MUHIMU: Somo hili limeelekezwa zaidi kwa kaka zetu na dada wa imani ya Kisababto ambao wanajifunza unabii. Hata hivyo, hii haina maana ya kusema kuwa wale walio nje ya SDA hawataweza kuona huu Ukweli kama vile ulivyo kwa sababu ni tukio la unabii hakika, na linatokea kwa uhakika katika siku zetu!
Katika historia yote ya watu wa Mungu
tunaona tabia moja inayojirudia na iliyobarikiwa. Imesemwa wazi kwa vielelezo
kwa muda kwamba siyo sifa tu, hata hivyo, lakini zaidi uhitaji. Bila shaka
ninaongea kutoka katika uhitaji wa moyo kuwa “Tokeni kwake, enyi watu wangu”
ili kumfuata Bwana vizuri zaidi popote anapoweza kuongoza.
Kama tukichunguza njia ambayo Baba
aliwaongoza watu wake kutoka Babeli, michakato mitatu ya iliyopita ya Kanisa lake; tutaweza kuona
vizuri zaidi mapenzi ya Roho Mtakatifu katika mchakato wa nne na wa mwisho wa
Kanisa la Mungu.
“Ninataka kusistiza ukweli, kwamba Makanisa ambayo Yohana aliambiwa
kutuma maelekezo aliyopewa huwakilisha Makanisa yote katika ulimwengu wetu, na
kwamba huu ufunuo kwake unapaswa kujifunzwa na kuaminiwa na kuhubiriwa na
Kanisa la Waadventista Wasabato leo. Kristo alikuja binafsi kwa Yohana
kumwambia, ‘Mambo hayo…yaliyopo, na yale yatakayokuwa baada ya hayo’ (Ufu 1:19). Na kisha akaniambia, ‘Haya
uyaonayo uyaandike katika chuo, ukayapeleke kwa hayo makanisa saba’ (Ufu 1:11).
Nuru haikutakiwa kufichwa chini ya pishi.”
“Katika ufunuo ambao Kristo alitoa
umeungwa pamoja katika mnyororo wa ukweli ujumbe muhimu wa onyo na kwa dhahiri
unapaswa kutolewa kwa ulimwengu kabla ya ujio wa pili wa Kristo. Ujumbe wa
mwisho wa rehema unapaswa kuhubiriwa mahali ambapo haujapata kusikiwa. Watenda
kazi wanapaswa kufanya kazi kwa kujinyima nafsi, kwa namna hiyo ya kujitoa,
kiasi kwamba ujumbe utapelekwa kwa wale ambao hawajapata kuusikia” (“Manuscript
Releases,” 1:372).
Ujumbe kwa Makanisa saba, pasipo swali, ni
lazima uhubiriwe katika karne zote. Leo, kikiwa ni kipindi wa Kanisa la mwisho,
tumeitwa kupokea ujumbe wote kutokana na uharaka wa wakati tunaoishi ndani
yake. Ni maarifa ya kawaida kwamba Ibilisi anajua kuwa ana muda mchache, kwa
hiyo, kusema kweli, anazunguku kila mahali ulimwenguni akimmeza kila anayeweza.
Haijapata kutoke katika historia ya Kanisa kabla tulipoona mchezo wa
ushambuliaji uliopangwa kwa watu wa Mungu. Adui amejifunza kila somo kwa kusoma
madhaifu ya watu wa Mungu zaidi ya miaka 6,000 na linatumiwa dhidi yetu.
Unabii hauongelei Makanisa manane balisaba. Hivi vipindi saba vya
unabii vilivyoongelewa katika Ufunuo sura ya pili na ya tatu vinaonyesha kile
ambacho ingemchukua Roho Mtakatifu kuweka sawa tabia za wale “walioitwa kutoka”
huko na kuingia katika ukamilifu huo uliotabiriwa. Masalio hawa humtukuza Baba
kuliko yeyote anavyoweza. Hawa ni watu wa pekee, “wazao wake waliosalia,” (Ufu 12:17) ambao wanapokea muhuri wa
Mungu aliye hai.
Mchakato wa watu wa Mungu wakati wa
kipindi cha Makanisa saba, bila shaka, ni wale walioitwa kutoka Babeli “kumfuata Mwana-Kondoo kila aendako” (Ufu
14:4). Michakato hii imepambanuliwa kuwa watoto wa Mungu wakitenda sawa na
mapenzi yake makamilifu yalivyowataka watende. Michakato yao inaonekana kama
bado ni njia ya kumthibitisha Bwana Yesu Kristo na ukweli wake kama wa juu. Kwa
sababu pasipo mkono wake kuhusishwa, wasingechukua hata hatua moja katika
sehemu ya kwanza. Na mahali pasipo na hatua, hakuna mchakato.
