEPUKA DHAMBI HII,EPUKA HAYA:
*kumsifia asiye mkeo/mmeo
*kum touch
*kumbusu
*kumkonyeza
*kumlembea sauti
*kuchat naye saana hasa masaa ya ucku
*usimtamani
*usiangalie films za uzinzi
*kusimlia yahusuyo uzinzi!
nk —yote haya ni kuvunja amri ya 7!
«Punde mara Shetani anapofanikiwa kuitenga
nafsi kutoka kwa Mungu,ambae ndiye chanzo
pekee cha nguvu,anatafuta kuamamsha tamaa
zisizo takatifu za asili ya mwanadamu.Kazi ya
adui sio ya ghafla anapoanza kuifanya ni siri
inayoondoa kanuni na ngome imara.Kwanza
huanza kama vitu vidogo—kutojali kuwa
waaminifu kwa Mungu na kumtegemea kwa
nguvu zote na kuelekea kufuata desturi na
mienendo ya ulimwengu»PP718
Yohana15:14“Ninyi mmekuwa rafiki zangu,
mkitenda niwaamuruyo”
BARIKIWA!
KWA MAWASILIANO ZAIDI WASILIANA NASI
0756959525,0752164685
Asante kwa somo zuri
JibuFutaAmina sana
JibuFuta