“Kutoka karne
hadi karne Kristo alikuwa ametoa hazina zake kwa Kanisa, na kutoka kizazi
kimoja hadi kingine watumishi wake
waaminifu wameendeleza talanta walizopewa. Karama ambazo miaka elfu moja mia nane iliyopita aliziweka katika
mikono ya wahudumu wake waliochaguliwa, mitume kumi na wawili, zimeshuka kwa
watenda kazi wake katika kizazi hiki. Na bado ni watu wachache kiasi gani kati
yetu wanatambua bahati hii, na nafasi yetu kama wahudumu wa neema yake”
(“Manuscipt Releases,” 5:358.).
Siku moja haitakiwi kuwa ya
kipekee. Bwana alisema waziwazi: “Mimi
nipo pamoja nanyi siku zote, hata ukamilifu wa dahari” (Mt 28:20). Yuko
pamoja nasi! Hatupaswi kuwa na jicho lililopofuka, au mgongo uliopoa kwa wito
tunaohisi ukivuta roho zetu kabisa. Kufanya hivyo kungekuwa udanganyifu kwa
mioyo yetu.
“Ulimwengu
unajiandaa kwa pambano kuu la mwisho, taifa kuinuka dhidi ya taifa jingine.
Jamii kubwa ya wanadamu wanachukua misimamo yao kinyume na Mungu. Lakini katika
kila kizazi Bwana Yesu amekuwa na mashahidi wake—masalio waliotumaini katika
neno la Mungu. Na leo, katika kila sehemu kuna wale wanaofanya ushirika na
Mungu. Mvuto muhimu wa mfereji wa chini unawaongoza kwenye nuru, na wakati
swali linapokuja kwao, ‘Nani aliye upande wa Bwana?’ watachukua nafasi zao
upande wake. Tabia yao imebadilishwa kufanana na tabia ya uungu, kwa sababu
wamesoma na wanatembea sawa na mafundisho ya Neno lake” (“Signs of the Times,” Novemba 23, 1904).
Kwa nini michakato minne? Mungu ni Mungu wa utaratibu na kanuni. Kila
kitu katika utendaji Wake kipo katika kanuni zake. Mungu hutenda kazi katika
hatua nne ili kufikia kukomaa kwa kazi Yake na mavuno kupatikana. Imeandikwa: “…..nawapatiliza wana maovu ya
baba zao, hata kizazi cha tatu na cha nne……Bwana
akamwambia Ibrahimu, Ujue hakika ya kwamba uzao wako utakuwa mgeni katika nchi
isiyo yake, watawatumikia watu wake, nao watateswa muda wa miaka mia nne. Na
kizazi cha nne kitarudi hapa, maana
haujatimia uovu wa Waamori bado.” Kutoka 20:5; Mwanzo 15:13, 16.
Katika amri ya pili Mungu
alimaanisha vizazi vinne kutoka kwa Adamu wa kwanza hadi Adamu wa pili yaani
Kristo. Vizazi hivyo ni kama ifuatavyo: kwanza Adamu – Nuhu (Mwanzo 5); pili
Nuhu – Ibrahimu (Mwanzo 11); tatu Ibrahimu hadi Yesu (Matthayo 1:2-16) na nne,
Yesu hadi mwisho wa dunia (Matthayo 24:34.)
Kwa Ibrahimu, Mungu alimuambia
kwamba kizazi chake cha nne ndicho kitarudi kwenye nchi ya ahadi baada kutumika
kwa miaka mia nne katika nchi ya utumwa. Kizazi cha kwanza cha Ibrahimu ni
Isaka, kizazi cha pili ni Yakobo, kizazi cha tatu ni watoto 12 wa Yakobo na
kizazi cha nne ni watoto wa watoto 12 wa Yakobo. Tunatambua kwamba watoto 12 wa
Yakobo walifia Misri na wakati Waisraeli wanatoka Misri walibeba mifupa ya
Yusufu na kuondoka nayo (Mwanzo 50:25.)
Katika Maandiko hayo tunatambua
kwamba haikuwa kwa kubahatisha kwamba Mungu alitoa Amri ya pili na kuielezea
katika mpangilio wa vizazi vinne kwa wale watakaokwenda kinyume na matakwa
yake. Pia alimwambia Ibrahimu kwamba uzao wake utakaa Misri kwa miaka mia nne katika
hali ya utumwa ambapo sababu ya kuwa huko kwa kipindi hicho ni kusubiri uovu wa
Waamori ufikie katika kipimo cha kujaa kikombe.
Akiwa hapa duniani, Yesu
alifundisha “Akasema, Ufalme wa Mungu, mfano wake ni kama mtu aliyemwaga mbegu
juu ya nchi; akawa akilala na kuondoka, usiku mchana, nayo mbegu ikamea na
kukua asivyojua yeye. Maana nchi huzaa yenyewe; kwanza jani, tena suke, kisha ngano pevu katika suke. Hata matunda
yakiiva, mara apeleka mundu, kwa kuwa mavuno yamefika.”
Hizi ndizo hatua nne katika kanuni
ya utendaji wa Mungu ili kupata mavuno katika ufalme wa Mungu; yaani hatua ya
kwanza ni jani, ya pili ni suke, tatu ni ngano pevu katika suke na nne ngano
iliyokwisha kuiva au kukomaa tayari kwa mavuno. Je, mavuno katika uharibifu yanapatikana kupitia hatua
ngapi? “Lakini kila mmoja hujaribiwa na tamaa
yake mwenyewe….Halafu ile tamaa ikiisha kuchukua mimba huzaa dhambi, na
ile dhambi ikiisha kukomaa, huzaa mauti.”
Yakobo 1:14,15. Hatua nne pia kuelekea kuvunwa katika uharibifu, kwanza tamaa,
pili mimba, tatu dhambi na nne mauti.
Ilikuwa ni kupitia hatua nne pia
kwamba Mungu aliwasafirisha Israeli wa kale kutoka Misri kwenda nchi ya ahadi
ya Kanani. Hatua ya kwanza ilikuwa ni kutoka Misri hadi bahari ya Shamu; hatua
ya pili ilikuwa ni kutoka bahari ya Shamu hadi Sinai; tatu kutoka Sinai hadi
Kadesh na nne ni Kadesh hadi Kanani. Ndiyo maana Israeli wa leo, yaani kanisa
la Mungu baada ya Israeli wa kale, lazima lisafirishwe na Mungu katika hatua
nne ndipo wale watakaokuwa wamekomaa kama ngano safi watavunwa katika ufalme wa
Mungu.
Ili kukamilisha safari ya Israeli
wa leo, Mungu analiongoza kanisa Lake kupitia katika vipindi saba
vilivyoonyeshwa kupitia nabii Yohana. Wengi kwa kutojifunza chini ya uongozi wa
Mungu, wameshindwa kutambua jinsi Mungu anavyoliongoza kanisa Lake katika siku
hizi za mwisho.
Kabla ya vipindi saba vya kanisa
saba havijajapata kuwepo, wokovu ulikuwa ni wa Wayahudi, na pasipo shaka, hili
ndilo lilikuwa Kanisa la Mungu. Lakini kwa sababu Wayahudi walimwasi Mungu,
hawakuwa tena kanisa lake. Mungu ataendelea kutenda kazi kwa kutumia kanuni hii
hadi kukomaa kwa mavuno ya kanisa lake.
Basi
tuna Michakato Minne sambamba na
vipindi Saba vya Kanisa la Yesu:
Kipindi cha kanisa Jina
Hatua
|
||||||
Efeso
Smirna Pergamo Thiatira |
Ukristo
|
1
|
||||
Sardi
Filadelfia
|
Uprotestanti
|
2
|
||||
Laodikia
|
Uadventista
|
3
|
||||
Masalio wa SDA
|
4
|
|||||
1. Efeso (31-100 B.K.) “…na
ya kuwa huwezi kuchukuliana na watu wabaya” (Ufu 2:2, 3, 6, 7).
Mchakato wa Kikristo – Mitume wanahubiri ukweli kwa
ulimwengu katika hali ya juhudi za umisionari uliobarikiwa sana uliojulikana
kwa mwanadamu (Mdo 13:46; 17:6; 18:6)
2. Smirna (100-313 B.K.) “...Naijua dhiki yako na umaskini
wako, (lakini u tajiri)” (Ufu
2:9, 10).
3. Pergamo (313-538 B.K.) “...nawe walishika sana jina langu,
wala hukuikana imani yangu” (Ufu 2:13, 17)
4. Thiatira (538-1517 B.K.) “...wowote
wasio na mafundisho hayo…sitaweka mzigo mwingine” (Ufu 2:24-26).
5. Sardi (1517-1798 B.K) “Lakini unayo majina machache...watu wasioyatia mavazi yao uchafu” (Ufu
3:4, 5).
Mchakato wa Kiprotestanti – Matengenezo ya Kiprotestanti na
mashahidi wake wengi (Ufu 7:13-17).
6. Filadelfia (1798-Ujio wa
pili wa Kristo) “Yeye
ashindaye…nitaandika juu yake…jina langu mwenyewe” (Ufu 3:7-13, angalia
dondoo Na. 1).
7. Laodikia (1844-Ujio wa pili
wa Kristo) “Nayajua matendo yako, ya
kuwa hu baridi wala hu moto” (Ufu 3:14-21).
Mchakato wa Waadventista – Uamso mkuu ambao ulitoka ulimwenguni kote sawasawa na unabii wa
siku 2300 wa Danieli 8:14 na ulihubiriwa kuonyesha kuwa saa ya hukumu ilikuwa
imekuja (Ufu 10:1-11; 14:6-8; angalia pia Dondoo Na. 2).
Mchakato wa Masalio wa Siku
ya Saba – “Joka akamkasirikia yule mwanamke (kanisa la SDA),
akaenda zake afanye vita juu ya wazao wake waliosalia (Masalio wa SDA),
wazishikao Amri za Mungu, na kuwa na ushuhuda wa Yesu. Hapa ndipo penye
subira ya watakatifu, hao wazishikao amri za Mungu, na imani ya Yesu.” (Ufu 12:17; 14:10-12, 17; 15:2, 3).
|
||||||
Joka alifanya vita na wazao wa
kanisa waliosalia (Masalio) ambao walidumu katika kuzishika Amri za Mungu na
ushuhuda wa Yesu (Roho ya Unabii).
“Mungu ana Kanisa duniani, ambao ndiyo watu wake
waliochaguliwa, wanaotunza amri zake.Anaongoza, siyo kundi la waliopotoka
[machotara], siyo mmoja hapa na mwingine kule, lakini watu” (“Faith I Live By,”
ukr. 2).
Mungu amekuwa siku zote na Kanisa duniani.
Michakato iliyopita ya Kanisa la Kikristo ni uthibitisho wa matunda yanayonena
kwa ujasiri juu ya mioyo bikira ya watoto wa masalio waliopata kuwepo katika
vizazi vyote. Ni kile tu “kisemwacho na Bwana” kinachoweza kushika kamba za
moyo wa kitu hiki, watu wake. Hata kama wale wanaowazunguka wakitafuta kuua
miili yao, njia yao pekee ni kwenda popote Mwana-Kondoo aendapo. Hata kama hii
inamaanisha kuacha familia na marafiki, masalio wanapaswa kutembea na Bwana na
kufanya sawa na walivyoumbwa kufanya. Wateule hawawezi kufanya zaidi ya hili.
“Kwa kukataa njia za Mungu na kufuata njia za
wanadamu, anguko la Israeli lilianza. Hivyo basi liliendelea, mpaka Wayahudi
walipokuwa mawindo hasa kwa mataifa ambayo matendo yao walikuwa wamechagua
kufuata.
“Kama
taifa, wana wa Israeli walishindwa kupokea bahati ambayo Mungu alitamani
kuwapatia.Wa kuthamini kusudi lake au kushirikiana naye katika kulitekeleza.
Lakini hata kama watu binafsi na watu wanaweza basi kujitenga wenyewe kutoka
kwake, Kusudi lake kwa hao wamtumainio halibadiliki. ‘Najua ya kwamba kila kazi
aifanyayo Mungu itadumu milele’ (Mhu 3:14).
“Wakati kuna viwango tofauti vya maendeleo
na udhihirisho tofauti wa nguvu yake kukidhi mahitaji ya watu katika vizazi
tofauti, Kazi ya Mungu kwa wakati wote ni ile ile. Mwalimu ni yule yule. Tabia
ya Mungu na mpango wake ni ile ile. Kwake yeye ‘hakuna kubadilika, wala kivuli
cha kugeuka-geuka’ (Yak 1:17).
“Mapitio ya Israeli yaliandikwa ili
kutuelekeza sisi. Basi mambo hayo yaliwapata wao kwa jinsi ya mifano,
yakaandikwa ili kutuonya sisi, tuliofikiliwa na miisho ya zamani’ (1 Kor. 10:11). Kwetu sisi,
kama ilivyokuwa kwa Israeli ya zamani, mafanikio katika elimu hutegemeana na
uaminifu katika kutekeleza mpango wa Mwumbaji. Utii kwakanuni za Neno la Mungu
kutatuletea mibaraka mikubwa kama ambavyo ungeleta mibaraka mikubwa kwa
Wayahudi” (“Education,” ukr. 50).
Ushauri wa upendo Bwana wetu anaoutoa kwa
Kanisa la Laodikia unaongelea waziwazi kuwa kinachotakiwa ni toba ya kweli kwa
wote walionaswa katika fikra hizi za upofu. Hakuna tofauti yoyote kuliko ya
viongozi wa Kiyahudu wa wakati wa Yesu, sawa na tunayoiona kwa viongozi wenye
majivuno wa Kanisa la Waadventista wa leo wakikataa ushauri wa wazi ulio katika
Maneno ya Bwana wetu. Miaka mingi Bwana ametuma watoto wake waaminifu wengi
kuwaonya wale anaowapenda. Lakini maonyo mengi yamedharauliwa na wengi. Hata
wakati ukweli uliothibitishwa umeletwa machoni pao, wamegueza kisogo. Rehema
kwa kiasi kikubwa imefungwa kwa Kanisa hili, sawa tu na rehema ilivyofungwa kwa
taifa la Wayahudi muda mrefu uliopita na Waprotestanti mwaka 1844. kama ilivyo,
rehema imefungwa kwa Kanisa zima lakini si kwa watu walio ndani yake.
Wakati wa unabii wa miaka 490 ulipotimia,
Mungu aliwaita watu kutoka katika makosa na kuanza mchakato wa Kikristo kwa
kutumia wale walioitwa. Kusema kweli Paulo aliingia katika Makanisa ambayo
kiunabii yalikuwa yamefungwa ili apate kuwatoa. Leo, Bwana anafanya kitu hicho
hicho. Watoto wake watakwenda popote Mwana-Kondoo anapoongoza, na kama wote
tunavyojua, hawezi kuwaongoza kupokea uasi wa wazi.
“Njozi ambayo Kristo alimwonyesha Yohana, ikionyesha amri za Mungu na
imani ya Yesu, inatakiwa kuhubiriwa waziwazi kwa mataifa yote, watu, na lugha. Makanisa, yanayowakilishwa na Babeli,
yanaonyeshwa kuwa yameanguka kutoka katika hali yao ya kiroho na kugeuka kuwa
mamlaka ya kutesa wale wanaotunza amri za Mungu na wana ushuhuda wa Yesu
Kristo. Kwa Yohana hii mamlaka itesayo inawakilishwa kuwa ina pembe kama
mwanakondoo, lakini inanena kama joka” (“Testimonies to Ministers
and Gospel Workers,” ukr. 117; “Evangelism,” ukr. 197).
“Kama Kanisa la Mungu likiwa vuguvugu,
halisimami katika kupendwa na Mungu tena kama Makanisa ambayo yanawakilishwa
kuwa yameanguka na kuwa maskani ya mashetani na ngome ya kila roho mchafu, na
ngome ya kila ndege mchafu mwenye kuchukiza” (“Manuscript Releases,” 19:176).
“Ulimwengu usiingizwe kamwe Kanisani, na kuolewa na Kanisa,
ukifanya muungano wa umoja. Kwa njia hii Kanisa litapotoka kweli, na, kama
ilivyoelezwa katika Ufunuo, kuwa ‘Ngome ya kila ndege mchafu mwenye kuchukiza’”
(“Testimonies
to Ministers and Gospel Workers,” ukr. 265).
Hali ya Kanisa la Waadventista Wasabato
leo kwa uhakika imekuwa ni Babeli. Kila aina ya uasi na mafundisho ya uongo
yamepokelewa na viongozi wake, na wamefanya hivyo kwa miongo kadhaa. Uchunguzi
wa kina wa fungu lifuatalo utakuongoza kuona kwamba hii ni hali iliyokuwa
imetabiriwa kwa Kanisa hili. “Mwanamke sasa amefikia hatua ya kujikinai, na
wakati huo huo, masalio ya uzao wake wamesimama imara.
“Joka akamkasilikia yule mwanamke, akaenda
zake afanye vita juu ya wazao wake waliosalia, wazishikao amri za Mungu, na
kuwa na ushuhuda wa Yesu Kristo” (Ufu 12:17).
Imetabiriwa waziwazi kwamba joka
litazidisha mashambulizi yake na kufanya vita kwa masalio ya wazao wake, na siyo uzao wenyewe. Awali ya yote uzao wa
mwanamke, Kanisa mama [SDA], lilishikilia sheria na kujua unabii. Ndiyo,
Shetani ana hasira na hili Kanisa. Hata hivyo, hasira yake imelifanya
kumwinamia. Ni masalio ya uzao wake wanaomfanya aende vitani sasa, kwa sababu
hawako tayari kumsujudia. Masalio wanaotunza siku ya saba wanathibitishwa kuwa
ni wale wanaoshinda.
“Hata kama sheria ya Bwana itadharauliwa karibu ulimwenguni kote,
kutakuwepo na masalio wa haki ambao watakuwa watiifu kwa matakwa ya Mungu.
Hasira ya joka itaelekezwa dhidi ya watumishi waaminifu wa mbinguni. Nabii
anasema, ‘Joka akamkasilikia yule
mwanamke, akaenda zake afanye vita juu ya wazao wake waliosalia, wazishikao
amri za Mungu, na kuwa na ushuhuda wa Yesu Kristo’ (Ufu 12:17). Tunaweza kuona kutoka kwenye andiko hili
kuwa siyo Kanisa la kweli la Mungu ambalo linafanya vita na wale wazishikao
amri za Mungu na kuwa na ushuhuda wa Yesu Kristo. Ni wale wanaoidharau na
kuitangua sheria, wanaojiweka wenyewe upande wa joka, na kuwatesa wale
wanaoithibitisha sheria ya Mungu” (“Signs of the Times,” April 22, 1889).
Joka akaenda zake afanye vita juu ya wazao wake waliosalia.
|
|||||||||
“Niliona kanisa kwa jina na
Waadventista kwa jina, kama Yuda, watatusaliti kwa Wakatoliki ili wapate nafasi
ya kuwa kinyume na ukweli. Kisha watakatifu hawataeleweka, wakijulikana kidogo
kwa Wakatoliki; lakini makanisa na waadventisata kwa jina wanaojua imani yetu
(maana walituchukia kwa sababu ya Sabato), watawasaliti watakatifu na kupeleka
taarifa kwa Wakatoliki kuwashitaki watakatifu kama watu wasiojali taasisi za
wanadamu; yaani, wanaitunza siku ya Sabato na kutokuijali siku ya jua,
jumapili.” [Ellen G. White, SpM 1.5]
Hata leo, wengi wetu ambao
tunapeleka ukweli kwa moyo mzuri kwa wale wanaoanguka katika uasi, tumeona aina
zote za uovu zikibambikizwa juu yetu. Dada White alieleza hili kwa uyakinifu, “Ahabu
alimhesabu Eliya kama adui yake kwa sababu nabii alikuwa mwaminifu kukemea
maovu yake ya siri. Kwa hiyo leo mtumishi wa Kristo, mkemeaji wa dhambi,
hukumbana na dharau na kukataliwa makusudi” (“Spirit of Prophecy,” 3:12; “The
Desire of Ages,” ukr. 589).
Kama tunavyojua, kwa njia ya kujifunza
unabii, mchakato wa Ki-ekumene tunaouona ukienea kila mahali katika ulimwengu
wa leo, hatimaye utakusanya wale wote walio wa Babeli kufanya vita dhidi ya
Masalio waaminifu wa Siku ya saba. Tunayaona haya katika michakato ya Upapa
kupitia katika Kanisa moja la ulimwengu, na tunaona mshikamano wa Kikristo
ukitenda kazi kwa ushirikiano na Roma ili kufikia mwisho ule ule hapa hapa
Marekani. Muda si mrefu siku itawadia wakati ambapo tutashuhudia kile ambacho
Wakristo wote wa zamani waliona wakati wa zama za mateso makali. Wale wote
wanaochukia ukweli watawazunguka wana wa masalio wanaochukiwa ulimwenguni kote.
Ni wakati muafaka wa kuwakaribia ndugu
zetu na kaka katika Bwana na kujaribu kuwambia ukaribu wa mambo katika siku
zetu. Kitu cha kusikitisha ni kwamba, hii si kazi nyepesi kuifanya. Shetani
ameshawadanganya wengi tayari na utaratibu wa aina hiyo hiyo wa kuchanganya
alioutumia kipindi cha nyuma. Wengi wao sasa wanapokea kuwa Kanisa la
Waadventista Wasabato litapita hadi mwisho bila kujali ukweli kwamba kuna
ushahidi mwingi uliokusanywa dhidi yake kulifunua kama dada kwa Babeli
iliyoanguka. Kama wakipokea uongo ni namna gani wanaweza kusimama upande wa
ukweli? Bado, baadhi wataruhusu dhambi ya wazi kutamalaki kwa kile wanachokiona
kuwa “kizuri zaidi.” Kuchanganyikiwa huku tu kunatosha kutambulisha kuwa hii
niishara mojawapo ya kutangaza kwamba mkono wa Bwana uko upande wa mchakato wa
Masalio wa Siku ya saba.
|
||||||
Hata
hivyo kujitenga ni kanuni ya Mungu. Musa aliwaambia waisraeli wajitenge na
waasi kule jangwani kabla Mungu hajawaangamiza kwa kufunua kinywa cha ardhi na
kuwafunika waasi wote. “Kulikuwepo na
kutoka nje, utengano wa kujitenga na waovu uliotolewa maamuzi, kukimbia ili
kuokoa maisha. Ndivyo ilivyokuwa katika siku za Nuhu; ndivyo ilivyokuwa kwa
Lutu; ndivyo ilivyokuwa kwa wanafunzi muda mfupi kabla ya angamizo la
Yerusalemu; na ndivyo itakavyokuwa katika siku za mwisho. Sauti ya Mungu
inasikika tena ikiwa na ujumbe wa onyo, ikiwataka watu wake wajitenge kutoka
katika wimbi la uovu.” [E.G. White, Wazee na Manabii uk. 167, kurasa za ndani.]
Kwa kuangalia neno lake, mtu anaweza kuona
waumini wakimfuata Bwana wao kwa uaminifu kufanya kazi aliyowaitia kuifanya.
Mwanzoni kabisa tulikuwa na Kanisa la Kiyahudi ambalo lilikuwa limechaguliwa na
Baba kutangaza ukweli wake kwa Ulimwengu. Lakini uovu uliingizwa na hatimaye
walikutwa hawastahili kupata uzima wa milele. Kwa hiyo watu wa Bwana walitoka
kati yao kufanya kazi ya Bwana na kuanza mchakato wa Kikristo. Baada ya hapo
tunaona tena Kanisa likiingiliwa na uovu wakati Ukatoliki wa Kirumi
uliporuhusiwa kuchanganyika na Upagani na Ukristo.
Tena
watu wa Bwana walitoka kwenye uovu ili kufanya kazi katika matengenezo ya
Kiprotestanti. Hatimaye tena uovu ulikumbatiwa na sauti ya Bwana wetu ilisikika
kwa Waadventista waaminifu kutoka Babeli na kufanya kazi yake. Bila shaka,
historia ilirekodi hili kama mchakato wa Waadventista Wasabato. Mwishoni, leo
katika saa ya kumi na moja tunaona Kanisa la Waadventista Wasabato likikumbatia
uovu kama ukweli. Kwa hiyo Bwana kwa mara nyingine tena anatangaza kwa Masalio
wake waaminifu kutoka kati yake na kufanya kazi ambayo ni ya haraka sana katika
siku zetu. Je, unaweza kuona uhakika wa unabii wa matukio haya? Je, hii yote
haijaonyeshwa kwa vielelezo kamili katika mfano wa wakulima katika shamba la
mizabibu uliotolewa na Bwana Yesu mwenyewe?
“Kwa maana ufalme wa mbinguni umefanana na
mtu mwenye nyumba, aliyetoka alfajiri kwenda kuajiri wakulima awapeleke katika
shamba lake la mizabibu. Naye alipokwisha kupatana na wakulima kuwapa kutwa
dinari, aliwapeleka katika shamba lake la mizabibu. Akatoka mnamo saa tatu, akaona
wengine wamesimama sokoni wasio na kazi; na hao nao akawaambia, Enendeni nanyi
katika shamba langu la mizabibu, na iliyo haki nitawapa. Wakaenda.Akatoka tena
mnamo saa sita na saa kenda, akafanya vile vile. Hata kama saa kumi na moja
akatoka, akakuta wamesimama, akawaambia, Mbona mmesimama hapa hapa mchana kutwa
bila kazi? Wakamwambia, Kwa sababu hakuna mtu aliyetuajiri. Akawaambia,
enendeni nanyi katika shamba la mizabibu”
(Mt. 20:1-7).
|
||||
Ukweli ni kwamba waumini wa kweli
walijitenga kutoka kwenye sinagogi la Shetani la taifa la Kiyahudi, kwamba
walitoka pia kutoka katika Upagani wa Ukatoliki wa Kirumi, na kwamba hata
walitoka pia kutoka katika uovu wa Kiprotestanti. Na sasa tunaona Masalio tena
wakielekea katika mwelekeo wa kweli tu ambao mtoto wa Mungu anaweza kuufuata.
Tunaweza kuongozwa tu na Mwana-Kondoo wa Mungu. Hatutakiwi kunajisiwa na
wanawake hawa (au Makanisa yaliyoasi—angalia Ufu 14:4).
Wateule wa Mungu hawawezi kudanganywa.
Tunapaswa kufuata popote anapoongoza! Tunafanya hivyo tu kwa sababu sisi tu
kondoo wake, na tunaisikia kwa uhakika sauti yake. Wakati viongozi wa Kanisa
wanapokumbatia uovu hadharani na kukataa kila onyo la kutubu, masalio hawawezi
kusimama nao tena. Hasa baada ya mambo mengi kuwa yamefanyika kujaribu
kuwajulisha uasi ambao hawaukumbatii tu bali pia wanauhamasisha.
Je,
sisi siyo watu wanaoelewa kanuni ya unabii? Je, hatuvutwi sana katika mioyo
yetu kutafuta makimbilio mahali ambapo tunaweza kuabudu katika kweli sawa na
mioyo yetu inavyotusukuma kufanya? Wateule hawawezi kusimama na uovu, sawa na
ambavyo Shetani hawezi kusimama katika kweli. Haiwezekani kabisa kutokea.
Hivi karibuni nilitoa swali hadharani
kuhusiana na “kutoka” katika Kanisa la Waadventista Wasabato. Nilitaka kujua
kama kila mtu alikuwa analiona. Kwa muda mfupi tu, nimepokea mamia ya barua
pepe zikieleza ukweli katika ukweli huu, na kuomba ushauri juu ya nini cha
kufanya hatimaye. Watu kutoka ulimwenguni kote wanatafuta wale wanaoweza
kuwaamini na kumwabudu Bwana pamoja nao katika roho na kweli. Wana njaa ya
ukweli tunaoutoa. Hauhubiriwi katika mimbari ya Makanisa yao tena. Kondoo
hawalishwi tena katika Makanisa haya. Wametoka, kwa sababu hakuna nafasi kwa
ajili yao tena katika Makanisa haya. Ni wazi kuwa sauti ya Bwana inasikika.
Watoto wake wanaitikia wito wake “Tokeni kwake, enyi watu wangu.”
Litunze hilo mawazoni. Watoto wake ni
kweli huisikia sauti yake. Wanatoka kabisa kati yake.Hili siyo jambo ambalo
yeyote anahitaji kushurutishwa tena zaidi. Kutoka kwa watu wengi kunatokea
ulimwenguni kote. Kwa baadhi yetu tulio na huduma duniani kote, ukweli huu
unajirudia kila siku mbele za macho yetu kutoka katika kila sehemu ya maisha.
Watu nje na ndani ya Kanisa wanaona hili waziwazi.
Wale wanaokubali au kupinga utengano
wanakiri, kuna mchakato mwingine unaoonekana leo! Hii tu iko wazi kabisa. Kama
nilivyosema mapema, mkono wa Bwana unaonekana hapa. Kwa sababu pasipo mkono
wake kuhusika, Wafuasi wa Mungu wasingechukua hata hatua moja kutoka katika
Kanisa lililoanguka. Mahali popote pasipokuwa na hatua, hakuna mchakato. Na kwa
yakini kuna mchakato wa watu wa Mungu siku hizi kabisa. Je, usingependa kuwa
sehemu ya Mchakato wa
Masalio?
KUMBUKA
1: Wengi wanaamini kwamba Filadelfia
iliishia mwaka 1844, lakini mlango ule uliofunguliwa kwa Filadelfia ulikuwa ni
mlango wa Patakatifu pa Patakatifu kule mbinguni (angalia “Spirit of Prophecy,” 4:268-269). Hivyo hali ya Filadelfia inazidi
baada ya Oktoba 22, 1844 mpaka kazi ya huduma ya Kristo imekamilika.
KUMBUKA
2:Kristo ameauacha mchakato wa Kiadvenista
na hali kadhalika Kanisa la SDA (“Testimonies
for the Church,” 8:250) kwa sababu ya uasi kama vile alivyofanya kwa Kanisa
la Kiyahudi (Mwa 49:10; Mt 21:43; 23:12-24:2; 27:50, 51). Roho Mtakatifu
anagusa mioyo ya watoto wake kutoka katika Makanisa yaliyoanguka ili kupokea
ukweli wake. (Ufu 3:15-17; 16:9, 11; 18:1-5).
Fanya
uamuzi wa kujitenga sasa kutoka katika mifumo ya madhehebu yaliyopotoka madamu
Mungu anapataikana na mlango ukingali wazi.
MUNGU
akubari.
KWA MAWASILIANO ZAIDI WASILIANA NASI
0756959525,0752164685
Thanks alot
JibuFuta